Padri Hauawi, Hata Sheikh Pia...!

Padri Hauawi, Hata Sheikh Pia...!

mabingwa wa 'intelijensia ya polisi' wanashughulikia waliom'sms' makinda. Ofkoz wengine wapo mtwara kusaidia wataalam gesi kutinga dar. Hawana muda na intelijensia ya kuzuia uhalifu. What're early warning systems, security and peace
inasikitisha mno.
 
Alikuwa anajaribu
kuonyesha kuwa mauaji ya Fr Mushi yana uhusiano na tukio la Sheikh
kumwagiwa tindikali

Na hili ndio tatizo la viongozi wetu. ni wanafiq na vipofu. Je haikusemwa wazi kuwa tukio la kumwagiwa shekh tindikali lina uhusiano na waislam wenyewe kupingana?
 
Alikuwa anajaribu kuonyesha kuwa mauaji ya Fr Mushi yana uhusiano na tukio la Sheikh kumwagiwa tindikali

Huyu mtu ana ujasiri wa kipekee! Anaongelea tukio la Sheikh kumwagiwa tikindikali wakati hajafanya chochote kukamata wahusika? Incredible!
 
wewe acha siasa za kidini kwani hili sio udini tuu, kuna mtu/watu nyuma ya pazia (maarufu kwa jina la spin masters) wanaoagiza mambo kama haya yafanyike, mbona vatican iliidhini mashambulio ya dikteta musollini dhiidi ya ethiopia miaka ile? ukristo au uislamu ni kisingizio tu, kuna mtu kibao kanisani na msikitini wanafuata mkondo angalau wapate chao. mi ni mkristo lakini nina marafiki weng wa karibu wa dini tofauti alafu tunaheshimiana swafi kabsaa bila kudharau imani ya mwenzie. again i say this is the result of outside influences bringing chaos to my homeland.
 
Watanzania mjilaumu wenyewe kwa matukio mabaya yanayoendelea nchini kwa sasa!! Serikali ya ccm haikuingia mstuni na kutwaa madaraka bali mliipa kura kwa ushabiki wenu wenyewe!!! Hiyo ndiyo kasi mpya... na ndiyo madhara ya kupiga kura kama vipofu!!
 
si waisilamu ni genge la wahuni wanaotumia dini kufanya mabaya.'hakuna dini inayohlalisha kuua. hawa wahuni wadhibiyiwe inatutia aibu amani inatoweka jamani. serikali iko wapi?
Unasemaje?, Hakuna dini inayohalalisha kuua?, kama hujui ni bora kuuchuna.
 
.....je tunahitaji ishara gani zaidi ya hizi ili kujua kuwa baba Mwanaasha nchi imemshinda kuongoza?
 
ishu ya kuwa waislam ndio waliohusika na mauaji ni fikra potofu,tusuburi jeshi la polisi wafanye kazi yao walete majibu.inaweka pia kua kauawaw na wakristo wenzie

Tukio hili linaweza likawa limefanywa na watu wenye chuki dhidi ya serikali ili kukoleza mgogoro wa kidini unaonekana kukua kwa kasi. Japo uhalifu kama huo Zanzibar hutokea sana
 
nimesikiliza mafundisho ya shehe ILUNGA,SIO TU NIMEICHUKIA DINI YAKE BALI NIMEIOGOPA SANA KULIKO NILIVYOKUWA NAIJUA,in fact kumbe niliyaelewa mambo haya ya dini kiuwepesi
 
Hofu Ya Vurugu Za Udini Na Kisa Cha Mtego Wa Panya!
Ndugu zangu,

Mengine tuandikayo tulishayaandika zamani. Tunayarudia maana yanayotokea sasa ishara zake tulishaziona, isipokuwa, tu mahodari sana wa kupuuzia.

Nimepata kuandika ( Raia Mwema) juu ya nilichokiona Jumapili moja nilipokuwa nikipita mitaa ya Kariakoo. Pale kona ya Mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe nikamkuta kijana na mkokoteni wake. Alikuwa akiuza filamu na CD za kidini.
Kijana yule alikuwa akionyesha pia mkanda wa video. Mzungumzaji kwenye mkanda huo alikuwa akihubiri chuki. Ni kuanzia nilipoanza kumsikiliza hadi nilipoondoka mahali hapo.

