Ccm msipowaelewa mtapata shida sana. Kuanzia mwenyekiti wao na kila mtu wanajua kwenye ballot boxes walishapoteza miaka mingi. Hawana uwezo wa kushinda kwa kura na ndiyo sababu hawanashida wala mpango wa kufanya uchaguzi zaidi ya changa la macho ili wahalilishe utawala kwa kutumia majeshi kama wlaivyofanya kwa magufuli.
Kinachorudiwa Zanzibar siyo uchaguzi. uchaguzi ni lugha ya kuuhadaa ulimwengu lakini lengo kubwa ni kuchukua utawala wa nchi kwa jina la kura lakini nguvu ya majeshi.
Swali la kujiuliza, kwa nini ccm inalazimisha utawala wa mabavu wakati watanzania hawaitaki? Kwa utawala huu wa mabavu huku wakijua wananch hawawataki, kweli ccm itakuwa na dhamira safi ya kuwatumikia wananchi? Hilo liko dhahiri. hata kikwete alipofanya kampeni ya yeye, mkewe na mtoto, akahalalisha uraisi, mnajua nyote kwamba alitawala kwa maslahi ya familia. Vivyo hivyo utawala wa mabavu wa ccm hauwezi kuwa ni kwa maslahi ya uma kwa sababu uma wa Tanzania ni zaidi sana ya ccm na uma ndiyo hauitaki baada yakuwa si imeshindwa tu bali bila imegeuka na kuwa zimwi la taifa.
Kinachotafutwa ni matumizi ya nguvu kujitangazia ushindi. Je majeshi yetu yataendelea na utii katika missions za kiharamia hivi hadi lini? Ni kweli wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi hayana dhamira, utu wala uchungu kwa taifa? Na kwamba yamefanywa misukule ya ccm na yataendelea kuwa vile kwa muda gani? Hili jibu lake sina.
Je Watanzania ambao ndio wananchi wanaolipa kodi zao ili kuendesha serikali dharimu ya ccm, na kulipa mishahara ya watanzania wanofanya kazi katika majeshi yetu, na kununulia silaha ambazo ndizo zinawaua Watanzania na kuwatishia ili waendelee kuwa chini ya maharamia ccm, wataendelea kutishika na kutiil huku wakilia machozi?
Kuna binadamu ambaye uvumilivy wake hauna kikomo? kikomo cha uvumilivu kikifika ccm na hao agents wake watakuwa katika hali ya furaha na ubwanyenye walionao?
Tuendeleeni kujadili huku tumeweka miguu kwenye maji ya baridi ili macho yetu yaone kile kinaijilia Tanzania kwa uharamia wa ccm.