Pamoja na madudu yote Kawambwa hakuwahi kufokewa hadharani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na madudu yote Kawambwa hakuwahi kufokewa hadharani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Apr 5, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wandugu,
  Ni swali la kizushi tu. Katika mawaziri waliopwaya wakiwa ujenzi ni Dr. Kawambwa. Ilikuwa kama wizara haina waziri. Ni kama alipokuwa wizara ya maji. Lakini nyakati zote hizo hatujawahi kusikia kikwete akiikemea wizara kwa kufanya mambo hovyo. Leo hii wameingia mawaziri wachapa kazi tunaona jamaa amechachamaa. Inakuwaje hapa? Au ndiyo kumalizana kwenyewe ionekane pombe imeshindwa kazi yake?
   
 2. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hawakukutana barabarani.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kawambwa -mbunge wa bagamoyo 2005-2015
  kikwete- mbunge wa bagamoyo 1995-2000
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kawambwa is a reflection of Kikwete. As the Boss illustrated above. Ukimfokea ni kama unajifokea mwenyewe.
   
 5. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  wachawi wakikutana huunda timu. Lakini wa kikutana na mtu wa Mungu hutengeneza uadui.
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Wale ni ndugu wanaitana mjomba!!pia Kawambwa ndio prestige ya JK kuwa wakwere wamesoma!!!!ingawa sio ****** mwenzie ila asili yake kaole bagamoyo kwa mamwinyi!!!!si wajua JK bagamoyo mjini hakubaliki maana sio mzawa wa pale ametokea 'bara' ndio maana waligawa lile jimbo!!!
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Jk mtu wa visasi jaman. Kamwambia magufuli,eti wizara na tanroads ni wazembe wa kutupwa. Jaman kweli?
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  rostam hawezi kumfokea Lowassa
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Wakati Kawambwa akiwa Waziri wa Ujenzi ulikuwa unaona kabisa anapwaya kwenye hiyo Wizara, sasa yuko Wizara ya Elimu i guess ndio kabisaa.
   
 10. Mwathirika

  Mwathirika JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Magufuli ni Doctor wa PhD ya kujisomea, lkn JK naye ni doctor sijui mwanzo wake!! Halafu inashangaza inashadadiwa kweli kweli wakati wengi tu walipata kupata hizo na hawakuwahi kuzitumia, JK mkubwa alikuwa nazo, Cigwiyemisi anazo aah!
   
 11. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Atamfokeaje mshikaji wake. Kazi ambayo ameshaifanya na anaendelea kuifanya Maghufuli inaonyesha kuwa uwezo wa JK ni mdogo kwa hiyo anafanya hivyo ili kumwonyesha kuwa hajafanya kitu. More is needed. Kawambwa hawezi kazi, in fact alishindwa kumuondoa fisadi Mrema TANROAD wakati Kilons Mprogomyi aliuanika ufisadi wa Mrema bungeni. Ila nadhani Maghufuli naye hawezi kukimbia kwa sababu akijiuzulu tu JK atamgeuka katika suala la uuzaji wa nyumba. Serekali isiyokuwa na dira na uwezo wa kusimamia katiba na maslahi ya wananchi wake ndiyo ilivyo. Kwa hiyo tusitegemee kitu cha maana kwenye serekali ya JK. Na JK alivyo bingwa wa kulipiza visasi, nakuambia siku Maghufuli akijiuzulu ndiyo siku hiyo hiyo anashitakiwa. Lakini RA, EL, Vijisent nk kamwe hawatashitakiwa. Hii ndiyo TZ
   
 12. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmmhhhhh mnataka kuanza kuleta hoja za ukabila sasa, hebu tuwe watanzania wenyewe hii dhambi itatutafuna wenyewe
   
 13. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bruker, suala sio ukabila. Lakini tuangalie kazi ambazo so far Maghufuli amezifanya na uzilinganishe na zile alizofanya Kawambwa. Pia, ujiulize kama kupeana maagizo na kuumbuana mbele ya wananchi ni jambo jema katika uongozi. JK ndiye aliyemteua Maghufuli kuwa waziri wa Miundo mbinu, wizara ambayo hapo nyuma wakati wa Mkapa, Maghufuli aliiongoza vema na wananchi tuliona barabara zikijengwa tena kwa kutumia hela ya watanzania na wala sio misaada. Je, kwani hakuna njia nyingine za kuwasiliana kati ya JK na Mawaziri wake mpaka kuwasiliana mbele ya watu. Kwanini Pinda alitoa matamko ya kumdhalilisha Maghufuli tena jimboni kwa Maghufuli? Wote Maghufuli, JK na Pinda wana mapungufu yao na mema yao. Lakini hili la kumdhalilishwa Maghufuli mbele ya wananchi ambao walikuwa wameshajenga imani kwake kwa sababu mara nyingi akishika wizara mambo yanaenda, sioni kama lilikuwa jema hata kidogo. By the way, JK ili kujoinyesha kuwa yeye ni bora, anasema ufanye kufuata sheria, najiuliza kuwa kwani hapo mwanzo alikuwa hafuati sheria? Na kama alikuwa hafuati kwanini hakukamatwa? Ile ilikuwa kupunguza umaarufu wa Maghufuli ili JK na Pinda waonekane wema wakati wema wao hatuuoni. Basi ngoja tuenjoy folleni za Dar es Salaam in the expense of kuwapaka mafuta Pinda na JK ili wang'are.
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kiukweli kabisa mawaziri wanaopwaya Kikwete anawabeba, yupo Sofia Simba, yupo Magembe, yupo Mkulo. Lakini wale wanaochapa kazi wanaonekana kama ma.vi vile, hatujasikia hata siku moja akiongelea vitisho anavyopewa Tibaijuka, wala kumsifia Magufuli kwa kazi nzuri. Kila siku tunasikia vijembe tupu sijui tutaishia wapi
   
 15. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  [SIZE="3"[SIZE="3"]]Naomba ufafanuzi ktk hiyo red. JF is for Great Thinkers tafadhali don't down grade it kwa watu kuweka sweeping statements kama hizo ambzo ni unsubstantiated.

  Hiyo Kanuni ya Sheria mpya ya barabara anayotamba nayo Dr Magufuli hivi sasa na kwa pupa kufikia hatua ya kuifanyia misquoting kiasi cha kutaka kulaza watu nje isivyo halalai ilitungwana kupitishwa wakati Dr Shukuru Kawambwa alipokuwa Waziri wa Ujenzi, but some people dont use the press for seekiing publicity and cheap popularity.

  Laiti kama Magufuli angekuta hakuna hata hiyo Kanuni hapo wizarani, angepata wapi ubavu wa kupayuka hayo nayopayuka kila siku?

  Tuache ushabiki lets go for reality!!!![/SIZE]

  [/SIZE]
   
 16. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  JK kawekwa,kawekeka
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  Kazi gani aliyofanya? TOA UFAFANUZI hiyo kushindwa kusoma na kutafisiri vizuri Kanuni za Sheria mpya ya barabara, kama ilivyo hapa chini:-
  Ibara ya 27 (2) ya Kanuni za Sheria hiyo inamtaka Waziri wa Ujenzi atakaporidhika kuwa ardhi fulani inahitajika kwa ajili ya maendeleo ya barabara atawasiliana na Wizara wa Ardhi, kwa ajili ya ardhi hiyo kuhifadhiwa. Kutokea upana wa hifadhi ya barabara kuongezwa kwa MIta 8 kupitia Kanuni za 2009, hakuna Waziri yoyote wa Ujenzi wala Mhe John Magufuli mwenyewe aliyewasiliana na Wizara ya Ardhi ili itimize wajibu wake wa kuhifadhi eneo hilo kwa mujibu wa sheria? Kitendo cha Magufuli kuwatuma wafanyakazi wa TANROAD kuweka alama ya X katika nyumba zilizoko katika upana wa MIta 8 kimekiuka sheria, tena alizojitungia mwenyewe?.

  Ibara ya 27 (3 na 4 ) inamataka Waziri wa Ujenzi baada ya kufanya mawasiliano na Waziri wa Ardhi atahakiksha ananunua ardhi hiyo kutoka kwa wananchi hao. Je Mhe John Magufuli alifanya hivyo? Badala yake Mhe Magufuli alitumia ubabe na kuwatuma kwa lazima na vitisho vya kufukuzwa kazi wafanyakazi wa TANROAD kuvamia nyumba za wananchi na kuweka alama za X katika Mita 8 zilizoongezeka 2009, huku kulikuwa ni kukiuka sheria ya barabara.

  Ibara ya 27 (5) inatamka kuwa baada ya siku 60 tokea wananchi kulipwa fidia Wizara wa Ujenzi kupitia TANROAD atawataka wananchi husika kuhama au kutoendeleza chochote. Je wananchi ambao nyumba zao zilizowekewa alama za X wamewahi kuarifiwa chochote na Wizara ya Ardhi, sembuese kulipwa fidia? kwakuwa hawajawahi kuarifiwa chochote wala kulipwa fidia ya aina yoyote kwa hizo Mita 8 zilizoongezeka 2009, hawakutakiwa kubughudhiwa kwa lolote hadi hapo watakapokuwa wamelipwa fidia.

  Ibara ya 27 (6) inatamka kuwa baada ya wananchi kuarifiwa kuhusu ardhi hiyo kutwaliwa na Serikali watalipwa fidia. Kwa kuwa hakuna fidia zozote zilizolipwa ndio maan Waziri Mkuu Pinda na Raisi Kikwete wakamkaripia.

  Kwa hali hii ni lazima tukubaliane kuwa Mhe John Pombe Magufuli ni mbumbumbu wa sheria, aidha ameshindwa hata kutafsiri na kutekeleza sheria alizojitungua mwenyewe. Je atawezaje kutekeleza sheria zingine?


  HIZO KANUNI ZA SHERIA MOYA YA BARABARA ANAZOTAMBA NAZO MAGUFULI HIVI SASA ZILIZTUNGWA WAKATI KAWAMBWA AKIWA WAZIRI WA UJENZI ILA HAKUWA MTU WA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KUJITAFUTA UMAARUFU HATA KAMA NI WA KULAZA WATU NJE ISIVYO HALALI
   
 18. S

  Shkh Yahya Senior Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duuh! yaani yupo Jumanne ( Magembe), Mustapha ( Mkullo)!!? Lakini hayupo Steven ( Wasira), William ( Ngeleja) wala Ezekiel ( Maige- ambaye kamati ya Mashirika ya umma iligundua mengi kuhusu kodi za mahoteli kwenye sehemu za hifadhi...Tshs. 19 billion zimepotea serikalini kutokana na Waziri kukataa mapendekezo ya wataalamu)... Lakini ah!! kina Omari na Yahaya ndio wanaopwaya zaidi.

  Ila tutafika tu!!! Wacha niangalie nyota zangu hapa kibarazani.

  Shkh Yahya,
  Magomeni.
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160


  Ikiwa wakati wa Mkapa Magufuli aliweza kujenga barabara pasipo kuleta misuguano mikali na kati ya Serikali na wananchi kwa kuwa alishughulika sehemu inayojengwa barabara tu, hivyo hayakuwepo malalamiko kutoka kila pembe ya nchi kama ambavyo strataegy aliyotumia 2010/11. Aliponzwa na ndoto za 2015 hivyo kuwa tayari hata watu walale nje nchi nzima ili mradi ajijenge kisiasa. Kwa pupa hiyo akatafsiri Kanuni za barabara vibaya.

  Pinda na Jk walimlinda sana baada ya kutosema mbele ya wanachi kuwa alichemka kutafisiri kanuni zaSheria ya barabara vibaya Kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za barabara si wizara ya Ujenzi wala TANROAD wenye jukumu ya kuhifadhi ardhi ya barabara na hifadhi zake, ni Wizara ya Ardhi. Endapo wangelisema hilo wale wote wanaoamini kauli zake za kinywani wangeiashiwa na imani kabisa. What more did you wany Pinda na Jk to do. Walimlinda vya kutosha
  .

  In Green:- Nafahama Magufuli ametumia sana kete ya msongaman wa magari ili kuvamia watu walioko mIta 120 kutoka katika ya barabara ili kujipata sifa . Hii inatokana na watu kama ninyyi ambao hamtaki kujishughulisha kutafuta sheria na kuzisoma badala yake mnaamini maneno ya vinywani tuu.


  Upana wa Road Reserve halali ni Futi 75 au Mita 22.86tu. Ibara ya 27 (1) ya Kanuni mpya za Sheria ya barabara namba 13 ya 2007 inatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara zote kuu hapa nchini (Trunk Roads) utakuwa si chini ya Mita 3.25.Kwa maana hiyo Futi 75 au Mita 22.86 zinao uwezo wa kuzalisha njia za barabara (lanes) 14; njia (lanes) 7 zikielekea DSM na njia (lanes) za barabara 7 zikielekea Kibaha. Je eneo hilo kwa saa limeshatumika? Kma halijatumika ni kwanini Magufuli aliagiza nyumba zilizoko mita 120 kutoka katika kati ya barabara ziwekewe X na kubomolewa? Dont yu realise there is a problem ndio maan wakubwa wake wakaingilia kati.
   
 20. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Na hao wote uliowataja na aliotaja Ntemi K wameteuliwa na kilaza mkuu mwenyewe!!! Kaazi kweli kweli.
   
Loading...