Othman: Shein akae pembeni, Jaji Mkuu aongoze Zanzibar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Othman-Masoud-Othman-620x308.jpg

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Othman Masoud Othman

MWANASHERIA Mkuu wa zamani wa Zanzibar, Othman Masoud Othman ametoa rai mpya ya kuondoa mkwamo wa kisiasa unaoikabili Zanzibar, akisema haiwezekani wananchi kuingizwa katika kinachoitwa “Uchaguzi wa marudio.

“Kule kwetu Pemba wanasema arudiwae ni mke. Uchaguzi haurudiwi kwa sababu mpaka sasa wananchi tuliopiga kura Oktoba 25 hatujaelezwa kwani kilichotokea ni nini hata uchaguzi ukafutwa. Hivi uliofutwa ni uchaguzi au matokeo ya uchaguzi?”

“Wazanzibari kuambiwa kwamba uchaguzi ulifutwa eti uliharibika ni kudanganyana. Na haifai kudanganya watu. Uchaguzi ulioharibika hauwezi kushuhudia wawakilishi na madiwani waliochaguliwa wakiwa na vyeti vyao mkononi walivyoandikiwa na wasimamizi wa uchaguzi majimboni, ilipofika siku uchaguzi ulipofutwa,” amesema.

Othman ameeleza hayo jana wakati wa kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kujadili changamoto za kisheria zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Kongamano lilifanyika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Amesema ufumbuzi wa haki kwa sasa ni Dk. Ali Mohamed Shein anayeng’ang’ania kuwa ni rais halali kukaa pembeni; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu kushika wadhifa wa urais kama Katiba ya Zanzibar inavyosema, na kuunda Tume ya kumchunguza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Amesema ni muhimu ukafanywa uchunguzi wa kina sasa kuchunguza kama uchaguzi ulifutwa kihalali. Kama ni kihalali kama wanavyoshikilia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), basi ufanywe uchaguzi mpya kwa taratibu mpya.

“Kama hakukuwa na uhalali wa kuufuta uchaguzi uliokwishafanyika kama tunavyoamini wengi wetu, turudi kwenye Katiba ya Zanzibar kukamilisha kazi iliyoachwa kufanywa na Tume ya Uchaguzi.

Amesema suala la Zanzibar kwa sasa ni sawa na busha ambalo dawa yake ni kulipasua wala sio kulitumbua kama afanyavyo Rais John Magufuli. “Hili la Zanzibar ni busha lipasuliwe tu,” amesema huku akisikitishwa na hali iliopo Zanzibar kwa sasa ya viongozi wachache kutangaza uchaguzi wa marudio sambamba na kujaza vikosi vya ulinzi na usalama nchini kote.

Amesikitishwa pia na kitendo cha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), kushindwa kutoa kauli itakayoonesha uwajibikaji wa kiutawala katika tatizo la mtu mmoja kuhujumu uchaguzi mkuu na kuitia nchi katika matatizo makubwa ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi.

“Tunaendelea kuona jinsi Tume za uchaguzi zilivyo sawa na Mkalimani ambaye akikosea tu kutafsiri alichokisikia kikisemwa ameharibu kila kitu. Hapa kuna suala la kasoro ya uadilifu upande wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Ameifanya Tume mle ndani kuwa kama Jeshi. Na kwa hapo huwezi kusema kutaendeshwa uchaguzi wa maana,” amesema Othman ambaye alifukuzwa uanasheria mkuu wa serikali mwaka juzi baada ya kukataa ibara za Katiba Inayopendekezwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma.

Bali Othman pia amesikitika kuona kwamba baadhi ya wanasheria wenye uelewa mpana wa mambo, wanafanya upotoshaji wa vifungu vya sheria na katiba badala ya kuweka wazi kila kitu kwa lengo la kusaidia jamii.

Amezungumzia wanasheria waliotoa maoni kwa kuvizonga vifungu vya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya mwaka 1984 ya Zanzibar kwa mtizamo wa kuhalalisha alichoita vurugu za Jecha na waliomtuma kusema uongo.

Amesema Jecha mwenyewe amekiri mbele ya makamishna wa Tume ya Uchaguzi kuwa alilazimika kusema uongo kwa “vyombo” ambavyo hajavitaja waziwazi. Alitoa kauli hiyo ya kukiri kusema uongo alipokutana na makamishna Novemba mosi, 2015, alipojaribu kutafuta kuhalalisha haramu aliyoitenda siku tatu kabla, tarehe 28 Oktoba 2015, alipojificha na kuibuka kwenye televisheni kutoa tangazo la kufuta uchaguzi mkuu.

Chanzo
: Mwanahalisi
 
Kitu binadamu alichofikiri na kukifanya kwa usahihi kinakuwa ni bora sana kuliko chakula kitamu ulichokula muda uliopita.
Nia aibu kwamba Tanzania tumeamua kutelekeza fikra na mawazo sahihi kwa ajili ya njaa na uroho wa matumbo yetu!
 
Asome katiba ya Zanzibar inasema Raisi aliyeko madarakani ataendelea kuwa Raisi hadi mwingine atakapochaguliwa na kutangazwa na tume ya uchaguzi.Huyu mwanasheria alitaka Raisi aachie madaraka baada ya Seif SHariff Hammad kujitangaza kuwa raisi?????????????? Kwani Seif ni tume?
 
Ccm msipowaelewa mtapata shida sana. Kuanzia mwenyekiti wao na kila mtu wanajua kwenye ballot boxes walishapoteza miaka mingi. Hawana uwezo wa kushinda kwa kura na ndiyo sababu hawanashida wala mpango wa kufanya uchaguzi zaidi ya changa la macho ili wahalilishe utawala kwa kutumia majeshi kama wlaivyofanya kwa magufuli.

Kinachorudiwa Zanzibar siyo uchaguzi. uchaguzi ni lugha ya kuuhadaa ulimwengu lakini lengo kubwa ni kuchukua utawala wa nchi kwa jina la kura lakini nguvu ya majeshi.

Swali la kujiuliza, kwa nini ccm inalazimisha utawala wa mabavu wakati watanzania hawaitaki? Kwa utawala huu wa mabavu huku wakijua wananch hawawataki, kweli ccm itakuwa na dhamira safi ya kuwatumikia wananchi? Hilo liko dhahiri. hata kikwete alipofanya kampeni ya yeye, mkewe na mtoto, akahalalisha uraisi, mnajua nyote kwamba alitawala kwa maslahi ya familia. Vivyo hivyo utawala wa mabavu wa ccm hauwezi kuwa ni kwa maslahi ya uma kwa sababu uma wa Tanzania ni zaidi sana ya ccm na uma ndiyo hauitaki baada yakuwa si imeshindwa tu bali bila imegeuka na kuwa zimwi la taifa.

Kinachotafutwa ni matumizi ya nguvu kujitangazia ushindi. Je majeshi yetu yataendelea na utii katika missions za kiharamia hivi hadi lini? Ni kweli wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi hayana dhamira, utu wala uchungu kwa taifa? Na kwamba yamefanywa misukule ya ccm na yataendelea kuwa vile kwa muda gani? Hili jibu lake sina.

Je Watanzania ambao ndio wananchi wanaolipa kodi zao ili kuendesha serikali dharimu ya ccm, na kulipa mishahara ya watanzania wanofanya kazi katika majeshi yetu, na kununulia silaha ambazo ndizo zinawaua Watanzania na kuwatishia ili waendelee kuwa chini ya maharamia ccm, wataendelea kutishika na kutiil huku wakilia machozi?

Kuna binadamu ambaye uvumilivy wake hauna kikomo? kikomo cha uvumilivu kikifika ccm na hao agents wake watakuwa katika hali ya furaha na ubwanyenye walionao?

Tuendeleeni kujadili huku tumeweka miguu kwenye maji ya baridi ili macho yetu yaone kile kinaijilia Tanzania kwa uharamia wa ccm.
 
Asome katiba ya Zanzibar inasema Raisi aliyeko madarakani ataendelea kuwa Raisi hadi mwingine atakapochaguliwa na kutangazwa na tume ya uchaguzi.Huyu mwanasheria alitaka Raisi aachie madaraka baada ya Seif SHariff Hammad kujitangaza kuwa raisi?????????????? Kwani Seif ni tume?
Mbona unapumua pande zote za mwili halufu mbaya hivyo
 
“Wazanzibari kuambiwa kwamba uchaguzi ulifutwa eti uliharibika ni kudanganyana. Na haifai kudanganya watu. Uchaguzi ulioharibika hauwezi kushuhudia wawakilishi na madiwani waliochaguliwa wakiwa na vyeti vyao mkononi walivyoandikiwa na wasimamizi wa uchaguzi majimboni, ilipofika siku uchaguzi ulipofutwa,” amesema.
Othman ameeleza hayo jana wakati wa kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kujadili changamoto za kisheria zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Kongamano lilifanyika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Amesema ufumbuzi wa haki kwa sasa ni Dk. Ali Mohamed Shein anayeng’ang’ania kuwa ni rais halali kukaa pembeni; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu kushika wadhifa wa urais kama Katiba ya Zanzibar inavyosema, na kuunda Tume ya kumchunguza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Amesema ni muhimu ukafanywa uchunguzi wa kina sasa kuchunguza kama uchaguzi ulifutwa kihalali. Kama ni kihalali kama wanavyoshikilia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), basi ufanywe uchaguzi mpya kwa taratibu mpya.
“Kama hakukuwa na uhalali wa kuufuta uchaguzi uliokwishafanyika kama tunavyoamini wengi wetu, turudi kwenye Katiba ya Zanzibar kukamilisha kazi iliyoachwa kufanywa na Tume ya Uchaguzi.
Amesema suala la Zanzibar kwa sasa ni sawa na busha ambalo dawa yake ni kulipasua wala sio kulitumbua kama afanyavyo Rais John Magufuli. “Hili la Zanzibar ni busha lipasuliwe tu,” amesema huku akisikitishwa na hali iliopo Zanzibar kwa sasa ya viongozi wachache kutangaza uchaguzi wa marudio sambamba na kujaza vikosi vya ulinzi na usalama nchini kote.
Amesikitishwa pia na kitendo cha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), kushindwa kutoa kauli itakayoonesha uwajibikaji wa kiutawala katika tatizo la mtu mmoja kuhujumu uchaguzi mkuu na kuitia nchi katika matatizo makubwa ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi.
“Tunaendelea kuona jinsi Tume za uchaguzi zilivyo sawa na Mkalimani ambaye akikosea tu kutafsiri alichokisikia kikisemwa ameharibu kila kitu. Hapa kuna suala la kasoro ya uadilifu upande wa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Ameifanya Tume mle ndani kuwa kama Jeshi. Na kwa hapo huwezi kusema kutaendeshwa uchaguzi wa maana,” amesema Othman ambaye alifukuzwa uanasheria mkuu wa serikali mwaka juzi baada ya kukataa ibara za Katiba Inayopendekezwa kwenye Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma.
Bali Othman pia amesikitika kuona kwamba baadhi ya wanasheria wenye uelewa mpana wa mambo, wanafanya upotoshaji wa vifungu vya sheria na katiba badala ya kuweka wazi kila kitu kwa lengo la kusaidia jamii.
Amezungumzia wanasheria waliotoa maoni kwa kuvizonga vifungu vya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi Na. 11 ya mwaka 1984 ya Zanzibar kwa mtizamo wa kuhalalisha alichoita vurugu za Jecha na waliomtuma kusema uongo.
Amesema Jecha mwenyewe amekiri mbele ya makamishna wa Tume ya Uchaguzi kuwa alilazimika kusema uongo kwa “vyombo” ambavyo hajavitaja waziwazi. Alitoa kauli hiyo ya kukiri kusema uongo alipokutana na makamishna Novemba mosi, 2015, alipojaribu kutafuta kuhalalisha haramu aliyoitenda siku tatu kabla, tarehe 28 Oktoba 2015, alipojificha na kuibuka kwenye televisheni kutoa tangazo la kufuta uchaguzi mkuu.
 
