Hii Picha imenitoa Machozi
nauhakika katika mechi hii nilikuwa ndani ya nyumba, jukwaa kuu.
kuanzia kuchoto kwenda kulia waliosimama
Madata Lubugisa
Rajabu Musoma
Beya Simba
Nteze John
Kitwana Suleiman
Fumo Felician
Nimemsahau (naomba nikumbushwe)
Paul Rwechungura
Waliokaa kuanzia kushoto
George Gole
Khalfani Ngasa
Ali Bushiri
Nimemsahau (Naomba nikumbushwe)
Mao Mkami
Salehe Mohamed
Nimemsahau (Naomba Nikumbushwe)
Niko Bambaga.
Tupo hata kama kwa sasa tupo nje ya Mwanza. Daima mji wa Mwanza utabaki kuwa kitovu chetu. Nasubiri watu tujitokeze tubadilishane mawazo humu...saa nne ishatimia.Wananzengo mpooo?
Mkakati wa kwanza na wa pili ndio lengo kuu. Timu irudi ligi kuu, lakini si tu kurudi ligi kuu bali ilete ushindani. Siamini kama tunataka kuishia kutaja tu majina ya nyota wa zamani.Mkakati wa kwanza mnaonaje watu wakatengeneza kama kikundi cha kuhamasisha ili kuchangisha pesa kwa wadau wa mkoa ili kufanikisha options 2. Mosi timu kuiwezesha kupanda daraja kwa hali na mali. Optin 2 kama ya kwanza ikishndikana ni kutumia njia niliyosema hapo jana. Njia hiyo ni kununua mojawapo ya timu ya jeshi ambazo kuanzia mwakani inatakiwa ibaki moja.
Wataalamu wa mambo ya soccer mtusaidieOk,
Mimi sitaweza kuwepo kwenye mazungumzo haya, mawazo hayo mazuri maana ndio options pekee zilizopo. Lakini, cha muhimu zaidi mnataka uongozi gani na mfumo upi wa viongozi kuwa accountable na sio wafujaji? Je mikakati gani iwepo ili timu iwe na self generating income?
Juweni kwamba hata kama pesa inawekezwa, kuna kikwazo kikubwa cha Simba na Yanga. Azam wamewekeza sana lakini sababu ya U-Simba na Yanga, pesa yake ni kama inapotea, ingawa Azam ni kama chombo cha marketing kwa mwenye kampuni. Pamba walikuwa na backup nzuri kutoka bodi ya Pamba....apart ya kuwalipa mishahara wachezaji, pia kuna wachezaji wengine walikuwa na ajira Bodi ya Pamba penyewe e,g madereva etc.
Kwahiyo basi, hata kama Timu inapanda within 1 or 2 seasons au kununua timu ya Jeshi, swali muhimu....kuna misingi gani ya kusaidia longterm stability/continuity? Hii misingi ikiwekwa, hata wafadhili/makampuni yatakuja. Pamba was only successful because there was financial stability. Lakini pamoja na yote hayo hawakuwahi kushinda Ligi Kuu? Why? Kashikashi alizopitia Pamba ndio anapitia Azam!!
Tufikiri hayo mambo ndio hatua zichukuliwe!
Wataalamu wa mambo ya soccer mtusaidie