Padre Aliyejiteka ana changamoto ya Afya ya akili

Lucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2018
Posts
20,324
Reaction score
62,218
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limemfutia kesi ya kujiteka na kutoa taarifa ya uwongo mtandaoni iliyokuwa ikimkabili Padre Jodan Kibiki wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyololo, Jimbo la Mafinga baada ya uchunguzi wa kitabibu kugundua Padre huyo ana changamoto ya afya ya akili.

Akitoa taarifa hiyo Askofu mkuu wa Jimbo la Mafinga, Mhasham Vincent Mwagala, amesema Padre Jodan Kibiki, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Yololo, alitoweka katika mazingira tatanishi Septemba 18, 2025 baada ya kutelekeza gari lake katika msitu wa Sao Hill mkoani Iringa.

Amesema baada ya kufanya malipo ya shilingi milioni tatu na nusu kwenye tovuti ya biashara mtandaoni ya eBay ndipo alipogundua kuwa alikuwa ametapeliwa imebainika ni kweli Padre huyo ana madeni ya Tsh 2,000,000/ million mbili, ambapo kiasi cha Tsh 500,000/= laki tano aliazima kwa Paroko, Tsh 1,500,000/= milioni moja na nusu aliazima kwa muhasibu wa jimbo, na pesa hiyo alienda kuweka kwenye tovuti ya biashara mtandaoni ya eBay, kwenye uchunguzi ilibainika kafanya Transaction ya Tsh 3.5M kwenye mtandao huo, huko ndipo alipo tapeliwa na kupata msongo wa mawazo uliopelekea atoe taarifa kuwa ametekwa.

Taarifa ambayo ilisababisha Jeshi la polisi limkamate kwa kosa ya kutoa taarifa za uongo hivyo kuzua taharuki kwenye jamii.

Screenshot_20250930_234645_Instagram.jpg
 
Unakuta kuna wadau wanaenda kwa huyo padre kuomba toba ili awapelekee maombi yao mbinguni kumbe mwamba mwenyewe mcheza kamari mzee wa mikeka na fix nyingi, Padre kuwa muongo kiasi hicho ni aibu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limemfutia kesi ya kujiteka na kutoa taarifa ya uwongo mtandaoni iliyokuwa ikimkabili Padre Jodan Kibiki wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyololo, Jimbo la Mafinga baada ya uchunguzi wa kitabibu kugundua Padre huyo ana changamoto ya afya ya akili.

Akitoa taarifa hiyo Askofu mkuu wa Jimbo la Mafinga, Mhasham Vincent Mwagala, amesema Padre Jodan Kibiki, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Yololo, alitoweka katika mazingira tatanishi Septemba 18, 2025 baada ya kutelekeza gari lake katika msitu wa Sao Hill mkoani Iringa.

Amesema baada ya kufanya malipo ya shilingi milioni tatu na nusu kwenye tovuti ya biashara mtandaoni ya eBay ndipo alipogundua kuwa alikuwa ametapeliwa imebainika ni kweli Padre huyo ana madeni ya Tsh 2,000,000/ million mbili, ambapo kiasi cha Tsh 500,000/= laki tano aliazima kwa Paroko, Tsh 1,500,000/= milioni moja na nusu aliazima kwa muhasibu wa jimbo, na pesa hiyo alienda kuweka kwenye tovuti ya biashara mtandaoni ya eBay, kwenye uchunguzi ilibainika kafanya Transaction ya Tsh 3.5M kwenye mtandao huo, huko ndipo alipo tapeliwa na kupata msongo wa mawazo uliopelekea atoe taarifa kuwa ametekwa.

Taarifa ambayo ilisababisha Jeshi la polisi limkamate kwa kosa ya kutoa taarifa za uongo hivyo kuzua taharuki kwenye jamii.

View attachment 3481471
FUTUHIIIIIIIIIIIII NDIYOOO NI FUTUHIII.
 
Aiseee! Mbinguni tutaenda kweli? kama viongozi wenyewe ndo hawa wanabet mtandaoni, huyu lango la mbinguni atalisikia tu, naona shetani kanyakua point 3 muhimu hapa.
 
Unaelewa unachoandika lakini ? Èbay sio betting mkuu......online suoermarket chochote utakacho unaweza kununua kupitia wao....yeye sijui alifanyaje hadinakatapeliwa lakini ebay uhakika kupats utakacho
 
ina maana waislam hawafanyi dhambi, ni watukufu? Sijawahi kuona muislam akiomba toba, anatubu
Muislam anaomba toba kila siku moja kwa moja yeye na Mungu wake na siyo kwenda kumueleza sheikh ili amuombee kama ilivyo wakatoliki kwenda kuomba toba kwa padre
 
Aiseee! Mbinguni tutaenda kweli? kama viongozi wenyewe ndo hawa wanabet mtandaoni, huyu lango la mbinguni atalisikia tu, naona shetani kanyakua point 3 muhimu hapa.
kuna padri mmoja aliulizwa mbingu ipo? Akajibu hata yeye hana uhakika kama ipo. Mapadri ni binadamu wa kawaida, si malaika wale, wanaishi duniani na wanatenda dhambi kama kawaida, Mungu ndiye anajua unyoofu wao
 
Muislam anaomba toba kila siku moja kwa moja yeye na Mungu wake na siyo kwenda kumueleza sheikh ili amuombee kama ilivyo wakatoliki kwenda kuomba toba kwa padre
hii haimaanishi kuwa waislam ni wanyoofu kuliko wengine, jamii nzima iko sawa, hakuna iliyo bora kuliko nyingine, makosa yapo kila dini na imani ulimwenguni, unaambiwa shetani yupo duniani anazungukazunguka apate wafuasi wake wa kufanya ushetani
 
Back
Top Bottom