Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20?

Na mawazo ya wanadamu ni mabaya siku zote.
Dah, nimegundua ngozi nyeusi sio maskini sababu hatuna akili, ila sababu ya roho mbaya.
Yani unataka namba ziongezeke na watu wafe ili iweje? Au kuna faida unapata?
Kama mataifa mengine namba inashuka na huduma zinarudi, kwanini Tanzania isishuke!?

Kama unaona raha, umwa wewe na familia yako. Period
 
Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje hapa kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20? Hivi kweli kupunguza hofu au kuupuuza huu ugonjwa na kukubali kuishi nao ndiko kumefanya wagonjwa wapone haraka na maambukizi yakome haraka?

Idadi alizotoa jana na PM kituo kwa kitu wagonjwa walobaki nchi nzima kama 20 hivi, kweli ndani ya wiki mbili wagonjwa wanaweza pungua kutoka 509 mpaka 20 kwa nature ya kirusi cha Corona??
Kama ni muujiza nakubaliana nao lakini kitaalamu hesabu inagoma.

Najiuliza viongozi wetu na wananchi wanapoona na kusikia vifo na cases kama Brazil, Marekani, Urusi kutaja kwa uchache wanahisi nchi hizi zimemkosea nini Mungu?

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.


Mkuu, inawezekana kwamba watu wengi tumeambukizwa huo ugonjwa na tumekuwa "Herd immuned" na hivyo tunaishi na virus bila kujua, hawa virus wana nguvu katika:

1----- Watu wenye kinga dhaifu dhidi ya virusi na kinga dhaifu ya miili kutokana na sababu mbalimbali.

2---- Katika mazingira ya ubaridi.

Katika hayo mazingira mawili Wazungu na nchi zingine wamo.

Njia rahisi na ya pekee kujua kiwango cha maambukizi ni kupima watu wote (mass testing).

Watu wengi tunaishi na Corona bila kujijua.
 
Chadema nao wako pamoja na WHO kwenye maombi ya kutaka tupukutike utafikiri wao wako sayari nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mtu anayeomba watu wapukutike. Hivi hao "watu" si sisi sisi watanzania. Hivi kwa mfano ugonjwa ukiingia Mtwara na mimi nipo Mtwara si inawezekana nikadhurika pia? Yaani tuombee watu wafe ili iweje. kwani hao wanaokufa sasa ni kwa sababu kuna mtu aliomba wafe kwa huo ugonjwa?

Kinachozungumzwa kingine na nyie mnazusha mambo yenu ya Propaganda. Ili mtu aseme mtu wake kafa kwa COVID 19 ni lazima Madaktari waseme, jee madaktari wetu wana uhuru huo? Hili jambo ni la kisayansi lakini linafanywa kisiasa sana.

Mimi nina rafiki yangu kaumwa sana wiki hii kwa dalili za mafua makali, kupumua kwa shida, kutapika, kukosa nguvu, homa kali pamoja na kukohoa, lakini alipokwenda Hospitali aliambiwa ugonjwa haujaonekana. Hivi mgonjwa wa hivyo kweli haumwi??
 
Hesabu zako ni mbovu kwani hazijikiti kwenye data bali zimejikita kwenye hisia tu. Marekani walianza na 1 mpaka sasa wana takriban laki moja za vifo, wakati Wuhani nayo walianza na 1 lakini sasa wana vifo zero. Kwa hiyo namba zilianzaje na zikaishaje siyo scientific reasoning bila kujua model halisi ya jamii yako.
Most of non- democratic coutries the covid 19 cases has sharply decreased with no known stratetgies. On the other wing for more democratic contries the number shows to increase daily! Im totally confused on such scenario.
 
Most of non- democratic coutries the covid 19 cases has sharply decreased with no known stratetgies. On the other wing for more democratic contries the number shows to increase daily! Im totally confused on such scenario.
Sijajua una maana gani kwa sababu German na Sweden ni nchi ambazo ni democratic sana lakini haziingii kwenyeconclusion yako.
 
Watu wengi wanapona vifo ni vichache sana
Unapotoa hoja . Uwe na data zinazo support hoja yako.
So far ni siasa tu.
Ili kuku prove wrong. Mpaka sasa s.afrika wana 21343 cases
Ikifuatiwa na egypt yenye 16513 cases
Cameroon wana 4597 cases
Algeria 8113 cases
Morocco 7429
Hizo ni nchi zenye mambukizi zaid afrika.
Lakin total number ya cases afrika nzima ni 108,463
Mpaka sasa.
So embu niambie huo ugonjwa wa mabeberu umefikaje kwa hizi nchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama mtu yupo positive na anajiweza akae hospitali kufanya nini? Na hapo hospitali kuna dawa? Ok nchi za wenzetu wanatangaza takwimu za wagonjwa mfano kenya, maambukizi yanapungua au yanaongezeka? Wameweka lockdown na carfew, wagonjwa wameongezeka au wamepungua? Takwimu zitasaidia nini?

