Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,159
- 93,075
Na, Robert Heriel.
(upepo unavuma nje ya ukumbi na kelele kutoka chumba cha giza zinasikika)
"Nilikaa porini miaka ishirini na nane kukuwinda wewe paka. kipindi nakuwinda Wapo waliokuwa wakinitukana na pia hata wale uwaonao katika nyumba hii hawakuhangaika Kama nilivyofanya Mimi. kazi yao walikuwa wakilewa. Leo hii anatokea mwendawazimu mmoja ananishikia mshale. heeeheee! pumbavu!!"
sauti ya mtu aliyeonekana kughadhibika iliendelea kubwata bwata. mvumo wa sauti ya upepo sasa ulikoma. sauti pekee iliyokuwa ikisikika na ya yule mtu ambaye bado sikumtambua kwani alikuwa ndani ya chumba cha Giza.
Waandishi wa habari na makachero walikuwa wamewasili kuchukua habari ambazo waliamini kuwa zinaweza kuuza kwa siku ya kesho. msongamano wa Waandishi katika ukumbi ule ulifanya hewa kuwa nzito na Kama mtu angesema ateme mate chini basi asingepata pa kutemea.
"mwindaji! mwindaji! mwindaji! mwindaji wa paka"
sauti zilitoka vinywani mwa waandishi Mara baada ya kumwona aliyekuwa anaongea katika chumba cha Giza. hapo ndipo nilipojua jina lake.
nilijisemea kimoyo moyo "ahaa kumbe huyu ndiye mwindaji"
sasa roho ya udadisi ilinipiga kikumbo nikajikuta naangukia katikati ya watu kutaka kumwona Mwindaji.
mwindaji alikuwa anatoka jasho haswa. uso wake ulionyesha kila dalili ya ghadhabu. midomo yake ilikuwa ikitetemeka Kama mkia wa kondoo dume. Ni dhahiri alikuwa amekasirika.
"sema sema! sema tuu mwindaji"
sauti zilitoka huku na huko kumshinikiza Mwindaji aseme.
Ilinibidi niulize kuna nini kwa aliyekuwa jirani yangu ambaye muda wote alikuwa akirusha mikono huku akiisindikiza na maneno "sema Sema! sema mwindaji.
mazungumzo yalikuwa hivi;-
Robert: kuna nini hapa lakini?
Jirani: (akiwa hajanisikia) Sema! Sema!
Robert: Aseme nini?(Nikimshika bega naye anageuka kunitazama)
Jirani: Kuhusu Paka aliyemwinda kushindwa kumla Panya.
Jirani wa 2: (Anadakia) tena panya buku.
Jirani: kweli, nimekumbuka ni panya buku.
Robert: huyo Paka alimtolea wapi?
Jirani wa 2: Msituni, msitu wa kijani.
Robert: Msitu wa kijani?
Jirani wa 2: Alikuwa paka Shume katika msitu huo.
Jirani: Shume kidogo. Hakuwa paka wa nyumbani.
Robert: Sasa ilikuwaje mwindaji akamleta nyumbani?( Kelele zinaendelea kusikia "Sema sema sema!)
Jirani: Tulimuambia Mwindaji lakini hakutusikia.
Jirani wa 2: Alisema paka wa msituni ndiye atakaye wala panya vizuri.
Jirani: Tena akasema panya watakimbia wenyewe.
Robert: Je huyo paka alimkamataje huko msituni?
Jirani wa 2🙁akinong'ona) Nilisikia alitunia bao la mkono.
Jirani: Tena bao lile alilichongea kule kule msituni.
Robert: Ikawaje sasa?
(Sauti zinatulia kidogo na sauti kutoka katika kipaza sauti inasikika).
"Tawanyikeni! tawanyikeni! kwa usalama wenu tawanyikeni"
Sauti hiyo inafanya watu wanazomea na jirani zangu wanatukana matusi makubwa.
Jirani wa 2: tukimbieni naona siafu wanakuja, wasijekutuuma.
Naangalia chini kuona Kama kuna siafu huku nikisukumwa na watu ambao walikuwa wakikimbia.
nilipigwa kikumbo na kupepesuka mfano wa mlevi. nilishangaa kuona Askari wakija kule tulipo. na mwindaji alikuwa tayari kapanda kwenye Gari nzuri.
akilini nikajua huenda hawa ndio Siafu.
Nilikimbia kuelekea nyumbani. Nikiwa njiani nilisikia sauti iliyochoka ikiniita.
"wee Kijana"
niliipuuzia hata hivyo lakini kadiri nilivyokuwa nikitembea ndivyo ilivyozidi kuita.
Nilisimama nakugeuka nyuma. Nilimuona mzee mwenye mkongojo na barakashee kichwani. Mzee alikuwa amevaa Shati kuu kuu lililochorwa mtu fulani na maandishi yaliyoonekana kupotea kwa uchakavu wa shati.
Alinikaribia nikamsalimia huku nikisoma yale maneno katika shati lake.
" KAZI NI UTU"
Nilishangaa kuona maneno yale katika shati la babu.
Nikamuuliza; Kazi ni utu?
akanijibu huku akijitazama katika tisheti take yalipo Yale maandishi.
"Ndio kazi ni utu Kijana"
tulianza kuzungumza kwa kirefu huku tukiwa tumekaa kando ya barabarani mbu wa jioni wakiwa juu ya vichwa vyetu.
"Umetoka wapi kijana"
Babu aliniuliza.
"kule ukumbini Babu!"
nikinyosha kidole kuelekea upande ukumbi ulipo.
kimya kidogo.
"Babu unamjua Paka Shume?"
Niliuliza.
"Shiiiiii!! usiongee tena hivyo"
Babu alionyesha wasiwasi akitazama huko na huko hali iliyonifanya niogope.
Babu akaanza kusema;
Paka shume! paka wa porini, paka wa Msituni. Paka asiye na huruma. Aliyeletwa nyumbani na mwindaji, Mwindaji wa Panya. Si wale panya road, au Panya vijiweni watoto wa masikini bali panya buku walioihujumu nyumba, nyumba yenye makabila zaidi ya 120.(Babu anaacha kusimulia kisha anafukuza mbu). Kuna mbu kweli hapa.
Hawa mbu ni kutoka msitu ule(ananyooshea kidole). Mbu wanyonyao damu za wanyonge. Nao Panya buku watuuzia madawa na Chandarua hata malaria ituue"
"Huyo paka yupo wapi sasa?"
Niliuliza tena na Mimi nikipigana na mbu wa jioni.
Babu akaendelea;
Sio paka Sema Paka shume. Mwindaji alienda porini kumuwinda Hilo jipaka Shume. ilikuwa tabu kulikamata kutokana na makucha lililokuwa nayo. ilimchukua miaka 28 Mwindaji kumkamata Paka shume"
(Ananyanyuka na kuanza kulia)
lakini paka shume badala ya kuwinda panya buku. panya waliotulia mahindi yetu, chakula chetu, Nguo zetu, mbegu zetu, na vyeti ya watoto wetu hata wasiajiriwe.(Anaongeza kilio)"
"Mzee nyamaza basi uendelee na hadithi"
nilimuambia.
Babu alipenga kamasi akachukua ugoro na kuuweka puani. Mara akapiga chafyaa!
Babu akaendelea;
Paka shume akaanza kula vifaranga vya kuku na bata. basi akaona haitoshi akaanza kula na kuku wenyewe. ikawa Majogoo walipotaka kuwatetea kuku wengine akawapiga kwa kucha zake. paka!! paka Paka shume!(Mzee anaonekana Kama amevurugwa). Twende! twende tukamuue Paka shume"
Aliongea akinivuta pale chini yeye akiwa kasimama.
"Subiri basi Babu, endelea kwanza huoni huu usiku?"
Nilimponyoa mkono wake kwangu.
"Usiku ndio hupenda kula mayai, unajua paka shume kamparua mpaka yule mwindaji aliyemkamata?"
Babu aliniuliza.
"Mwindaji yupi?"
Nikauliza.
"huko ukumbini hukumwona?"
"ahaa ndio yule!!"
Nilishangaa na akili yangu ikaanza kuunganisha doti.
"Basi yule mwindaji ndiye aliyemkamata paka shume porini"
babu kabla ya kumaliza kuongea Mara Akakatisha hadithi na kusema kimbia siafu hao wanakuja.
Nilikimbia mpaka nyumbani.
paka shume nakuasa acha yako Tabia. Nasikia umeficha panya buku. katika dari yako. aliyekuwinda asema alikuwinda ule panya.
iweje panya buku kumhifadhi?
Makucha yako tayachoma, na meno yako kuyang'oa. sharubu tutazishika na mkia wako tutauchezea.
paka Shume jirekebishe naona hata waliokuwinda wakuogopa. umegeuka zimwi lisilomjua muwindaji.
[HASHTAG]#TaikonWaFasihi[/HASHTAG].
Niite Mfalme wa Fasihi.