Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Huwezi kuwaza kama sisi kwa sababu tunayoyapitia kila siku huyajui....
Ingependeza sana ukifanya operesheni kwenye vichwa vya wamarekani wenzio ili watende yanayostahili...!!

Mtu unakesha kwenye internet kuandika upuuzi wako kwa lengo tu la kupotosha ukweli wa matukio...
Wengi wamechoka na suluhisho wanaona lipo kwa kuiondoa ccm.... Haijalishi inaondoka kwa stahili gani...!!!
Mzee kama unazeeka vibaya utuambie.... Hatuwezti tena kuipa ccm miaka mingine 5-10 ikiwa yenyewe imejitenga na waTanzania...!!
Umeishi maisha na ktumia pumzi yako nyingi kupambana kulaghai kuiondoa ccm...leo inakaribia kuondoka ndo unaibuka katika ubora wako kwa rangi zako zote... STAY AWAY FROM US or LEAVE US ALONE.... Shame on you..!! If you are not on our side; you are just like them - you are our enemy..!!

Wapeni waTanzania nchi yao wakiwa bado wapole na wenye shauku ya kuipata kupitia sanduku la kura.... Fanyeni hivyo haraka kwa kusoma alama za nyakati.!

ukiwa rofa kazi kweli etibwapeni watanzania nchi yao hivi akili mnazihifadhi wapi
 
Mwanakijiji hili swala umeliongelea kwa nafsi yako wewe ili uweze kuwashawishi na watu wengine hapa jf
Lakini watu wenyewe ndio hao wanakubishia
Inamaana kwa kupitia hilo inaonyesha kwamba ni jinsi gani wazo lako limefeli kwa 99%
Hilo swala achana nalo utapoteza muda na watu hawezi kuacha kumpenda lowasa na wasimpe kura kisa mwanakijiji kasema. Hilo swala ni gumu sana mwanakijiji tafuta wazo lingine la maana watu watakuelewa.

Tulieni asombe kura zote ata hizo zenu chache ndio mshike adabu nyie vijana wa Lowassa mbona mnaogopa.

Nyinyi mnalalamika mwanakijiji anasaidia CCM ila nyinyi kumsaidia Lowassa wengine mnaona noma ata kuwa straight mnajificha nyuma ya kutaka ccm iondoke.


Kama mwanakijiji kumpinga Lowassa ni kuisaidia CCM basi na nyinyi kuupigia debe upinzani ni kumnadi lowassa, kwa nini ni wazito kusema Magufuli hafai anaefaa ni lowassa nchi inamuitaji lowassa.

Hivyo yani sio mnakata viuno kwenye misimamo ya wenzenu.
 
Huwezi kuwaza kama sisi kwa sababu tunayoyapitia kila siku huyajui....
Ingependeza sana ukifanya operesheni kwenye vichwa vya wamarekani wenzio ili watende yanayostahili...!!

Mtu unakesha kwenye internet kuandika upuuzi wako kwa lengo tu la kupotosha ukweli wa matukio...
Wengi wamechoka na suluhisho wanaona lipo kwa kuiondoa ccm.... Haijalishi inaondoka kwa stahili gani...!!!
Mzee kama unazeeka vibaya utuambie.... Hatuwezti tena kuipa ccm miaka mingine 5-10 ikiwa yenyewe imejitenga na waTanzania...!!
Umeishi maisha na ktumia pumzi yako nyingi kupambana kulaghai kuiondoa ccm...leo inakaribia kuondoka ndo unaibuka katika ubora wako kwa rangi zako zote... STAY AWAY FROM US or LEAVE US ALONE.... Shame on you..!! If you are not on our side; you are just like them - you are our enemy..!!

Wapeni waTanzania nchi yao wakiwa bado wapole na wenye shauku ya kuipata kupitia sanduku la kura.... Fanyeni hivyo haraka kwa kusoma alama za nyakati.!

Hawezi kuwaza kama sisi kwa kuwa yupo nje si ndio? Ila wengine walio nje wakiandika mnachokipenda ndio wanawaza kama nyinyi ata kama wapo nje?

Kweli nyie mnaumwa unyumbu.
 
Mwanakijiji hili swala umeliongelea kwa nafsi yako wewe ili uweze kuwashawishi na watu wengine hapa jf
Lakini watu wenyewe ndio hao wanakubishia
Inamaana kwa kupitia hilo inaonyesha kwamba ni jinsi gani wazo lako limefeli kwa 99%
Hilo swala achana nalo utapoteza muda na watu hawezi kuacha kumpenda lowasa na wasimpe kura kisa mwanakijiji kasema. Hilo swala ni gumu sana mwanakijiji tafuta wazo lingine la maana watu watakuelewa.


