GE2025 Padri Kitima: Bunge lililopita lilikuwa la chama kimoja, wapiga kura wa vyama vya upinzani hawakutendewa haki

GE2025 Padri Kitima: Bunge lililopita lilikuwa la chama kimoja, wapiga kura wa vyama vya upinzani hawakutendewa haki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
440
Reaction score
3,211
Lilikuwa Bunge (2020-2025) la aina yake katika historia ya Tanzania tangu tuanze mfumo wa vyama vingi wa mwaka 1995. Katika kuwa na wabunge waliochaguliwa, mwaka 1995 tulianza na wabunge wa upinzani 23, 2000 wakawa 26, 2005 wakawa 41, 2010 wakawa 84, 2015 wakawa 112 wa upinzani, mwaka 2020 wakawa wabunge 8, Tanzania Bara wakiwa 2 wa upinzani waliochaguliwa.

Halikuwa bunge lenye uwakilishi wa kutosha uliochaguliwa na wananchi wenyewe kwa kupiga kura zao kutoka vyama vya upinzani.

Chama cha Mapinduzi kilichoongoza kwa kura ndicho kilikuwa na wabunge wengi na sababu za historia ya nchi yetu, Bunge lilikuwa la chama kimoja na chama kimoja lazima kilishika dola.

Wale wapiga kura wa vyama vya upinzani hawakutendewa haki ya kutosha, wagombea wengi walienguliwa, mawakala wengi walienguliwa hivyo kuweka dosari kubwa kwa uchaguzi wa 2020.


Katibu Mkuu wa TEC
Padri Dkt. Charles Kitima
August 4, 2025-DW
 
Back
Top Bottom