Na watu, hususan vijana, waliuzunguka mkokoteni ule kusikiliza chuki ile ya kidini iliyokuwa ikipandikizwa. Ndipo tulipofikia. Kwamba mijini si tu kuna wanaouza sumu za panya na mende. Bali siku hizi kuna wanaosambaza bure, ’sumu za kijamii.’

Vyombo vinavyohusika vimebaki vikiwaangalia wenye kupandikiza mbegu hizi za chuki.Kosa kubwa tulifanyalo, ni kudhani yanayotokea Kariakoo au Unguja hayatuhusu wa Kinondoni, Iringa au Mwanza.

Nimepata kusimulia kisa cha mtego wa panya uliosababisha madhara hata kwa wasio panya.

Panya kwenye nyumba aliubaini mtego wa panya uliowekwa na mwenye nyumba uvunguni mwa kitanda. Panya yule akamwendea jogoo wa mwenye nyumba. Akamwambia: “Ewe jogoo, kuna mtego umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane namna ya kuutegua kabla haujatudhuru wote."

Jogoo akajibu: "Ondoka zako, mie mtego wa panya unanihusu nini wakati sina kawaida ya kufika uvunguni mwa kitanda?" Panya yule akaenda hadi kwa mbuzi wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe mbuzi mwema, unajua kuna mtego wa panya uvunguni mwa kitanda cha mwenye nyumba. Tusaidiane mawazo ya kuutegua kabla haujatudhuru sote."

Mbuzi akajibu: "Hivi tangu lini ukaniona nikiingia chumbani kwa mwenye nyumba? Mtego huo wa panya haunihusu mie mbuzi." Panya akaenda hadi kwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe ng'ombe wa Bwana, kuna mtego wa panya umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane mawazo namna ya kuutegua kabla haujatuletea madhara."

Ng'ombe akajibu akionyesha mshangao! "Sijapata kusikia jambo la ajabu kama hilo. Yaani, mie ng'ombe nidhurike na mtego wa panya ulio uvunguni mwa kitanda! Hilo halinihusu."

Basi, ikatokea siku moja, nyoka akaingia chumbani kwa mwenye nyumba. Katika kutambaa kwake uvunguni mwa kitanda, mkia wa nyoka ukanasa mtegoni. Kishindo kilisikika. Mwenye nyumba alikwenda kwa furaha akiamini hatimaye panya aliyekuwa akimsumbua sasa amenaswa. Hapana, ni nyoka aliyenaswa mkia. Na ni mwenye hasira pia. Akamng'ata mguu. Sumu kali akamwachia. Mwenye nyumba akafa.

Jirani wakafika msibani. Siku ya kwanza watu walikuwa wachache. Wakahitaji kitoweo. Akakamatwa jogoo wa mwenye nyumba. Jogoo akachinjwa. Siku ya pili watu wakaongezeka. Kilihitajika kitoweo pia. Akakamatwa mbuzi wa mwenye nyumba. Mbuzi akachinjwa. Na siku ya maziko watu wakawa wengi zaidi. Akakamatwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Naye akachinjwa!

Ni jogoo, mbuzi na ng'ombe wa mwenye nyumba walioamini kuwa madhara ya mtego ule wa panya yasingewahusu wao. Walikosea. Panya alikuwa sahihi, na wala mtego haukumdhuru panya! Kuna cha kujifunza kutoka kwenye kisa hiki. Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,
0788 111 765
http://mjengwablog.co.tz
 
Mkuu Maggid umenena vyema. Lakini ebu angalia hii klipu alafu ujue kwanini tumefika hapahttp://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=BaJHhlIdXK8

- Padri hauawi, hata Sheikh pia...

Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Kwa nini sasa?

Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni.

Maggid Mjengwa,
Iringa.[/QUOTE]
 
One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!

- Padri hauawi, hata Sheikh pia...

Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Kwa nini sasa?

Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
Maggid, hili tatizo limeanza muda mrefu. Tofauti na huko nyuma siku hizi washenzi na wahalifu wameachiwa kufanya watakavyo. Zamani usalama wa taifa ulikuwa na maana ya usalama wa taifa na hili tatizo lingeshashughulikiwa kabla ya kufika hapo lilipofikia.

Usalama wa taifa siku hzi ni kulinda misafara ya viongozi baasi kazi yao imekwisha.
Ni kwasababu hizo imefikia hata ndege za kijeshi kutua nchini na kufanya kazi zao bila taifa kujua!
Tembo wanauawa na meno yanakamatwa Hong Kong! siyo Dar, Serengeti au mikumi.

Usalama wa taifa wanajua kuwa Zanzibar ni tatizo la usalama hata kabla ya tatizo la mauaji. Tumeonya mara nyingi kuwa chuki za wazanzibar si dhidi ya muungano ni dhidi ya watu wa imani nyingine, na hata wa imani yao wasiotoka Zanzibar.

Ukiwa mwislam basi kule visiwani wewe ni wa bara ingawa hutachukiwa kama mtu mwingine. Hili ndilo tatizo la Zanzibar haya mambo ya muungano ni kisingizio tu.

Kajeruhiwa padri na risasi Zanzibar kwa mara ya kwanza, hakuna aliyekamatwa wala kushtakiwa. Tilichokiona ni kauli za kawaida za kipuuzi za viongozi wetu ''tutawasgughulikia, hatutavumilia n.k.)

Watanganyika walichomwa moto Zanzibar hakuna aliyekamatwa wala kushtakiwa.
Tukaonya kuwa chuki hii ni mbaya sana hasa kwa vile kuna mahusiano na Zanzibar kupiatia muungano.

Watu wote waliofanya uhalifu Zanzibar hakuna aliyefikishwa mahakamani na wote wameaachiwa. Hii maana yake ni kuwa serikali (SMZ) inawaogopa kama si kuwaunga mkono wauaji. Kwahiyo mauji ya padri Mushi hatutakosea tukisema yana barala za serikali ya mapinduzi Zanzibar. Tunasema yana baraka kwasababu hakuna, narudia hakuna mtu aliyewahi kuhukumiwa kwa uhalifu wa chuki za dini na Uanganyika, leo kipi cha ajabu!

Sio suala la kukemea wahalfu tu, ni suala la kuhofia usalama wetu maana wale waliopewa dhamana hawajui wafanye nini.
Rais Kikwete anajua na serikali inajua kuwa sheikh mmoja anauza DVD za kuhubiri mauaji. Sheikh huyo amekuwa anazunguka ZNZ na bara katika chuki zake za muungano na ukristu. Serikali haijafanya lolote.

Mwenendo wa matukio kama haya ni udhaifu wa Rais Kikwete na nchi inatumbukia kubaya! Rias Kikwete ameacha wahalifu watambe kwa jinsi watakavyo iwe katika radio, mikutano, DVD na kila aina ya mawasiliano.
Hayo hayamtishi kiongozi huyu dhaifu, kinachomgusa ni kumpokea Juliana! Real! Rais wa nchi ! real! serious

Ungeniuliza ninashauri nini, ningekujibu wananchi waone hatari iliyo mbele yao na kwamba suluhu ni kuhakikisha Prseident Kikwete steps down before the country plunge into anarchy.

Hakuna sababu ya wananchi kujibizana au kuandamana, hapa ilikuwa wananchi waungane Rais kikwete ajiuzulu mara moja .Sababu kubwa ni kushindwa kuongoza taifa, he is a failure!
 
Mkuu Nguruvi3,

Ubarikiwe! Hili suala sio la kumumunya maneno na hadithi za Alfa-Lela-Ulela. Muda umefika kwa serikali ya Kikwete kujitazama na kuamua kuwajibishana. Mustakabali wa taifa letu huko kwenye mstari hapa! Tanzania ni zaidi ya Kikwete, au chama chochote cha siasa. Utawala wa Kikwete lazima ukomeshe hili suala mara moja. Maneno matupu hayatatusaidia kitu.
 
padr amekufa kwasababu ni mkristu pia kwasababu ni mtu kutoka bara.....
nchi yangu haitawaliki tena.....
 
Mkuu maggid, Shehe ilunga anavyonukuu kitabu chenu kikisema ni lazma kulipiza kisasi, je unapingana na kitabu chenu?
wewe unamsikiliza na kumuamini yule ----- (sheikh Ilunga)..... amechanganyikiwa yule huoni et anajiita kijana mpaka leo.
 
vipi kuhusu ustaadh juma alivyouawa 2001 kwa kupigwa risasi mbili akiwa katoka kuswali sala ya ijumaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom