Operation London Bridge

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,915
6,710
Hii ni code name inayosimama kwa ajili ya utaratibu mzima wa hatua kwa hatua ya kile kitakachotokea baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II. Mpango mkakati huu ulitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1960 na umekuwa ukifanyiwa maboresho karibia mwaka hadi mwaka. Malkia mwenyewe ameshiriki kutoa maamuzi katika mpango huu japo watakaobaki baadà ya kifo nao wana sehemu katika mpango mkakati huu. Kuandaliwa kwa mpango huu kunatokana na maandalizi duni ya mazishi ya familia za kifalme miaka ya nyuma ambapo katika tukio moja Princes Charlotte aliwahi kuzikwa na walevi.

Hali ilianza kubadilika wakati wa utawala wa Malkia Victoria pale alipoanza kupanga mkakati kwa kwa ajili ya mazishi mwaka 1875 miaka 26 kabla ya kifo chake. Mwaka 1952 alipofariki Mfalme George VI viongozi waandamizi walitaarifiwa kwa kutumia code name (Hyde Park Corner) lakini pia mazishi ya Mama yake na Malkia Elizabeth II yaliyipewa code name (Oparation Tay Bridge) yalifanyiwa mazoezi kwa muda wa miaka 22 na ilitumika katika mazishi ya Princes Diana mwaka 1997 kabla ya kutekelezwa kabisa kwenye kifo chake mwaka 2002.

Wahusika wakuu katika mpango huu ni Idara za serikali, jeshi la Polisi, jeshi la ulinzi, kanisa, vyombo vya habari na maeneo mbalimbali yenye hadhi ya kifalme.

Nini kitafanyika

Baada ya kifo cha Malkia mtu wa kwanza kupewa taarifa ukitoa wanafamilia na madaktari, atakuwa ni secretari wa Malkia mwenyewe , Baada ya hapo atamtarifu waziri mkuu na baadae maafisa waandamizi wa serikali kwa kutumia sentensi "THE LONDON BRIDGE IS DOWN" taarifa hii ataituma kwa kutumia simu maalumu. Baada ya hapo ofisi ya mambo ya nje itatoa taarifa kwa nchi zote wanachama wa jumuia ya Madola ambazo Malkia ndio kiongozi mkuu, vyombo vya habari vitatarifiwa kupitia Umoja wa vyombo vya habari, shirika la habari la Uingereza( BBC) na baada ya kupata taarifa hizo waendesha vipindi watalaazimika kupiga wimbo maalumu kama maandalizi ya kutoa habari hiyo!

Baadae taarifa ikiwa kwenye karatasi itawekwa kwenye geti la kuingilia kasri la Buchngham ambayo ndo offisi kuu ya ufalme wa Uingireza na muda huo huo tovuti ya Buchngham itaweka taarifa hiyo na Bunge litaitishwa ikiwezekana ndani ya saa moja ambapo waziri mkuu atalihutubia bunge la makabwela (The House of Commons).

Siku moja baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II baraza maalumu kwa ajiri ya kumuidhinisha Mfalme au Malkia mpya litakutana katika kasri la S. James na jioni ya siku hiyo bunge litakutana kwa ajili ya kumuidhinisha Mfalme au Malkia mpya!

Utaratibu kama Malkia atafia nje ya Kasri la Kifalme la Buckngham Kama atafia kwenye kasili la Windsor ambalo ni sehemu ya Mali za ufalme au kwenye Nyumba ya Sundningham ambayo ni Nyumba binafsi ya Malkia Elizabeth II, basi mwili wa Malkia utapelekwa Buchngham kwa gari. Kama Malkia atafia nje ya Uingereza basi mwili utapelekwa Uingereza na kikosi cha “The No:32 (the Royal) Squadron” ambalo ni jeshi maalumu la anga kwa ajiri ya familia ya kifalme kupitia uwanja maalumu ulioko eneo la South Ruislip!!

Kama Malkia atafia kwenye kasri la Balmoral liliopo Scotland mwili utapelekwa kwenye Cathedral ya mtakatifu Giles na baadae kuchukuiliwa na treni maalumu ya kifalme na kuletwa mjini London! Katika mazingira yoyote yale mwili utachukuliwa na kupelekwa katika kasri la Buckingham ndani ya siku 4. Mwili wa Malkia utaagwa kitaifa katika eneo la “Westminster abbey” siku tisa baada ya kifo na baadae atazikwa kwenye Jeneza katika kanisa la Mtakatifu George lililopo kwenye Kasri la Windsor.
G:
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Huyo hakuna cha London bridge wala nini alikuwa Jambazi kuu kwa watu weusi ametunyonya sana na kutufanya maskini wa kufa mpaka vizazi vyetu,kapora mali kibao hasa madini yetu
Aende motoni tu huyo kama mnavyosemaga watu wa dini
 
Wanaokunyonya na kukufanya kuwa maskini wanabainishwa kwenye report za CAG kila itokapo hebu ukawazabe kelebu kwanza.
 
Huyo hakuna cha London bridge wala nini alikuwa Jambazi kuu kwa watu weusi ametunyonya sana na kutufanya maskini wa kufa mpaka vizazi vyetu,kapora mali kibao hasa madini yetu
Aende motoni tu huyo kama mnavyosemaga watu wa dini
Mnyonyaji mkubwa uliyenae kwa sasa ni samia vp umechukua hatua gani kupata haki yako?
 
Tunaomboleza kwa siku 5 na ndani ya siku hizo nasikia hakuna tozo Rip bibi
 
Huyo hakuna cha London bridge wala nini alikuwa Jambazi kuu kwa watu weusi ametunyonya sana na kutufanya maskini wa kufa mpaka vizazi vyetu,kapora mali kibao hasa madini yetu
Aende motoni tu huyo kama mnavyosemaga watu wa dini
Kipindi anapora, viongozi wa nchi zenu walikuwa wapi?
Alaumiwe yeye au viongozi wako?
 
Back
Top Bottom