Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

K sal ft ferooz Mwana mkiwa

Hii ngoma ilivuma sana miaka ya 2000, baadaye K sal akatoa ngoma ingine aliofanya na Mandojo & Domokaya inayoitwa starehe na fedha ila haikufanya pouwa baada ya hapo kimya hadi leo

Kali P - Imekaa vibaya

Baada ya hii ngoma sijawahi mskia tena huyu jamaa mpaka leo

Kalapina - Mstari wa mbele

Hili dude la Mwana kikosi cha mizinga ni kali sana, na mpaka leo Kalapina hajawahi tena hit nyingine kama hii, ngoma zote zilizofuata ni average

K basil - Ridhiki

Ni moja ya nyimbo pendwa kwa wakati ule, ila jamaa hakufanikiwa kutengeneza Hit song nyingine mpaka leo

John mjema - Wachumba 30

Jamaa alitoa hit song moja, mpaka anafariki hakuweza kutoa ngoma ingine kali

Ziggy D -Eno mike

Hii ngoma ilivuma sana kipindi imetoka naweza kukiri ni moja ya ngoma nnazopenda hadi leo, ila Ziggy dee hakufanikiwa kutoa ngoma ingine kali kama hii

Fresh P ft Juma Nature Tina

Jamaa alitamba sana mwaka 2006 kipindi hii ngoma inatoka baada ya hapo mpaka leo hajaweza kurudi tena

Richie longomba -Funguo

Hii ngoma ilikua kali sana ule mdundo sijui nani aliupiga ila ni moja ya ngoma iliyovuma sana

Ocg ft Juma nature Aqwelina

Hawa jamaa walikua watatu wakitumia herufi za mwanzo za majina yao ndo wakaunda hilo kundi walifanikiwa kutoa hit song moja iliyotengenezwa studio za Bongo record na producer alikua Soggy doggy

Rich one ft Juma nature Hatuna kitu

Huyu jamaa naona mziki anafanya kama fani tuu, alitoea hii ngoma yake moja ambayo mpaka leo hajaweza kurudi na ngoma ingine

Dolo ft Juma jature Razia

Dolo naye ni kama rich one tuu amebebwa sana na crew yake ya TMK ila uwezo wa kawaida, ndo maana baada ya radhia hakuweza kurudi tena

Mazense crew ft Juma nature - Riziki

Hawa jamaa nao walipata ngekewe kupata chorus ya juma nature ngoma ikawa kali sana ila tangu kipindi hiko hawajaweza kurudi tena

Adili -ft Mandojo & Domo kaya - Peke yangu

Huyu jamaa hii ngoma ilimtambulisha vizuri sana lakini kwa bahati mbaya hajawahi kufanya ngoma ingine kubwa kama hii

Sat B - Fagio la chuma

Hii ngoma ilivuma sana miaka ile ya 2000 baada ya hapo jamaa hakurudi tena

Univeral corner - T.shirt & jeans

Hii ngoma ilifanya watu wakaanza kuvaa T.shirt na jeans ilivuma sana ila jamaa hawakuweza kuja na ngoma ingine

Tng squard - Bongo dotcom

Hii pia ilitikisa sana miaka ile inatoka lakini hawa jamaa ni kama walibahatisha tuu

Man ex ft Duly sykes - Nimechezea bahati

Huyu jamaa alifanya hii ngoma kwa beat ile ile ya wimbo wa Bwana misosi nitoke vipi, ngoma yake ikawa kubwa sana ila hakuweza kurudi tena

Picco - Kikongwe

Huyu jamaa hii ngoma ilipendwa sana miaka ya 2002 baada ya hapo jamaa yuko chalii

Stopper ryames - Mtu tatu ndani ya track moja

Jamaa namkubali sana kwa uwezo wake ila hajaweza kutengeneza heat song nyingine kama hii

H mbizo - mpenzi wangu

Huyu jamaa baada ya kutoa hii ngoma akapotea mazima

Pingu na deso ft Mr blue - Jonita

Hawa jamaa walikua ni member wa Tiptop connection chini ya kaka yake Babu tale, the late Abdu bonge, walifanikiwa kutoa heat song moja wakapotea mazima

Dani msimano - siku nzuri
Huyu jamaa alikua ni rafiki wa karibu sana na Mr ebo & wagosi wa kaya, hii ngoma yake ilipendwa sana, ili akashindwa ku maintain akapotea mazima

Pig black - Nini mnataka

Huyu jamaa alipata bahati ya bit kali sana na ngoma yake ilivuma sana baada ya hapo jamaa akapotea

Mack dizo ft Duly sykes Suger mamy

Hii ngoma ilimtambulisha vizuri sana mack dizo ila hakuweza kuendelea kutoa ngoma nyingine kali

Alcom ft mishi - selina

Huyu ustazi ana roho safi sana watu wanaokaa kinondoni B wanaweza kumuelezea vizuri anaishi jirani na Hardman yule aliyetamba na ngoma ya Tamala,
Alcom baada ya selina hajawahi kufanya hit song nyingine

Chelea man - Msela

Huyu jamaa alishawahi kupita pale tiptop connection, alibahatika kutoa hit moja tuu hii ya msela , baada ya hapo alitoa ngoma ingine inaitwa heshim ft Afande sele ila haikufanya pouwa sana baada ya hapo akapotea mazima

Oten -Nicheki

Hii ngoma ya Oten ilivuma sana miaka ile ya 2000, baada ya hapo alitoa ngoma kadhaa zilifanya pouwa lakini hajawahi kutoa heat song kali kuifunika hii ngoma yake ya kwanza iliyo mtambulisha


JI -kidato kimoja

Ngoma ilitoka 2008 na ilifanya pouwa sana ila mwamba baada ya hapo akapotea mazima

Roho saba - Nakupenda hiphop

Huyu jamaa namkubali sana, nafaham ngoma zake nne
•Nakupenda hiphop
•Waite polisi
•stay
•Focus

Ila zote hizi hazikufikia level ya Nakupenda hiphop, nliskia jamaa ni mwanajeshi na ameacha music

Rado- Usiulize

Hii ngoma ilifanywa studio za Baucha kinondoni, ilikua ni dis truck kwa Fid q, ngoma ilisumbua sana, baada ya hapo rado alitoa ngoma zingine lakini mpaka leo hajaweza kutoa ngoma kali tena na ameshapotea

Sajna - Iveta

Hii ngoma ilifanya pouwa sana, akaja na ngoma ingine akimshirikisha Lina, baada ya hapo kapotea mazima

2 berry ft shirko - Wewe tuu

Hawa jamaa walitia hitsong moja baada ya hapo wakagombana kila mmoja akawa anafanya kazi kama solo artist, Berry black aliweza ku maintain kwa kipindi kifupi akaja kupotea , Berry white hakuweza ku maintain kabisa

Offside trick ft AT - Samaki

Hawa jamaa baada ya hii ngoma hawakufanikiwa kutengeneza hit nyingine

Amini - Bado robo saa

Amini licha ya kua THT baada ya robo saa mpaka leo hajatoa hit nyingine

Vumilia - Utanikumbuka

Huyu dada naye alipita THT, na anaonekana alitokea maisha magumu sana, alifanya ngoma kama mbili ila hii ya Utanikumbuka ndo ilimtambulisha kwenye game baada ya hapo, akatoa ngoma ingine inaitwa tatizo ni umaskini haikufanya poa sana, na kuna ngoma alifanya na Ney wa mitego pia haikufanya vizuri, akapotea mazima

Edru g ft barnaba - Scola

Baada ya scola alifanya ngoma zingine lakini hakuna iliyopenya akapotea mazima

Mataluma -Mama mbaya

Huyu jamaa naye alibahatisha ngoma moja na akapotea

Top c ft Ali kiba -Ulofa

Ngoma ilitengenezwa chini ya studio za Bob junior magomeni, ngoma ilipendwa sana hii, ila top c hakuweza kutengeneza hit nyingine safari yake ikaishia hapo

Spince ft Ali kiba - Ayaya

Huyu bwana mdogo naye baada ya ayaya hajaweza kurudi tena

Chibwa ft juru - Nishai

Chibwa anauwezo mkubwa sana nashindwa kuelewa alipatwa na nini baada ya hii nishai sijamskia tena kwenye solo project mpaka leo

Mo music - basi nenda

Jamaa alitubariki ngoma moja ya mapenzi iliyopendwa sana ila hakuweza ku maintain akapotea mazima

Juru- Mbulula

Huyu bwana mdogo wa arusha alituletea hit song moja akachimba mazima

Coyo - Itakucost

Huyu ngosha alikimbiza sana na hii ngoma, akatoa zingine zikawa average baada ya hapo kapotea

Gigy money-Nampa papa

Gigy naye alibahatisha hii ngoma moja na mpaka leo hana ngoma ingine kali kama hii

Lody music - Kubali

Huyu bwana mdogo hii ngoma aliitendea haki sana, baada ya hapo kajitahidi kurudi lakini wapi

Kontawa ft Nay wa mitego- Champion

Baada ya champion,sijawahi kuskia ngoma ingine kali kutoka kwa huyu bwana mdogo, ngoma zote anazotoa ni average, sahv kinachomfanya aendele ku rotate ni content zake anazofanya instagram ila huku kwenye music simuoni kama ana safari ndefu

Dayoo - Mwaka wa kuforce

Baada ya mwaka wa kuforce dayoo hajaweza kutoa hit nyingine mpaka leo japo anapambania nafasi

Kama kuna wengine nimewasahau ongezea kwenye comment
Waswahili - Pengo
 
Fagio la Chuma uliimbwa na kundi linaloitwa sawa na jina la wimbo huo - Fagio la Chuma.

Kuhusu Sat B, yeye ni msanii wa Burundi ambaye alitoa wimbo wenye jina linalofanana mwaka jana. Inawezekana wakati ulikuwa unatafuta kwenye Google ukaletewa matokeo ya wimbo huo wa mwaka jana, hivyo ukachanganya.


Dani msimamo ana hit nyingine - we mic


Mac Dizzo ana hits nyingine

-Cheza nami
-Baishoo , kaimba na Unique sisters
Mkuu uko vizuri, hii game ya bongo unaonekana unaijua
 
Kuna wasanii hapo walitoa ngoma kali zaidi ya moja... uwatoe kwenye list..
Pig black baada ya nini mnataka mazee, akapiga ngoma nyingine kali ft mr blue niskilize kama sikosei
dany msimamo ana ngoma nzuri zaidi ya moja
Longombaz ni ngoma zaidi ya moja.
fagio la chuma haijaimbwa na sat b, ni kundi hilo hilo fagio la chuma, uko sahihi hawakuwa na hit nyingine
Picco alitoa swaga zangu
tng squad wana ngoma nyingine pia.
Man x najaribu kuvuta kumbukumbu zinagoma kupata ngoma nyingine, japo nahisi anayo
 
Kuna wasanii hapo walitoa ngoma kali zaidi ya moja... uwatoe kwenye list..
Pig black baada ya nini mnataka mazee, akapiga ngoma nyingine kali ft mr blue niskilize kama sikosei
dany msimamo ana ngoma nzuri zaidi ya moja
Longombaz ni ngoma zaidi ya moja.
fagio la chuma haijaimbwa na sat b, ni kundi hilo hilo fagio la chuma, uko sahihi hawakuwa na hit nyingine
Picco alitoa swaga zangu
tng squad wana ngoma nyingine pia.
Man x najaribu kuvuta kumbukumbu zinagoma kupata ngoma nyingine, japo nahisi anayo
Ngoja nirudi maktaba nimskilize tena Pig black, Dani msimamo,
Hawa TNG squad hiyo ngoma nyingine nayo ilikua hit?
 
Ngoja nirudi maktaba nimskilize tena Pig black, Dani msimamo,
Hawa TNG squad hiyo ngoma nyingine nayo ilikua hit?
Tng ngoma inaitws ring on it, sijui ni step on it kama sikosei.
Pig black ft mr blue bonge la ngoma
 
Sidhani, unaonekana kabisa hiyo list umeambulia hawa wasanii watatu wa mwisho kwenye list
Wengi sana, Ferooz, Nature, Kalapina n.k nilichoshangaa kuna majina ndiyo nmeyasikia leo 🙌😂
 
Na stopa pia ako na Ngoma nyingi Kali ila hiyo mtu tatu ndani ya track moja ndio ambayo ilipigwa sana kwenye radio, na huyo mo music pia ako na Ngoma nyingi Kali ukiachana na hiyo uliyoitaja hapo, pazia jeusi na nakupenda hip hop nadhani zote ni Ngoma zenye mizania sawa...
 
Na stopa pia ako na Ngoma nyingi Kali ila hiyo mtu tatu ndani ya track moja ndio ambayo ilipigwa sana kwenye radio, na huyo mo music pia ako na Ngoma nyingi Kali ukiachana na hiyo uliyoitaja hapo, pazia jeusi na nakupenda hip hop nadhani zote ni Ngoma zenye mizania sawa...
Mkuu unaweza ukataja ngoma ingine kali ya stopper ambayo tunaweza weka hapa zikakaa kwenye mzani mmoja
 
Back
Top Bottom