Pamba za masikio ni mbaya.

Mhhhhhhhhhh! maisha haya tabu sana kila kitu kibaya tu. sasa tukae na masikio yenye asali ndania yake. maana huwa najisikiavibaya sana, unamkuta kaka mtanashati au dada mrembo haswaaa lakini masikio yake kwa ndani yamejaa huo uchafu mpaka kinyaa!Tutumie nini sasa wakuu, toeni ushauri. Tutumie nini mbadala wake.
 
mkuu pamba za masikioni si nzuri hata kidogo. mi kuna siku nilisoma article kwenye gazeti
wakaeleza kuwa sikioni kuna wax ambayo inatengenezwa na kuta za sikio. mtu atumiapo
pamba basi hiyo wax na unyevunyevu hukaushwa kabisa na pamba na kuacha sikio kavu
hivyo kuufanya uchafu kuwa na uwanja mkubwa wa kwenda moja kwa moja mpaka kwa ngoma
ya sikio na kulisababishia matatizo lukuki. wataalamu hawashauri kabisaaa kutumia pamba za
masikioni kuchokonolea sikio. take care
Wakuu kuna ndugu yangu aliwahi kuumwa sikio wk nzima yupo ndani,alikwenda hospitali akapewa dawa wapi! Mpaka kuna rafiki yake mmoja akamuelekeza kwa doctor mmoja mtaalamu wa kusafisha sehemu za ndani za masikio.anasema alitolewa uchafu aibu na kupona.huyu jamaa alikuwa na tabia ya kuchokonoa masikio hadi na vizibo vya pen! Yule doctor akamwambia aache hiyo tabia na kama anaweza awe anakwenda hospitali kusafisha masikio mara kwa mara.hivyo huduma ya usafi ndani ya masikio ipo ingawa sifahamu huyu jamaa alienda hospitali gani.nikimpata nitamuuliza kusaidia wengine acheni kujiwekea vimiminika kujitibu ni hatari.maumivu makali ya masikio sababu ya uchafu dawa yake ni usafi tu hospitali kule kuna vifaa maalum vya kutoa uchafu wote!
 
kama kuna anaefahamu sehemu wanazotoa huduma ya usafi masikioni anaweza kutuambia kusaidia wadau hapa.hospitali kubwa kama muhimbili nafikiri itakuwepo ingawa watz wengi hawaifahamu hii huduma
 
Back
Top Bottom