Pole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!Tatizo akiona wafuatiliaji wamekuwa wengi anaanza kuringa, mara ana majukumu, mara anaumwa halafu baadae anasema inauzwa.
Hujanikwaza mkuu ila nimesema nionavyo mimi, sijui nikoje lakini mimi ni mtu ninayeamini katika taarifa kuwa ukianza kupost hadithi sema kabisa utaweka mpaka sehemu fulani halafu utauzaPole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!
Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.
Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.
Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!
Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..
Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.
Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.
Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.
Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!
Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.
Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.
Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.
Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....
Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!
Nisameheni wote niliowakwaza!!
Haitoisha ndugu kumchangia mda wake na mb zake,,yatupasa zikibaki sehem tatu au nne tumchangie Sawa mkuu ujue huyu mtunzi tofauti na wengine yeye huwa haizidi buku tatu au mbili na mpaka Mia tano huwa anatuuzia.Ila wengine mpaka elfu tano na kuendelea wanatuuzia vipandeItaisha au itahamia wasap?
Saluti komlediPole Sana kama huwa nakukwaza hadi uone naringa kiasi hicho!!
Pia nisamehe kwa maringo yangu yanayokukwaza!!.
Tazama sehemu ya tatu jana nimejitahidi kuiposti saa saba usiku nadhani utaelewa kwa nini iwe huo muda wewe ukiwa umelala.
Lakini nisamehe pia kwa kuwa huwa naipeleka whatsapp wakati wewe unataka usome bure kabisa bila hata kunitumia vocha ya kukwangua nijiunge ili usome!!
Lakini pia naomba nikuulize upo nchi gani ambayo huwezi kupata mia tano tu (500) ya kununua riwaya mwanzo mwisho?.
Huna whatsapp tumia email, huna email tumia whatsapp..
Nchi yoyote Duniani unaweza kunitumia na nikapata mia tano tu, au elfu moja ikizidi sana huwa elfu mbili.
Na mwisho nikukumbushe kuwa hii ni kazi kama kazi zingine wala si kufurahisha watu bure, ndo mana ili uandike lazima ufanye utafiti kwa kina ikibidi usafiri mkoa au nchi kutafuta ukweli wa kile unachotaka kuandika.
Nadhani umeona kuna mdau huko juu kanitisha kwamba naandika vitu deep sana, unadhani nikiandika kwa kukurupuka bila tafiti nitapata vitisho hivyo ambavyo watu wanakuja hadi pm kuniomba nipunguze ukweli katika riwaya zangu hizi? Unajua garama inayotumika hadi naandika kitu kinachokuvutia bila kukutoa kwenye reli ya usomaji?.
Lakini dada yangu nikwambie kitu, duniani hakuna kitu cha bure na ndo mana hapa Jf unanunua vocha na bado google wanakulipia ili uingie bure kwa kuwa wanamlipa Melo. Kama wasingekuwa wanamlipa basi tungeingia kwa kulipia kama zilivyohuduma zingine duniani za kupata habari!!!
Narudia tena kukuomba radhi kama nimekukwaza ama nimekwaza yeyote kwa utaratibu wangu huu, ila hii ni kazi kama kazi zingine na ndo mana ina hati miliki kila kazi unayoona naweka hapa na huko pia nalipia ili kulinda kazi yangu.
Hivyo nisamehe bure kwa maringo yangu yanayokukwaza lakini jifunze kuheshimu kazi za watu bila kutoa lugha ya kuudhi ama kukera. Wapenzi wa riwaya hawana lawama wanajua ugumu wa kazi na faida wanazopata kwa kusoma kazi za wengine!!.
Afu mi niko poa Sana sema gubu lako tu, mimi wengi nimekuwa nawapa bure kama hawana pesa!! Waniomba kistarabu tu nawaelewa!!
Wapo hapa labda watakupa ushuhuda wa vile nilivyo.
Lakini pia kuna wezi wa kazi za watu, ukiweka hadi tamati anachukua na kuwek kwenye page yake au blog na kuuza! ....
Nimeamua kukujibu kirefu ili unielewe na wengine wenye kuniona nina maringo nao wajue kwa nini ipo hivyo!! Hakuna mwandishi anaetoa bure siku hizi,hii ni kazi kama kazi zingine!!
Nisameheni wote niliowakwaza!!
Nilitaka kuuliza hivihiviItaisha au itahamia wasap?
Saafi...endelea mkuuRIWAYA; OPERESHENI KUKU (KUFA KUPONA)
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA TANO
Adha kwake ilikuwa ni hawezi kujipangusa kwa kuwa mikono ilifungwa.
Lakini ilikuwa ni mara mia zaidi usumbufu wa mende na mbu kuliko alichokutana nacho Sami.
Sami alikutana na kundi kubwa la nge na walianza kushambulia miguu yake huku wengine wakipanda kuwahi nafasi kwenye kwapa na sehemu zingine za mwili.
Sami alipiga kelele za maumivu huku kelele zile tena zikigeuka kuwa kero kwake mwenyewe kwa kuwa hazikwenda mbali kwa ufinyu wa shimo alilokuwamo.
Angefanya nini wakati mikono imefungwa!!!
***
Kila mmoja alipiga kelele kwa uweza wake huku kila mmoja akijitahidi kujizuia kwa kujitikisa tikisa ili lau aweze kuondoa wadudu wale waliokuwa wametumwa kufanya yale waliokuwa wanayafanya.
Bado ilikuwa heri kwa Kakere kuliko kwa Sami ambae sumu ya nge na maumivu yake vilizidi uwezo wa ubongo na kujikuta akianza taratibu kupoteza fahamu bila kupenda huku maumivu yakiwa kedekede mwilini mwake.
Kakere yeye alizidi kupata adha ya kuliwa na mbu huku mende wakijaribu kunyonya ngozi iliokuwa imegandiwa na jasho lenye chumvi chumvi na kumwachia maumivu yasiosemekana.
Ilikuwa ni kulia hawezi Kia sababu sauti yake ilirudi kuwa kero masikioni mwake bila kupenda!
Ilikuwa ni lazima aishie kukugumia tu kama fisi anaefika mshindo.
Kitu kimoja pia alifikiria namna ambavyo mbu walikuwa wanamshambulia kwa kupokezana na ni kama vile walikuwa wanafundishwa kazi ile ya kumla mtu ngozi yake.
Mende na mbu walianza kummaliza nguvu za mwili kwa kazi waliomfanyia lakini pia kutokwa na jasho jingi kulimpunguzia ufanisi wa mwili kufanya kazi na akabaki kama mlevi aliepigwa denda na mtoto mchanga.
Hakujua itachukua muda gani kuondolewa kwenye shimo lile na hakuwa na hakika kama Sami nae alikuwa anapitia adha kama ya kwake kwa kuwa alijua kabisa Sami ni lazima atapewa mateso zaidi yake kwa kuwa yeye ni mwanaume na mbali ya hivyo pia alikuwa ni mwenye jina kubwa katika medani za ushushu hivyo jicho kubwa litakuwa kwake kuliko yeye.
-------
Chepe alikuwa anakuna kidevu chake kwa ncha ya kidole cha shahada huku macho yake yakiwa makini kutazama vijana watatu waliokuwa wapo makini kufanya jambo fulani kwenye mitambo ya mawimbi ya umeme yaliokuwa yanawasaidia kupiga simu za satellite na pia kujua mienendo ya mawimbi ya umeme yaliokuwa yanasogelea kwenye maeneo yao.
Mitambo hii ndio ilifanikiwa kujua kuna mawimbi ya ajabu yanatoka kwenye pakatarishi iliokuwa inawahangaisha Chepe na Sajini Lolo baada ya kupewa nywila zake na Kakere.
“Poison trap!! Hawa wajinga sana!” Chepe alijisemea huku akiendelea kufuatilia kwa makini kile kilichokuwa kinafanywa pale.
Kijana mmoja akamgeukia Chepe baada ya kompyuta yake kutoa mlio wa bip mara tatu huku alama nyekundu ikisoma kwenye ramani kuonesha pahali fulani ndani ya Afrika mashariki.
“Kamanda mawimbi yamesafiri hadi Dar es Laam Tanzania!” Alimwambia huku akigeuka tena na kuendelea kucheza na kicharazio cha kompyuta yake.
Chepe alipiga ngumi ukutani huku akitoa tusi zito la nguoni na kutupa baragashia yake ya thamani.
“Aisee sasa hii ni vita mpya inaanza na Tanzania haijawahi kufeli ila hii nitawafelisha nawajua nje ndani hawatanisumbua tena naanza na hawa vikaragosi wao waliowatuma” Alijiwazia peke yake huku macho yake yakiwa bado kwenye vioo vya kompyuta.
Mara akaingia Luteni daraja la kwanza bwana Amolo akiwa ameshika simu.
“Kamandi ya sita kule Beni juu wanataka kuzungumza na wewe!!” Amolo alimwambia Chepe .
“Unadhani wanataka kusema nini labda labda!” Chepe badala ya kupokea alimuuliza Amolo.
“Ni kuhusu wandishi wa habari tuliowazuia hapa!!” Amolo alijibu.
Chepe alitabasamu kisha akamwambia Amolo.
“Wambie sihitaji kwa sasa nitawatafuta mwenyewe!” Chepe akamwambia Amolo na Amolo nae haraka akaondoka mle ndani.
“Tanzania…… Tanzania mh!!” Chepe alijiwazia huku akitoa simu yake mfukoni iliokuwa na mkonga na nyuma ikiwa imetuna kama mgongjwa wa fufu.
Ilikuwa ni simu ya satellite.
Akachangua namba kadhaa kisha akaipata alioihitaji akapiga.
“Tap on the top, tunahitaji kuweka ukuta kila sehemu miguu ya mamba imeonekana huku na harufu imefika kiotani!!” Chepe alizumgumza na mtu aliepokea simu upande wa pili.
Na alitumia lugha ya kijasusi, lugha ya mafumbo akiwa na maana kumekuwa na vihatarishi kwenye maeneo yao na bado tarifa za vihatarishi imefika mbali na itakuwa shida kwao.
Mtu wa upande wa pili alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema
“Ina maana umewadaka nzi wao!?” Alihoji yule jamaa kwa kiswahili safi kabisa.
Akimaanisha nzi ni mashushu au majasusi wa kitanzania.
“Yes!! Wapo shimoni hadi sasa!!”Chepe alijibu.
“Umekosea sana!! Na umetangaza vita mbaya sana na hao jamaa, lakini kama ulijua wapo ulishindwa kuwapangusa bila kuwanasa?” Alihoji jamaa huku akionekana dhahiri kuogopa kitu kilichofanywa na Chepe.
“Usiogope najua cha kufanya!” Chepe alijibu.
“Kama kipi?” Jamaa alihoji.
“Naomba unitumie picha za watu wote wanaofanya kazi kwenye kitengo cha special operation chini ya Kamishina Zenge wa Zenge na Hawa Maiga kisha anza kutega huko na wakifanikiwa huku basi sisi tunamaliza!” Chepe alimwambia jamaa.
“Watanzania wajanja aisee wanaweza kukuleta operative ama considered spy ohoo!!” Jamaa alimtahadharisha Chepe.
“Huku watakuja madeep spy tu trust me!!” Chepe nae aliendelea kutetea hoja yake.
“Sawa ngoja nitege mingo na picha utapata hivi punde!” Jamaa alisema na kukata simu.
Chepe alitabasamu.
“Wajinga wametaka mchezo sasa mimi nawafungia kibwebwe tuserebuke wote na ndo watajua pombe ya ngoma haikeshi mana watainywa hadi vilembwe!” Chepe alijisemea huku akiandika ujumbe wa kikao cha dharura kwa watu fulani na kuutuma kwa wakati mmoja kisha akatoka kwenye kile chumba na kuelekea kule kwenye chumba cha shimo na kuamuru Kakere na Sami watolewe shimoni.
Agizo lilitekelezwa mara moja na waadishi wale wakaibuliwa na Kakere alikuwa hoi taabani lakini Sami yeye hakuwa na fahamu kabisa huku mwili wake ukiwa umekuwa mweusi kwa sababu ya sumu ya nge waliomshambulia mwili mzima.
“Wapelekeni rest in peace wapeni huduma wazinduke nitakuja badae!” Chepe alitoa maagizo na kisha akatoka na hakuna aliejua safari yake ilikuwa ni wapi.
--EAGLE WING HOUSE-DAR—
Mwanamke aliependeza kwenye sare zake za jeshi alishusha mkonga wa simu ya mezani huku uso wake ukiwa umejikunja na mdomo wake akiwa ameupeleka mbele kama kalambishwa konyagi.
Akakalia kiti chake cha kuzunguka na kuweka miguu juu ya meza iliokuwa mbele yake huku mikono yake akiufumbata pamoja na kuilaza juu kidogo ya kinena kisha macho yake yakatua juu ya ukuta na kukutana na picha ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Mwanamama yule mabegani mwake alikuw na kola yenye ngao (bibi na bwana) kisha nyota tatu kumaanisha cheo chake kilikuwa Brigedia Jeneral na juu kidogo ya mfuko wa vazi lake la juu kulikuwa kuna jina lake.
Alikuwa ni Brigedia Jeneral Hawa Maiga.
Muda huo alikuwa ametoka kuwasiliana na simu mbili huku simu ya kwanza ikiwa ni kutoka nchini Congo kwenye vikosi vya umoja wa mataifa na kuarifiwa kuwa mkubwa wa waasi Chepe alikuwa amegoma kuzungumza nao hivyo walikuwa hawajui ni nini shida yake kwa waandishi wale.
Bi Hawa Maiga alishindwa kuelewa kama Chepe alishindwa kuzungumza ni kwa kuwa amejua aina ya watu aliowateka ama anahisi tu.
Bi. Hawa Maiga alimtambua vyema Chepe kuliko mtu yeyote na alijua ni lazima Chepe atakuwa amejua wale ni Zedi na Mina kutoka kwenye kitengo chake cha MI chini ya mwamvuli wa special operations..
“Lakini nimekutengeneza mimi Chepe na huwezi kushindana na mimi hata kidogo, uliowaua wanatosha, familia zao zimelia vya kutosha nisingependa tena damu imwagike ni lazima nikutie mikononi hata kwa kuingia mi mwenyewe” Brigedia Jeneral Hawa Maiga alijisemea huku akitikisa mguu wake wa kulia na kwa waliomfahamu hapo walijua yupo kwenye kiwango cha mwisho cha hasira na hata ukimzingua unaweza kuchezea risasi ama mbata za kutosha.
Bi Hawa pia alikuwa amepiga Simu kwa Kamishina Zenge wa Zenge ambae nae alikuwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi la polisi huku yeye akiwa ni msimamizi wa operesheni maalumu upande wa jeshi yani Military intelligence (MI).
Kwa nini walishirikiana?
Kwa sababu vijana wa special operations walikuwa ni wale wale huku wakijigawa kimajukumu kulingana na uzito wa kazi kila pande hivyo wakiwa chini ya Zenge wa Zenge walipaswa kufanya kazi za kipolisi na wakiwa chini ya Hawa Maiga wanafanya kazi za jeshi kikamilifu kwa kuwa wote walikuwa ni makomando waliofuzu kila idara na pia walikuwa wameiva kwenye mafunzo ya ujasusi na upelelezi.
Simu aliopiga ilimhitaji Kamishina afike makao makuu yao wote kwa kikao chao cha dharura kuhusu jambo lile.
Na kikao kile ndicho kilizaaa balaa na kizaaa zaa kikubwa ndani ya Dar na nchini Congo na ikawa ni operesheni kufa kupona iwe jua iwe mvua.