Actually ni suala la mitazamo, wale jamaa ni wazuri sana na wabunifu kitu ambacho wachekeshaji wengi hapa Tz hawana, ila kwa sasa umaarufu wao umepungua na hiyo ni sababu ya mambo mengi sio kufulia katika kiwango chao cha uigizaji LA hasha, sababu kubwa ni Televisheni wanayoonekana kupoteza mvuto toka kwa watazamaji, hata use nzuri kiasi gani katika kile ufanyacho lakini kama hauonekani, haupewi nafasi ni ngumu kutambulika. TBC Imepoteza mvuto hali ambayo imechangia origino komedi kutoonekana na kuanza kusahaulika, mfano sasa kipindi chao kinarushwa usiku hata siku siijui ya uhakika ila nimewahi kubahatisha kama Mara mbili kwa siku tofauti kuanzia SAA 3 usiku tena kwa bahati kwakuwa nilikuwa najaribu kuangalia chaneli na sio kukitafuta kipindi husika. Nasimama kusahihishwa ila waigizaji Wa kundi lile wako vizuri, hapa tutofautishe hisia zetu za kutoipenda TBC na kikundi cha Origino komedi. Mpoki yuko vizuri sana na wengine kina joti, na wote kwa ujumla. Hayo ni mawazo yangu tu.