Paji la uso na siri ya jicho la tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by mshana jr, Jun 24, 2016.

 1. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hutaamini utakachogundua hapa kuhusu paji lako la uso...hapa ndio asili ya neno kipaji ilipatikana..hapa napo ni lango hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani jicho lisioonekana.lango kuu la kiroho.

  Tutaenda kwa mitazamo yote ya kidini na kiimani, kisayansi, kihisia na hata kwenye nguvu za giza.

  1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus[​IMG]

  Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.

  2. Mathematics[​IMG]

  Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.

  3. Tahjud (Meditation)
  [​IMG]

  Kwenye tahajudi wale waliosoma chakra na habari za milango nane, ukiangalia vizuri huo mchoro chakra ya sita ndio ya kuingilia mlango wa sita wa fahamu.

  4. Baptism & Sijda[​IMG][​IMG]

  Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..

  Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.

  5. A kiss on the Forehead
  [​IMG]

  Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.

  6. FREEMASONRY
  [​IMG]
  Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu

  7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)[​IMG]

  Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.

  8. Michezoni:
  Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.

  Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.

  Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.

  Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.

  Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.
   
 2. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2016
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,195
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Interesting....
   
 3. LUBEDE

  LUBEDE JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2016
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 2,876
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  nimewaza sana sana,nimekumbuka vingi kupitia hili paji la uso linavyotumika mara nyingi lakini kwa matukio flani muhimu na umakini bila wenyewe kujua,asante kwa elimu mkuu mshana jr.
   
 4. wasumu

  wasumu JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2016
  Joined: Oct 28, 2015
  Messages: 1,913
  Likes Received: 1,527
  Trophy Points: 280
  eeeh mshana ktk ubora
   
 5. wasumu

  wasumu JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2016
  Joined: Oct 28, 2015
  Messages: 1,913
  Likes Received: 1,527
  Trophy Points: 280
  mshana mediation inakuwaje how to mediate
   
 6. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
   
 7. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
 8. The Great Emanuel

  The Great Emanuel JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2016
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 1,378
  Likes Received: 1,727
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2016
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu nimeanza kukielewa hapo hasa nilivyosoma hicho kitabu cha KUTOKA 13:16 kwenye Biblia.

  Ngoja tuanze sasa kufukunyua nondo za huu uzi taratibu.

  Ipi ni athari ya kulala chali, na kwa nini watawala wengi wa zamani walikuwa hawalali kifudi fudi??

  Ukiangaliakumbu kumbu za mafarao wa misri walikuwa wanawekewa kabisa mto wa kulaliaambao ulikuwa hauwaruhusu kugeuza vichwa wakati wa kulala, na wote walikuwa wanalala chali.

  Kuna siri gani hapa.??
   
 10. QUIGLEY

  QUIGLEY JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2016
  Joined: May 23, 2015
  Messages: 23,910
  Likes Received: 71,419
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeipenda hii
   
 11. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
  Hata maiti halazwi kifudifudi
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2016
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,225
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Nahisi ulimaanisha MEDITATE, na sio MEDIATE. Ku MEDIATE ni kusuluhisha. Ku MEDITATE ni tahajudi
   
 13. souljah meditater

  souljah meditater JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2016
  Joined: Oct 15, 2012
  Messages: 2,045
  Likes Received: 1,842
  Trophy Points: 280
  ni fact zilizoshiba mkuu asante kwa kushare elimu hii
   
 14. ISIS

  ISIS JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2016
  Joined: Apr 20, 2016
  Messages: 57,207
  Likes Received: 358,859
  Trophy Points: 280
  NYUMBANI! asante sana.. Muhubiri 25: 2 Ni utukufu wa MUNGU kuficha jambo, bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo!
  Ubaikiwe sana..
   
 15. TRUE TANZANIAN

  TRUE TANZANIAN JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2016
  Joined: Jan 28, 2015
  Messages: 432
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 80
  Big up Mshana Jr! Nakusoma vyema brother!
   
 16. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
  Naamini tuna wanafunzi wengi wa Buddhism humu ndani hasa kwenye kipengele cha spiritual awakening.

  [​IMG]

  Unaposoma hiyo topic na ukaja kulinganisha na huu mchoro unapata mtiririko wenye kuleta uhalisia wa ajabu kabisa.

  [​IMG]

  Lakini pia kuna baadhi ya mimea hutumika kiimani kama stimuli/stimulas ya jicho la kiroho... Ni kama shortcut ya meditation au ya kuingia mlango wa sita kupitia moshi.

  [​IMG]

  Ndio maana mijadala haiishi kuhusiana na mmea... Shida moja ya mmea ni kwamba huamsha pande mojawapo kati ya zile mbili za mawasiliano ya kiroho ndani ya nafsi upande wa hasi na upande wa chanya... Inategemea kichocheo kipi kitawahi.

  Kuna hii kitu mtu akifanya mambo yasiyoeleweka anaambiwa ni madhara ya bhangi za kuvutia chooni, ni kama mzaha vile lakini chooni panajulika kama mlango wa kuzimu na makazi ya roho wachafu...

  Sasa bhangi inaamsha mlango wa sita kupitia jicho la tatu halafu unalivutia chooni, hapa unachanganya hasi na chanya. Matokeo yake lazima kichwa kipate moto.
   
 17. Tobinho

  Tobinho JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2016
  Joined: Nov 28, 2014
  Messages: 1,250
  Likes Received: 907
  Trophy Points: 280
  I liked it jinsi nilivyokuwa na meditate baada ya kula ganja,it was such an awesome moment. nilikuwa naweza kuyapanga na kuyapangua mambo yangu na yakaenda fresh kabisa...badae ikawa Kila nikivuta najuta sanaaa,yani hata kosa la mwaka 2000 nalikumbuka looote af najuta sanaaa, basi nkaiacha. Ila ntairudia after 4 years if God wishes.

  Nakufuatilia mkuu @ mshana jr.
   
 18. Michael Chairman

  Michael Chairman JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2016
  Joined: Apr 11, 2015
  Messages: 891
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 180
  Kuna jamaa kitaani akivuta bangi anasema anawasiliana na akina Obama , bush , putin n.k hiyo inakuwa kweli?
   
 19. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
  imebidi nicheke kwa kujibana hapa nilipo unajua ile kitu inaamsha hisia za mlango wa sita kupitia hilo jicho la tatu
  Lakini katika mlango ule wa hisia alishajenga mawazo ya kuonana na hao watu kwahiyo kinachotokea ni kama tu mlango wa hisia kubeba ujumbe na kuupeleka kama ulivyo kwenye mlango wa sita
   
 20. mshana jr

  mshana jr JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2016
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 81,558
  Likes Received: 81,805
  Trophy Points: 280
  Minds tricks and inner creation in two phases
  First phase all things related to positive states
  Second phase all things related to negative state
  Sometimes they work simultaneously and sometimes they work periodically
   
Loading...