Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20?

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,991
2,000
Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje hapa kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20? Hivi kweli kupunguza hofu au kuupuuza huu ugonjwa na kukubali kuishi nao ndiko kumefanya wagonjwa wapone haraka na maambukizi yakome haraka?

Idadi alizotoa jana na PM kituo kwa kitu wagonjwa walobaki nchi nzima kama 20 hivi, kweli ndani ya wiki mbili wagonjwa wanaweza pungua kutoka 509 mpaka 20 kwa nature ya kirusi cha Corona??
Kama ni muujiza nakubaliana nao lakini kitaalamu hesabu inagoma.

Najiuliza viongozi wetu na wananchi wanapoona na kusikia vifo na cases kama Brazil, Marekani, Urusi kutaja kwa uchache wanahisi nchi hizi zimemkosea nini Mungu?

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
iamokay

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
968
1,000
U are right. Ni muujiza. Na hii ni kwasababu tuliamua kumtumainia Mungu pekee, rejea matendo ya uponyaji yaliyofanywa na Yesu, vipofu kuona, viziwi kusikia, wafu kufufuka yote hiyo ilikuwa ni miujiza ewe mwenye imani haba. Ni dakatari gani amewahi kufufua mfu?
Unataka dalili gani kuamini uwepo wa Mungu?
 
Wamundemu

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
648
500
Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje hapa kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20? Hivi kweli kupunguza hofu au kuupuuza huu ugonjwa na kukubali kuishi nao ndiko kumefanya wagonjwa wapone haraka na maambukizi yakome haraka?

Idadi alizotoa jana na PM kituo kwa kitu wagonjwa walobaki nchi nzima kama 20 hivi, kweli ndani ya wiki mbili wagonjwa wanaweza pungua kutoka 509 mpaka 20 kwa nature ya kirusi cha Corona??
Kama ni muujiza nakubaliana nao lakini kitaalamu hesabu inagoma.

Najiuliza viongozi wetu na wananchi wanapoona na kusikia vifo na cases kama Brazil, Marekani, Urusi kutaja kwa uchache wanahisi nchi hizi zimemkosea nini Mungu?

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
Sasa ndugu unataka watoe takwimu unazozitaka wewe. Kilichotangazwa ndiyo uhalisia wenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,349
2,000
Taarifa nyingi za serikali zimejaa hadaa.
Ukweli ni kuwa Corona ipo na bado inatutafuna taratibu. Kwa kuwa ugonjwa huu utaendelea kuwepo muda mrefu zaidi duniani, na sisi ni sawa na watu wengine duniani, muda utatupa majibu mazuri zaidi. Taratibu tu tutaelewana.

Kwa kifupi sana hichi tunachotangaziwa sasa na serikali (kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona waliokuwa wamelazwa hospitalini imepungua) tulikuwa hatukihitaji sana kuambiwa na kile tulichokuwa tunakihitaji sana kuambiwa (idadi ya watu waliopimwa, wagonjwa wapya, mahali walipo, wagonjwa waliopona, waliokufa) hatuambiwi tena. Kifupi serikali imehamisha goli bila kubadili sheria za mchezo.

Nini haswa kimetokea na kinafanywa na serikali kwa sasa?

Kwa takribani wiki tatu sasa serikali imebadilisha mwelekeo wa mambo yake makuu matatu kuhusu ugonjwa wa Corona pasipo kuutangazia umma na dunia wazi wazi. Watendaji wakuu wa serikali na wahudumu wa afya wanajua vyema hayo. (Mambo hayo; Mosi, kwa sasa hakuna tena kuwalaza wagonjwa wa Corona hospitalini ikiwa wanaweza kujihudumia wenyewe nyumbani, Pili hakuna tena kutangaza wagonjwa wapya wa Corona na Tatu hakuna tena kutangaza kifo cha mgonjwa wa Corona).

Ushahidi rahisi sana kwa wale wasioamini ni huu hapa.

