Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000, tasnia ya muziki wa Hiphop jijini Arusha ilishuhudia ugomvi mkubwa kati ya kundi la Nako 2 Nako lenye maskani yake Kaloleni ( Ololoo ) dhidi ya kundi la muziki wa Hiphop la Watengwa lenye maskani yake katika eneo la Kijenge Juu kipindi hicho likiongozwa na Umbwa Lutuno. Nitaelezea kwa kinaga ubaga chanzo cha ugomvi huu hapo baadaye. Moja kati ya hooks zilizokuwa zinawatumbilisha watengwa ni " huuuuuuuuuuu! katika nyimbo zao/ freestyles zao na live shows zao..Kwenye wimbo Hawatuwezi by N2N kuna mistari Lord EYEZ anasema " Game ngumu, nabadilikia humuhumu, nasukuma hiphop gurudumu nakomaa humu humu, nazidi kutema sumu, game ngumu, commercial niggaz wana pumu, mistari inawahukumu, hawajui wanachosema, kwenye show wanahema, wamechoka mapema, flows zao za KIHUUUUUUUU"
Hii ilikuwa ni diss kwa Watengwa.