Pajue Iringa kwa kupitia picha



Pichani ni muuza mapanga maarufu mjini iringa

Umaarufu wa muuza mapanga huyu umechangiwa na mambo yafuatayo

1) sura yake
Sura ya bwana hii haifanani kabisa na biashara anayofanya ,, wengi kwa kumuona tu wamekuwa wakihisi bwana huyu kuwa jambazi tokana na muonekano wake lakin yeye akaamua kuuza mapanga ,,je unafikiri mteja anaweza kuwa na ujasiri hata wa kumsogelea na kuulizia bei ???

2) sauti yake
Muonekano wa bwana huyu moja kwa moja hupelekea watu kuhisi bwana huyu atakuwa na sauti nzito ya mwanaume .. wengi wanahisi huenda akawa na sauti kama ya jaiva au chidi benzi wa enzi zile ..lakini huwezi amini huyu bwana anasauti nyembamba kiasi kwamba ikiongea watu humuangalia mara mbili kuhakikisha kama kweli ni yeye ndiyo kaongea ..

3) style yake ya kufanya biashara

Bwana huyu ukienda kununua panga hataki uchague panga ,, yeye atakalo kupa ndiyo hilo hilo uchukue ukichagua tu anakurudishia pesa yako na kuondoka na mapanga yake ..

4) popote atakapoenda kuuza mapanga yeye ni ya mguu tu ,, hajawai panda gari na kuna wakati unaweza kumkuta kapanga mapanga yake sehemu ambayo hamna hata wateja wanaopita

5) hilo koti alilovaa hapo kubadilisha mpanga lichakae ndiyo anaenda kuvaa jingine ,, likini kubwa zaidi watu mpaka sasa hawajiu ni wapi anapata makoti ya style hiyo

6) wengine uhisi labda bwana huyu ni mpelelezi
Labda anapeleleza sehemu wanazouza bangi au madawa na kuwachoma wahusika
 
Huyu mwamba Bado yupo
 
Toka nipo mdogo anafanya hiyo biashara ,now Nina miaka 30+.

Nimeondoka iringa 10yrs ago
🤣🤣🤣🤣🤣 Zamani tukiwa wadogo tukimuona tulikuwa tunakimbia ,, afu jamaa kama hazeeki hivi ujue
 

Mambo ya Gangilonga na Uhindini...na FFU, kwa Askofu Ngalekomtwa. Highlands Secondary School karibu na Lugalo.

Mziki tunacheza Railway Hotel, na wahasibu wa Iringa Girls....maisha yetu chini ya jua yanapita kwa kasi sana
 
Umesahau semtema
 
Aisee Iringer!
 
Kwa kweli sina uhakika kama hapa ni Iringa kwa sababu sioni Wahehe wakining'inia kwenye vitanzi kujiua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…