Serikali ya kihafidhina imegoma kuachia madaraka ila ss tunamtegemea Allah maana ndio anaeijua kesho, kwasababu wao wanawaza ya dunia pekee! ccm haina tofauti na firauni.
 
Jecha amesema hakutakuwa na mabadiliko ya wagombea kwenye marudio ya uchaguzi. Hii maana yake ni kwamba, mzee wa 'sawa sawa' hata asiposhiriki uchaguzi kwa hiari atashirikishwa tu!!
 
Asome katiba ya Zanzibar inasema Raisi aliyeko madarakani ataendelea kuwa Raisi hadi mwingine atakapochaguliwa na kutangazwa na tume ya uchaguzi.Huyu mwanasheria alitaka Raisi aachie madaraka baada ya Seif SHariff Hammad kujitangaza kuwa raisi?????????????? Kwani Seif ni tume?
kidudu mtu hata hicho kifungu hukijui ila ni kushangilia tu ili mradi mmeo kasema
 
Asome katiba ya Zanzibar inasema Raisi aliyeko madarakani ataendelea kuwa Raisi hadi mwingine atakapochaguliwa na kutangazwa na tume ya uchaguzi.Huyu mwanasheria alitaka Raisi aachie madaraka baada ya Seif SHariff Hammad kujitangaza kuwa raisi?????????????? Kwani Seif ni tume?
Kweli Sefu si tume,basi ieleze tume imtangaze aliyeshinda kigugumizi cha nini???
 
Tufanye sawa mwenyekiti wa ZEC ndio mwenye mamlaka yote kuhusu uchaguzi, swali langu dogo tu Je, ANARUHUSIWA KUFUTA UCHAGUZI KWA SABABU ZOZOTE ZILE BILA KUHOJIWA?

Nitoe mfano, mwenyekiti wa NEC angeweza kutangaza kufuta uchaguzi wa rais wa JMT na isihojiwe kwa sababu ndio mwenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi?
 
Kweli Sefu si tume,basi ieleze tume imtangaze aliyeshinda kigugumizi cha nini???

Imtangaze mshindi yupi? Tume katika matatizo iliyogundua ni kuwa idadi ya waliopiga kura ilikuwa kubwa kuliko waliojiandiksha daftari la wapiga kura.Mfano daftari la wapiga kura waliojiandikishakama wapiga kura ni 100.Waliopiga kura ni 800.SEIF KAPATA KURA 400 na shein Kapata kura 400.Hivi unaweza kutangaza matokeo kama hayo? Idadi ya wapiga kura hailingani na walionjiandikisha daftari la wapiga kura!! Wanazidi kwa 700 nzima!! Hilo ni tatizo moja kati ya mengi
Dawa ni kufuta uchaguzi na kuanza upya na kuwa makini kuhakikisha awamu hii kila kitu kinafanyika kwa umakini zaidi
 
napata was was sana na viongoz wa ccm wa zanzbar kama ni wa zanzbar kweli au ni mapandikizi ya bara toka enzi za mwalimu kama kweli ww ni mzazbar original uwezi kuweka nchi katika risk namna hyo Leo ikitokea vurugu unajua watakao pigwa mabomu, kubinywa pumbu, ni ndugu zako ,wajomba zako, shangazi zako, binam zako, babu zako
 
"Kule kwetu Pemba" ukimuliza mara ya mwisho kaenda lini huko kwao anakojidai atabakia na kigugumizi.
 
"...... ni nchi ya kimapinduzi, nchi ya kimapinduzi haitolewi kwa njia ya vikaratasi.... jussa..... jussa hatuitoi....hatuitoi...hatuitoi.... labda mtupindue.... hata hivyo hamuwezi kwasababu sisi ndiyo tumeshikilia dola" yule mama yule R.I.P.
 
Back
Top Bottom