Operesheni ya Magufuli yatikisa Dar

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
magufuli-top-mikono.gif

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli

Dotto Kahindi(Gazeti Mwananchi)

OPERESHENI ya kusafisha jiji la Dar es iliyotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli imeshika kasi baada ya tingatinga kubomoa vibanda vya biashara kando ya barabara ya Dar- Morogoro, eneo la Kimara jana.
Tukio hilo lilizua taharuki kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki mabanda hayo, ambao walihaha kuokoa mali zilizokuwa ndani, bila mafanikio.

Msimamizi mwandamizi wa operesheni hiyo, Hamis Abdul alisema kazi hiyo ni endelevu na kwamba baada ya kutoka Kimara, watahamia barabara ya Bagamoyo eneo la Tegeta huku akiwatahadharisha wafanyabiashara waliovamia maeneo hayo, kuhama mara moja.

Abdul aliwataka wafanyabiashara wote wanaofanya shughuli zao katika hifadhi za barabara kuondoka maeneo hayo kwa hiari yao kuepuka hasara ya kubomolewa mabanda yao.

“Zoezi hili ni endelevu na kwamba baada tu ya kumaliza barabara hii ya Morogoro, operesheni hii itahamia katika maeneo ya Tegeta, kwa hiyo ningependa kutumia fursa hii kuwapa tahadhari wafanyabiashara waliovamia maeneo ya barabara kuondoka kabla hatujafika huko,” alionya.

Wenye vibanda
Baadhi ya waliobomolewa vibanda, walilieleza gazeti hili kuwa pamoja na kufanyika ubomoaji huo, hawako tayari kuondoka.
Walisisitiza kuwa watarudi katika maeneo yao hayo ya awali mara tu baada ya operesheni hiyo kukamilika.
Rwezaura Gerasian mfanyabiashara wa nguo na viatu eneo la Kimara mwisho, alisema Serikali imeshindwa kuwahudumia wananchi na kwamba inakiuka haki za binadamu.

Alisema kitendo cha Waziri Magufuli kutoa amri ya kuwaondoa katika maeneo hayo si cha kiungwana, kwani kinawakandamiza wananchi wa chini na kuendeleza uonevu kwa jamii.

“Sielewi lengo la Serikali yetu, maana inatenda mambo ya ajabu kwa wananchi wake bila hata huruma, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu, tunahaki ya kufanyabishara kwa uhuru katika nchi yetu, kwanini tuishi kama wakimbizi?” Alihoji Gerasian.

Zoezi hilo la bomoabomoa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Magufuli kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, kuwaondoa katika hifadhi za barabara wafanyabiasha wote waliovamia maeneo hayo.
Dk Magufuli alitoa amri hiyo hivi karibuni wakati akizindua kituo cha daladala cha Mbezi Mwisho.

Agizo la Magufuli na foleni Dar
Machi 4 mwaka huu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa stendi hiyo mpya ya mabasi Mbezi mwisho, Dk Magufuli alisema hakuna sababu ya watu hao kubaki katika hifadhi za barabara wakati sheria zipo na kusisitiza, "Hata kama mkikuta milingoti ya bendera ya CCM vunjeni."

Dk Magufuli alisema, Sheria ya Barabara ya mwaka 1987 inasema wazi kuwa mtu ambaye atakutwa anafanya biashara, kuegesha gari, kumwaga mafuta au uvamizi mwingine wa namna yoyote katika hifadhi ya barabara, adhabu yake ni faini ya Sh1 Milioni.

Alimwagiza meneja huyo kuwa Tanroads haipo kisiasa na wao wapo kusimamia sheria na sio vingine. "Mpo kusimamia sheria, acheni kupiga siasa," alisisitiza.


Dk Magufuli alitoa mfano wa wafanyabiashara wa eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam ambao wamekuwa wakikwaza ujenzi wa barabara ya Bagamoyo kutokana na kupanga bidhaa zao barabarani.

''Ukienda Tegeta watu wamepanga biashara barabarani, Mkuu wa Mkoa upo, Mbunge yupo, Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) yupo, diwani yupo, mkuu wa wilaya naye pia na wote hao wanaangalia tu, ndio Tanzania hiyo?," alihoji na kusisitiza kuwa ifike mahali sheria iachwe ifanye kazi.
 
Pinda atampiga ban tena.....

hilo ndilo tatizo letu viongozi wanaingiza siasa sana,hatuwezi fika popote pale,hao hao wananchi ndio wa kwanza kulalamika kuwa serikali haijafanya kitu kupunguza msongamano wa magari barabari,lakini inapofika wakati wa Magufuri kufanya kazi yake wanapiga kelekele

Magufuri ni bora chama chako kikufukuze lakini utuachie barabara
 
si kweli huyu ni mpenda sifa hafanyi kazi kwa sababu anajua, kinachonishangaza tunamchekea tutaingia nae chooni, Jerry Slaa you are my hero uko wapi please put this insane where he belongs,
 
sheria ni msumeno! pia busara itumike kutekeleza sheria.
 
si kweli huyu ni mpenda sifa hafanyi kazi kwa sababu anajua, kinachonishangaza tunamchekea tutaingia nae chooni, Jerry Slaa you are my hero uko wapi please put this insane where he belongs,

these are serious accusations, unaweza kutupa wasifu kiutendaji wa Jerry slaa na Magufuli? i want to know his insanity
 
si kweli huyu ni mpenda sifa hafanyi kazi kwa sababu anajua, kinachonishangaza tunamchekea tutaingia nae chooni, Jerry Slaa you are my hero uko wapi please put this insane where he belongs,

Ila baadae ucje lalama hapa kuwa nimefiwa na ndugu yangu kwa kuchelewesha na fuleni,maana nyie ndie huwa wakwanza kupiga kelekele na kutoa lawama
 
si kweli huyu ni mpenda sifa hafanyi kazi kwa sababu anajua, kinachonishangaza tunamchekea tutaingia nae chooni, Jerry Slaa you are my hero uko wapi please put this insane where he belongs,
This is serious you cant compare Jerry Slaa with John Pombe Magufuli, acheni mchapa kazi afanye kazi kwa kufuata sheria.
 
Lakini kwa nini mamlaka za manispaa zinawaacha hawa wafanyabiashara wanavamia haya maeneo? Kwa nini wasiondolewe siku ileile wanapoanza kuvamia maeneo haya?
 
Lakini kwa nini mamlaka za manispaa zinawaacha hawa wafanyabiashara wanavamia haya maeneo? Kwa nini wasiondolewe siku ileile wanapoanza kuvamia maeneo haya?


Watanzania wengi hadi Rais wameleta huu usemi kwa wakti tofauti kuwa mlikuwa wapi mpaka mtu/watu wanamaliza kufanya kitendo fulani kibaya kama kujenga sehemu isiyoruhusiwa. Yaani tunataka kugeuza mamlaka zake kama City, Tanroads, etc. kuwa za kupita mitaani kutafuta nani anafanya kosa badala ya kufanya kazi zao husika? Hawa si wavunjaji sheria tu? Mbunge wa Ubungo naye alisema watu wanaofanya biashara barabarani watafutiwe kwanza mahali pakwenda halafu ndiyo watolewe. Kazi ya kuatafuta sehemu kama hizo zipo ndani ya uwezo wake. Amefanya hivyo?

Serikali ni lazima isimamie sheria zake. Rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae aliamuru karibu kijiji kizima kilichojengwa kwa kuvamia ardhi ya serikali kivurugwe. Waliovamia walikuwa ni watu wazito na majengo yaliyojengwa pale yalikuwa ni ya gharama kwelikweli. Tingatinga zilivuruga majengo yote. Wahanga walilalama kuwa wathamasisha asihaguliwe tena kuwa Rais. Aliwajibu kuwa wafanye hivyo tu lakini yeye asingependa kuwa rais wa wavunja sheria. Alichaguliwa kuwa rais tena.
Kumbuka kuwa huyu ndiye aliyepata tuzo la Mo Ibrahim baada ya urais wake.
 
Lakini kwa nini mamlaka za manispaa zinawaacha hawa wafanyabiashara wanavamia haya maeneo? Kwa nini wasiondolewe siku ileile wanapoanza kuvamia maeneo haya?

Mpita njia

tatizo letu kubwa ni kwamba,wanasiasa huwapa ruksa wafanyabiashara hao kwa lengo la kulinda kura zao,mbunge,diwani ama mwenyekiti yupo radhi aende hata mahakamani kwa lengo la kutetea kura yake,eti wakiondolewa mwisho wa siku hawatawapigia kura

hilo ndilo tatizo kubwa sana

hata bwana mdogo Slaa, Jerry yeye anachokiangalia ni upatikanaji wa pesa za papo kwa papo,pasi kuangalia taabu na msongamano wa magari wanaoupata wakazi wa DSM
 
Bravo magufuli.tz hatuwwezi kuwa na mfumo mzuri wa barabara kama sheria zitakiukwa kila siku.ni ajabu sana mtu anapotekeleza sheria analaumiwa. Wakati wa ujenzi wa barabara inayoanzia ubungo tanesco(ubungo maziwa) via kigogo,jangwwani to kariakoo inaanza kujengwa,eneo la kuanzi pale mabibo mwisho anzia pale relini karibu na marie stopes mpaka eneo la shungashunga(junction ya njia ya kwenda external mandela road) bomba la ges la Songas lilikuwa limefukiwa eneo la barabara na ilichukua muda sana kulihamisha,sasa jiulize wakati wanachimbia bomba hilo hawakujua ni eneo la barabara? Au kwa sababu waliona ni eneo la wazi tu wakaamua kuchimba mitaro na kufukia bomba ilimradi kazi imeisha. Ni lazima sheria za hifadhi za barabara na za mipango miji zizingatiwe.hatuwezi kuwa na barabara nzuri na miji mizuri kama kila mtu atakuwa anajiamulia kujijengea kibanda kila sehemu anayotaka ilimradi afanye biashara.
 
Back
Top Bottom