Orodha ya vitabu nilivyosoma 2018

Mkuu umesahau kile cha Dr. Reginald Mengi
 
13 a monk who sold his Ferrari
 
Not yet sir.
Kuna uzi mmoja uliandikwa na jamaa anajiita LIBRARIAN nafikiri hivi vitabu viliwekwa soft copies za kumwaga.

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa ule uzi ulikuwa na title ya namna ya kudownload vitabu (sina hakika sana)
 
Mkuu hao wote wameshakuona we ndio fursa ya wao kuendelea kiuchumi.

Tajiri anaandika ili amuuzie maskini, maskini ananunua kwa kutoa hata kidogo alichonacho akidhani atapata mafanikio kama tajiri kwa kusoma mavitabu tu.

Sasa kwa vile Billgate mzungu anatoa orodha ya vitabu anavyosoma na wewe kalumanzira ndo unaiga kichwa kichwa bila kufahamu haswa siri iliyoko nyuma ya mafanikio yake.

Hao wazungu ni wajanja sana wanacheza na uvivu wenu wa kufanya kazi na kujituma.
Wanatengeneza fursa kupitia kwenu.

Nawewe anza kusoma vitabu alafu baada ya miaka kadhaa tupe mrejesho kama umefikia hata asilimia sifuri kama sio hasi ya ukwasi wa hao wanaokuandikia vitabu

Fahamu, hao ni wajasiliamali wanaandika vitabu na kukuuzia wewe masikini ili usifanye kazi uendelee kununua vitu vyao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi nisingemjibu

Mengi tu Tajiri wa Tanzania ametuandikia kitabu!
Vitabu anagawa bure?

Tangu uanze kuvisoma umesha msogelea sogelea kwa utajiri.

We kama unategemea kutoka kwa kusoma vitabu vya Mengi muulize yeye ni vitabu gani vilivyompatia utajiri.

Narudia,
Wenye muda wa kusoma mlolongo wa vitabu ni watu wavivu kufukiri na tegemezi kimawazo.

Na watu kama nyie huwa mnaiahia pabaya na misongo ya mawazo.

Acheni kudanganywa na wazungu.

Waulize vijana wangu pale kariakoo wanaokimbiza nani anasoma hayo mavitabu yenu au mwenye muda huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Mimi sidhani kama mafanikio ya maisha yanaweza kupatikana kwa kusoma jinsi wengine walivyofanya mpaka wakafanikiwa. Formula ya kufanikiwa iko moja tu: kufanya kazi kwa bidii na akili huku ukiwa na nidhamu ya matumizi. Hata hzi semina za kufundisha ujasirimali mimi sioni kama zinasaidia. Ila kusoma vitabu kwa nia ya kupanua mawazo na kuelimika ni muhimu sana sana na mtu anapata elimu kubwa kuliko hata ya darasani!
 
You are right!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu was navyo jamani mtuwekee soft copy tafadhali
Sina softcopy mkuu. Nimebahitika tu kuwa sehemu ambayo ina library zenye vitabu vya kila aina na mtu unaazima ukimaliza unarudisha. Mimi ni mpenda kusoma vitabu na huwa na enjoy mno naposoma. Ukiweza kupata na hivi soma hutajuta:
1: Born Crime -by Trevor Noah: Huyu jamaa ni comedian, chotara wa South Africa na alizaliwa kwa baba Mswiss-mweupe na mama Msouth mweusi. Ni story ya kweli na amekiita kitabu chake ''Born Crime'' kwa sababu alipozaliwa ilikuwa ni wakati wa ubaguzi wa rangi na mzungu haruhusiwi kuzaa na mweusi. Basi alivyoelezea maisha na mikasa aliyokutana nayo utacheka mpaka...Si kitabu cha kukosa.
2. Under the Bearskins -by Mark Evance: Na hiki nacho ni stoty ya kweli inamhusu ofisa mmoja wa jeshi la Uingereza aliyepekwa vitani Afghanistan. Anaelezea mikasa mingi aliyokutana nayo na experience yake ya vita. Ni moto.
3. Red Platoon -by Clinton Romesha: Ni story ya kweli ya platoon ya jeshi la Marekani iliyokuwa Afghanistan. Kambi yao ilikuwa imejengwa sehemu mbaya sana kwani ilikuwa imezungukwa na vilima pande zote. Walilalamika sana kuwa ni hatari mpaka wakuu wao wakasikia kilio chao na kuamua kuhamisha kambi. Lakini kabla hawajahamisha wakazungukwa na wanamgambo wa Taliban na ikawa na kufa na kupona. Kuna waliofariki na wachache wakapona. Mmoja ya waliopona ndiyo akaja kutunga hiki kitabu..
 
Nimesoma
Mathayo
Luka
Marko
Efeso
Wagalatia
Mwanzo
Kutoka
Zaburi (sio chote)
Kumbukumbu la torati(sio chote)
Yeremiah(sio chote)
Isaya (sio chote)
Methali (sio chote)
 

Ngoja nami nikumbuke orodha ya Picha za Ngono nilizowahi Kuziangalia hadi jana Usiku ili nitiririke na niserereke nazo hapa.
 
No 2 Na 13 unaweza kuweka hapa

 
3,4,5 unaweza viweka hapa pia nami nifaidi.
 
Mkuu hicho kitabu cha A COFFIN FROM HONG KONG kinahusu nini maana nimependa Tittle yake?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…