P MAWENGE: Nahamia weusi

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,330
105,163
Nawasalimu kwa jina la HIP HOP

Mwana mziki wa Hip hop P mawenge a.k.a P the Mc katuacha na mshangao wadau na wapenzi wa muziki wa hip hop baada ya kutoa ngoma inayokwenda kwa jina la NAHAMIA WEUSI.

Ikumbukwe kwamba P mawenge ni member wa kundi pinzani la weusi linalotamba kwa jina la Kikosi kazi. Ngoma yao iliyo hit ni diss track dhidi ya weusi, ambapo humo P mawenge ndio alionekana kua na punch lines nzito kwa wahasimu wao. Imekuwaje tena aungane nao?

Kuna nini kinachoendelea pale kikosi kazi? Nakumbuka humu kuna wadau walishawahi kutoa maoni yao juu ya hilo kundi wakidai halina maisha marefu kwasababu puporse ya group ilikua ni ku attack kundi la weusi, na kwasababu weusi hawa respond basi hawa Kikosi kazi hawawezi kudumu kwakua wanahitaji respond ya weusi ili waendelee kubaki kwenye trend.

Wapo wadau wengine waliodai kua miongoni mwa members wa lile kundi ni wakorofi hivyo hawawezi kudumu lazima migogoro ya wao kwa wao itakuwepo na ndio itakayokuja kuleta matabaka na mwisho kuliua kundi.

Wiki kadhaa zilizopita mwanachama wa kikosi kazi songa ambaye alikua mshabiki wa timu ya mpira arsenal alitoa ngoma kua ana hamia manchester united na kweli ikawa hivyo, vipi kwa huyu itakua hivyo hivyo au ni kafanya hivyo kutafuta attention tu?

Nini maoni yako?
 
Nahamia weusi
Bom Bronx……Maweeenge….wuuuh!

[Verse One:]
Nishachoka kuimba ngoma za haraka na ukombozi/
Wanetu wanakamata tu nafasi za uongozi/
Kila miziki kwetu ni visasi na uchokozi/
Haya maamuzi yaheshimiwe wala staki gozigozi/
Arusha city ndo hood ya Xplastaz, Watengwa/
Kipindi Nelly anaukandia ushanta, nlipenda/
So acha nieleweke before I be dead gone/
Kwanza Mbeya, Dar, na Chuga iwe third home/
Nafurahi nikimwona Joh Makini yuko na G/
Wamepiga picha wakiwa ofini kwa DC/
Na hii ndo hiphop love, mimi ni mc/
Wanaowaza shobo huwa napiga chini siwaskii/
Machizi wanajihepusha na maugomvi na fujo/
Ni kikundi cha rap wala sio cha ndondi na judo/
Wako smart kwenye brain, smart kwenye kazi/
Wako kasi kwenye game hawataki ubabaishaji/
I was a good fan wa nako2nako na river camp/
Kabla P Mawenge halijaja bado katika game/
Na mambo yakanoga tangu Joh aje na Nikki/
Nawaona kwenye chupa la niaje ni vipi/

[Chorus:]
Nahamia weusiiii….
Mana machizi wako busy na game na hawataki haribu name/
Nahamia weusiiii….
Hawajawahi kujihusisha na dramas na wakapata fame/
Nahamia weusiii….
Wanafanya kazi zao kwa plans wala hawanaga complain/
Nahamia weusiii…..
Na ndo sababu walipotoka na walipo now….is not the same/


[Verse Two:]
Unaikumbuka nako2nako ya bang na ndo zetu kuwakilisha/
Pindi wao na kikosi yechu yechu hamna vita/
Kabla ya Beef kabla ya kaka zetu kuchapika/
“Show love to each other”, mpaka Yesu akatajika/
Mambo yalikuwa fresh pindi Lord yuko na Ray/
“Hii kwa ajili yako baby”, nice back in a days/Huku Bu huku Ibra kabla hawaja-part ways/
“Hawatuwezi” was fav track to play/
Bila kipingamizi mi weusi naikubali/
Mmefanya mengi mmebisha sana kwenye safari/
Nidham na Juhudi ndo zimewafikisha mbali/
Napenda nijoin kundi so nkikaribishwa shwari/
Kushindana kwenye game isitujengee chuki/
Mwishoni tulogane rodi tutembee uchi/
Waambie wagombanishi wasituletee uzushi/
Tupigeni ngoma kali chorus atembee jux/
We never been friends I know that for sure/
Its over now I gotta bottle bring glasses to pour/
Allow me to get in ya plane let’s start the tours/
“Vipi Kuhusu kikosi Kazi?” hilo staki kujua/

Chorus:]
Nahamia weusiiii….
Mana machizi wako busy na game na hawataki haribu name/
Nahamia weusiiii….
Hawajawahi kujihusisha na dramas na wakapata fame/
Nahamia weusiii….
Wanafanya kazi zao kwa plans wala
hawanaga complain/
Nahamia weusiii…..
Na ndo sababu walipotoka na walipo now….is not the same/
 
Back
Top Bottom