Unafikiri ila mtu ambaye anaamini yuko sahihi angeamua kukaa kimya kwa sababu wengi wanaonekana kumbishia kuna vitu vingefanyika? Ukiwa sahihi usiogope kusimamia usahihi wako hata kama utabakia kuwa peke yako sahihi.
 
Naungana na MZEE mwankijiji. Ni keli tunataka mabadilio, lakin pia lazma tiwaze kwabmakini juu ya mabadiliko hayo tunayafanyaje!!? Ni kujitoa ufaham kusema Tz ya 1961 ni sawa na ya 2015.Naamini bado mabadiliko yanaweza kufanyika ndani ya CCM kama wapinzan bado hawajaamua kuleta mabadiliko. Hata China ilikiwa hvyo. Ni wazo tu kwa vile waamuzi ni wananchi wenye vichinjio ambao kila Moja anaamua atachinjaje. Ni ujinga pia kiamini CCM itashinda kwa asilimia kubwa au upinzan watashinda kwa asilimia kubwa kwavile kura hazipigwi na group la wanajamii forum tu. Na watu wapo katika mpambano. Then yyte anaweza kushinda ktk hili game.nashauri, tusitukanane hmu ndani kwa maana waamuzi ni watanzania watakaopiga kura. Kuhusu umri sio kigez cha kufikiri kwa usahihi MTU anaweza kuwa mtu mzima acjue anachokifanya na hata umwambie vitu vinavyoeleweka yy hatak na hashauriki. Then Oct 25 ndo kila kitu. Ukiwa one side centered utakufa kwa pressure bure cku hyo ukiambia mgombea wako kashindwa kwa kwa 20% yaan 58.5% kwa 38.5%. Tutashindwa hata kuchangia hoja humu after 25october. Good morning members.
 
Nyinyi mnalalamika mwanakijiji anasaidia CCM ila nyinyi kumsaidia Lowassa wengine mnaona noma ata kuwa straight mnajificha nyuma ya kutaka ccm iondoke.

Hiyo contradiction wao hawaioni kabisa na hawawezi kuiona kwa sababu zilizo wazi. Na mimi hapa bado sijasema "mpigieni kura Magufuli". Miye ninachosema ni kile kile nilichokisema miaka nane sasa. Lakini naonekana nimebadilika!
 
Jenerali Ulimwengu.

KATIKA mazingira ya ukinzani wa kisiasa, kila unapotokea uchaguzi, ukweli huwa unatumika kwa nadra sana, na kila upande unaohusika katika ukinzani huo hujijengea dhana yake ya hicho unachokiita ukweli, lakini ambacho kinaweza kuwa mbali kabisa na ukweli halisia.

Wanafalsafa wa kale walinena kwamba inapofumuka vita katika mazingira yoyote yale, huwa kunatokea waathirika kadhaa, lakini mwathirika wa awali katika vita yoyote huwa ni ukweli. Hii ni kwa sababu kila upande unajaribu kuunda “ukweli’ wake kwa madhumuni ya kuwafanya watu waamini kwamba upande huo ndio wenye kuelekea kwenye ushindi.

Taarifa kama hizo zikitolewa kwa umahiri na watu wanaojua kufanya propaganda za mawasiliano, huwafanya wafuasi wa upande unaozitoa kujenga imani kwamba upande wao ndio unaoongoza, na kuwafanya wafuasi wa upande wa wapinzani wao kufa moyo kwa kuamini kwamba hawana cha kutumai. Ni umuhimu huu wa propaganda katika kampeni za uchaguzi unaovifanya vyama kujali sana namna vinavyoendesha mawasiliano na umma.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hauwezi na wala hautaweza kuwa tofauti na hayo niliyoyasema hapo juu. Kwa hakika, uchaguzi wa mwaka huu unaonyesha kwamba propaganda inatumika zaidi kuliko ukweli. Ukali wa propaganda ya safari hii ni kwamba uchaguzi wenyewe unaonekana kama wa “kufa na kupona,” ukiwa na viwango vya upinzani ambao labda haujawahi kuonekana hapa nchini.

