Pamoja na madudu yote Kawambwa hakuwahi kufokewa hadharani?

Na hao wote uliowataja na aliotaja Ntemi K wameteuliwa na kilaza mkuu mwenyewe!!! Kaazi kweli kweli.

Na kioja zaidi..huyu jamaa licha ya the kutuhumiwa ukilaza....amechagiliwa mara 2 mfululizo kuwa Rais....sasa hapa Kilaza ni nani? kama sie mimi na wewe?
 
Na kioja zaidi..huyu jamaa licha ya the kutuhumiwa ukilaza....amechagiliwa mara 2 mfululizo kuwa Rais....sasa hapa Kilaza ni nani? kama sie mimi na wewe?

Mimi na wengine wengi sana hatukumchagua.....mapaka leo tunashangaa alichaguliwa na nani wakati wengi wetu hatukumchagua........labda alijichagua mwenyewe
 
Mimi na wengine wengi sana hatukumchagua.....mapaka leo tunashangaa alichaguliwa na nani wakati wengi wetu hatukumchagua........labda alijichagua mwenyewe

Mimi pia sikumchagua na wala siwezi kumchagua mtu wa aina yake kuwa kiongozi wangu (kwa ngazi yoyote ile). Inawezekana amechaguliwa na wakulima ingawa pia nina wasiwasi wakulima wa kijijini kwetu walimchagua kwani ukiwasikia wanamuongelea unashangaa ni akina nani walimchagua... labda majini ya Sheikh Yahya!
 
Kandoro,Kawambwa na KIKWETE ni ndugu wa damu mama zao wamezaliwa pamoja kwa hiyo kiubinadamu hawezi kumgombeza ndugu yake japo shemeji yake Hawa Ghasia alimbarasa sana ndugu wa mkewe
 
Jk anamwita kawambwa mjomba yaani wana undugu wa karibu kabisa na jeykey ndiye aliyemshawishi kawambwa aache kazi pale udsm idara ya mechanical engineering "Internal combustion" ambapo kawambwa alikuwa mhadhiri, ili akagombee ubunge kwa mihadi ya kumpatia ulaji.

Alipofanikiwa kupata ubunge kila mtu alishangaa kuwa hata huko kwenye kampeni kawambwa aliongea kitu gani maana jamaa ana aibu hadi anajionea aibu yeye mwenyewe. Jamaa ni non-performer kwani hata pale Udsm hakuwahi kupata hata ukuu wa idara japo wahadhiri walikuwa kibao na yeye akiwa wa siku nyingi na mavyeo yalikuwa ya kumwaga.

Kama alishindwa kuhudumia watu wasiozidi 100, atawezaje kuhudumia watu millioni 43? Haiwezekani kamwe.
 
Shukuru Kawambwa akiwa waziri wa ujenzi barabara ya jimboni kwake itokayo Msata mpaka Bagamoyo ilihujumiwa na contractors ambao walilipwa fedha za ujenzi wa barabara halafu wakakimbia; hakuna hatua zozote zilizochukuliwa badala yake fedha nyingine zikatengwa na serikali na Subash Patel amepewa kuijenga hiyo hiyo barabara kwa mabilioni ya fedha!! Kama wasemavyo waswahili, wachawi wakikutana huunda timu basi wachawi wetu ndio hao na ndio maana hawafokeani hata pale wanapolitia hasara taifa. Huyu huyu Kawambwa akiwa wizara ya ujenzi alilidanganya bunge mara chungu nzima kuwa mazungumzo na muwekezaji wa ATCL yalikuwa yanakamilishwa lakini mpaka sasa hivi muwekezaji hajapatikana na shirika linakufa!!
 
[SIZE="3"[SIZE="3"]]Naomba ufafanuzi ktk hiyo red. JF is for Great Thinkers tafadhali don't down grade it kwa watu kuweka sweeping statements kama hizo ambzo ni unsubstantiated.

Hiyo Kanuni ya Sheria mpya ya barabara anayotamba nayo Dr Magufuli hivi sasa na kwa pupa kufikia hatua ya kuifanyia misquoting kiasi cha kutaka kulaza watu nje isivyo halalai ilitungwana kupitishwa wakati Dr Shukuru Kawambwa alipokuwa Waziri wa Ujenzi, but some people dont use the press for seekiing publicity and cheap popularity.

Laiti kama Magufuli angekuta hakuna hata hiyo Kanuni hapo wizarani, angepata wapi ubavu wa kupayuka hayo nayopayuka kila siku?

Tuache ushabiki lets go for reality!!!![/SIZE]

[/SIZE]

Ni mpumbavu na mjinga tu asiyeona tofauti ya kiutendaji kati ya magufuli na kawambwa. Kuunda sheria kuna kazi gani! Ebu niambie wanaounda sheria ni waziri au ni watendaji?? Hoja yako imelegea kama mlenda.
 
Ni mpumbavu na mjinga tu asiyeona tofauti ya kiutendaji kati ya magufuli na kawambwa. Kuunda sheria kuna kazi gani! Ebu niambie wanaounda sheria ni waziri au ni watendaji?? Hoja yako imelegea kama mlenda.

Utendaji gani huo, kushindwa kutafisiri sawasawa kanuni za sheria ya barabara na hivyo kukurupuka kuiamuru tanroad kuvamia nyumba za watu zilizoko katika eneo la upana wa mita 8 kutoka hifadhi ya barabara ya awli ya mita 22 kuja inayoopendekezwa na sasa ua mita 30 nchi nzima, na kuziwekea alama za x badala ya kuwasiliana na wizara ya ardhi kwa lengo la kuhifadhi ongezeko hilo ikiwemo kufanya tathmini ya kuwalipa wahusika fidia, ndipo aweze kuwataka kuondoka miezi sita baada ya kulipwa fidia hizo. Hivyo ndivyo ibara ya 27 (2,4,5,6) ya kanuni za sheria ya barabara namba 13 ya 2007, kama zilivyopitishwa kupitia tangazo ktk gazeti la serikali namba 21 la tar 23 jan 2009 zinavyoelekeza.
 
Majuha wawili wanawake!

Angetaka kumzima si angemuacha kwenye baraza; mbona kawaacha kibao. Ondoa uzushi wako!

Majitu yanamtetea mtu akitaka kuvunja nyumba. Kesho yatasema JK anavunja nyumba za raia wake.

Nyie toeni sifa mtakazo lakini ni huyuhuyu aliyeuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa.

Hongera mchapakazi Magufuli na JF oyeee!
 
Back
Top Bottom