Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri

Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri

Pinda haponi
• Ya Lowassa yamnyemelea, Kamati teule yaibua hofu CCM

na Josephat Isango
Tanzania Daima


HOFU ya kung'oka kwa mawaziri wasiopungua watano akiwamo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imeanza kushika kasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Hofu hiyo inatokana na ukweli kwamba, huenda safari hii usiwe upepo unaopita tu bila madhara, bali kikawa kimbunga cha kuwaondoa madarakani mawaziri hao kwa madai ya kushindwa kuwajibika.
Pinda na mawaziri wenzake, Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Mathayo David Mathayo (Mifugo na Uvuvi), Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) wanashinikizwa kujiuzulu.
Mawaziri hao juzi walishambuliwa na wabunge kuwa taasisi na watendaji walio chini yao wameendesha operesheni za kupambana na ujangili na kuhamisha mifugo zilizosababisha vifo, ubakaji, majeruhi na uharibifu wa mali kwa wananchi wasio na hatia.
Tayari Bunge limepitisha azimio la kuunda kamati teule ambayo inatarajiwa kutangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, bungeni kesho.
Hatua ya kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kumekitia hofu Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho tangu mwaka 2008 kimekuwa kikihaha kutibu majeraha ya makundi yanayohasimiana yanayodaiwa kushamiri mara baada ya Edward Lowassa kujiuzulu.
Majina ya kamati teule yanayotarajia kutangazwa kesho, ndiyo yatakayotoa picha ya mwelekeo wa siasa za chama hicho.
Iwapo kamati teule ikibaini tuhuma walizotoa wabunge, za watu kubakwa, kuuawa, kuteswa, ng'ombe kupigwa risasi, wafugaji kutozwa faini kubwa, kulazimishwa kuuza mifugo yao kwa bei ndogo, Pinda na mawaziri wenzake waliotajwa watalazimika kujiuzulu au rais kutengua uteuzi wao.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanadokeza kuwa kuendelea kuwapo madarakani kwa Pinda kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye mara kwa mara amekuwa akimkingia kifua licha ya kupelekewa malalamiko ya utendaji hafifu wa Pinda.

Baadhi ya makada waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wamedokeza kuwa kitendo cha wabunge kuunda kamati teule ya kuchunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi hakitamnusuru Pinda.
Makada hao wanasema Pinda hawezi kuepuka kimbunga hicho kwa madai kuwa baadhi ya wabunge na hata mawaziri hawaridhishwi na utendaji wake, hivyo matokeo ya tume hiyo yatatoa fursa ya azima yao ya siku nyingi ya kutaka kumng'oa madarakani.

Rais Kikwete ndiye tegemeo pekee la kusalia madarakani kwa Pinda anayedaiwa kushindwa kuimudu ofisi hiyo iliyoachwa na mtangulizi wake, Lowassa, aliyejiuzulu Februari mwaka 2008, baada ya kuguswa na kashfa ya Richmond.
Historia ya kamati inaonyesha kuwa ripoti zake mara nyingi zimesababisha kujiuzulu au kuondolewa madarakani kwa watu wanaoguswa nazo.

Mtangulizi wa Pinda ambaye ni Mbunge wa Monduli, Lowassa, alilazimika kuondoka madarakani baada ya ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Dk. Harrison Mwakyembe, kubaini kulikuwa na upendeleo katika zabuni iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond.
Pinda inadaiwa amekuwa si mtoaji maamuzi kwa masuala yanayowagusa watendaji walio chini yake, hivyo kuathiri utendaji kazi wa serikali.

Kama Pinda atajiuzulu, Rais Kikwete atalazimika kuunda baraza jipya la mawaziri ambalo litakuwa la nne tangu aingie madarakani mwaka 2005.
Rais Kikwete aliunda serikali mwaka 2006 mara baada ya kuingia madarakani lakini Aprili 2008 alifanya mabadiliko baada ya Lowassa kutuhumiwa na kamati teule iliyoundwa kuchunguza kashfa mbalimbali zilizohusu kampuni za kuzalisha umeme.

