OPRAS kwa Watumishi wa umma iondolewe

OPRAS kwa Watumishi wa umma iondolewe

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,953
Watumishi wa umma wenzangu hii kitu sijui nimeiandika kwa usahihi, Mimi inanikera sana, nina miaka karibu 3 sijaijaza.

OPRAS ifutwe bongo na badala yake waweke kitu kingine chenye kueleweka kitakachompima Mtumishi
Kinachofanyika kwasasa ni kukopi nakala za nyuma tu. Misingi na kanuni zake hazifuatwi.

Walioileta kutoka ng'ambo walikuwa na nia njema lakini hapa Tanzania mambo ni tofauti.

Utawakuta watumishi wanaelekezana namna ya kujaza, hii ni sawa na kusema mipango kazi hawapewi watumishi badala yake wapowapo tu.
 
Unakumta Mkuu wa Shule anawateesa walimu wake kwa mambo hayo ya kipuuzi kabisa..

Yani Ualim ni mzigo
 
Unakumta Mkuu wa Shule anawateesa walimu wake kwa mambo hayo ya kipuuzi kabisa..

Yani Ualim ni mzigo
Siyo Ualimu tuuu ni taasisi zote za Serikali Opras ni Usumbufu na lupoteza Karatasi. Mara Section 2, section 3 section 4 na Five. Ukikosea umeshaprint nakala 4 unaambiwa kaprint tena. Opras haileti Promotion ,training wala kuhamishwa kitengo.MHR walete upimaji mwingine.
 
Ni rahisi sana kujaza, anza na stratgic plan ya organization.
Ukiweka objective ngumu shauri lako. Mwisho wa siku utapata wastani wa 2 huku vijamaa vilivyoweka malengo ya kawaida vina 1.
 
Waiyache tu watu tunacopy Basi,la msingi hatujazi mwaka,unakua na copy nyiiingi,Mimi yangu nilijaza 2015 mpaka leo wakitaka nachukua copy najaza mwaka nawapa,ndenge Nini papaa! Wacha iendelee tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Performance evaluation ina njia nyingi za kuifanya, watu wanafanya kazi isipokuwa upimaji sahihi wa opras bado unachangamoto....lakini upimaji wa kiidara na ki sekta unaonekana
 
Sasa mambo yenu ya chumbani na utumishi wenu mnatuletea huku??? hoprasi mnaijua nyie.... ifanyeni huko huko, mvumilieni mume wenu msitoe ya chumbani huku unless otherwise muanze kutufundisha kwanza hiyo ndio nini....
 
Open performance appraisal system.ni njia ya wazi na ya kidemokrasia ya kupima watumishi.tatizo lako hujui kujaza,sio wewe tu watumishi wengi hawajui hata namba moja hajui.

Back
Top Bottom