TASK FORCE RANGER:
Tarehe 8 August 1993, vikundi vya wanamgambo vilivyoongozwa na Aidid vililipua bomu la kutumia rimoti gari la wanajeshi wa marekani na kuua polisi jeshi (military police) wanne wakimarekani. Wiki mbili baadae, bomu jingine lilipuliwa na kusababisha majeruhi zaidi. Katika kujibu mashambulizi hayo, rais Clinton aliainisha maombi ya kupeleka kikosi maalum kilichokua na askari 400 (US Army RANGERs) na maafisa viongozi wa Delta force. Kikosi hiki maalum kiliitwa 'Task Force Ranger' na pia kilihusisha askari wapatao 160 wenye weredi wa hali ya juu (elite troops).
Naam, shughuli ilikua imeanza kuiva. Askari hawa wakasafiri mpaka Mogadishu kuanza rasmi msako dhidi ya Mohamed Farrah Aidid. Tarehe 22 August, kikosi hiki maalum kikatumwa kwenda Somalia chini ya uongozi wa meja jenerali William F. Garrison, aliyekua kamanda kiongozi wa JSOC ( Joint Special operations command) kwa wakati huo. Rejea makala mbali mbali za nyuma kufahamu zaidi kuhusu JSOC.
Kikosi hiki maalum kilijumuisha:
B Company kutoka 3rd battalion 75th Ranger regiment,
C Squadron kutoka 1st Special Forces Operational Detachment-Delta (1st SFOD-D),
Helikopta 16 na marubani kutoka 160th Special operations Aviation regiment (160th SOAR) ambapo kulikua na helikopta aina ya MH-60 Black Hawks na AH/MH-6 little birds,
NAVY SEALS kutoka Naval Special Warfare Development Group ( DEVGRU),
Wataalam wa uokoaji kutoka jeshi la anga la marekani ( Airforce Pararescuemen) na wataalam wakivita kutoka katika kikundi cha mbinu maalum za kivita ( 24th Special Tactics Squadron). It was good to go......