Baada ya Uchaguzi Mkuu 2010 Rais Kikwete alifanya mabadiliko kwa mara ya pili, baada ya kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili, huku waliokuwa mawaziri 2005-2010 wakiangushwa katika kinyang'aro cha ubunge kwenye majimbo yao.
Kikwete alifanya mabadiliko mengine Mei mwaka jana, mabadiliko yaliyomwacha aliyekuwa Waziri wa Fedha Mustapha Mukulo, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, aliyekuwa Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Waziri mmoja wa zamani anasema wabunge watakaoteuliwa na Spika kuunda kamati teule wanaweza kutumia mwanya wa makundi ya kisiasa kumwajibisha Pinda na wenzake kwa lengo la kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi wa rais mwaka 2015.
Historia za kamati teule
Historia inaonyesha kuwa kila kamati teule ilipoundwa haikuwaacha salama watuhumiwa, ikiwa ushahidi utatolewa wa kutosha. Juzi Spika Makinda aliafiki wazo la kuundwa kwa kamati teule.
Hata hivyo kamati teule hizo kila zinapoundwa na ripoti yake kusomwa zimekuwa zikisababisha kuondoka madarakani kwa watendaji mbalimbali.
Februari 8, 2008, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alilazimika kujiuzulu baada ya kamati teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza zabuni iliyoipa ushindi wa kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond kumgusa.
Mwaka juzi, Bunge liliunda kamati teule kuchunguza matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, ambayo ilidaiwa kuchangisha sh milioni 50 kwa idara na taasisi zilizo chini ya wizara, ili kufanikisha upitishwaji wa bajeti, na ripoti yake ilimng'oa Katibu wake, David Jairo.
Mvutano
Wakati hofu hiyo ikitanda Bunge limegawanyika katika suala hili, kukiwapo mvutano mkubwa kama mawaziri hao wawajibishwe au la, licha ya mawaziri hao kutoa kauli za serikali na kuomba radhi ili wahusika waweze kuwajibishwa.
Tayari Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), amejitokeza na kusema hoja yao imetekwa na Spika wa Bunge, Makinda, na kuifanya ni ya kwake na si ya wabunge waliotoa hoja.
"Hoja imechukuliwa na Spika, akaanza kuamua baadhi ya mambo yaanze kuchunguzwa na Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, ambayo imeteuliwa na yeye, tulitegemea tupewe fursa ya kuhitimisha hoja zetu kisha iundwe kamati teule kutegemea hadidu za rejea za wabunge, lakini kwa utaratibu uliofuatwa na Spika, watoa hoja hatujapewa nafasi ya kuhitimisha hoja zetu," alilalamika Lugola.

Lugola aliongeza kwamba damu zilizomwagika hazitaenda bure, watu wakileta majibu mepesi yasiyowawajibisha Pinda na wenzake hatakubali, maana wananchi wameuawa, wamebakwa, wameteswa, ng'ombe wakauawa kwa kupigwa risasi, kama kuna mbunge asiyewapenda Watanzania apeleke utetezi kwa masuala hayo mazito.
Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) alisema kila chama kilichoko madarakani kinapenda kutawala, hivyo mawaziri waliozembea iwapo hawatachukuliwa hatua chama kinachoongoza kinajiandalia anguko katika uchaguzi mkuu ujao.
Hata hivyo baadhi ya wabunge wa chama tawala wanaona haikuwa busara kwa Spika Makinda kuruhusu hoja ya kuundwa kwa kamati teule, hasa katika kipindi hiki ambapo vyama vya upinzani vimeonekana kuimarika zaidi.
Kuimarika kwa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kumechangia makada wa CCM kujawa na hofu ya kile kitakachogunduliwa na kamati teule.
Wabunge hao walisema hivi sasa bado chama chao hakijapata uungwaji mkono katika mchakato wa sheria ya Katiba mpya, hivyo kamati teule inaweza kuongeza utete ndani ya serikali na CCM.
 
Mkuu Yegella, hata kama ni kweli, au si kweli, comment hii ni kinyume cha utu wa mtu, huu ni unyanyapaa ambao ni kosa against morality!. VVU ni janga la kitaifa, kuna wengi ama tunaishi na vvu ama wanaishi na vvu, kitendo cha kuandika tumdharau fulani kwa sababu ni muathirika wa vvu, ni kuwadhalilisha waathirika wote wa vvu!, tena usikute unaandika haya huku hujapima!.

Pamoja na utani na mizaha yote tunayotoleana humu jukwaani, tusivuke mipaka ya utu na ubinaadamu!.
This comment is not fair!.
Pasco.

May be ni ukweli coz kaanza na mambo ya mbege tofauti na mada kabisa yegella akajaribu kutufafanulia kwanini huyu mtu yuko namna hii
 
Last edited by a moderator:
Tumdharau ... kwa sababu ni muathirika wa vvu.
Mkuu Yegella, bado hujachelewa kusema sorry kwa comment hii, hata kama hukumaanisha bali uliitoa kwa utani tuu wa ki jf!, think of waathirika wa vvu kiukweli, how would we/they take it?!.
Pasco.
 
May be ni ukweli coz kaanza na mambo ya mbege tofauti na mada kabisa yegella akajaribu kutufafanulia kwanini huyu mtu yuko namna hii
Hata kama ni kweli, mtu mzima mwenye akili timamu, utu na ustaarabu, huwezi kutoa comment ile kuhusu mtu mwenye kuishi na vvu, iwe ni kweli anaishi navyo au sii kweli, kule ni kuwanyanyapaa wengine wote tunao/wanaoishi navyo!.

Wangapi tunajijua/wanajijua/tunawajua kuwa tu/wanaishi na vvu na hatuwesemi, kuwanyooshea vidole seuze kuwa ridicule kwa stutus zao?!. Naombeni msitetee unyanyapaa kwa kisingizio chochote!. There is no any justification for that!. Na kama umenote, tangu jana baada ya post hii
Tumdharau ... kwa sababu ni muathirika wa vvu.
, huyu jamaa hakurudi tena humu jukwaani!. This is not fare jamani!.
Pasco.
 
Mkuu kaizer , hii ndo tz ukigusa masilahi ya wakubwa ujue hufiki mbali. Si uliona amri ya magufuli kuhusu malori walivyomfanya.

Aisee....usinikumbushe bana.....sasa umesikia yamekamatwa meno ya tembo vipande 700 viko na wachina...kisha umesitisha operesheni tokomeza ujangili?
 
Huu ni mgongano wa maslahi ndani ya ccm wenyewe
 
Shehena pembe za ndovu yakamatwa Dar


pembe+px.jpg

Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki (wa pili kushoto), akiwa ameshika pembe za ndovu zilizokatwa jana jijini Dar es Salaam toka kwa raia watatu wa China katika operesheni aliyoiongoza.PICHA|FILE

Na Goodluck Eliona, Mwananchi

Dar es Salaam. Siku moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar es Salaam.

Pembe hizo 706 ni sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi za wanyama pori mbalimbali hapa nchini. Tukio hilo lililotokea jana jioni katika Mtaa wa Kifaru, Mikocheni, wilayani Kinondoni, liliongozwa na Waziri Kagasheki ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tarish Maimuna.

Waliokamatwa na shehena hiyo ya pembe za ndovu ni raia watatu wa China ambao ni Xu Fujie, Chen Jinzha na Huang Qin wote kutoka mji wa Guandung .


Raia hao wa China wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo kwa miaka mingi wakifanya biashara ya kuingiza nchini vitunguu swaumu kutoka China na kusafirisha nje ya nchi makombe yanayopatikana baharini.

Alipoingia ndani ya nyumba hiyo, Kagasheki ambaye aliambatana na askari polisi na baadhi ya maofisa usalama alishuhudia shehena kubwa ya pembe za ndovu ikiwa imehifadhiwa kwenye viroba vyenye uzito wa kilo 50.

Mbali ya kushuhudia shehena ya pembe hizo, alionyeshwa gari maalumu aina ya Toyota Noah ambalo watuhumiwa hao hulitumia kutoa pembe porini na kuyaingiza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika eneo la tukio mara baada ya kuwakamata alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imesitishwa na Serikali juzi baada ya wabunge kuilalamikia.

Waziri Kagasheki alisema kwamba katika harakati za kutaka kuwakamata watuhumiwa hao walitoa Sh30 milioni kwa ajili ya kujaribu kuwahonga askari.

"Walitaka kuwahonga askari ili wasikamatwe," alisema huku akionyesha noti za fedha hizo.

Alisema wabunge wanaomtaka ajiuzulu kwa madai kwamba Operesheni Tokomeza Ujangili imesababisha mauaji ya watu na mifugo wanapoteza muda kwa kuwa mwenye mamlaka ya kumtoa ni Rais Jakaya Kikwete pekee.

"Sasa mimi nasema kunitoa haitakuwa rahisi anayeweza kunitoa ni yule aliyeniweka," alisema.

Alisema ipo mikakati inayofanywa na baadhi ya wabunge kutaka kuwang'oa baadhi ya mawaziri kwa masilahi binafsi ya kisiasa.

Itakuwa ni jambo la ajabu kwamba kila mtu akiingia madarakani wanataka atoke, watatolewa wangapi?" alihoji na kuongeza kuwa operesheni hiyo ni muhimu kwa ajili ya kunusuru tembo wasiishe.

Alisema kwamba ni kweli kuna baadhi ya dosari zimejitokeza kwenye operesheni ikiwamo kuuawa kwa baadhi ya mifugo, lakini siyo kwamba zoezi zima halina manufaa.

Kagasheki alisema kama kasi hii ya kuuawa kwa tembo itaachiwa iendelee baada ya miaka 10 tembo wote watakuwa wameisha nchini.

Alisema hataki kuona utawala wa Rais Kikwete ukiondoka madarakani ukiwa na lawama ya kuachia majangili wawamalize tembo.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Huang Qin alisema shehena yote ya pembe za ndovu iliyokamatwa nyumbani kwake ilikuwa ikiletwa kidogo kidogo na rafiki yake ambaye hakumtaja jina.

Akiongea kwa Kiswahili Qin alisema: "Mimi hii si yangu, kichwa yangu mbovu. Rafiki yangu alileta hii (pembe) kidogo kidogo."

Januari mwaka huu, Gazeti La Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba Serikali ya Kenya imekamata shehena ya vipande 638 vya pembe za ndovu ambavyo ni sawa tembo 320 waliouawa.

Mzigo huo wa tani mbili ulikuwa kwenye kontena la mawe ya urembo (marumaru) kutoka Tanzania.

Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 3.4 milioni sawa na takriban Sh5.4 bilioni zilikamatwa Hong Kong Oktoba 20, mwaka jana, huku ikielezwa kuwa meno hayo yalikamatwa yakisafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.

Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na pembe za ndovu yenye thamani ya Sh18.4 milioni yaliyotengenezwa kama bangili tayari kusafirisha kwenda nje ya nchi.
 
Mimi nimeshangaa sana mkuu manning. Yaani nimewangalia jana wakati wanajadili..hakuna hata mbunge mmoja aliyejaribu kuonyesha ubaya wa ujangili na hali ilivyokuwa mbaya sasa hivi....wala kuonyesha kwamba ni kwa nini hii operation ni muhimu.

Mi nadhani kwenye.operation kama hii haiwezi kukosa majeruhi na kuisitisha pamoja na kiwalaumu watekelezaji kwa maaana ya JWTZ Polisi na askari wa wanyamapori ni kuwaondolea morale kabisa

Wabunge.wameshindwa kuona ni kwa nini ujangili uliokithiri utaathiri sana utalii.ambao unachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.

Suala la ujangili limeshakuwa systemic...wamekamatwa watu hapa lakini unasikia wanaachiwa au watu wanalobby waachiwe..huo.ni.udhaifu wa utekelezaji wa sheria na ingepaswa wahusika wote waadhibiwe vikali....

Suala la mifugo kuingi hifadhini ni kinyume cha sheria ya wanyamapori ..so ikikamatwa ndani inabidi mwenye nayo alipe faini nk...kuwaachia namna hii inaset precedent kwamba unaweza tu ukaswaga mifugo yako hifadhini kisha ikaachiwa kiroho safey. Kila siku watu wanahubiriwa wapunguze idadi ya mifugo lakini wapi....matokeo yake ndo kama hivi.

Kikubwa ninachoona hapa ni uchaguzi unakaribia na kura za wafugaji.ni muhimu sana...
kuna Kigogo mmoja walimkamata katibu wake na kupigwa vibaya miguuni na ndiye alilivalia njuga suala hili ingawaje kuna tetesi kuwa na yeye ni mtaalam wa mambo hayo kama dentist K......bariiidi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom