Orodha ya diss tracks za kibongo, Sehemu ya Kwanza

Orodha ya diss tracks za kibongo, Sehemu ya Kwanza

Vipi kuhusu M-LAB MUSIC,TAMADUNI MUSIC ikiwakilishwa vyema na SONGA,MOKO WA MIUJIZA,6 O'CLOCK,KAD GO,AZMA,GHETO AMBASSADOR,SHASHOW,CLIFF MITINDO,STEREO,YOUNG KILLA,NIKI MBISHI mbona hawa hujawazungumzia? Esp.Niki wa II VS MBISHI,na bifu ya NAY WA MITEGO VS NIKI MBISHI VS FID Q VS BUMKUBAM WEUSI

Nitaizungumzia baadaye
 
Kwenye wimbo wa Roma 2030 kuna mstari anasema " Pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu", hapa Roma anamaanisha kuwa harakati zote alizokuwa akizifanya SUGU kwenye Anti-Virus na Vinega ilikuwa ni kwa sababu ya njaa. Roma ana tuambia kuwa Sugu alikuwa akipigania maslahi yake binafsi na sio ya wasanii wengine wa Tz ndo maana alikubali kumaliza beef baada ya kulipwa pesa na Ruge. Hapa kwa maana nyingine, Roma anatuambia kuwa Sugu ni mtu anayeweza kununulika. Ndio maana, SUGU took offence on this, alipokuwa anahojiwa na Sam Misago kwenye FNL aliuponda sana mstari huu wa Roma na kumuita Roma sio emcee.

Uongo mtupu.
 
Baadaye ya saa ngapi mkuu? Nataka kujua what you have and what the MEDIA have said so far!

Maelezo ni marefu kidogo na sasa hivi nipo busy, nadhani jumatatu itakuwa accurate!
 
Maelezo ni marefu kidogo na sasa hivi nipo busy, nadhani jumatatu itakuwa accurate!

Mkuu uko vizuri kwenye sanaa ya Bongo.....Hasa zamani ambapo alikua hanitoi mtu kwenye Redio free na Godwin Gondwe, Abubakari Sadiki Radio One....ilikua burudani kwa kweli sasa hivi wanabana pua tu.!!
 
Kilio changu - wimbo wa solothang,kuna mistari alikuwa anamdiss shigongo .....pale aliposema ''wengine wanirubuni eti nashindania gari/kumbe wameshapanga wampe nani toka awali..........sintorudia kosa hata zawadi waweke meli,waongeze ghorofa mbili wanikabidhi na shell

kweli mkuu umenikumbusha mbali sana hii nyimboSolo hapa aliumia sana na alifunguka vizzuri sana siyo mbaya wadau wakiiitia hapa Solo Thang ft. Q. Chillah - Kilio Changu | Muziki.net
 
Ila Fid Q amezidi, anakopi sana., hana tofauti na Mwana FA, unajua ni bora kuiga staili ya flow kuliko kuchukua mistari na kuitafsiri ni mbaya sana kaka. Ila nimeipenda sana hiyo diss ya Nash kwa Fid
mkuu LIKUD kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri sana uliyoifanya umechambua vitu vingi tena vya engine kuna members walikuwa hata hawajaanza kufatilia huu mziki ila kuna kitu hapa naona kuna mda unataka kuegemea sehemu kwa sababu ya mapenzi binafsi kwa sababu labda msanii humendi mfano hapa kwa fidQ inaonekana hampikiki chungu kimoja naona uachane na hii kitu wewe jikite katika kuchambua bilaa kuegemea upande wowote
Nirudie tena hongera sana umefanya kitu kikubwa sana nina imani hii itakuwa ni moja ya thread bora kabisa binafsi najitahidi kutafuta link za hizi nyimbo ila watu wawe wanazikiliza kwa ajili mjadala mpana zaidi

Kuna beef zingne unaztengeneza mwenyewe tu kwa kuelewa tofauti. Yani jay amdis fid q halaf amwite kwenye video ya same song? Rejea hapo vipi video
 
nimejifunza mengi mkuu LIKUD thanks alot na endelea kutudondoshea hayo madini usije ukaondoka nayo cuz we have no guarantee of living kwenye hii dunia ya mola wetu,leo upo kesho haupo lakini hicho unachokifanya ni hazina ya kipekee kwa vizazi vijavyo.
 
Last edited by a moderator:
Kwenye wimbo wa Roma 2030 kuna mstari anasema " Pesa ndo ilimaliza vita ya Ruge na Sugu", hapa Roma anamaanisha kuwa harakati zote alizokuwa akizifanya SUGU kwenye Anti-Virus na Vinega ilikuwa ni kwa sababu ya njaa. Roma ana tuambia kuwa Sugu alikuwa akipigania maslahi yake binafsi na sio ya wasanii wengine wa Tz ndo maana alikubali kumaliza beef baada ya kulipwa pesa na Ruge. Hapa kwa maana nyingine, Roma anatuambia kuwa Sugu ni mtu anayeweza kununulika. Ndio maana, SUGU took offence on this, alipokuwa anahojiwa na Sam Misago kwenye FNL aliuponda sana mstari huu wa Roma na kumuita Roma sio emcee.

Sugu alimwambia Roma sio wa kubishana na yeye kama anataka beef basi apambane na Sasha(binti wa sugu) ndio saizi yake...na ukiangalia ni ukweli Roma ni katoto kachanga kwa Sugu,analazimisha kujiweka level isiyo yake..
 
hizo diss ungeambatanisha na nyimbo husika ingekuwa poa xana like dis;
dis ya ECT vS TMK~piga manati
TMK halisi Vs ECT~lakuvunda
Ni mtazamo2 raia mcjenge chuki.
 
Dah heshima sana Mtu mzima, kwa kuweka kumbukumbu za Game yetu! Nimependa sababu una data sana unaifuatilia game.
Thanks a lot Mkuu...

Ila wakati mwingine hizi diss za kuchukua mstari mmoja tu kwenye track inakuwa sio nzuri sana labda huo mstari uwe dhahiri kabisa kwa kutaja jina la Emcee mwingine au kuhusianisha kitu moja kwa moja. Ila still diss ni diss tu.

Diss tamu ni zile za mtu anakutungia nyimbo kabisa kama "Kiraka Uso wa Mbuzi aka Rado" alivyomshukia Fid kwenye "usiulize".....
Pia kuna zile diss za kutoa mixtape maalum, nadhani hii kwa bongo iliasisiwa na Kikosi Cha Mizinga (Ya Hashimu Dogo sio hii ya Pina)
Mixtape yao ya kwanza nadhani ilikuwa mwaka 2003 kama sijakosea tena waliifanyia Arusha "Watengwa Records" ule Mzigo ulikuwa aibu asikwambie mtu, ile ilikuwa ni diss ya Industry nzima ya music ya Bongo.

Humo unampata Miraji Kikwete alimtukana sana Ruge na Clouds kuliko hata Vinega Magenge!

Diss zinatia radha sana ya game ila kwakuwa game yetu imelala basi hatufaudu, raha ya diss ni pale watu mnapeana diss kwenye records then mnakutanishwa kwenye freestyle hapo ndio inaamua nani mkali.

Hata diss za Nas na Jigga ziliishia kwenye freestyle battle ambapo Jigga alikaa....

Ukumbi wako kamanda tupe radha, nitakuwa msikilizaji hapa!
 
Hebu zungumza kidogo kuhusu hiyo mix tape ya kikosi.
 
fid q dissing kala pina
fid q dissing rado
rado dissing fid q
rado dissing ect
mwanafa dissing ect
ay dissing tmk
 
Ila nakupinga unaposema Fid anatranslate baadhi ya mmistari si kweli anachokifanya ni kuqoute na hii nikawaida kwenye game ya HIP HOP,kingine Fid is Lyrical MC,haimbi ilimradi vina vikae,anasoma sana na kuuleta huo ujumbe wa makala mbalimbali nakuufanya kuwa somo moja kwa hadhira,Fid na weza kumfananisha KRS1,Nas,Common and other real guyz in HIP HOP,angalia vijana wengi wanao kuja kwenye game bongo hasa wanao rap wanajaribu kumcopy au kukicopy anachokifanya Fidq
 
jouneGwalu

hapo kwa Miraji niomba maelezo kaka,maana baadae Pina alikuja kumdiss Miraji imekaaje hapa..!!??
 
Last edited by a moderator:
Hebu zungumza kidogo kuhusu hiyo mix tape ya kikosi.

Dah, Mkuu unanipa kibarua sana hapa kwanza hiyo kazi ni ya kitambo hata CD ina-scratch balaa, halafu nadhani nimeibiwa hiyo CD....

Pia sina mda wa kupitia track kwa track ila generally ni mixtape iliyochanganya freestyle za Hashimu "Dogo" , Kala Pina na baadhi ya washkaji wa pale Kikosini na washkaji wengine wa Atown kama "Majeruhi" na washkaji wengine wa huko Atown.

Walitoa Version nyingi ila kwenye kupatikana huku mtaani zilikuwa zinapatikana vipande-vipande mfano CD niliyoipataga Mimi ilikuwa na track kama 14 hivi ila niliiambiwa original yenyewe ilikuwa na Track zaidi ya 20.

Kwa kifupi humo pamoja na Diss, lakini ni kazi ambayo inawakilisha ustadi wa sanaa ya hiphop wa hali ya juu kwa mtu anayemjua Hashimu "Dogo" sihitaji kueleza sana basi, ila jua tu humo Hashimu ameharibu sana na amefundisha namna ya kufanya diss na jinsi ya ku-freestyle ambapo alieleza aina 3 za Freestyle... lol..!

Bado nashangaa sana game ya sasa kumtawaza Fid kama ndio eti emcee mkali wa hiphop, mweh! Game yetu hii full kupotea.

Tutazidi kushirikishana kuhusu vitu tofauti vya Game yetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom