Mudawote tuwe wakweli ukiamua kuingia kwenye siasa kubali yote...hebu ona kinachoendelea marekani kwasasa, siasa hazina adabu,hazina staha hazina heshima
Na hili wewe ni mmojawapo umeshawatukana sana hao uliowataja matusi makubwa tu si mara moja bali mara nyingi umewakashifu kuwabeza na kuwakejeli, ni wakubwa zako hawa watu na familia na ndugu na majukumu yao...
Kwasababu tu ya kutofautiana mitazamo ya kisiasa ukaamua kujivua utu wako ukisaidiwa na ID bandia kuwatusi hasa....na shida yako kubwa huzungumzii mfumo, hujadili hoja bali mara zote umepeleka kashfa kejeli na matusi kwa hawa watu...hii pia ni siasa lakini siasa chafu siasa majitaka
Niangalie mimi tunatofautiana mitazamo lakini sijawahi kufanya kama ufanyavyo wewe na kundi lako...
Namkosoa Magufuli lakini simvunjii heshima yake wala utu wake kwakuwa nje ya cheo chake yule ni mkubwa wangu ni kaka yangu nk...nakushauri sana jizuie dhihaka kejeli na matusi tubishane na kupingana kwa hoja tena zenye mashiko...upinzani sio uadui