Ottoman empire - mrithi aliua ndugu zake wote

Ottoman empire - mrithi aliua ndugu zake wote

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,101
Reaction score
5,399
Jana nimetazama documentary flani inayohusiana na dola iliyowahi kuwa kubwa sana dola ya Ottoman ambayo ilianza kama kabila dogo la wafugaji ikakua na kuwa dola moja kubwa ambayo mpaka leo ushawishi wake na alama zake ziko wazi.
Katika mambo ya kustaajabisha niliyo yaona ni kwamba mrithi wa kiti cha ufalme ilikuwa anawaua ndugu zake wote pindi anaposhika kiti cha ufalme ili kuzuia mvutano na kugombea madaraka.
Kuna kipindi mmoja aliua ndugu zake 19 ambapo japo ulikuwa ni utamaduni uliokwisha zoeleka ila watu wengi walisikitaka baada ya kuona majeneza 19 yakitolewa kwenye kasri ya kifalme asubuhi kuashiria kwamba mrithi kateketeza ndugu zake 19 akiwemo watoto wadogo kabisa.
Jambo lingine lilinifurahisha ni kwamba mfalme alikuwa haoi ila alikuwa na vimada ambapo angeweza kuwa na vimada hata 1,000 ambao walikuwa wanachaguliwa kutoka kwenye watumwa ambao ni mabikra na warembo lakini kati ya hao wote ni wachache walikuwa wanapata anfasi ya kulala na mfalme. Na pia mfalme alipokuwa akimjaza mimba kimada basi hafanyi naye mapenzi tena yani utamaduni wao ulikuwa ni kwamba mfalme haruhusiwi kuzaa na mwanamke mmoja watoto wa kiume zaidi ya mmoja hivyo kila Prince alikuwa na mama yake.
Huu utamaduni alikuja kuuondoa mfalme mmoja baada ya kulala na mtumwa mmoja kutoka syria akampenda na kuzaa naye watoto sita na kuamua kumuoa kabisa, jambo ambalo liliwafanya watu waamini huyo mtumwa alikuwa anatumia miziziology kwakuwa hakuwa mrembo kama wengine lakini mfalme alikuwa hachomoi kwake.
Jambo lingine ambalo lilinivutia ni kwamba utawala wa Ottoman ulipokuwa ukichukua miji na nchi walikuwa hawaui Wakristo wala kuwatesa walikuwa wanawaruhusu kuendelea na imani zao. Mfano baada ya kushinda na kuuchukua mji ambao ulikuwa umeimarika kwa ukristo mji wa Constantinople, mfalme wa Ottoman alitangaza kwamba wakristo wanaruhusiwa kurudi na watapewa makazi ya bure pia alichukua kanisa la kirumi akaligeuza msikiti akajenga soko moja hatari la kibiashara akaugeuzwa mji kitovu cha biashara.
Na kati ya vitu vilivyo fanya dola kupungua nguvu moja wapo ni kuacha utaratibu wa kuwa na vimada wakaanza kuoa na kuacha utaratibu wa kuaa ma prince. Kumbe utaratibu wao wa zamani ulikuwa wa kishenzi sema uliisaidia dola kuendelea kuwa imara....
 
Mimi naipenda sana tamthilia ya
Sultan inaoneshwa azam two,nmekuwa nikiwasikia watu wengi wakiidharau na hapa jukwaan watu wanasema ni ya kidemu ila kwa mtu mwenye akili kama wewe nnauhakika ungeipenda maana ulichokiandika ndicho kinachoigizwa..asante kwa kushare.
 
Mimi naipenda sana tamthilia ya
Sultan inaoneshwa azam two,nmekuwa nikiwasikia watu wengi wakiidharau na hapa jukwaan watu wanasema ni ya kidemu ila kwa mtu mwenye akili kama wewe nnauhakika ungeipenda maana ulichokiandika ndicho kinachoigizwa..asante kwa kushare.

Hata mimi naipenda sana mkuu..
 
Documentary waaapii??? Wewe mwanaume wa Dar free market umeangalia sultan
Usikalili hiyo tamthlia sijawahi kuitazama siyo kwamba naidharau ila ni kwamba kingámuzi nianchotumia hakina hiyo channel otherwise ningeitazama. Neno langu siyo sheria na wala sikulazimishi kuamini..............
 
Hahahah Heron eti "Rubbish" Hahaha!! takataka
 
Back
Top Bottom