kwani nani kasema aliyeua ni muislamu? na hata kama ni muislamu unajuaje kama ameua kutokana na visa vya kidini? mimi binafsi sitaki kuamini hivyo labda kama vyombo vya usalama vitupe ukweli lakini sio vyema kuhukumu moja kwa moja kuwa walioua ni waislamu ndugu zanguni.
Ivi unajua kuwa huyu shekhe Ilunga ni mpinzani ndani ya uislam. Haya madhehebu ya kisasa ni balaa tupu.
Acha uhuni wewe!.. Nani kamuua padri kama si waislamu?!!!!... Serikali tumeipigia kelele tangu CD za mipango ya mauaji ilipotoka septemba mwaka jana mpaka sasa hawajali na waandaaji wa CD za kuhamasisha waislamu kuua wakristo zinaendelea kuzagaa mitaani. Wewe unaswali wapi?!!!!
Naona wewe ni mkristo na umeumia sana!
Just cool down, for sure, mimi nimeumia sana lakini lazima tujue dini yetu inasemaje? Mwombee hata adui!
Wakristo wanaouawa ndio hao Watakatifu, tutende kazi zetu kama kawaida bila kuogopa, maana hata Yesu mwenyewe aliuawa bila sababu maalum katika nchi hizo hizo za kiisalam,
na wakati huu ambao dhambi zinajirudia ni muda wa kuomba sana! Mwisho umekaribia na watajibu kwa huyo huyo Kristo!
Kama nasi tutakuwa na ghadhabu tuna tofauti gani nao??
Lets Pray more and more when difficult times come!
Be blessed!.. Dini yetu hiruhusu visasi!.. ILA UKIMYA WA SERIKALI UMEWACHOSHA WAKRISTO!... Waliomo mtaani ni wengi kuliko waliomo kanisani na mafundisho haya hawayajui!...
Sikuzote Mkuki kwa Nguruwe kwa Binadam Mchungu Jamaa hivi unaushahidi kuwa Waislam ndo Wamehusika ?
Je mbona walipouliwa Waislam Mwembe Chai mlikaa kimya?
Je mbona Sheikh alipomwagiwa tindikali mlikaa kimya?
Acheni kupotosha maana waache Police wafanye Uchunguzi ukweli utabainika
umemsahau na Mohamedi Mtoi MANI na wapo wengi tu wengine humu.Mambo mengi mabaya na ya kishetani yatatekelezwa kwa jina la uislam, ajenda nyingi zitajivalisha umbo na sura ya uisilam, lakini havitanishawishi eti nimchukie AshaDii
Nchimbi ni bogus
What is he saying?
ukitafakari sana utagundua kuwa kwa sasa ZAnzibar sio sehemu salama sana ya kuishi hususani kwa Wakristo.
Maggid siku nyingi tunalalamika serkali kutomchukulia hatua Unstaadh illunga aliyezunguka nchi nzima pamoja na Zainzibar akihamasisha waislamu wasibweteke bali watafute namna nzuuuuuuuuri wawashughulike viongozi wa kikristo kama njia ya kupambana na mfumo Kristo. Hivyo hakuna sababu ya kujiuliza kwa nini sasa!!One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either! - Padri hauawi, hata Sheikh pia... Ndugu zangu, Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo. Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh. Kwa nini sasa? Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni. Maggid Mjengwa, Iringa.