Ugonjwa huu unaathiri saikolojia zaidi kuliko uhalisia, jamaa yangu alikutwa positive lakini haumwi chochote... Naye apelekwe hospitali? Hoja ni takwimu... Za nini hizo takwimu?
Taarifa nyingi za serikali zimejaa hadaa.
Ukweli ni kuwa Corona ipo na bado inatutafuna taratibu. Kwa kuwa ugonjwa huu utaendelea kuwepo muda mrefu zaidi duniani, na sisi ni sawa na watu wengine duniani, muda utatupa majibu mazuri zaidi. Taratibu tu tutaelewana.

Kwa kifupi sana hichi tunachotangaziwa sasa na serikali (kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona waliokuwa wamelazwa hospitalini imepungua) tulikuwa hatukihitaji sana kuambiwa na kile tulichokuwa tunakihitaji sana kuambiwa (idadi ya watu waliopimwa, wagonjwa wapya, mahali walipo, wagonjwa waliopona, waliokufa) hatuambiwi tena. Kifupi serikali imehamisha goli bila kubadili sheria za mchezo.

Nini haswa kimetokea na kinafanywa na serikali kwa sasa?

Kwa takribani wiki tatu sasa serikali imebadilisha mwelekeo wa mambo yake makuu matatu kuhusu ugonjwa wa Corona pasipo kuutangazia umma na dunia wazi wazi. Watendaji wakuu wa serikali na wahudumu wa afya wanajua vyema hayo. (Mambo hayo; Mosi, kwa sasa hakuna tena kuwalaza wagonjwa wa Corona hospitalini ikiwa wanaweza kujihudumia wenyewe nyumbani, Pili hakuna tena kutangaza wagonjwa wapya wa Corona na Tatu hakuna tena kutangaza kifo cha mgonjwa wa Corona).

Ushahidi rahisi sana kwa wale wasioamini ni huu hapa.

1. Toka awali serikali haikuwa na utaratibu wa kutangaza idadi ya wagonjwa wa Corona waliopo hospitalini (kwanini? Idadi ya wagonjwa huenda ilikuwa kubwa kuliko takwimu zilizotangazwa na serikali, kwa sababu ingejumuisha na washukiwa (wale wenye dalili lakini majibu ya vipimo vyao yalikuwa bado)). Hivyo kututangazia sasa kuwa idadi yao imepungua inatupa picha kubwa hilo jambo limeficha kitu ndani yake. Linatumika kama hadaa fulani.

2. Zoezi la kuwapunguza wagonjwa wa Corona vituoni lilianza kufanywa wakati huo huo serikali ilikuwa imesitisha upimaji wa Corona kupisha uchunguzi wa maabara ya taifa (Hapo awali kiutaalamu mgonjwa wa Corona alikuwa anaruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupimwa tena na kukutwa Negative). Hivyo huenda wagonjwa waliruhusiwa wakiwa bado Positive.

3. Mpaka leo hii serikali imegoma kabisa kutangaza idadi ya wagonjwa wa Corona waliopona (yaani waliopimwa tena na kukutwa Negative) lakini hapo hapo inakazana kutangaza idadi ya wagonjwa wachache waliobakia hospitalini. Kwa sababu wanaujua ukweli.

Corona bado ipo.
Tuendelee kuchukua tahadhali zote.
Tuwasikilize wataalamu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje hapa kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20? Hivi kweli kupunguza hofu au kuupuuza huu ugonjwa na kukubali kuishi nao ndiko kumefanya wagonjwa wapone haraka na maambukizi yakome haraka?

Idadi alizotoa jana na PM kituo kwa kitu wagonjwa walobaki nchi nzima kama 20 hivi, kweli ndani ya wiki mbili wagonjwa wanaweza pungua kutoka 509 mpaka 20 kwa nature ya kirusi cha Corona??
Kama ni muujiza nakubaliana nao lakini kitaalamu hesabu inagoma.

Najiuliza viongozi wetu na wananchi wanapoona na kusikia vifo na cases kama Brazil, Marekani, Urusi kutaja kwa uchache wanahisi nchi hizi zimemkosea nini Mungu?

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
Hata hesabu za WHO zimegoma maana walitegemea kufikia katikati ya mwezi wa nne maiti ziwe zimetapakaa Afrika. Halafu mbona wewe hujaugua na kufa? Mimi naishi karibu na makaburi na kola siku lazima nipite mahali hapo lakini sasa ni wiki ya tatu sioni watu wakizikwa. Sijajua wewe ulitaka iweje maana kitaalam covid-19 imekwishafika kwenye peek kwa hiyo imeanza kudrop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..halafu hapo katikati tukanyimwa 'daily briefing' kwa kweli hizo number sio za kweli
 
Back
Top Bottom