Kwa hiyo, tunalazimishwa na mazingira ya kampeni hizi kuwa waangalifu ili tuweze kung’amua na kumaizi ni nini kinasemwa na nini hakisemwi ambacho katika kusemwa au kutosemwa kwake kinageuka kuwa propaganda badala ya ukweli. Hebu tuangalie ni jinsi gani kampeni zetu zimekuwa zikienenda, na tuweze kuona ni namna gani propaganda zinatawala na ni kwa kiasi gani ukweli unaachiwa mwanya angalau kwa kiasi fulani.

Jambo la kwanza lililowekwa wazi kupitia kampeni hizi ni kwamba wananchi wanataka mabadiliko, na ndiyo maana wagombea wote wanatangaza kwamba wataleta mabadiliko. Upande wa kwanza kudhihirisha kiu hiyo ya mabadiliko ulikuwa ni ule wa Ukawa, na hali hiyo imetokana na sababu kuu mbili: Moja ni kwamba kaulimbiu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilichochukua mwelekeo huo mpya miaka michache iliyopita pale kilipotangaza vuguvugu jipya la “M4C”, au “Movement For Change”, maana yake, Harakati kwa Mabadiliko.

Ya pili ni kwamba Chadema na vyama vingine vya upinzani vilivyowakilisha ndani ya Bunge Maalumu la Katiba vilikerwa na mienendo ya Bunge hili iliyoonekana kukataa na kutaka kuitupilia mbali misingi ya Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuja kuitwa “Tume ya Warioba.” Samuel Sitta, Andrew Chenge na wenzao walionyesha kutaka kuanzisha mchakato wa kuchukua maoni ya wananchi upya na kuyadharau yale yaliyokwisha kuratibiwa na Tume ya Warioba.

Ni hatua za Sitta, Chenge na wenzao ndizo zilizozaa Ukawa, au Umoja wa Katiba ya Wananchi, na vyama vilivyoungana kwa lengo hilo vikiwa ni Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD. Lengo kuu lilikuwa ni kufanya kazi usiku na mchana ili ipatikane Katiba inayoendana na maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na kutangazwa na Tume ya Warioba. Huu ndio msingi mkuu wa Ukawa, tukiacha mambo mengine ambayo yanavitofautisha vyama hivyo vilivyojiunga kwa sababu hiyo kuu.

Ni dhahiri, basi, kwamba vyama vya upinzani ndivyo vilivyodhihirisha kwanza kabisa utashi wake wa kuleta mabadiliko ya kina yakisimikwa juu ya “Katiba ya Wananchi.” Lakini ajenda hiyo ya Ukawa imechukuliwa sasa na kampeni ya Magufuli, ambayo hata hivyo haiwi ajenda ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Inavyoelekea ni kama vile Magufuli anataka kusimamia mabadiliko bila kusaidiwa wala kupitia chama chake.

Nasema hivyo kwa sababu kama ni mabadiliko ya kweli anayoyataka Magufuli, na mabadiliko hayo hayana budi kujengwa juu ya misingi ya kikatiba, hilo halitawezekana chini ya usimamizi wa CCM. CCM imeonyesha wazi kile ambacho Jaji Warioba hakukiona alipokubali uteuzi wa Rais Kikwete kuongoza Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Ingawa Warioba hakuliona hili, ni jambo lililokuwa wazi kabisa.

Baada ya Celina Kombani (sasa marehemu) kutamka kwamba hakukuwa na haja ya kuwa na mabadiliko ya Katiba, tulifanya mdahalo pale Nkrumah Hall, chini ya mwavuli wa Chama cha Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDASA, mimi nikichangia jukwaa na Profesa Issa Shviji.

Miongoni mwa maoni niliyoyatoa pale ni kwamba hatuna mazingira ya kutuwezesha kuandika Katiba mpya, na kwamba tulihitaji kwanza kuwa na maridhiano ya kitaifa juu ya misingi ya kisiasa na kifalsafa ndipo tuweze kuandika hiyo Katiba mpya. Hili halikuwezekana kwa sababu wakuu wa CCM hawajazoea mijadala, na jambo lolote lisilozoeleka huogopwa na hao wasio na mazoea nalo.

Matokeo yake ni kwamba Warioba na timu yake wamezunguka kote, wamehangaika na wakati mwingine kukesha bila kulala, wakifanya kazi, lakini wakimfanyia kazi tajiri ambaye hakuwa pamoja nao. Mwisho wake ukaja kuwa ni kazi yao kutupwa, na wajumbe wenyewe kudhalilishwa na kutendewa kama vile walikuwa ni wahalifu: kunyang’anywa magari bila taarifa, kusitishwa ukaazi wao jijini Dar es Salaam na kufungiwa tovuti yao.

Nyanyaso la mwisho lilikuja pale Warioba alipochuuzwa na akakubali kwamba awasilishe rasimu yake mbele ya Bunge kabla ya Rais Kikwete hata hajalizindua Bunge lenyewe, utaratibu ambao sijawahi kuusikia duniani kote. Rais akachukua nafasi hiyo na kuyachanachana na kuyapondaponda yale yote yaliyokua ndani ya Rasimu ya Warioba.

Hapa, Rais Kikwete alikuwa anateua upande wa wana-CCM wenzake, yaani akina Sitta na Chenge, na siyo upande wa Warioba, ambaye pamoja na mapenzi yake makubwa kwa CCM, chama hicho hakina mapenzi yoyote kwake; mapenzi ya CCM ni kwa akina Sitta na Chenge. Waingereza husema, “Birds of a feather flock together”, wakiwa na maana kwamba ndege wanaofanana kwa manyoya yao, huruka pamoja”

Warioba angependa apate manyoya hayo, lakini hakujaliwa kuyapata, na kama angependa wakuu wa chama chake wabadilike na wawe na manyoya yanayofanana na ya kwake, hilo haliwezekani pia. Kimsingi, wakuu wa CCM, wakiwamo akina Sitta na Chenge, wanayaogopa mabadiliko kama ukoma, kwa sababu mabadiliko ya kweli yaliyojengwa juu ya misingi ya kikatiba, yataondoa fursa zao za kujipatia “vijisenti” bila kuzuiwa na katiba wala sheria iliyo wazi.

Sasa, Magufuli amechukua nembo ya Chadema ya M4C, lakini M yake inatokana na jina lake. Hajaona, ama hajali kwamba M ya Chadema haina maana ya Mbowe, Mdee, Mbilinyi wala Myinka; ni “Movement” na wala si jina la mtu mmoja.

Na hiyo ndiyo tofauti kubwa ninayoiona mimi. Magufuli amekuwa akitangaza “mabadiliko” kwa kutumia jina lake mwenyewe. Kila lipokwenda amesikika akisema “Serikali ya Magufuli itakuwa.....”, au “Tanzania ya Magufuli itajenga....,” na kadhalika.

Hii haitokei kwa bahati mbaya, bali imepangwa kwa makusudi mazima. Imekuwa ni lazima kuweka ufa kati ya mgombea John Magufuli na chama chake, kwa sababu anakijua vyema chama chake, na anajua kwamba chama hicho kimejijengea sifa mbaya ndani ya jamii.

Baada ya nusu karne ya kuendesha serikali, ni vigumu kwa yeyote anayekiwakilisha chama hicho kuahidi lolote litakalosikika kama jipya kwa wananchi. Kila ahadi inayoweza kufikirika ilikwisha kutolewa na kutelekezwa; hakuna jipya tena.

Utashi wa kujiweka mbali unaweza kuwa si mkakati wa Magufuli peke yake, bali pia na chama chake, ambacho kingependa kubakia madarakani kwa sababu zinazoelezeka lakini kingependa kuwafanya wananchi waamini kwamba huu ni mwanzo mpya, na Magufuli anaweza kuaminika kuliko chama chake. Ni kama vile, ingewezekana, Magufuli angesimama kama mgombea binafsi, lakini hili lilikwisha kukataliwa na chama chake.

Kwa hiyo imembidi achanganye kidogo kutoka huku na kidogo kutoka kule: upande mmoja ni mgombea wa chama-tawala, lakini kwa upande mwingine ni mgombea nusu-binafsi anayekikosoa chama chake na serikali aliyoifanyia kazi kwa muda wa miaka ishirini sasa. Ni hali isiyoelezeka kirahisi.

Wale wanaokumbuka, tangu siasa za vyama vingii zianze tena nchini, tulizoea kuona mabango ya kampeni za CCM yakisema “CHAGUA CCM, CHAGUA MKAPA” miaka ya 1995 na 2000 na “CHAGUA CCM, CHAGUA KIKWETE” katika miaka ya 2005 na 2010. Leo tunaona mabango yanamuombea kura Magufuli bila kukiombea kura chama chake. Kulikoni? Bila shaka ni ule ufa nilioueleza hapo juu.

