Unajua kitu mnachokosea wajasiliamali wa tanzania ni tabia ya kuwaona watanzania(wateja/watumia huduma watarajiwa) kama wajinga kwa kutumia jitihada nyingi kuwanunulisha bidhaa au kuwafanya walipie huduma kwa nguvu ya ushawishi (wenyewe mnaita marketing)........bila kujua kuwa katika biashara ni jambo baya sana kumnunulisha au kumlipisha mtu kwa ushawishi wa kumhadaa akili ili wewe upate pesa halafu yeye umuache mataa........mwisho wa siku ndio maana kampuni huwa haziwezi kufika mbali maana zinabeba rekodi ya ulaghai kama sio utapeli.....
Sasa wewe mleta uzi unatuingia kwa staili ya ushuhuda wa kufanikiwa katika biashara yako lakini hata kwa mwanafunzi wa form six ataweza kujua au kutambua kuwa unatangaza kampuni fulani(si jambo baya) ila style yako imekaa kisanii zaidi kiasi kwamba unaweza kukosa wateja hivi mwanzoni tu. Kwanini usingeanza na approach nzuri ya kuitangaza direct ili uweze kuvutia wale wadau ambao wanashida ya huduma unayotoa yaani uwe muwazi moja kwa moja bila kutupiga kiswahili.........naomba ujitahidi kuufanyia kazi huu ushauri kama kweli umepania kutoka kibiashara na hiyo kampuni yako............sasa wewe unafanyaje huduma ya business consultancy halafu unakuwa msanii hivi......
Rekebisha approach.yako......business ethics hazikuruhusu kucheza na akili za watu maaana hata sheria za kibiashara zinakataa mtu kufanya biashara kwa lengo la kujipatia fedha huku aliyelipia huduma asifaidike na chochote........