Oppossition has abstained

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,133
0
The voting for approving the budget is underway. The oppossition has abstained! More details to follow

Asha
 
Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,133
0
The voting for approving the budget is underway. The oppossition has abstained! More details to follow

Asha

Spika achemsha. Ashindwa kupanda jina la wapinzani walio-abstain. Awaita kuwa ni sawa na ambao hawakuwepo wako Mtera.

Inachekesha sana: Wapinzani walikuwepo mkutanoni, wamepiga kura ya abstantion yeye anasema ni sawa ya watu ambao hawakuwepo.

Dr Slaa anafafanua hivi sasa kuwa duniani kuna makundi matatu ya kura:

NO

YES

ABSTANTION

Amesema ku-abstain ni ishara ya kukubaliana na baadhi ya mambo na kukataa baadhi.

Spika ameshikilia msimamo wake kuwa kura hiyo haihesabiki!
 
Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,133
0
Spika ameponda hivi sasa, amesema kuwa neutral ni........na amesema amefanya ruling.

Chacha ameingia kutaka mwongozo kwamba Malecela amevunja katiba, kwa maneno yake......ya kusema kwamba wapinzani kwa ku-abstain wameingia mitini, si sawa na walionda mtera!

Asha
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,225
MaCCM hayaelewi juu ya utaratibu huu wa kuabstain ,japo vyombo vya kieletronic vilivyopo bungeni vinaprovide hiyo choice.

Naona Wangwe anamuwashia moto MZEE MALECELA kwa kusema kuwa wapinzani hawaalikwi Mtera na katumia ibara ya kikatiba ,japo kapigwa changa la moto na spika kuwa kwenda mtera sio haki za msingi.
 
NakuliliaTanzania

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
560
0
Kwenda mtera ndo kufanyaje wajameni huenda am missing the point here?

On another note, naona bado kuna mawazo yaleeee ya chama kimoja na chama kushika hatamu na utamu hapo hapo
 
At last amefuata utaratibu:

Ametangaza kura za ndio ni 241

Kura za Abstain 35

Kura za hapana 0

Kwa kuwa wale wabunge wa CCM wamezidi 2/3 ambayo ilikuwa ni 212, bajeti ya serikali imepitishwa na bunge!

Spika amesema Malecela yuko sahihi tu kusema wapinzani wameingia MITINI, tofauti na Chacha Wangwe aliposoma kifungu cha katiba kinachoonyesha kuwa Malecela alifanya ubaguzi wa kisiasa!

Asha
 
Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,225
CHEYO kakubali ndio peke yake na hili linaashiria kitu gani?

Kwani mchana Kambi ilikaa na kukubaliana kuwa watapiga kura ya abstainance
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,874
2,000
CHEYO kakubali ndio peke yake na hili linaashiria kitu gani?

Kwani mchana Kambi ilikaa na kukubaliana kuwa watapiga kura ya abstainance

Cheyo yupo kazini sasa unauliza tena hili ?

Anyway nami J3 nitakuwa nanyi Bungeni tusaidieni kumwaga data hapa .Nimechoka kukaa Dar wacha nitafute kasafari .
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,670
2,000
Hakikisheni tunabainisha mchele na puya.
Cheyo alikuwa kwenye kamati ya madini na alipiga maji sana siku ya kuikabidhi ripoti huku akichekeana chekeana na Kikwete.
Huyu naona walimrudishia lile gorofa lake la mamia ya mamilioni liliokuwa lichukuliwe kwasababu ya kutokulipa mkopo...Huyu mapesa si mwenzetu...Leteni mambo yanayojiri hapa tulirekebishe taifa ili tusonge mbele.
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,670
2,000
The voting for approving the budget is underway. The oppossition has abstained! More details to follow

Asha

Mama Killango amepiga kura ipi?
Ya imani na mafisadi ama amerudi kwa wazalendo?
Hapa sasa ndio wakati wa kuchagua nani ni nani PERIOD.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Kwenda mtera ndo kufanyaje wajameni huenda am missing the point here?

On another note, naona bado kuna mawazo yaleeee ya chama kimoja na chama kushika hatamu na utamu hapo hapo

Mkuu,

Kwenda mtera ni kukimbia bunge .... kuingia mtini ili usijihusishe na jambo linaloendelea bungeni kama kupiga kura.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
At last amefuata utaratibu:

Ametangaza kura za ndio ni 241

Kura za Abstain 35

Kura za hapana 0

Kwa kuwa wale wabunge wa CCM wamezidi 2/3 ambayo ilikuwa ni 212, bajeti ya serikali imepitishwa na bunge!

Spika amesema Malecela yuko sahihi tu kusema wapinzani wameingia MITINI, tofauti na Chacha Wangwe aliposoma kifungu cha katiba kinachoonyesha kuwa Malecela alifanya ubaguzi wa kisiasa!

Asha

Dada Asha,

Kwani kama wapinzani wangepiga kura ya hapana ingeleta tofauti gani na hiyo ya abstain? Kuna maelezo yoyote yametolewa?
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
121,298
2,000
Inaashiria katumia haki yake ya kidemokrasia...

Haki ya kidemokrasia unaweza kuitumia vizuri na pia unaweza kuitumia vibaya, hapa Cheyo kachemsha. Miezi ya karibuni amejiweka sana karibu na CCM kwa kauli zake na matendo yake, sijui anangoja nini kuwatangazia Watanzania kwamba ameamua kurudi CCM.
 
Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
Wabunge wa CCM waliotengeneza vichwa vya habari kwa kuongea kwa ukali wakichangia hii bajeti, walisema ni nini kinawaudhi kwenye hii bajeti?

Na kwanini wamepiga kura ya ndio?

Je waliainisha kwa nini watapiga kura gani?

Kuna mtu ana hotuba nzima ya Kilango Malecela?
 
Kuhani taratibu mzee...Unakamata watu pahala pabaya!
Ila kwa utaratibu huu...Wazalendo waweza ibuka KIDEDEA!
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Wabunge wa CCM waliotengeneza vichwa vya habari kwa kuongea kwa ukali wakichangia hii bajeti, walisema ni nini kinawaudhi kwenye hii bajeti?

Na kwanini wamepiga kura ya ndio?

Je waliainisha kwa nini watapiga kura gani?

Kuna mtu ana hotuba nzima ya Kilango Malecela?

Haya maswali nasubiria kuona yatajibiwa vipi na wana ccm hapa jamvini. Hapa nilipo nawasiliana na wapinzani kujua tofauti ya kupiga hapana na kuabstain ni nini hasa na itasaidia nini kwenye bajeti hii.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Kuhani taratibu mzee...Unakamata watu pahala pabaya!
Ila kwa utaratibu huu...Wazalendo waweza ibuka KIDEDEA!

Sidhani kama watu wataanza kushikwa pabaya leo hii. Watu wamekuwa wanashikwa pabaya kuanzia zama za Bstimes lakini naona kuna wengine hadi leo wapo.
 
Makelele

Member
Sep 23, 2007
28
45
kupiga kura ya NDIO kwa CCM wakati walikuwa wanakosoa mambo si jambo la kushangaa. Hawa lao ni moja, mawazo yao ni yaleyale, watu ni walewale na maono yao yatakuwa yaleyale. Hiki ni chama cha mafisadi, hawa jamaa waliingia madarakani wote wakati wa takrima, na hata kama hawakutoa takrima harufu na upukupuku wa rushwa umewapitia, kuanzia fulana, kapelo nk za kampeni zote hizo zilitokana na rushwa, na wote walikuwa nazo.

Hiki ni chama kimeongoza kuanzia uhuru (nyuma kilikuwa TANU), kimeua viwanda, kilimo kinakufa, watu wakilima wanakopwa, na kama watalipwa ujue ipite miaka na tena watapunjwa kwa kuambiwa bei katika soko la dunia ilikuwa chini, sasa nani atakuwa na tija ya kulima wakati anapata hasara. Wameua elimu, hawawathamini waalimu, siku hizi mtu kupangiwa ualimu ni kama kudharauliwa, wakati zamani mwalimu alikuwa mtu muhimu kwa jamii (sasa tija ya kufanya kazi kwa waalimu itatoka wapi), huwezi endelea kama hutawekeza katika elimu, watoto wao wanasoma nje, wakirudi ndio wanaongoza makampuni yaliyobinafsishwa na serikalini pia. Wanauziana nyumba za serikali na hata NHC, ukiuliza watasema wanashindwa kuziendesha. Watu wanakufa mahospitalini kwa kukosa huduma, wao wanatibiwa S. Africa, India na kwingineko ughaibuni, wakati hospitali kibao zinakosa kipimo kidogo sana kama "Ultrasound". Kwa kutibiwa nje tungenunua vifaa vingapi. Wanarudi majimboni ikikaribia uchaguzi...

Hawa wapiga kelele kwa njia moja ama nyingine hawanufaiki kwa kukosa mambo fulani katika TANURU la chuma wajinga. Ndio nao unawaona kelele kibao. Sasa hawa si wakombozi, wala hatutakiwi kuwashangilia wakipiga porojo bungeni, kuwang'oa hawa inabidi kuwepo na tume huru. Na tume huru ni kuwa na katiba isiyo na viraka. Ila sasa watanzania tunapiga kelele mno za ufisadi, tunasahau kuwa kelele zetu tunatakiwa kuzipiga kwa katiba mpya. bila katiba ni bure, ukifika wakati wa uchaguzi hapo tu 2010, tutabaki midomo wazi kwa kishindo kingine. TURUDINI KATIKA MSTARI WA KUDAI KATIBA, HIYO ITAONDO YOTE HAYA TUNAYOYAPIGIA KELELE.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom