Orodha inaendelea kuongezeka

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,036
Reaction score
168,673
Nã Malisa GJ
Kijana Erick Raphael Msyaliha, anayeishi Sinza (Mugabe) usiku wa tar.13/03/2017 alifuatwa nyumbani kwake na watu wanaodhaniwa kuwa Polisi ambao walimchukua wakihitaji maelezo kutoka kwake. Majirani wanasema tangu Erick achukuliwe na watu hao hadi sasa hajarejea.

Ndugu zake hawajui alipo licha ya juhudi mbalimbali za kumtafuta. Simu zake hazipatikani na hajaonekana popote wiki ya 3 sasa.

Jeshi la Polisi limekanusha kumshililia kijana huyo, kama lilivyokanusha kumshikilia Ben, na kama linavyokanusha kumshililia Roma. Familia ya Erick inaomba yeyote atakayepata taarifa za kuwepo kwake akiwa hai au maiti awasiliane na familia kwa namba 0718 105959.

Hapa ndipo nchi yetu ilipofikia. Binadamu wanapotea na serikali haioneshi kujali, ila Faru anapotea serikali inatumia Mil.700 kumtafuta. Matukio tuliyokua tukiyaona Rwanda, Congo, Sudan na Somalia sasa yanatokea kwetu. Si hadithi ni kweli. Ila Mungu yupo.!!
 
tunahitaji ukombozi. ni busara tu kutathmini namna gani tujikomboe kwa amani tu, ila ukombozi unahitajika kiuchumi, kisiasa na kiusalama.
 
Wenye maono waliposema walipuuzwa, walikejeliwa,kusutwa n.a. kupewa majina.Wengine kuonyeshwa shubiri. Leo sehemu kubwa tunazinduka tumeshasafiri mwendo mrefu.je, utruzi tulipopotea njia au tuendelee kupuyanga?
 
Rais wa wanyonge anainyosha nchi..acheni kelele
 
Utaambiwa uchochezi. Ndo maana Magu anatamani malaika waje kufunga mitandao. Kuna ******* wanadhani ni zama za Nyerere kufungiana ndani kikum.... kama walivyomfanyia Tuntemeke Sanga.
 
Utaambiwa uchochezi. Ndo maana Magu anatamani malaika waje kufunga mitandao. Kuna ******* wanadhani ni zama za Nyerere kufungiana ndani kikum.... kama walivyomfanyia Tuntemeke Sanga.
 
Kwenye la Roma yaani muvi inajileta kabisaaaaaaaa, mwisho wa siku mtasikia someone is a herooo!!!

Nimenusa harufu kama yako. Nlipita kwenye page ya instagram ya mtu mmoja anaitwa sijui babu tale. Aliyoyaandika akimuomba bashite awasaidie nikajua hapa kuna bonge moja la kiki inanukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…