Padre Mapunda amepinda, Tumuelimishe sehemu ya kwanza

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,532
Na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed

SIKU ya Jumatano tarehe 17/09/2014 nimebahatika kusoma makala ya kaka yangu Padre Baptiste Mapunda yenye kichwa cha habari "CCM na kitanzi chake cha Mahakama ya Kadhi".

Nilipoisoma mara ya kwanza nilistaajabu "hoja dhaifu" alizozitoa Padre Mapunda, lakini nilipoipitia kwa mara ya pili nilijiridhisha kwamba kwa misingi ya kutetea "imani" yake aliwajibika kuandika aliyoyaandika. Pamoja na kustaajabu hayo, kuna "maeneo" ya makala yake yamenihuzunisha na baadhi ya maeneo yamenifurahisha sana.

Katika makala hii niliyokusudia kumuelimisha Padre Mapunda na Mtanzania mwengine yeyote, nimeigawa katikaeneo makuu matatu

(1) Maeneo yaliyonistaajabisha katika maneno ya padre Mapunda.

(2) Maeneo yaliyonihuzunisha katika maneno ya Mheshimiwa Mapunda.

(3) Na maeneo yaliyonifurahisha.Kabla sijaanza uchambuzi huo, nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi ufuatao juu ya kadhia ya Mahakama ya Kadhi hapa kwetu Tanzania:Mahakama ya Kadhi ni mahakama maalum inayohusika na kesi za ndoa, talaka, miirathi, waqfu, wasia na malezi ya watoto kwa mujibu wa sheria ya Dini ya Kiislamu.

Hakimu wa Mahakama hiyo ambaye anaitwa Kadhi, ni Muislamu anayejua vyema ufumbuzi wa kadhia hizo. Kesi zote za jinai hata kama iwe kati ya Muislamu na Muislamu zitabakia katika mfumo wa kawaida wa Mahakama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kukosekana kwa Kadhi kunawanyima Waislamu haki ya kutekeleza Ibada ya Ndoa kwa ukamilifu wake, kwani kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni Mahakama tu, wakati Uislamu unafundisha mtoaji talaka ni yule yule aliyeoa.

Na pindi Muislamu akitoa talaka, serikali haiikubali talaka hiyo muda wa kuwa haijathibitishwa na Mahakama. Na pindi Mahakama ikitoa talaka, Uislamu hauikubali talaka hiyo kwa kuwa ndoa iliyofungwa kwa sheria za Kiislamu haivunjiki kwa sheria nyengine.

Hii ni adha kwa Waislamu na mtatuzi wake ni Mahakama ya Kadhi.Waislamu wanaamini kuwa zipo baadhi ya ndoa haziwezi kuendelea kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao.

Kwa mfano; ndoa ya mume aliyefungwa gerezani muda mrefu na hana mapato yatakayomkimu mkewe mpaka amalize kifungo, au ndoa ya Muislamu aliyekwenda nje ya Tanzania akazamia huko kwa muda mrefu kutafuta maisha na mkewe amemtelekeza, au Muislamu yupo hapa hapa nchini lakini ni mjeuri, anamtesa mkewe na anasema anajua kuoa hajui kuacha, kiasi kwamba mkewe huyu anataabika sana.

Kuzivunja ndoa za aina hiyo kunahitajia nguvu mbili: kwanza, nguvu ya Kidini ili imani na sheria ya Kiislamu iliyotumika kuwafungisha ndoa ifanye kazi yake kwani ndoa iliyofungwa kiimani inavunjwa kiimani pia.

Pili, nguvu ya kiserikali ili mume kama hatoridhika asiweze kuleta madhara baada ya ndoa yake kuvunjwa, na serikali pia ikubali kuwa ndoa imevunjika ili isimtambue mwanamume huyo kuwa ni mume wa mwanamke huyo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Katika muda huu ambao hakuna Mahakama ya Kadhi, ndoa zote zinazovunjwa na Mahakama za kawaida bila ya wale waume zao kutoa talaka, pindi watalaka wao (wanawake) wakiolewa tena na waume wengine, hizo ni ndoa ndani ya ndoa. Na ndoa hii ya pili haiswihi (haikubaliki) kwa mujibu wa sheria ya Dini ya Kiislamu na ni batili.

Tatizo hili haliwezi kuondoka kama hakuna Mahakama ya Kadhi, na mwanamke huyu Muislamu analazimishwa imma azini (endapo atafuata hukumu hiyo ya Mahakama ya kawaida na yeye kukubali kuolewa tena na mume mwengine) au afe mjane (kwa kukubali talaka hiyo ya Mahakama ya kawaida na kukataa kuolewa tena).

Waislamu wa Tanzania kwa kuzingatia umuhimu huo waliiomba serikali yao "huduma" hiyo katika awamu zote za utawala wa nchi hii kuanzia awamu ya kwanza hadi hii awamu ya nne, lakini bado hawajafanikiwa katika hilo na bado Waislamu wanaendelea kuomba.

Sasa nirudi kwenye makala ya kaka yangu padre Mapunda katika maeneo matatu niliyoigawanya:

(1) Maeneo niliyostaajibishwa katika maneno ya padre Mapunda:Nimestaajabishwa sana na kauli yake yenye lengo la "kumsaliti" Mzee Ali Hassan Mwinyi ili aonekane katika jamii kwamba ndiye anayewachochea Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi.

Namnukuu Mheshimimwa Mapunda aliposema:"Raisi wa Awamu ya Pili, Alhajj Ali Hassan Mwinyi siku si nyingi alisikika akitetea Mahakama hizo za Kadhi, Je, alikuwa wapi kuanzisha alipokuwa madarakani? (mwisho wa kunukuu).

Katika hoja hiyo naomba nimkumbushe padre Mapunda kuwa Raisi Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi hana kosa kufanya hivyo kwa sababu yeye alikuwa Rais wa Zanzibar kabla ya kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kule Zanzibar Mahakama ya Kadhi ipo na Wakristo wapo tena ni wachache na wala haina madhara yoyote .

Kuhusu suala kwamba, kwanini hakusema wakati yuko madarakani? Huenda alisema lakini "mfumo" ambao wewe kaka yangu Mapunda unaujua "ulimdhibiti" na hakufikia mafanikio katika hilo.Naomba nimkumbushe tena Mapunda ili aelimike.

Awamu ya Tatu chini ya Mheshimiwa Raisi Mstaafu Benjamin William Mkapa,

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliunda Tume ya kufuatilia Mahakama ya Kadhi chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Athumani Janguo (Mbunge mstaafu wa Kisarawe) na Tume hiyo ilitumia fedha za walipa kodi hawa hawa.

Miongoni mwa wajumbe wa Tume hiyo ni:(a) Marehemu Mzee Abdallah Saidi Fundikira, Rosemary Nyerere, Nimrod Mkono, katibu mkuu wa chadema Dr. Wilbroad Slaa, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mheshimiwa Shoka kutoka Zanzibar.

Mheshimiwa Padre Mapunda "anapolikoleza" suala la Ukadhi kwa kulihusisha na CCM ili Waislamu wajenge "hasira" na CCM, hiyo ni mbinu ya kitoto kwa sababu CCM wameliweka suala la Ukadhi kwenye ilani yake katika Uchaguzi wa mwaka 2010 na Tume ya Mheshimiwa Arcardo Ntagazwa ambaye baada ya kuteuliwa kuwa waziri iliongozwa na Mheshimiwa Athumani Janguo juu ya suala la Ukadhi ilikuwepo kabla ya mwaka 2010.

Je, kuihusisha CCM kwa sababu tu Waislamu waamini kwamba "mbaya" wao ni CCM ili waigomee kuipa kura hauoni kuwa ni usaliti kwa CCM ambayo Mwenyekiti wake kwa sasa ni Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete?

Mbona CCM ilipokuwa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, yeye hakubebeshwa shutuma hizo ijapokuwa hiyo ilani inayoelezea ahadi ya Mahakama ya Kadhi imetayarishwa chini ya uenyekiti wake?

Kwanini utayarishaji wa ilani hiyo uliofanywa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Mkapa lawama zake abebeshwe Mheshimiwa Jakaya Kikwete? Je, kweli huo ni uadilifu kaka Padre Mapunda?

(2) Maeneo niliyohuzunishwa katika maneno ya Mapunda: Nimehuzunishwa sana na maneno ya Mheshimiwa Padre Mapunda aliposema (namnukuu):"Viongozi wa dini ya Kikrsito kwa upendo wote waliposema Mahakama ya Kadhi haitakiwi kujadiliwa bungeni walijua walichokuwa wakikisema.

Wanajua ubaya wa Mahakama hizo na wanajua kwa mifano kwa nchi nyengine kama Sudan, Somalia, na sasa Nigeria jinsi ambavyo kumezuka mizozo." (mwisho wa kunukuu).

Nimehuzunishwa sana kwa maneno hayo ya "uongo" kutoka mdomoni mwa kiongozi wa kidini mwenye cheo cha Upadre. Kama Padre anaweza kusema uongo ili kufanikisha matakwa yake,

Je waumini wafanye nini? Hivi mgogoro wa Sudan kumbe wanagombea Ukadhi? Hivi mgogoro wa Somalia nao wanagombea Ukadhi? Na hata Nigeria kumbe Boko Haram nao wanataka Ukadhi?

Inahuzunisha sana kuusema uongo huo ili Watanzania waogope na wasitamani tena kusikia chochote kuhusu Mahakama ya Kadhi. Padre Mapunda alikusudia kusema ukweli kwanini hakuitaja Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ina Mahakama ya Kadhi?

Kwanini hakuitaja Kenya (ambayo Waislamu ni chini ya asilimia ishirini) lakini Mahakama ya Kadhi ipo? Mahakama za Kadhi zipo Kenya na Zanzibar na hakujaripotiwa mauaji au migogoro kama ya huko Sudan, Somalia na Nigeria?
Ni vipi kiongozi wa dini anakuwa mwongo? Na kwa nini amelazimika kuwa mwongo? Hivi pale Mahakamani pakiandaliwa chumba maalum kisha akawepo Sheikh ambaye zikija Mahakamani kesi zinazohusu ndoa, talaka, miirathi, waqfu, wasia na malezi ya watoto; yule Sheikh awe anazitolea maamuzi, Je, huyo mtu mwengine anauliwa kwa kosa lipi?Kwa kitendo cha ndugu yangu Padre Mapunda kufananisha maombi ya Waislamu juu ya Mahakama ya Kadhi na kuuliwa kwa watu Sudan, Somalia na Nigeria, amefanya uchochezi, kejeli na dharau dhidi ya Uislamu na Waislamu.

ITAENDELEA
 
Duuuuuuuuuuuuuuuuuh!!!!!!!!!!!!!!!!! This is Tanzania. What if tungekua wote wapagani?????????????
 
mimi naomba kujua mipaka ya mahakama ya kazi itakuwa wapi katika mambo yafuatayo.

1. Ndoa iliyofungwa Kiislam lakini mmoja wa wanandoa akaamua kubadili dini na kuwa Mkristo je, ikitokea issue ya talaka mahakama ya kadhi itakuwa na haki ya kuhusika kwa sababu ndoa ilifungwa kiislam ingawa mmoja alisha achana na uislam?

2. je kati ya MAHAKAMA YA KADHI NA MISINGI YA HAKI ZA BINADAMU ambazo tanzania imeridhia kipi kitakuwa juu ya kingine, kwa mfano, HAKI YA MWANAMKE KURITHI TOKA KWA WAZAZI WAKE, Tuchukulie mfaano Wazazi ni waislam mtoto akaamua kuwa mkristo je, kama mzazi akufurahishwa na jambo la kubadili dini la mtoto wake akamnyima haki ikiwamo urithi hapa pengine maamuzi ya mahakama ya kadhi na mahakama ya kiraia yatatofautiana, naamini mtoto atakwenda mahakama za serikali huku mzee akilindwa na mahakama za kadhi, katika mazingira haya haki sahihi ni ile itakayoamriwa na mahakama gani?

napendekeza badala ya kuwa na sheria ya mahakama ya kadhi, tuwe na sheria itakayokuwa inatambua maamuzi yanayofanywa na mabalaza ya kijamii, yakiwamo yanayofanywa na taasisi za kidini, sheria itakayo kuwa general kwa wote hata maamuzi ya kimila kwa jamii zinazofuata dini za asili.

Naamini hakuna imani isiyoumizwa na baadhi ya maamuzi ya mahakama za serikali, mfaano issue ya talaka kwa upande wa wakristu talaka haikubaliki isipokuwa kwa sababu maalum tu, na sio kuchokana au kutofautiana katika misingi ya maisha, vilevile ndoa za wake wengi haziruhusiwi ebu tujiulize kama mkristu akiyafanya hayo ni wapi ambapo heshima ya ukristo italindwa kwani kwenye mahakama za serikali kutoa talaka au kuoa wake wengi sio kosa.

SERIKALI LAZIMA ISAIDE KULINDA MAADILI YA IMANI ZOTE WALA SIO MOJA TU, SHERIA IWE GENERAL KWA JAMII NZIMA WALA SI KWA WAISLAM TU.

HAYO NI MAWAZO YANGU SINA NIA YA KUMKOSOA WALA KUMUUDHI MTU,

Pole sana ndugu yangu. Kama utampata mtu wa kuchangia hapa ni wachache sana. Wengi wa humu ni wale wanaotukana au kutumia lugha isiyo na staha kwa wenzao. Hebu tusubiri tuone na si ajabu ukaambulia matusi pia.
 
Na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed

ITAENDELEA

Ukimsoma huwa unamwelewa vizuri? Naona kama mengine umeongeza mwenyewe... hili la "uchochezi, kejeli na dharau dhidi ya Uislamu na Waislamu" ni maoni yako tu, lakini hapa unayaweka kama ya Fr Mapunda. Unaweza kuleta makala ambayo ameandika kwa "kuchochea, kejeli na dharau dhidi ya Uislamu na Waislamu". Nia yangu ni kutaka tujadili kitu kilichopo na siyo kile kinachowekwa kinywani mwa mtu.
 
Na Sheikh Mohamed Iddi Mohamed

ITAENDELEA

Mimi binafsi sina tatizo hata kidogo na mahakama ya Kadhi, kuna watu kweli hawaelewi vizuri umuhimu wa mahakama hiyo kwa waislam na wengi wamekuwa wakiioanisha na matukio au maamuzi kadhaa ambayo dunia iliyatafsiri kama ukiukwaji wa haki za binadamu pindi hukumu zilizopitishwa na mahakama hiyo. Katika nchi hii mahakama ni moja ya mihimili muhimu ya kitaifa ya kimaamuzi, Bunge pia ni mojawapo ni vipi jambo linalogusa jamii ya watu fulani liingie peke yake kwenye mhimili muhimu wa Kitaifa? nafikiri au niseme jambo linalonitatiza mimi ni kuwa Dini ya Kiislam ni taasisi kubwa inauwezo wa kuanzisha jambo lake bila hata kutegemea fadhila za serikali, kwanini BAKWATA au taasisi za kiislam zisipigani kuianzisha mahakama hiyo kwa nguvu zao mpaka kuanza kuhangaika na serikali? mara kadhaa nimesikia ikielezwa kuwa mahakama hiyo ni ruksa kuanzishwa. Jambo ambalo ningewashauri waislam wafanye ni kupata uhakikisho kuwa HUKUMU ZITAKAZOTOLEWA ZITAKUWA NA NGUVU KISHERIA na kutambuliwa na mahakama za serikali.!! Taasisi za kiislam zingekubaliana kuanzishwa mahakama hiyo na kuweka utaratibu mzuri wa kumpata Kadhi mkuu na wengine, pia kuweka hadharani mfumo wa mahakama hiyo na uendeshwaji wake na aina za kesi zitakazotatuliwa na mahakama hiyo ili watu waelewe. Sasa hivi watu wengi hatuelewi na hatujaeleweshwa umuhimu wa hiyo mahakama, kumbukeni kuwa kwa muda mrefu kuna malalamiko kuwa Serikali inamkataba na Kanisa wa kuendesha huduma (kama hospitali na vituo vya afya) na hili jambo lilileta malalamiko kwa waislam mpaka serikali ilipoeleza ukweli kuwa mkataba huo. Mimi sina tatizo na hiyo mahakama ila HEBU ANZISHENI KWANZA halafu kama ni jambo jema lenye manufaa kwa wananchi serikali ni sikivu itasaidia. Wekeni muundu wa mahakama hiyo hadharani watu waelewe mnataka kitu cha namna gani, tafuteni ufadhili wa ndani na nje mtaweza. Sasa hivi tu mahakama zetu zipo hoi bin taaban bado kuna zigo lingine mnataka kuibebesha, hao makadhi wakikosa mishahara patakalika hamtasema ni hujumaa? hamtaanza maandamano na kashfa???
 
Mimi kila siku nauliza "Kenya, Zanzibar & Uganda wana mahakama ya kadhi. Je, ni kipi ambacho waislamu wa Zanzibar au Lamu wanakipata kwa kupitia mahakama ya kadhi ambacho waislamu wa Tanganyika wamekikosa kwa kuikosa mahakama ya kadhi?". Mahakama ya kadhi kwa upande wa Zanzibar imeanza kunyonyeshwa kidogo na kina mama wengi kwa kupendelea wanaume kuanzia ktk hukumu zao hadi ktk mifumo ya uongozi wa mahakama hizo. Hebu tusijitoe akili tukubali kwenda Zanzibar na kufanya utafiti huu kwani kina mama wengi leo hawataki mshauri yao yapelekwa kwenye mahakama ya kadhi. Ukiondoa wawili watatu hatuzisikii "KAULI" za kina mama wanaodai mahakama ya kadhi. Waungwana tunajiuliza ukimya huu wa mama & dada zetu tafsiri yake ni nini hasa?
 
Upadri siku hizi umeingiliwa, na hawa ni watu wanaopandikizwa kuja kuharibu sifa ya katoliki. Mapunda mbwa kabisa.
 
mimi naomba kujua mipaka ya mahakama ya kazi itakuwa wapi katika mambo yafuatayo.

1. Ndoa iliyofungwa Kiislam lakini mmoja wa wanandoa akaamua kubadili dini na kuwa Mkristo je, ikitokea issue ya talaka mahakama ya kadhi itakuwa na haki ya kuhusika kwa sababu ndoa ilifungwa kiislam ingawa mmoja alisha achana na uislam?

2. je kati ya MAHAKAMA YA KADHI NA MISINGI YA HAKI ZA BINADAMU ambazo tanzania imeridhia kipi kitakuwa juu ya kingine, kwa mfano, HAKI YA MWANAMKE KURITHI TOKA KWA WAZAZI WAKE, Tuchukulie mfaano Wazazi ni waislam mtoto akaamua kuwa mkristo je, kama mzazi akufurahishwa na jambo la kubadili dini la mtoto wake akamnyima haki ikiwamo urithi hapa pengine maamuzi ya mahakama ya kadhi na mahakama ya kiraia yatatofautiana, naamini mtoto atakwenda mahakama za serikali huku mzee akilindwa na mahakama za kadhi, katika mazingira haya haki sahihi ni ile itakayoamriwa na mahakama gani?

[/I][/B]

Maswali mazuri....
Na hii ni bora kuliko kupinga tu bila kutaka kujua.
Katika Uislamu masuala ya ndoa, talaka na mirathi yote ni ibada. Yana kanuni na taratibu zake kidini.
1. Kuhusu swali lako la kwanza, ndoa imefungwa kiislamu. Mmoja wa wanandoa atapoamua kutoka katika uislamu ndoa hiyo automatically inavunjika (Breach of terms and conditions of that marriage, ni kama mikataba mingine tu)
2. Swali lako la pili, Katika uislamu mtoto anapoamua kubadili dini anakuwa hana haki yoyote ile juu ya wazazi wake, hawarithi na hawamrithi. Na hii ni hata kwa mtoto ambae wazazi wake ni wa dini nyingine akaamua kuwa muislamu, haruhusiwi kuwarithi wazazi wake hao. Kwa nini utake mirathi kwa mzazi ambae si dini yako (ukizingatia kiislamu mirathi ni ibada)? Hivi unaweza kuukana uraia wako wa Tanzania ukachukua uraia wa nchi nyingine, halafu utegemee kupata haki za Mtanzania kweli?
 
Upadri siku hizi umeingiliwa, na hawa ni watu wanaopandikizwa kuja kuharibu sifa ya katoliki. Mapunda mbwa kabisa.

Duh! Ulishawahi kujadili kitu chochote na mtu mwingine? Naona wanaojadiliana na wewe huwa wanajuta. Very strange indeed and an example of an uncivilised person!
 
Ukiangalia kwa ulichoandika unaonesha wewe ndio umechanganyikiwa, Serikali haina dini unataka shekh akafanye nini mahakamani kama ni mahakama ya kadhi imesharuhusiwa lakini waislamu kupitia taasisi zao wajipange wenyewe kwanini mnataka kuingiza serikali. Ukiruhusu mahakama ya kadhi wakristo nao watataka mahakama yao, baadhi ya makabila nao watataka mahakama zao za mila sasa nchi itafika wapi.

Ni Udini uliopitiliza kutaka serikali kuingilia masuala ya dini lakini sio udini kutaka serikali kutojiingiza kwenye dini.

Serikali isirogwe kuleta mjadala wa mahakama ya kadhi tena, utaligawa taifa mambo ya dini yashughulikiwe na taasisi na viongozi wadini husika.

Back
Top Bottom