kupiga kura ya NDIO kwa CCM wakati walikuwa wanakosoa mambo si jambo la kushangaa. Hawa lao ni moja, mawazo yao ni yaleyale, watu ni walewale na maono yao yatakuwa yaleyale. Hiki ni chama cha mafisadi, hawa jamaa waliingia madarakani wote wakati wa takrima, na hata kama hawakutoa takrima harufu na upukupuku wa rushwa umewapitia, kuanzia fulana, kapelo nk za kampeni zote hizo zilitokana na rushwa, na wote walikuwa nazo.
Hiki ni chama kimeongoza kuanzia uhuru (nyuma kilikuwa TANU), kimeua viwanda, kilimo kinakufa, watu wakilima wanakopwa, na kama watalipwa ujue ipite miaka na tena watapunjwa kwa kuambiwa bei katika soko la dunia ilikuwa chini, sasa nani atakuwa na tija ya kulima wakati anapata hasara. Wameua elimu, hawawathamini waalimu, siku hizi mtu kupangiwa ualimu ni kama kudharauliwa, wakati zamani mwalimu alikuwa mtu muhimu kwa jamii (sasa tija ya kufanya kazi kwa waalimu itatoka wapi), huwezi endelea kama hutawekeza katika elimu, watoto wao wanasoma nje, wakirudi ndio wanaongoza makampuni yaliyobinafsishwa na serikalini pia. Wanauziana nyumba za serikali na hata NHC, ukiuliza watasema wanashindwa kuziendesha. Watu wanakufa mahospitalini kwa kukosa huduma, wao wanatibiwa S. Africa, India na kwingineko ughaibuni, wakati hospitali kibao zinakosa kipimo kidogo sana kama "Ultrasound". Kwa kutibiwa nje tungenunua vifaa vingapi. Wanarudi majimboni ikikaribia uchaguzi...
Hawa wapiga kelele kwa njia moja ama nyingine hawanufaiki kwa kukosa mambo fulani katika TANURU la chuma wajinga. Ndio nao unawaona kelele kibao. Sasa hawa si wakombozi, wala hatutakiwi kuwashangilia wakipiga porojo bungeni, kuwang'oa hawa inabidi kuwepo na tume huru. Na tume huru ni kuwa na katiba isiyo na viraka. Ila sasa watanzania tunapiga kelele mno za ufisadi, tunasahau kuwa kelele zetu tunatakiwa kuzipiga kwa katiba mpya. bila katiba ni bure, ukifika wakati wa uchaguzi hapo tu 2010, tutabaki midomo wazi kwa kishindo kingine. TURUDINI KATIKA MSTARI WA KUDAI KATIBA, HIYO ITAONDO YOTE HAYA TUNAYOYAPIGIA KELELE.