OUT kutoa shahada ya uzamili kuhusu ustawi wa jamii

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
OUT kutoa shahada ya uzamili kuhusu ustawi wa jamii

Tuesday, 11 January 2011 20:02 newsroom




NA MWANDISHI WETU
CHUO Kikuu Huria Tanzania (OUT) kimeingia mkataba na vyuo vikuu vya Hurbert Kairuki, Chuo cha Ustawi wa Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kutoa shahada ya uzamili ya ustawi wa jamii. Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo jana, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Profesa Tolly Mbwete alisema pamoja na vyuo hivyo, pia chu chake kitashirikiana na Chuo Kikuu cha Adiss Ababa, Ethiopia na Chicago, Marekani ambao vyuo vyao vinatoa kozi hiyo. Profesa Mbwete alisema hivi sasa baada ya kuingia makubaliano hayo, Hurbert Kairuki imepewa jukumu la kuwasilisha mitaala kwa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) ili kupata baraka za kuanza rasmi kwa mafunzo hayo.
Alisema iwapo TCU itatoa ruhusa ya maombi hayo, kozi hiyo itaanza Machi, mwaka huu. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Profesa Hosera Rwegoshora alisema miaka ya nyuma, wanafunzi waliokuwa wanataka kusoma zaidi chuoni hapo walijikuta wakihangaika kutafuta elimu hiyo nje ya nchi. "Wanafunzi waliomaliza hapa walikuwa wakiitafuta Shahada ya Uzamili Makerere au Zimbabwe na wengine kwenda vyuo vya mbali zaidi," alisema. Alisema shahada hiyo itakuwa na viwango vya kimataifa, hivyo hakutakuwa na haja ya watu kukimbilia kusoma nje ya nchi.
 
Hongereni....distance education is the future...............it cuts cost tremendously and it is flexible..............................
 
Back
Top Bottom