Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

Ccm kampeni za ahadi zilishapitwa na wakati,kama zipo basi zisizidi uwezo. Hizi ahadi zimekuwa chanzo cha anguko la ccm,kwa nini utoe ahadi wakati ni wajibu wako?
 
BADO WANAFANYA FEASIBILITY STUDY, itakayofuatiwa kabla ya KUTAFUTA MSHAURI MWELEKEZI atakayefanya CONTENT DESIGN.......
Mlifikiri anatoa ahadi halisi nyie! Ahadi zake hazikufanyiwa utafiti kabla ndiyo maana kila siku wabunge wake wanalalama kwamba AHADI za RAIS,ahadi za RAIS.....na hapohapo bado ahadi za ILANI...
Tehe!
 
Mkuu ulisahau ahadi ya mshahara kwa watumishi itakuwa kila tarehe 21!
 
Mwaka 2005 Alikuja na Maisha bora kwa kila Mtanzania,hili halina ubishi lilikuwa ni changa la macho kwa Watanzania,Kama haitoshi akasema anawajua kwa majina wala rushwa,lakini hatuoni hata mmoja aliyemchukulia hatua===hii ni kutaka sifa na popularity.

-Pia alikuja na mpya ya kumpatia kila mwanafunzi Computer ambayo iko connected kwa internet, it's high time now kwa watanzania kuhoji uwezo wa RAIS wetu,ni kwamba anafanya Wa Tanzania ni wapumbavu sana kiasi kwamba hawawezi ku reason kuwa hilo sual haliwezekani???

Hata kwa wanafunzi tu wa vyuo vikuu hilo suala halitekelezeki leo anatuambia ataanza na shule za msingi,umeme ni tatizo..hivi jk anajua kuwa its only 10% ya wa Tanzania wana access na umeme na 0.05% ya watanzania ndo wanaweza kutuima computer na wana access na internet,hata kwa nchi ambazo zimeendelea kuzidi sisi hilo suala halipo,,yeye anataka kuhadaa Wa Tanzania aili aendelee kubaki madarakani!!!!!me nadhani pia JK na uwezo mdogo sana wa ku reason ndo maana hata hafikirii kuwa suala kama hilo watu wenye akili timamu hawawezi kusadiki,inahitaji mtu mwenye akili za mwenda wazimu kuamini ahadi kama hizo

By Arusha one
 
Hakika hutapata majibu labda tuulize ile 70% ya utafiti mpya wanaweza kutupatia majibu. CCM inaudhi sana.

FaizaFoxy, Simiyu yetu, Chamviga, Marcopolo, Chris Lukosi, Le mutuz Ritz na wenzao
 
Last edited by a moderator:
Hizo ahadi zote zimetekelezwa kwa 89%. Taabu ya bavicha ni kukaa vujiweni hata hamfanyi utafiti angalau wa kijinga, Acha kukaa kijiweni na kuvuta bangi ukisubiri maisha bora. Huo ni uppuzi na ufinyu wa kufikiri. Nasema sema kafanye kazi hata ya kufagia manispaa kama hutapata maisha bora. Lakini ukidanganywa na maandishi uchwata kwenye jf ukisubiri babu aende A merika ukidhani kuna lolote atakuletea uta... mapema sana. Take from me from now on fanya kazi huna mjomba CDM- HAWAKUJUI(wenye ruzuku yao cdm_,WEWE HAUMO KABISAAAAAAA. Unapoteza muda. Hiyo shilingi 500 ninayokupa unaipeleka internet jf nunua fagio anza kazi la sivyo you're finish
 
Hivi unataka tuwe mapunguani kama wewe na kuanza kukuandikia moja moja lililofanywa?

Mbona ni mengi sana kuliko hako ka List kako? Tuoneshe kwenye list yako vyuo vikuu.
 
Hivi unataka tuwe mapunguani kama wewe na kuanza kukuandikia moja moja lililofanywa?

Mbona ni mengi sana kuliko hako ka List kako? Tuoneshe kwenye list yako vyuo vikuu.

we punguani nini jk kajenga chuo gani kama siyo nguvu ya mkapa
 
Mwenye macho haambiwi tazama, mwenye njaa haambiwi kula.

Hiyo singo imepitwa na wakati.

Katika hizo ahadi tuoneshe vyuo vikuu.
 
huo si utaratibu wa chama chetu.uwongo,ushambenga,ushoga ni abaadhi tu kktk ilani yetu (CCM).Utakaa sana adi uliwe mchwa ukitegemea tuombe msamaha lakini hatuombi ng`o ,kama unataka ukweli nenda kajiunge na vyama pinzani nyambaf!
 
Ajira millioni moja ziko wapi?
Watu wote wanakushangaa na dread kwenye avatar yako.Hizo ajitra unazouliza kwani wewe hujaona punda wanavyokamatwa kwa wingi ktk mataifa mbalimbali wakiwa na shehena ya sembe, je hujasikia mauaji ya tembo ktk mbuga zetu au hujaona drama za kigaidi za na mauaji ya kina Miguu michemba.Ila ajira kubwa zaidi ya mzee wa gombe na seleka zake kwenye juisi za ikulu.
 
Sijachelewa kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya 2014.Hongereni mliouona.

Wakuu tukiwa tunajadili mambo mbalimbali yaliyotokea katika Taifa letu kwa mwaka uliopita, kama yale ya Chadema na Zitto, Rasimu ya katiba mpya namba 2, kujiuzuru kwa waziri wa Maliasili na Utalii na kufukuzwa kwa mawaziri 3 na la mwisho kifo cha waziri wa fedha Mh W.A.Mgimwa, tusisahau kumkumbusha Rais Kikwete na chama chake kuwa kuna ahadi kadhaa bado hawajatekeleza kwa wananchi.

Ahadi ya Kuunganisha Gridi ya Taifa katika mikoa ya Ruvuma na Kigoma
Ahadi hii ilitolewa kwanza Septemba 16, 2005 katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kuwa kufikia mwaka 2010 mikoa hiyo ingekuwa imeunganishwa na grifdi ya Taifa ili wakazi wake nao wanufaike na umeme wa uhakika. Ahadi hii ilishindwa kutekelezwa.Octoba 10, 2010 iliahidiwa tena kuwa wazo la kuunganisha gridi ya Taifa katika mikoa hiyo bado ipo pale pale.Ahadi hii ilitolewa mjini Songea katika uwanja wa Majimaji.Je, tujiulize ikiwa imebakia miezi 22 tu toka sasa wamefikia wapi?Je kazi imeanza kweli huko Kigoma? Maana najua Songea bado hata kukata nyasi hawajaanza ili kuweka njia ya umeme.

Ahadi ya maji eneo la Mshangano na Ruhuwiko
Siku hiyo hiyo wakisaidiana na Waziri aliyefukuzwa Bwana Emmanuel Nchimbi waliahidi kuweka maji ya bomba katika maeneo husika, na si tena kina mama kwenda kutafuta maji zaidi ya kiliometa 10.Bwana mkubwa akachombeza kuwa CCM haipo tayari kutengeneza mazingira ya kuvunja ndoa za watu, kisa mama kafuata maji mtoni.

Uwanja wa Ndege Misenyi
Katika kampeni hizo hizo za mwaka 2010 Kikwete aliwaahidi wana Misenyi kuwa atajenga uwanja wa ndege wa kimataifa kabla ya 2015. Je wana wa mkoa wa Kagera tayari matayarisho yameanza?Na je imefikia wapi kazi hii? Maoni yenu tafadhali.

Meli Ziwa Nyasa
Ahadi hii aliitoa akiwa Mbambabay na huko Mbeya kuwa atanunua meli mpya ili kurahisisha usafiri wa wakazi wake katika Ziwa Nyasa.Je mipango hii bado ipo kweli au ndio wamesahau kama waliahidi?

Machinga Complex Temeke na Kinondoni
Bila kusahau wakazi wa Dar waliahidiwa kujengewa Machinga Complex zingine katika wilaya zao maana kwa wakati huo walikuwa wamejenga pale Ilala. Sasa akasema kila wilaya itapata machinga Complex yake.

Naomba maeneo mengine waongezee kama zimetekelezwa au Zipo nusu ya kumalizika.

Naomba kwa muda tuwasahau Chadema na Zitto maana CCM kwa matatizo hayo ndio wanapata pa kujisahaulisha zaidi.Wanajua wanachi wako "busy" kujadili mambo yasiyokuwa na tija kwao moja kwa moja bali kwa watu wachache.

Nawasilisha
 
Nashukuru kwakunikumbusha ila inanifanya nilie ninapo ona mtu anashabikia ccm na ahadi zao zisizo tekelezwa kwa miaka hamusini,na maisha yanaendelea kua magumu kwa wananchi.natumia fulsa hii kuwa tahadhalisha wananchi wote kuto wapigia kura ccm walio bobea kwa ahadi zakipuzi kwa wananchi wenye shida.watanzania tuamke kwani tunaangamizwa na ccm kuiweka madarakani
 
2015 wananchi wataahidiwa kutoenda chooni maana ccm wakuwa wanaleta choo kila unapoktaka
 
Huko Ziwe victoria aliahidi kupeleka meli kubwa ka ile ya MV Bukoba,the same Lake Tanganyika. Tatzo ccn wameishatuona wehu,so wataendele kutuburuza maana ukisikia vichwa ngumu ndiyo watanzania hawaelelewi hawakomi,na wanachokera kulalamika lalamika tu. Huu ni ujinga kabisa.
 
Back
Top Bottom