Oscar Oscar: Ni kweli Tshabalala na Kapombe wamezeeka?

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
996
SIJAMUELEWA kocha wa Taifa Stars. Sijamuelewa kabisa Adel Amrouche. Nimeshangaa sana kuona timu yetu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inaitwa bila kuwa na majina ya Mohammed Hussein, Aboubakary Salum na Shomary Kapombe. Kwenye kizazi hiki Kapombe na Mohammed ndiyo mabeki wetu waliocheza michuano mikubwa zaidi kuliko mtu mwingine yeyote.
Ndiyo wachezaji ambao hata pale Simba wageni wote wameshindwa kuwatoa kwenye nafasi zao. Ndiyo wachezaji bora kwenye eneo la ulinzi wa pembeni. Sidhani kama kocha wetu mpya Amrouche ameshauriwa vizuri.
Sidhani kama wasaidizi wake na Kurugenzi ya Ufundi kama wamefanya kazi yao sawasawa.
Tanzania inataka kufuzu kwa mara ya tatu kwenye michuano ya Afcon, lakini inakwenda vitani bila askari wake wenye uzoefu. Tanzania inakwenda vitani bila wachezaji wake bora wa kulia na kushoto kwenye eneo la kujilinda.
Amrouche amejiweka mwenyewe kwenye mtego. Hakuna kitu kingine anachoweza kuwapa Watanzania wakamuelewa tofauti na kufuzu fainali za Afcon. Taifa Stars ikishindwa kupata matokeo mazuri, tayari kocha ameshawapa watu sababu.
Kapombe na Tshabalala bado tunawahitaji sana kwenye kikosi cha Taifa Stars. Nilidhani Amrouche amepata nafasi ya kutazama hata mechi zetu tatu za Stars zilizopita.
Nilidhani Amrouche amepata nafasi hata kutazama mechi za Simba dhidi ya Vipers ya Uganda kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Sidhani kama kocha amewatazama vizuri wachezaji hawa. Sidhani kama alipata nafasi. Tumeita wachezaji wengi sana wanaocheza nje ya Tanzania, lakini tumepata nafasi ya kufuatilia maendeleo yao huko nje hivi karibuni? Sina hakika.Mchezaji anaweza kuwa anacheza soka nje ya Tanzania, lakini kwa kiwango cha kawaida. Nadhani ni muda sahihi sasa kwa kocha kuanza kutembea na kuwaona wachezaji wakiwa na klabu zao. Kuna muda nahisi tunawaita tu. Kuna muda ni kama tunawaonea aibu. Timu ya taifa sio mahali ambapo kila mtu anacheza. Ni mahali ambapo walio bora tu ndiyo wanaitwa. Kumuacha Kapombe na Tshabalala sidhani kama tumewatendea haki. Kumuacha Tshabalala na Kapombe sidhani kama tumejitendea haki hata sisi wenyewe. Wachezaji wa aina hii huwa hawaachwi tu kama mahindi. Huwa kunakuwa na sababu za msingi ambazo wananchi wanapawa kuelezwa. Mohammed Hussein na Shomary Kapombe ni wachezaji wakubwa huwezi kuwaacha tu bila walau kuwajuza Wananchi sababu za kuwatema kikosini.
Kama kocha mgeni ameweza kumuona David Luhende akiwa Kagera Sugar hawezi kushindwa kumuona Tshabalala pale Simba.
Ukitazama vizuri kikosi chetu unapatwa na wasiwasi mkubwa juu ya leo na kesho yetu. Kapombe anapaswa kucheza leo, ameachwa. Clement Mzize anapaswa kucheza kesho, ameachwa. Tunahitaji matokeo mazuri leo lakini tunahitaji kuandaa vijana wa kesho.
Kwa kiwango ambacho Mzize amekionyesha hivi karibuni akiwa na Yanga nilidhani anastahili kuitwa timu ya taifa. Amrouche ana kazi kubwa. Kitu pekee ambacho kitamuweka salama ni ushindi.
Haya malalamiko yote huwa yanazimwa na matokeo mazuri. Hakuna mtu atamkumbuka Tshabalala kama Uganda watafungwa. Hakuna mtu atasikitika kuachwa kwa Kapombe kama timu itashinda. Unapoacha wachezaji wakubwa kama hawa ni kama kujivisha mabomu. Muda wowote Amrouche anaweza kulipuka. Ni muda wa kuanza kuwaandaa kina Kelvin John na Mzize. Hawa vijana kucheza na gwiji kama Mbwana Samatta inasaidia sana kwenye ukuaji wa vijana wadogo.
Ni kweli Kapombe na Tshabalala wamezeeka? Majibu yote nadhani yako kwa kocha wetu mkuu, Amrouche. Nimetazama eneo la kiungo sijaona jina la Aboubakary Salum “Sure Boy”.
Huyu nadhani alistahili pia kuwa sehemu ya kikosi. Huyu ni kiungo fundi kutoka kwa Wananchi ambao wamekuwa bora sana siku za hivi karibuni.
Kocha wetu Amrouche amefanya uamuzi mgumu sana ambao anatakiwa kueleweka kwa kufuzu kwa michuano ya Afcon.
Timu yetu iliyoitwa imeacha wachezaji wengi ambao wamekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni.
Zawadi pekee ambayo Watanzania wanatakiwa kupewa na Kocha Amrouche ni ushindi dhidi ya Uganda. Wachezaji kama Kapombe, Tshabalala, Mzize na Sure Boy wote walistahili kuitwa Taifa Stars, lakini tunaheshimu uamuzi wa kocha.
Uganda ndilo taifa lililoshiriki michuano ya Afcon mara nyingi zaidi kuliko nchi yoyote ile kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Tuna mechi ngumu sana, lakini kocha wetu anaweza kutupigania. Mara ya mwisho tulipofuzu kwa fainali za Afcon tuliifunga pia Uganda. Kocha kafanya uamuzi mgumu, lakini naamini tutapata matokeo mazuri kwa kuifumua Uganda. Kila la heri Taifa Stars.

Credit: Mwanaspoti
 
Mi ni mchambuzi Utopolo Lia Lia japo nadhani ninaeipenda Taifa Stars kuliko hata Utopolo yangu.

Nimeshaanzisha uzi nyingi kuhusu Taifa Stars.

Na ni Mimi nilishauri humu jukwaani nikataja kikosi na kumuomba kocha mpya hao wazee wasiwemo na nimefurahi sana Kocha Adel amesikia.

Iko hivi zama hizi Kapombe na Tshabalala ni uchochoro kwasasa hawajitumi tena Timu ya Taifa kama wafanyavyo wakiwa Simba.

Wakiwa Taifa Stars Huwa hawapandi kupiga krosi na kushuka kama wafanyavyo wawapo Simba.

Hawa ni mzigo maana Timu ya Taifa wameizoea sana kama ya mjomba wao wanapigwa matobo tunafungwa ovyo Wala hawajali na haiwaumi. Hawa jamaa ndio shida pale Taifa Stars pamoja na Mzamiru.

Angalia Kibu Denis akicheza Taifa Stars anapambana mpaka sisi utopolo tunamshangilia.

Poleni sana Simba ila ziko beki Bora kama Manyama unaona kabisa jinsi anapambana, kibabage, kichuya, Ndemla etc
 
Datius peter Moja ya fullback 2 mzuri kwa msimu wa pili mfululizo..Tokea akiwa polisi tz alikuwa na kiwango kizuri Hadi Kagera wakamsajili.yupo offensive na anakaba


Yahya mbegu Moja ya fullbeki 3 ninayemtabiria makubwa mbeleni tokea polisi tz alifanya vizuri Hadi geita wakaona kipaji chake na bila shaka Sasa hv aidha ihefu au singida wamemsajili


Nimemkubali sana kocha kwa.kuwaita hawa mafullbeki
Hakika hapa tumepata kocha haswa ukiwa unajuwa mpira hawa jamaa wamekuwa na consistency Kwa mwaka wa pili mfululizo au 3 na ukiwatizama wakicheza utaona ubora wao ..
 
Mi ni mchambuzi Utopolo Lia Lia japo nadhani ninaeipenda Taifa Stars kuliko hata Utopolo yangu.

Nimeshaanzisha uzi nyingi kuhusu Taifa Stars.

Na ni Mimi nilishauri humu jukwaani nikataja kikosi na kumuomba kocha mpya hao wazee wasiwemo na nimefurahi sana Kocha Adel amesikia.

Iko hivi zama hizi Kapombe na Tshabalala ni uchochoro kwasasa hawajitumi tena Timu ya Taifa kama wafanyavyo wakiwa Simba.

Wakiwa Taifa Stars Huwa hawapandi kupiga krosi na kushuka kama wafanyavyo wawapo Simba.

Hawa ni mzigo maana Timu ya Taifa wameizoea sana kama ya mjomba wao wanapigwa matobo tunafungwa ovyo Wala hawajali na haiwaumi. Hawa jamaa ndio shida pale Taifa Stars pamoja na Mzamiru.

Angalia Kibu Denis akicheza Taifa Stars anapambana mpaka sisi utopolo tunamshangilia.

Poleni sana Simba ila ziko beki Bora kama Manyama unaona kabisa jinsi anapambana, kibabage, kichuya, Ndemla etc
Tena mngemuambia huyo kocha, awaache wote wachezaji wa simba, hata sio shida zetu.
 
Tena mngemuambia huyo kocha, awaache wote wachezaji wa simba, hata sio shida zetu.
Mshukuru tu hata kuwaita hao 3! Ningekuwa mimi ndiyo kocha, hata magolikipa wenu wawili ningewapotezea tu.

Timu gani inamtegemea mchezaji mmoja tu! Asipokuwepo Chama ndiyo basi tena.
 
Back
Top Bottom