Na zipo sababu nyingi za kuielezea hali hii. Mojawapo kubwa ni rekodi ya utendaji wake Magufuli. Kwa mfano, gazeti hili lilipata fursa ya kumhoji siku za hivi karibuni, na akaelekeza apelekewe maswali kabla ya siku ya mahojiano. Pamoja na kupeleka maswali kabla ya mahojiano, alishindwa kujibu maswali aliyoyaona kama nyeti.

Mojawapo ya maswali yaliyomshinda ni lile lililohusu “uuzaji” wa nyumba za serikali (uuzaji ambao kwa kweli haukuwa uuzaji bali ugawaji). Swali hilo lilimshinda kujibu pamoja na kuwa alikuwa amekwisha kupelekewa maswali kabla ya mahojiano. Hili ni suala ambalo nitalirejea wiki ijayo nikiliangalia katika mwanga wa masuala mengine yanayowahusu wagombea wakuu wa urais na wapambe wao, na jinsi kampeni zinavyoendeshwa.

Chanzo: Raia Mwema
 
NB: Video Inafuata

Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.

La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.

Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.

Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.

Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.

"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"

MMM

ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"


Program Note: Operesheni Zinduka - Episode 2 "Makosa 2 ya Dr. Slaa na 1 la Mbowe - Jumatano Oktoba 7, 2015) Stay tuned


Binafsi nahis hauna hata justification ya kutuchagulia au kutupa mawazo tumezaliw ndan ya ccm na tumekulia ndan ya ccm natumeona manyanyaso haya Mfalme katik utawala wa kinazi hawez kuw na roho ya huruma akiw katik chama hik cha kinazi Kam una moyo wa kutusaidia sisi ambao tushaaamua NJOO UISHI HUKU ili tuonje wote joto hil la jiwe Njoo tuonje wote shida hizi. Unajarbu kumtumia Dr slaa kam sehem ya tatzo il uonyesh uko neutral NIMEKUPUUZA TWENDE NA ENL
 
Last edited by a moderator:
Wagombea wako 8, Lowassa ana nini chenu kila mtu hamtaki amchague mbn za ACT hamzitaki?? hoja hujibiwa kw hoja na si ushabiki. mswada w vyama vingi uliletwa na Mw nyerere na ukapata baraka za kina kingunge leo mnamtukana kisa tu katoka kwenu, bila kumjibu hoja zake za kutofuata kanuni za chama chenu pale dodoma. Lowassa hamuwez shindana nae mngebadili mbinu ishajidhiirisha jamaa ni maji marefu sana kw viongozi wote wa ccm. anajua sn siasa. sio ushabiki anawazidi mbali wagombea wengine.watu wata chagua chama sio magufuli,na wasionaushabiki na chama watapigakura kw Lowassa.
 
Binafsi nahis hauna hata justification ya kutuchagulia au kutupa mawazo tumezaliw ndan ya ccm na tumekulia ndan ya ccm natumeona manyanyaso haya Mfalme katik utawala wa kinazi hawez kuw na roho ya huruma akiw katik chama hik cha kinazi Kam una moyo wa kutusaidia sisi ambao tushaaamua NJOO UISHI HUKU ili tuonje wote joto hil la jiwe Njoo tuonje wote shida hizi. Unajarbu kumtumia Dr slaa kam sehem ya tatzo il uonyesh uko neutral NIMEKUPUUZA TWENDE NA ENL

Mweh.. sasa kilichokufanya uingie huku na kusikiliza nini?
 
Usiwe na shaka, hakuna yeyote humu ambaye anasema atamchagua Lowassa na akanisikiliza huu mwezi halafu akaenda kumchagua Lowassa. Isipokuwa wale ambao kura kwao haina maana hasa.
Mkuu hao ambao hawatataka kusikiliza hoja zako huwa tunawaita 'stiff necked fools'...ni watumwa wa Lowassa..they have no chains around their feet, but they are not free...ni wachache, huwa hawakosekani kwenye jamii
 
MM Kwanza nikuombe uweke maslahi yako wazi,wewe kama mwandishi wa riwaya mimi kama mwandishi wa vitabu na makala tunatofautiana sana pale unapojificha chini ya uvungu wa jambo fulani na kupaza sauti,Mwanzo nilijaribu kuelewa mantiki ya makala zako sikuweza ila sasa nafahamu huyu anae jiita mzee mwanakijiji ni nani? kumbe ni mganga njaa kama wale mitume kumi na mbili wa ufisadi, Natumaini nilipokuwa naandika huku elewa nilikuwa nasemea nini ila Mwenye enzi Mungu hamfichi mnafiki tukawaona wanapewa vyeo na kunyamaza,Enzi zile za rai tuliandika baada ya watu kumpamba mtu matokeo yake walipewa cheo.Swali wewe umeahidiwa cheo gani?Karibu mwalimu forum tunaposema ukweli kwa ajili ya mama yetu Tanzania na sio uchonganishi kwa watanzania.Mungu ibariki Tanzania
 
Nimesikiliza show ya pili ni kweli Chadema imetupwa mbali sasa hivi ni Lowassa tu.

Wafuasi wa Chadema sasa hivi wanaimba kwenye mikutano huku wanazungusha mikono Lowassa mabadiliko hawasemi tena Chadema.

Kila kitu wanamuuliza Lowassa na Lowassa anawajibu niachieni mimi.

Daah!!...
 
Usiwe na shaka, hakuna yeyote humu ambaye anasema atamchagua Lowassa na akanisikiliza huu mwezi halafu akaenda kumchagua Lowassa. Isipokuwa wale ambao kura kwao haina maana hasa.
Kujiaminisha kwamba una ushawishi ni kitu kimoja, kufanikisha ushawishi ni kitu kingine.....kusema 'hakuna yeyote' ni kujidanganya mchana kweupe.....

Kutengeneza 'series' za videos ndani ya huu mwezi na kuaminisha watu kwamba kuna cha kusikiliza chenye kuweza kubadilisha mawazo yao ni aina ya makakati wa kuwafanya wazifuatilie hizo video kama zina 'substance', wakati tayari hizo mbili za mwanzo ambazo zingeonesha mwelekeo mzima hazina 'substance' yoyote......

Pia umesahau kwamba kura kutokuwa na 'maana' haimaanishi mpiga kura ameshindwa kuchagua kiongozi anaefaa.....
 
CCM namba 8 kaondoka.wewe ni nani haya ubaki huko.mwanzilishi na mmoja wa waasisi na wasimamizi wa itikadi ndani ya ccm kaona hii sio ccm tena wewe unabaki kuishabikia ni aibu.sera zile zile ,uzembe ule ule,ulaghai uleule kwa miaka yote hatujaona mabadiliko ya kuridhisha.rejea ilani zao za uchaguzi kwa mwaka 1990,1995,2000,2005,2010,na sasa 2015.sera nzuri masikioni lakini utendeaji kazi hakuna au niseme negligible(kidogo sana)
Kuna haja gani ya kuendelea kudanganywa?
Nasema ccm haifai tena.haifai hata chembe.
Tumchague LOWASA na UKAWA sasa.
 
Unafikiri ila mtu ambaye anaamini yuko sahihi angeamua kukaa kimya kwa sababu wengi wanaonekana kumbishia kuna vitu vingefanyika? Ukiwa sahihi usiogope kusimamia usahihi wako hata kama utabakia kuwa peke yako sahihi.
bwana mkubwa mwanakijiji uko sahihi na labda kwasababu mwenzetu upo marekani unakula raha na swala kama lingetokea marekani na ungewashauri wamerekani wenzako ingekuwa sahihi zaidi na watu wangekuelewa lakini sisi watu ambao tunaishi hapa bongo na tunaifahamu ccm vizuri na shida zake kuliko wewe unae ishi huko marekani hilo swala hauwezi kutushawishi tukarudi nyuma kwa maamuzi tuliyo fikiria kwa miaka 5 na zimebaki wiki mbili tu tukapige kura na ikiwapo pamoja na wewe ulitushauri kwamba tukichagua ccm tumechagua umaskini
Na sera kuu ya ccm wanasema ukitaka kuishi na mjinga milele mnyime anachotaka.

Kwa tanzania hii hamna mtu atakaa akuelewa zamani mtu alikua akumuambia ccm haifa alikua haamini lakini saizi mtu akiambiwa ccm haifai anamini kwasababu yeye mwenyewe anaona kwanza umeme hamna mara shilingi kushuka thamani nk.inakua ni ngumu sana kumbadilisha mtu wa namna hiyo kwasababu maamuzi aliyo chukua ni magumu embu fikiria watu wanakuambia ukawa hata kama lowasa angesipo patikana kugombea kupitia ukawa basi wangeweka hata jiwe nalo wange lipigia kura.
 
Back
Top Bottom