Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri

Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Operesheni Kimbunga yazoa mawaziri
• Wabunge wataka Pinda, Nchimbi, Kagasheki, Mathayo wang'oke

na Salehe Mohamed, Dodoma
Tanzania Daima


HATIMA ya mawaziri watano kuendelea na nyadhifa zao iko shakani baada ya wabunge kuwatuhumu kushindwa kuwajibika ipasavyo na kusababisha migogoro ya wafugaji na wakulima.
Kufuatia kadhia hiyo iliyojitokeza wakati wa kutekelezwa kwa Operesheni Kimbunga na Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge limeamua kuunda kamati teule kuchunguza migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imesababisha vifo, ukiukaji wa haki za binadamu na upotevu wa mali.

Wabunge wengi waliochangia hoja hiyo waliwataja wazi mawazi kadhaa akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakitaka wawajibishwe kwa kuondolewa kwenye nyadhifa zao kutokana na kushindwa kuchukua hatua wakati operesheni hizo zikipoteza maisha ya watu na mifugo.
Mbali na Pinda, wamo pia Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), David Mathayo David (Mifugo na Uvuvi) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa).

Dalili mbaya kwa viongozi hao zilianza kuonekana jana asubuhi baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutangaza kuwa amekubali hoja za wabunge wawili waliotaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili kujadili jambo la dharura.

Alisema Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM) alitaka Bunge lijadili kuhusu migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, huku Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alitaka Bunge lijadili vitendo vinavyofanywa na watendaji katika Operesheni Tokomeza Ujangili.
Lugola alidai watendaji wamekuwa wakiwaua kwa risasi ng'ombe waliowakamata kwenye operesheni hiyo pamoja na kuwatesa wamiliki wasiotoa fedha zinazohitajika.

Kutokana na hoja hizo, Makinda alitoa fursa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo kuelezea Operesheni Tokomeza Ujangili na migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Kagasheki ndiye aliyekuwa wa kwanza kueleza operesheni hiyo inaendelea. Alisema inalenga kutokomeza ujangili ulioshamiri hapa nchini kiasi cha kutishia sekta ya utalii na tembo.
Hata hivyo, Kagasheki alisema kutokana na malalamiko ya watu mbalimbali juu ya mwenendo wa operesheni hiyo, serikali imeamua kuisitisha ili kufanya tathmini.

Waziri huyo pia alisema mifugo yote iliyokamatwa ndani ya hifadhi kabla na baada ya operesheni hiyo iachiliwe bila gharama yoyote na watu wenye ushahidi wa ng'ombe wao waliouawa kwa risasi wawasilishe vielelezo ili achukue hatua zaidi.
Mara baada ya Kagasheki kutoa taarifa hiyo, Waziri Mathayo alitoa taarifa kuhusu migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Aliwaomba radhi waliopata hasara ya kujeruhiwa, kupoteza mifugo au vifo katika operesheni hiyo.

Wabunge wacharuka
Mara baada ya mawaziri hao kumaliza kutoa taarifa zao, Spika Makinda alitoa fursa kwa wabunge kuchangia. Mbunge wa Kilolo, Peter Msolla (CCM), alitoa hoja ya Bunge liunde kamati teule kuchunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Alifuata Lugola, ambaye alisema anashangazwa na mawaziri Nchimbi, Nahodha, Kagasheki na Mathayo kuendelea kuongoza wizara wakati damu za wananchi waliofariki katika operesheni zinazohusisha wizara wanazoziongoza zinawakabili.

Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani (CCM), aliifananisha serikali na ugonjwa wa miguu na midomo kwenye mifugo, maarufu kama Sotoka, ambao miaka ya nyuma ulikuwa ukiua ng'ombe wengi.
"Hii serikali ya ajabu sana, yaani ukiwa na mifugo mingi ni kero kwao. Badala ya kuweka mazingira mazuri ya kukuza uchumi, wanaiua. Mimi naifananisha na Sotoka," alisema.

Mbunge wa Maswa, Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), aliwataka wabunge wa CCM waache unafiki na wamuondoe Waziri Mkuu, Pinda kwa kuwa hachukui hatua kila anapopelekewa matatizo.
"Wewe Waziri Mkuu, taarifa za kiintelijensia hazikufikii? Je, husomi magazeti kujua kinachotokea kwenye maeneo mbalimbali na mbona huchukui hatua? Nyinyi watu wa CCM msileane," alisema.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul (CHADEMA), alimtaka Rais Jakaya Kikwete awafukuze kazi mawaziri wake waliosababisha operesheni za kinyama zilizosababisha vifo vya binadamu, mifugo na unyanyasaji.

Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM), alisema serikali inatia aibu kwa kukamata meno ya tembo, lakini inashindwa kuwakamata majangili waliohusika.
Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM), aliwataka mawaziri waache porojo za kisiasa wanapoambiwa matatizo ya wananchi na wabunge.
"Wabunge humu ndani tunaeleza matatizo ya wananchi, eti waziri anasema si mambo ya msingi…acheni porojo, fanyeni kazi, maana tuna ushahidi wa kile tunachokisema," alisema.


Kamati teule
Akihitimisha mjadala huo, Makinda aliafiki wazo la kuundwa kwa kamati teule.
Hata hivyo kamati teule hizo kila zinapoundwa na ripoti yake kusomwa zimekuwa zikisababisha kuondoka madarakani kwa watendaji mbalimbali.
Februari 8, 2008, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alilazimika kujiuzulu baada ya kamati teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza zabuni iliyoipa ushindi wa kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond kumgusa.

Mwaka juzi, Bunge liliunda kamati teule kuchunguza matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, ambayo ilidaiwa kuchangisha sh milioni 50 kwa idara na taasisi zilizo chini ya wizara, ili kufanikisha upitishwaji wa bajeti, na ripoti yake ilimng'oa Katibu wake, David Jairo.

 
Ngoja tuangalie Mkuu, isije kuwa ni usanii tu kuelekea 2015. Maana hawa kwa usanii ndio wenyewe. Waliahidi kulivua gamba wakawa wanabadilisha kauli kila kukicha na gamba likabaki miilini mwao.

Duh,

Ngoja tuone mwisho wake maana isije kua upepo tu na ukapita
 
Naona 2015 inasogea kwa kasi ya ajabu, hatudanganyiki na kubweka kwenu kwa muda mfupi.

endeleeni kushabikia serikali yenu ya ccm sikivu.!
 
Hivi ni kweli bei ya mbege imeshuka kwa asilimia 75?

WASIFU WA LUKOSI 1.Huyu jamaa alikuwa polisi akafukuzwa sababu ya ajali katika msafara wa pm wakati ule John Malecela na kukimbilia Botwana kwa dada yake ambaye ni Nurse.2 2.Lukosi alifuatana na dadake nchini uk baada ya kupata kazi uk nayeye alipata nafasi ya kuambatana naye uk. 3.Lukosi alipata nafasi ya kujifanya mkimbizi na kuukana utanzania pamoja na porojo zake yeye uk anafahamika kama mkimbizi wa kisiasa na njaa. 4. Lukosi alipata kazi ya kuwa traffic warden kwa bahati mbaya alipata ajali ambayo ilimfanya adhurike kichwani alilazwa kwa muda mrefu na aliathirika na ajali ile kichwani.Kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi ilimlipa malipo kutokana na ajali hiyo,na baada ya muda aliacha kazi na kuanza biashara. 5 Lukosi alianza biashara za kupeleka magari mabovu Tanzania na baiskeri za wizi kutokea maeneo ya barking&dagenham na baada ya muda alianza biashara nyingine ambazo wengi wanazijua. 6 Lukosi alijaribu kujiingiza kwenye siasa baada ya kukutana na mbunge Lema jijini London,na nia kubwa akifikiri atapata tender za kusafirisha mizigo na magari ya chadema.Alipewa nafasi kukaa hotelini kwa mzee ndesambulo jijini Dar kwa week moja free of charge. 7 Baada ya kukosa tender hiyo Lukosi alirudi ccm ambapo hajawahi kuwa mwanachama uk,na alianza kashfa nyingi kuhusu chadema na hii ni kutokana na waajiri wake wa biashara (sizisemi) kutoka Tanzania ambao ni wafadhiliwa na ccm kutokana biashara hizo.Ametumia muda mwingi mtandaoni ili wamkubali kuwa katoka chadema na anaichafua. 8. Tumdharau Lukosi kwa sababu ana ugonjwa wa pressure na inasemekana ni muathirika wa vvu si mwana siasa ila ni stress zinamsumbua..
 
Hii vita mbona km inawshusu vigogo watupu? Dah siasa mbaya sana yani operation ndio imeisha hivyo
 
...mbunge wa
Busega Dk.Titus Kamani
(CCM),aliifananisha
serikali ya CCM na
ugonjwa wa miguu
na midomo kwenye
mifugo,maarufu
kama "Sotoka",ambao miaka ya
nyuma ulikuwa
ukiua ng’ombe
wengi...

HERI MIMI SIJASEMA!
 
ccm imechoka-ni majanga!
mipango na operation zao zote ni majanga.

`operation kimbunga' imeishia kwa ukiukaji mkubwa wa misingi ya haki za binadamu, kuwafilisi watu na hata kuhamisha raia wa watanzania kwenda Rwanda eti nao ni wahamiaji haramu. majanga!

`operation tokomeza ujangili' imeishia kuwafilisi wananchi, kuwaua watu na mifugo yao. majanga!

`big results now' imeishia kushusha viwango vya ufaulu (mfano😛ointi 18-24 ni division two; 25-31 ni division three; 32-39 ni division four;na 40-49 ni division five). majanga!

ccm = mkosi + laana.
(majanga)
 
WASIFU WA LUKOSI 1.. Tumdharau Lukosi kwa sababu ana ugonjwa, inasemekana ni muathirika wa vvu stress zinamsumbua..
Mkuu Yegella, hata kama ni kweli, au si kweli, comment hii ni kinyume cha utu wa mtu, huu ni unyanyapaa ambao ni kosa against morality!. VVU ni janga la kitaifa, kuna wengi ama tunaishi na vvu ama wanaishi na vvu, kitendo cha kuandika tumdharau fulani kwa sababu ni muathirika wa vvu, ni kuwadhalilisha waathirika wote wa vvu!, tena usikute unaandika haya huku hujapima!.

Pamoja na utani na mizaha yote tunayotoleana humu jukwaani, tusivuke mipaka ya utu na ubinaadamu!.
This comment is not fair!.
Pasco.
 
Mhh! Huyu mtoa habari za wasifu Lukosi naye angetoa yake ingependeza.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Duh,

Ngoja tuone mwisho wake maana isije kua upepo tu na ukapita


huo ni utumbo na upumbavu wa wabunge wetu kwani kwani kamati ngapi ziliumdwa na mapendekezo yakafanyiwa kazi?...wabunge tulishawazoea hao akina nkumba wanasubiri waitwe ktk kamati ili wakapige posho, nyie tunawasubiri 2015
 
Mkuu Yegella, hata kama ni kweli, au si kweli, comment hii ni kinyume cha utu wa mtu, huu ni unyanyapaa ambao ni kosa against morality!. VVU ni janga la kitaifa, kuna wengi ama tunaishi na vvu ama wanaishi na vvu, kitendo cha kuandika tumdharau fulani kwa sababu ni muathirika wa vvu, ni kuwadhalilisha waathirika wote wa vvu!, tena usikute unaandika haya huku hujapima!.

Pamoja na utani na mizaha yote tunayotoleana humu jukwaani, tusivuke mipaka ya utu na ubinaadamu!.
This comment is not fair!.
Pasco.

Naunga mkono hoja ;ILA NA YEYE AJIHESHIMU SASA NA AANGALIE MIPAKA YAKE!!!!!!!!!

Hoja hapa.ni Rasilimali, Haki za binadamu na jinsi ya kufikia muafaka wa kuweza kufaidisha pande zote kwa njia endelevu. Sasa habari ya bei ya mbege imetoka wapi?????!!!!!

Ajiheshimu!!!!!
 
...mbunge wa
Busega Dk.Titus Kamani
(CCM),aliifananisha
serikali ya CCM na
ugonjwa wa miguu
na midomo kwenye
mifugo,maarufu
kama "Sotoka",ambao miaka ya
nyuma ulikuwa
ukiua ng’ombe
wengi...

HERI MIMI SIJASEMA!

hiyo ndiyo serikali iliyoundwa na ccm ambacho ni chake kama ameichoka ccm ajiuzuru hata chadema hatumhitaji
 
Mkuu Yegella, hata kama ni kweli, au si kweli, comment hii ni kinyume cha utu wa mtu, huu ni unyanyapaa ambao ni kosa against morality!. VVU ni janga la kitaifa, kuna wengi ama tunaishi na vvu ama wanaishi na vvu, kitendo cha kuandika tumdharau fulani kwa sababu ni muathirika wa vvu, ni kuwadhalilisha waathirika wote wa vvu!, tena usikute unaandika haya huku hujapima!.

Pamoja na utani na mizaha yote tunayotoleana humu jukwaani, tusivuke mipaka ya utu na ubinaadamu!.
This comment is not fair!.
Pasco.

Unajua bwana pasco wakati mwingine huyu lukosi anakera sana anataka kuhamisha mwelekeo wa kinachojadiliwa kwa kuleta utani kwenye suala nyeti, kilichofanywa na yegella ni kataka kulionyesha jukwaa mtu anayetaka kupindisha mjadala ni mtu wa aina gani. Kwa hiyo huyu lukosi sio kila hoja uchangie wakati mwingine ni vema kuwa msomaji kama huna cha kuchangia badala ya kuchangia ujjnga na kuamshi hasira kwa wengine
 
Back
Top Bottom