Kwa kadri ya reporter wangu, kadai hizi pamba za masikio sio nzuri, kwa kadri unavyozidi kutumia, unaousukumiza kiasi flani cha uchafu katika interior part of the ear. Sasa huu uchafu ukigusa part flani ya sikio kwa ndani(kiwambo-not sure) unasababisha maumivu makali ya kichwa, hata unywe pain killer au mseto, mamumivu hayo hayaishi na huwezi hata kulala. kwa ufupi uchafu wa sikio ukizidi, unajikusanya na unatoka wenyewe auto. So the use of earstick is highly restricted!
Habari ndo hiyo.
cotton buds ni adui wa masikio yangu kwa kweli, kila wakati nikijaribu huwa najiskia maumivu fulani hivi(sijui ni uoga ?)
lol,u dont know what u ar missing,muulize samito akuambie kwa nini anarembua ,macho!
Mhh uenda pana ukweli hapo! tunaomba wataalamu muchangie zaidi maana waifu anasumbuliwa na masikio yapata mwezi sasa, tushatumia aina kibao za dawa mpaka vitunguu swaumu, mafuta ya jogooo, cjui nini lakini bado yanauma, je tatizo laweza kuwa ni hizi earstick kweli? maana twazinunua sana home, na kama hizo ndo sababu je tutumie nini sasa? kumbuka hizi hutumika kuanzia kwa watoto wachanga kabisa.
Wataalamu fungukeni zaidi katika hili.
mmh! mi huwa nikionaga pamba za maskion, maskio yanaanza kuwasha najikuta nimechukua naanza kuzungusha taratiibu.. kama unavyojua ukijichokonoa lazima ulegeze macho hata uwe nani.. maana kuna raha flan hivi..! sasa kumbe ni its not advisable?!!
Hahaha mkuu sijachakachua ila hii ni habari zinazohusina maana zote zinahusu kuchokonoa sehemu ya uso (nasisitiza ya Uso ) yenye tundu na kitu kinachoweza kukusababishia madhara kama hizo pamba za masikio.Aag mkuu hapa umechakachua!!khaaaaa..
Sizinga uko sahihi. Mimi si daktari lakini yamemkuta mtu wangu aliyekuwa akipenda sana kuchokonoa maskio kwa hizo cotton buds. Sasa hivi ana hali ngumu, alipokwenda kwa dr alielezwa kama ulivyoeleza kwenye post yako kwamba hakuhitaji kutoa huo uchafu kwani hutoka wenyewe.
Mbaya zaidi, sikio moja ndilo lililokuwa gonjwa lakini sasa limeambukiza lingine. Amejaribu dawa zote za hosp kwa mabingwa Nairobi nk nk lakini wapi. Mwinshowe ameamua kutafuta mafuta ya kenge baada ya kuambiwa ni dawa. TUWE WAANGALIFU NA MASKIO.
Mwenye maelezo juu ya matumizi ya MAFUTA YA KENGE kama dawa ya masikio atujuze tafadhali.