Padri Hauawi, Hata Sheikh Pia...!

Padri Hauawi, Hata Sheikh Pia...!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!

- Padri hauawi, hata Sheikh pia...

Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Kwa nini sasa?

Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
 
TATIZO MATAMKO MENGI HAKUNA KINACHOFANYIKA!!! Wakumwachia ni Mungu adhabu yake ni haki tosha
 
Mkuu maggid, Shehe ilunga anavyonukuu kitabu chenu kikisema ni lazma kulipiza kisasi, je unapingana na kitabu chenu?
 
Nyakati za matatizo tunahitaji kumtazama yeye aliyetuumba. Alituumba tukiwa wa thamani kuliko viumbe wote, wengine wote alitamka lakini kwa sisi alitufinyanga kwa mikono yake na kutuwekea pumzi ya uhai. tuonapo haya tuziulize nafsi zetu na kumtazama YEYE Muumbaji wetu na kupatizama tulipomkosa ili tutubu atusaidie kutekeleza wajibu wetu kama vimbe katika dunia hii na maisha haya.
 
why is this happening? let's get to look deeply and keenly behind this scene coz the less serious we are the more is stinging in this sin of hatrad! RIP paroko!
 
Ninamfahamu Padre Mushi...kabla ya kuwa Z'bar nafikiri alikuwa Nairobi!mpole na mwenye hekima!nimefanya nao kazi na mwenzake Padre Manfred Mjengwa aliyeongozana na vijana kwenda Hispania mwaka jana!huyu Mjengwa ni Padre kijana mwenye muono wa kisasa sana,muelewa na anayeweza kuishi mazingra yoyote!alijitolea kuwafundisha vijana bila kujali tofauti za dini zao!Vip Fr.Mjengwa bado yupo Zenji?usalama wake je?vipi mna undugu nae?
 
Asante maggid kwa maoni yako, ila bibi yetu Kirobo anaendeleaje na habari za sms?
Ni kweli maggid uliyaeleza ni sahihii.lakini kichguu hakijai kwa rundo la mchanga.haya ni matikeo ya uhuru wa kusema na kutenda bila mipaka.tumekuwa tukitetea sana watu viongozi wa dini na waandishi wa habari kuongea lolote hata kama kaulizao hatimaye zitakuja kuwa msingi wa chuki baina ya makundi.haya ndio matunda yanayojitokeza tusilalamike tumejijengea misingi mibovu sana.E mungu tuepushe na mabalaa haya
 
wakristo wategemee mengi zaidi, ikiwa watu wanaahidi na kutoa nyaraka zenye vithibitisho vya kuwashughulikia wakristo, na wakaendelea kutekeleza adhma zao bila measure zozote kutoka kwa watawala unategemea nini? tena mtawala anaposimaa na kuwatahadharisheni wote as if wote mna makosa, unategemea mwenye kosa hasa atakaa ajirekebishe? hata watoto wako ukishuhudia mmoja akimchokoza mwenzie, halafu wewe unawaambia wote acheni kuchokozana kaeni kwa amani, unategemea yule mchokozi ataacha uchokozi? never, kaeni sawa tu wakristo mkijua kabisa kuwa mko vitani. na viongozi wa kikristo ambao wangeweza tu kutahadharisha na kuongeleaa huko juu kuhusu hii hali ili solution ipatikane through level ya juu, wako hoi wamekamatwa ufahamu, hawajui hata wanachofikiria
 
Mambo mengi mabaya na ya kishetani yatatekelezwa kwa jina la uislam, ajenda nyingi zitajivalisha umbo na sura ya uisilam, lakini havitanishawishi eti nimchukie AshaDii
 
Last edited by a moderator:
Hao wauwaji na dini yao walisaidia kuweka serikali madarakani, hasa baada ya kuambiwa CDM ni chama cha kidini.
Tusitegemee serikali kuwakamata, tujilinde wenyewe wakristu wenzangu.

Wakuu wanadhani kwenda kuhudhuria misiba ndo kutaonyesha wanajali na wanalaani mauaji.
 
Hivi Allah gani anayeshabikia kuua binadamu mwenzako? Hebu tujitsfakari

Sikuzote Mkuki kwa Nguruwe kwa Binadam Mchungu Jamaa hivi unaushahidi kuwa Waislam ndo Wamehusika ?
Je mbona walipouliwa Waislam Mwembe Chai mlikaa kimya?
Je mbona Sheikh alipomwagiwa tindikali mlikaa kimya?
Acheni kupotosha maana waache Police wafanye Uchunguzi ukweli utabainika
 
One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!

- Padri hauawi, hata Sheikh pia...

Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Kwa nini sasa?

Hakika, sote bila kujali tofauti zetu za kiimani, tuna lazima ya kuukemea uovu huu. Na mamlaka husika zihakikishe hakuna kinachoachwa bila kugeuzwa hadi waovu waliohusika na uovu huu watiwe nguvuni.

Maggid Mjengwa,
Iringa.

mabingwa wa 'intelijensia ya polisi' wanashughulikia waliom'sms' makinda. Ofkoz wengine wapo mtwara kusaidia wataalam gesi kutinga dar. Hawana muda na intelijensia ya kuzuia uhalifu. What're early warning systems, security and peace
 
Tukio hili linaweza likawa limefanywa na watu wenye chuki dhidi ya serikali ili kukoleza mgogoro wa kidini unaonekana kukua kwa kasi. Japo uhalifu kama huo Zanzibar hutokea sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom