Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 25,149
- 27,294
Wakati Rais wa Kenya akisaini muswada wa kutoa mamlaka kwa serikali kumshikilia mtuhumiwa wa ugaidi kwa kipindi kirefu hadi siku 360 na kuadhibu chombo cha habari kitakachotoa habari za uchochezi, huko Pakistan serikali ilirudisha chap chap adhabu ya kifo baada ya magaidi wenye msimamo mkali wa kidini kuwaua watoto wa shule kwa madai kwamba wanafundishwa Elimu ya Magharibi!!! Kama vile inavyoonekana kurudishwa kwa adhabu ya kifo kulihusiana na mauaji ya wanafunzi hao, serikali iliwakamata magaidi wawili na kuwanyonga mpaka kufa. Pia Pakistan iliendesha msako mkali na kuwaua magaidi wengine 77.
My take: Magaidi watakimbilia wapi iwapo nchi zilizokuwa zinawalealea zimeanza kuwaua!
cc: FaizaFoxy, kahtaan
My take: Magaidi watakimbilia wapi iwapo nchi zilizokuwa zinawalealea zimeanza kuwaua!
cc: FaizaFoxy, kahtaan