1. Toka awali serikali haikuwa na utaratibu wa kutangaza idadi ya wagonjwa wa Corona waliopo hospitalini (kwanini? Idadi ya wagonjwa huenda ilikuwa kubwa kuliko takwimu zilizotangazwa na serikali, kwa sababu ingejumuisha na washukiwa (wale wenye dalili lakini majibu ya vipimo vyao yalikuwa bado)). Hivyo kututangazia sasa kuwa idadi yao imepungua inatupa picha kubwa hilo jambo limeficha kitu ndani yake. Linatumika kama hadaa fulani.

2. Zoezi la kuwapunguza wagonjwa wa Corona vituoni lilianza kufanywa wakati huo huo serikali ilikuwa imesitisha upimaji wa Corona kupisha uchunguzi wa maabara ya taifa (Hapo awali kiutaalamu mgonjwa wa Corona alikuwa anaruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupimwa tena na kukutwa Negative). Hivyo huenda wagonjwa waliruhusiwa wakiwa bado Positive.

3. Mpaka leo hii serikali imegoma kabisa kutangaza idadi ya wagonjwa wa Corona waliopona (yaani waliopimwa tena na kukutwa Negative) lakini hapo hapo inakazana kutangaza idadi ya wagonjwa wachache waliobakia hospitalini. Kwa sababu wanaujua ukweli.

Corona bado ipo.
Tuendelee kuchukua tahadhali zote.
Tuwasikilize wataalamu zaidi.
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
11,868
2,000
Africa haijaathiriwa na corona Mkuu huo ni ugonjwa wa mabeberu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unapotoa hoja . Uwe na data zinazo support hoja yako.
So far ni siasa tu.
Ili kuku prove wrong. Mpaka sasa s.afrika wana 21343 cases
Ikifuatiwa na egypt yenye 16513 cases
Cameroon wana 4597 cases
Algeria 8113 cases
Morocco 7429
Hizo ni nchi zenye mambukizi zaid afrika.
Lakin total number ya cases afrika nzima ni 108,463
Mpaka sasa.
So embu niambie huo ugonjwa wa mabeberu umefikaje kwa hizi nchi?
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,083
2,000
Kuna watu huwa ni kama wachawi wanapenda kusikia habari mbaya tu ili kuwapruvu mahasimu wao wrong. This time around God stands with Africans COVID-19 won't sweep us kama WHO na wapambe wao kama mleta sledi walivyotabiri.

"African God is not a lesser god" PLO Lumumba 2017

Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema nao wako pamoja na WHO kwenye maombi ya kutaka tupukutike utafikiri wao wako sayari nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,622
2,000
Pamoja na jitihada zote ikiwemo ya lockdown jirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda maambukizi ya Corona yanapanda iweje hapa kwetu yashuke kutoka 509 mpaka 20? Hivi kweli kupunguza hofu au kuupuuza huu ugonjwa na kukubali kuishi nao ndiko kumefanya wagonjwa wapone haraka na maambukizi yakome haraka?

Idadi alizotoa jana na PM kituo kwa kitu wagonjwa walobaki nchi nzima kama 20 hivi, kweli ndani ya wiki mbili wagonjwa wanaweza pungua kutoka 509 mpaka 20 kwa nature ya kirusi cha Corona??
Kama ni muujiza nakubaliana nao lakini kitaalamu hesabu inagoma.

Najiuliza viongozi wetu na wananchi wanapoona na kusikia vifo na cases kama Brazil, Marekani, Urusi kutaja kwa uchache wanahisi nchi hizi zimemkosea nini Mungu?

Mungu ibariki Tz, Mungu ibariki Afrika.
Hesabu zako ni mbovu kwani hazijikiti kwenye data bali zimejikita kwenye hisia tu. Marekani walianza na 1 mpaka sasa wana takriban laki moja za vifo, wakati Wuhani nayo walianza na 1 lakini sasa wana vifo zero. Kwa hiyo namba zilianzaje na zikaishaje siyo scientific reasoning bila kujua model halisi ya jamii yako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom