Operation Barracuda: "Mission hatari ya kijasusi nchini Kongo"

OPERATION BARRACUDA: "MISSION HATARI ZAIDI YA KIJASUSI KUFANYIKA AFRIKA" ILIYOSUKWA KUTAMATISHA MAISHA YA PATRICE LUMUMBA, NA KUZIMA NDOTO YA KILE KILICHOITWA MUSTAKABALI WA KONGO.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA).
Saturday -10/07/2021
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania

Tarehe 16 January 1961 kwenye ofisi ya shirika la ujasusi la Uberigiji lijulikanalo kama "Veiligheid van de Staat - Sûreté de l'Etat" au kwa kifupi 'VSSE' walipokea barua kutoka wizara ya kigeni ya Uberigiji yenye kuonesha kuidhinishwa kwa kifo cha Patrice Lumumba kwa kupigwa risasi na wadunguaji hodari kutoka Marekani na Uberigiji yenyewe, barua hiyo yenye code Vsse-L551-30 ilipokelewa na kukabidhiwa waziri aliyekuwa anashugurikia masuala ya Afrika bwana Harold Charles d'Aspremont Lynden ambae ofisi yake ipo jengo Namba 62534 mtaa wa 6, jengo ambalo linatazamana na ofisi ya shirika la ujasusi la Uberigiji lililopo mtaa huo huo wa No.6 street, kitongoji cha Boulevard du Roi Albert, jijini Brussels, Belgium.

Waziri Harold Charles d'Aspremont Lynden bila kuchelewa alituma ujumbe kwa kutumia fax kwenda Nairobi, kwenye ubalozi wa Marekani, ikumbukwe kuwa ubarozi wa Nairobi nchini Kenya ndio uliokuwa na ofisi za siri za CIA zilizokuwa zinafanya kazi za ujasusi wote katika nchi za Afrika mashariki na kati kwa kipindi hicho, Harold Charles d'Aspremont Lynden kupitia ujumbe huo alitaka maafisa udunguaji wa CIA waondoke siku hiyo hiyo kuelekea Kinshasa kwa kazi maalumu ya kifo cha Patrice Lumumba.

Usiku huo maafisa CIA, ambao ni wataalam wa udunguaji risasi walisafiri kuelekea Kinshasa wakitokea Nairobi, waliondoka na ndege ya shirika la Uingereza la British airways, maafisa hao kwasababu za kiusalama ilibidi watumie uwanja wa ndege wa Nairobi international airport (Sasa jomo Kenyatta international airport) kuelekea Kinshasa ila iliwabidi kupitia Luanda Angola.

Sababu ya kupita Angola ili kuwa ni kwa sababu za kiusalama zaidi, hili ntalieleza kwa upana zaidi huko mbeleni, lakini jambo la kujua hapa ni kwamba maafisa hao ilibidi kuwapoteza maafisa kadhaa nchini Kenya kwakuwa operation hii ilitakiwa kufanyika kwa siri kubwa bila vyombo vingine kujua.

Hati ya kuidhinisha Operation Barracuda (ambayo Picha yake nimeiambatanisha) Juu ya mission ya kifo cha Patrice Lumumba ilikuwa na shariti moja kubwa la kuwa mission hii itatakiwa kufanyika kwa usiri mkubwa sana bila kuhusisha vyombo vingine vyovyote vile vya nje ya Marekani wala ndani ya Marekani.

Raisi wa Marekani Dwight Eisenhower alitaka mission hii ihusishwe na vyombo vya kijasusi vya CIA, Ml6 na VSSE pekee, kwasababu hii iliwalazimu maaofisa hao kupitia Angola kwanza kabla ya kuingia Kinshasa.

Walipo wasili Angola, walisafiri kwa ndege ndogo mpaka Brazzaville, hapo Brazzaville walisafi kwa gari ndogo aina ya pegeout 364 mpaka Kinshasa, kisha wakasafirishwa mpaka elizabethiville (Sasa Lubumbashi) kwajili ya kazi maalumu ya kumfyatulia risasi Lumumba, Je maafisa hawa wa CIA ni wakina nani? Hilo na mengi kuhusu wao ntalieleza huko mbeleni.

Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa mtu wa mwisho kutia muhuri mwekundu kuidhinisha kifo cha Patrice Lumumba ni Harold Charles d'Aspremont Lynden.

Ikumbukwe kuwa Harold Charles d'Aspremont Lynden alikuwa ndie Waziri wa mwisho wa Ubelgiji anaye husika na Makoloni, ni yeye ndie aliye amuru Patrice Lumumba na marafiki zake wawili Mpolo, na Okito ambao pia walikuwa viongozi waandamizi kwenye serikali ya kwanza ya Uhuru wa Kongo wapelekwe jimboni Katanga baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa siku mbili nyuma.

Turudi Kinshasa usiku wa tarehe 16/1/1961.........

Usiku majira ya saa 2:18, Patrice Emiery Lumumba na marafiki zake wawili waliokuwa wameshikiliwa kinguvu walipelekwa Elisabethville (ambayo ndio Lubumbashi ya sasa) Walipofika huko, yeye na wenzake walipelekwa kwenye gereza la kificho linalojulikana kama jengo la Brouwez, huko Lubumbashi, ambapo huko Lumumba na wenzake wakiwa hapo walipigwa kikatili na kuteswa sana.

Wakiwa hapo Katanga maafisa wa Ubelgiji, kwa kushikiliana na Moise Tshombe, kiongozi wa Jimbo la Katanga lilo kuwa limejitenga pamoja na baraza lake la mawaziri walikabidhiwa Lumumba na wenzake na kisha kupewa utaratibu wote wa kutamatisha maisha ya Lumumba na wenzie.

Siku iliyofuata yani tarehe 17/1/1961 majira ya usiku, Patrice Lumumba na wenzie walipelekwa msituni mahali ambapo vikosi vitatu vya kulenga shabaha vikiwa vimekwisha adaliwa, kwa ushirika na Serikali ya Uberigiji na maafisa kadhaa wa CIA kutoka Marekani walisimamia kutekeleza mauaji ya Lumumba na wenzake wawili, taarifa ya kueleza hili ilielezwa na mwanahistoria na mwanasosholojia Ludo De Witte mwaka 2006 miaka 55 baada ya kifo cha Patrice Lumumba, ntalieleza hili kwa undani zaidi huko mbele.

Sasa basi.................

Kamishna wa Polisi wa Ubelgiji aliyeitwa Frans Verscheure ambaye alikuwa na amri ya kuuwawa kwa Lumumba na wale wengine wawili ndie aliyeruhusu wauwawe kwa risasi huko msituni, baada ya amri hiyo kutoka kwa Frans Verscheure ndipo afisa maalumu kutoka Uberigiji aliyeitwa Julien Gat aliamuru risasi zifyatuliwe kwa Lumumba na wenzie.

Patrice Lumumba, na marafiki zake wawili, Mpolo, na Okito walifungwa kwenye mti na kisha kufyatuliwa risasi moja moja kwa kila mmoja, tukio hilo lilitekelezwa mnamo Januari 17, 1961, majira ya saa 21:40 na 21:43 kulingana na ripoti ya shirika la ujasusi la Ubelgiji VSSE iliyotolewa mwaka 2012, kwa mujibu wa ripoti hiyo inaeleza kuwa baada ya kuwawa kwa Lumumba na wenzie muda mfupi baadaye, Afisa wa Ubelgiji aliye itwa Gerndarmerie Gerard Soete na timu yake walizikatakata vipande maiti ya Lumumba na wenzake, na kuzudumbukiza kwenye asidi.

Tukio hili lilifanyika baada ya kuizika miili hiyo na kuifukua baada ya kuhofia kujulikana kwa vifo vyao ndipo walipo amua kuzudumbukiza kwenye asidi.

Swali la kujiuliza hapa kwanini Uberigiji iliamua kumuua Lumumba? Lakini swali la kujiuliza zaidi ni kwanini Uberigiji na mataifa ya magharibi walichagua njia ya kikatili kiasi hiki kumuua Lumumba? Wakati tunajiuliza maswali haya jiulize pia ni uhatari upi aliokuwa nao Patrice Lumumba mpaka kifo chake kikaandalia kwa ustadi na unyama kiasi hicho? Mujibu ya maswali haya yapo kwenye mission iliyoandaliwa na CIA na kuinjiniwa na MI6 na kisha kuratibiwa kwa ufundi na VSSE, mission hiyo ilipewa Jina la "Operation Barracuda".

Neno "Barracuda" ni neno lenye asili ya Latin America, lenye maana ya "Samaki wakubwa wa baharini walao Samaki wadogo", Hivyo misheni ya kutamatisha maisha ya Patrice Lumumba ilipewa jina "Operation Barracuda", ndio code name ya kijasusi iliyotumika kukamilisha unyama na mauaji ya Lumumba, Misheni hii iliratibiwa na mashirika ya kijasusi ya CIA ya Marekani, Ml6 ya Uingeraza na VSSE ya Uberigiji, na kutamatisha ndoto ya Uhuru ndani ya Kongo huku yakimwaga damu ya mwana Afrika, mwasisi, baba wa taifa na mkombozi wa Wakongomani Patrice Emery Élias Okit'Asombo Lumumba.

Maandalizi ya kifo cha Patrice Lumumba kupitia Operation Barracuda yalifanyika Washington DC, nchini ya utawala wa raisi Dwight Eisenhower, Huyu Dwight Eisenhower ndie raisi wa Marekani anaetajwa kuhusika na mission nyingi za kijasusi ndani na nje ya Marekani, ni yeye aliye imalisha mifumo ya shirika la ujasusi la Marekani kuwa imara na hatari mpaka Sasa.

Mipango inaanza kusukwa Washington DC.............

Jumatatu July 13, 1960 Washington D.C, wiki Ikiwa inaanza na pilikapilika zikiwa zinaanza ndani ya ikulu ya White House, kuliripotiwa kuwepo wageni waliotaka kumuona rais, "Put that away." Hiyo ndiyo ilikuwa sentesi ya kwanza ya Rais Dwight Eisenhower kuitamka mara baada ya kuingia ndani ya chumba cha Oval Office katika makazi yake ya White house, Maneno hayo Dwight Eisenhower aliyatamka mara baada ya kumuona moja ya wageni wake waliokuja ofisini kwake anatoa makaratasi kutoka kwenye briefcase iliyokuwa imebebwa na mmoja wapo.

Huu ulikuwa mtindo wa Rais Eisenhower pale anapotaka kuongea na mtu mambo ya siri nzito na akiwa hana mpango wa kuwashirikisha Baraza la Mawaziri au Baraza la Ulinzi, Huyu Dwight Eisenhower ndie rais anayetajwa kutekeleza misheni nyingi zaidi za kijasusi na zenye mafanikio makubwa, baada ya utulivu kidogo rais na wageni wake wakaanza kikao, Kikao hiki kilikuwa ni kikao cha siri kubwa na kilihusisha washiriki watatu tu, Yani Rais Dwight Eisenhower mwenyewe na wageni wawili ambao walikuwa ni ndugu, Mtu na kaka yake, katika wageni hao mmoja aliitwa John Foster Dulles ambaye alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje wa Marekani na Wapili aliitwa Allen Dulles ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Shirika la kijasusi la Marekani, CIA.

Eisenhower alikuwa na utaratibu wa kufanya mambo yake kwa siri sana, tena hakupenda kushilikisha masuala yake ya misheni za kijasusi na timu kubwa ya Pentagon au baraza lake la mawaziri, hivyo mtindo huo wa yeye kutotaka kuwepo na aina yoyote ya nyaraka inaweza kuihusisha ofisi ya Rais pale ambapo akitaka kuamuru ifanyike jambo ambalo alihisi linaweza lisiungwe mkono na jamii ya kimataifa, Na hii ndio ilikuwa sababu ya kumuamuru Allen Dulles arudishe makaratasi yake kwenye briefcase.

Wiki nne zilizopita yani tarehe 1 July 1960, kilifanyika kikao kama hiki kati ya watatu hawa, kikao hicho kilifanyika baada ya kupokea, file lilo beba barua iliyotumwa kwa telegram kuja kwa Rais Dwight D. Eisenhower, barua hiyo ilitoka London Uingeraza, kwenye shirika la kijasusi la Uingeraza la M16 , ilisomeka "Tunaitaji kutaarifu kuwa ofisi ya Waziri mkuu No.10 Downing street, inaitaji usaidizi juu ya mpango wa kumwua Lumumba". Hivyo barua hiyo ilionesha kuwa baraka na mipango yote kutoka kwa Waziri mkuu wa Uingeraza wakati huo Winston Churchill ilikuwa Imekamilika, isipokuwa iliitaji msaada kutoka Marekani.

Katika kikao hicho ndani ya ofisi ya rais wa Marekani ilibidi wazungumzie kukubali kushiriki katika misheni hii au watupilie mbali mpango huu kama walivyo tupia mbali mpango wa kumg'oa madarakani rais wa Misri wakati huo Abdul Nasser Gamal, na juu ya changamoto kubwa ya kufanikisha jambo hilo, jambo lenyewe ilikuwa ni kumuondosha madarakani Patrice Emiery Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo huru.

Mwezi mmoja nyuma Kongo DRC............

Wakati huo Kongo DRC ikiitwa Kongo Belgium ilikuwa ndio imepata uhuru wake, ilikuwa ni tarehe 30 June 1960, pale Uberigiji walipoamua kuwapatia wakongo uhuru wao, katika siku ya kukabidhiwa uhuru, mfalme wa Ubergiji Baudoin alihudhuria na kutoa hotuba yake, katika hotuba ya mfalme huyo alisifia nchi yake ya Ubergiji kwa kuwapatia maendeleo Kongo, na kumwagia sifa babu yake, mfalme Leopard ll kwa kuwastarabisha wakongomani, Lakini sherehe hiyo iliingia dosari wakati wa Lumumba alipotoa hotuba iliyo wakadhibisha sana Wabelgiji na mapebari wote walio hudhuria sherehe ile.(Unawaze kuitazama hotuba hiyo ya Patrice Lumumba aliyoitoa kwa lugha ya kiswahili kupitia hapa )

Kwani Lumumba hakufurahishwa hata kidogo na uhuru elekezi na mashariti yaliyo kuwa yakitolewa na mfalme huyo wa Ubergiji, Pamoja na kwamba hakuwekwa kwenye ratiba ya wazungumzaji wa siku ile, Lumbumba alisimama na kuhutubia ukumbi ule wa "Nàtiónal de Palace" na kutoa hotuba kali iliyo tibua hali ya mambo kwa kusema.....

“…Tulizoea matusi, dhihaka na vipigo asubuhi, mchana na usiku, kwa sababu sisi ni watu weusi… Tumeona ardhi yetu ikinajisiwa kwa sheria zilizowapendelea wazungu na kuwabagua weusi. Hatujasahau kwamba sheria hazikuwa sawa kwa mweupe na mweusi, zilikuwa rafiki kwao na katili kwa wengine.” Baada ya kutoa hotuba ile, Lumumba alikwenda kukaa kwenye kiti chake huku akipongezwa kwa makofi na wajumbe wake na marafiki zake wazalendo kutia ndani Anton Gizenga, na Pierre Mulele, rais kasavubu, mfalme Boudoin na wageni kutoka nje wakipigwa na butwa na kukadhibishwa na hotuba hiyo. Na Lumumba alipopita mbele ya mfalme wa Ubeligiji alimwangalia na kumwambia, '‘Sisi sio nyani wenu tena.’'

Kupitia hotuba hiyo serikali ya Uberigiji walianza kuamini kuwa Lumumba awafai kusalia Kongo kama kiongozi, hofu ya Wabelgiji juu ya siasa za mrengo wa kushoto za Patrice Lumumba na Chama chake cha “The Movement National Congolais” (MNC) kutumikia Congo, waliona ni tishio dhidi ya masrahi yao, Hofu yao iliongezeka zaidi baada ya MNC kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1960, na Lumumba kuunda serikali, lakini kwa upinzani mkubwa wa Wabelgiji walitaka Joseph Kasavubu, kibaraka wao wa Chama cha kikabila cha ABAKO ambacho hakikushinda, ndio kiunde serikali, kufatia hotuba ile na fununu za Lumumba kuwa na ushirika na siasa za kikominist uliwafanya Ubergiji kuanza mikakati ya kuidhofisha serikali halali ya Lumumba.

Hivyo Serikali ya Ubergiji walituma ombi Uingeraza kuwaomba wawasaidie kuandaa mpango wa kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Lumumba, mkuu wa mikakati na misheni za kijasusi wa CIA James Angleton,(CIA Chief of Counterintelligence), alieleza mwaka 1974, kuwa "mpango wa Mauuaji ya Lumumba yalipangwa nchini Ubergiji, kupitia shirika lao la kijasusi la VSSE, na baadae Uingeraza kuishirikisha Marekani..." Wasiwasi mkubwa wa Ubergiji na Uingereza mpaka kuamua kuishirikisha Marekani katika mpango huu wa kuuliwa Lumumba, ulikiwa ni mwenendo wa Lumumba dhidi ya masrahi ya kimagharibi na hasa hasa namna ambavyo aliiandama Uberigiji na makampuni ya kibepari yaliyo kuwa nchini Kongo, Aliwatia sumu zaidi pale alipo onekana kuukaribisha Ukominist Kongo.

Tishio la Usovieti na kuingia kwa siasa za ukominist nchini Kongo, ikitegemea kipindi hicho dunia ilikuwa kwenye minyukano mikali dhidi ya Ubepari na Ukominist, kulifanya kuchochea hasira kwa mataifa ya magharibi dhidi ya Lumumba, Hali hii ikaamsha hasira za Uingereza na Uberigiji na wakaweka nia kwamba ni lazima Lumumba aondoke madarakani, Kikwazo kikubwa kilikuwa ni kwamba Lumumba alikuwa amechaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura na kushinda na alikuwa anakubalika mno na wananchi wa Kongo kipindi hicho, hivyo kumuondoa kirahisi ingekuwa swala gumu sana, kufatia mazingira hayo ndipo wakaona umuhimu wa kuwaomba wamarekani wawasaidie kutimiza amza yao.

Sasa turejee tene White House, jijini Washington DC..............

Kwenye ikulu ya White house, Washington DC, Wiki nne nyuma katika kikao chao cha kwanza Rais Eisenhower alikuwa amewapa ''Majukumu'' waziri wake wa kigeni na mkurugenzi wa CIA wakaandae mkakati wa kutekeleza kumuondosha Lumumba ambao watakuja kuuwasilisha kwenye kikao cha leo hii, Ndipo Mkurugenzi wa CIA Allan Dulles akaanza kumpa mkakati alioufikiria namna ya kufanikisha kumuondosha Lumumba, Kwanza akaanza kumpa tahadhari kadhaa za kuzingatia kuhusu mpango ambao watauweka. Moja ya tahadhari ya mpango huo ni vyema usijadiliwe kwenye Baraza la Mawaziri au Baraza la Usalama wa Taifa, kwasababu lazima utazua mtafaruku mkubwa kwasababu ni dhahiri baadhi ya watu wataupinga.

Pia, Dulles alitaka mpango huo ubaki siri kwanza katika viongozi wa Marekani, alisema kama ni watu wachache wataufahamu hii ina maana uwezekano wa siri kuvuja utakuwa ni mdogo. Lakini pia Allan Dulles akashauri ni lazima oparesheni hii itekelezwa pasipo watu kujua kuna uhusika wa Marekani ili kufanya dunia na washirika wa Marekani kukubaliana na serikali mpya itakayo wekwa kama ikitokea oparesheni ikafanikiwa.

Kufatia hatua hiyo, Kwa kuzingatia hayo basi, Allan Dulles akamshauri Rais Eisenhower atumie mamlaka yake aliyopewa na sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1947 (U.S. National Security Act, 1947), kuidhinisha operation ya usiri mkubwa zaidi (Covert operation) kutekeleza Operation hiyo kumpidua Waziri mkuu Patrice Lumumba, ikumbukwe kuwa nchini Marekani Sheria hii inampa mamlaka Rais wa Marekani kuamuru kufanyika kwa "covert operation" pasipo kumuweka Rais kutambuliwa uhusika wake kwenye hilo ikitokea siri ya operation hiyo imevuja, Kwa maneno mengine Sheria hii inampa uwezo Rais kukana kuhusika kuamuru oparesheni kufanyika au kufahamu chochote juu ya kufanyika kwa oparesheni hiyo ikitokea siri imevuja kuhusu oparesheni hiyo, Hii ndio inajulikana kama 'Plausible Denialbility'.

Kwahiyo baada ya kukubaliana wote kwa pamoja juu ya kutekeleza operation hiyo, Allan Dulles mkurugenzi wa CIA, pamoja na Rais Eisenhower na John Dulles ambae alikuwa waziri wa mambo ya nje, waliamua kuipa kazi hii idara ya CIA-SAD, hii ni moja ya idara katika vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya Marekani yenye weledi, uwezo, watu, ufanisi na ruhusa ya kisheria kutekeleza mkakati wa kuingilia (intervention) nchi nyingine kwa lengo la kutekeleza mapinduzi au, mauaji maalumu kwa masrahi ya Marekani. Idara hiyo ya SAD (Special activities division), ilundwa na Marekani kama kitengo maalumu ndani ya CIA, Kutokana na changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya Marekani lakini Marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.

Kwa mantiki hiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya Marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya Marekani, Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2013 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953, Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960, kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa "Operation Mockingbird" katika taifa la Marekani, Oparesheni hii ilikuwa na lengo la ''kucontrol na kuremot" habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo.

Baada ya kuafikiana kwa pamoja na rais Dwight Eisenhower kusaini, Allan Dulles mkurugenzi wa CIA akaanda mkakati wa kuingia Kongo, mkakati huo wa kumshughulikia Lumumba ukapewa jina, (code name) "Operation Barracuda", siku iliyofuata ndani ya Ofisi za CIA zilizopo kitongoji cha Langley jijini Virginia, Dulles akapanga askari wa SAD ndani ya CIA, watakao simamia mpango huu. Jasusi nguli wa CIA, Frank Carlucci, akapewa jukumu hilo la kumuangamiza Patrice Lumumba.

Huyu Carlucci Kabla ya kupelekwa Kongo kumshughurikia Lumumba, amewahi kufanya kazi Ureno alikopewa jina la “The Hangman of Portugal” ikimaanisha "Mnyonyaji watu wa Ureno" kwa ukatili wake dhidi ya wanaharakati wa kikomunisti, Na baada ya kutekeleza mission hizo za kijasusi mwaka 1965, Carlucci alirejea Marekani na alipanda cheo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa CIA. Carlucci baada ya kupokea jukumu hilo, asubuhi ya July 18 akawasiliana na maafisa wa kijasusi wa Ml6 wa Uingeraza, aliwapatia mpango mzima wa operation ile ya Barracuda, na namna ya kumuangamiza Lumumba.

Maafisa ujasusi wa CIA, M16 na wale wa VSSE wa Uberigiji, wakiongozwa na Carlucci wakawasili Leopardville (sasa ikijulikana Kinshasa), August 19 1960, Leopardville walipokelewa na jasusi maalumu aliyeitwa Larry Devlin, huyu alitangulia mapema Kongo ili kuanza kazi, mpango wa kwanza ilikuwa ni kumuua Lumumba kwa sumu, hivyo jukumu hilo alipewa daktar wa kimarekani ambae pia alikuwa ni askari wa CIA, aliyeitwa Dr, Sidney Gottlieb (Senior CIA scientist), Dr Sidney Gottlieb akatengeneza sumu na kuituma Kongo, sumu hiyo ilitoka Virginia Marekani kupitia Accra Ghana, kupitia "diplomatic pouch" hizi diplomatic pouch ni 'Vifurushi' maalumu vya kidiplomasia ambavyo huwa havikaguliwi mahali popote pale.

Huyu jasusi wa CIA, Dr.Sidney Gottlieb alichagua kutumia njia ya sumu ya kumuangamiza Lumumba kwakua ndio njia nyepesi isiyo acha madhara kijasusi wala alama yoyote baada ya kutekelezwa, sumu hiyo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani madhara yake hayana tiba, Dr.Sidney alisafiri kwenda Kongo ili kumuelekeza afisa wa CIA aliyekuwa Leopardville Kongo, Larry Devlin jinsi ya kuitumia, mpango wa sumu hiyo ilikusudiwa waiweke kwenye chakula au dawa ya meno atakayotumia Lumumba, Lakini bahati mbaya CIA walishindwa kukamilisha mpango huo kwa wakati huo, kutokana na sumu ku-expire (kupitia muda wa kutumika), kutokana na kuchelewa kufika Leopardville, Hivyo ikatupwa mto Kongo na mpango huo wa plan "A" ukaferi.

Plan "B" ikasukwa....................

Taarifa ikatumwa Washington DC kwa Waziri wa mashauri ya kigeni, John Dulles, juu ya kuferi mpango huo, Waziri huyo kwa kushirikiana na mkurugenzi wake wa CIA Allan Dulles, haraka wakawasiliana na maafisa wa London, M16 na wale wa VSSE, Brussels Uberigiji, na kuazimia kutumia njia ya kuipa nguvu serikali haramu ya Kasavubu, Mobutu na ile ya Katanga chini ya Moise Tchombe, Ili kuivuluga (paralized) serikali halali ya Lumumba, mpango huu ukaonesha matunda na mafaniko ya mission yenyewe.

Sasa turudi mpaka Leopardville (Kinshasa)..................

Ilikuwa ni asubuhi ya saa 10:00, Tarehe 11July 1960, pale Jimbo la Katanga lenye utajiri mkubwa wa madini, lilipo jitangazia uhuru wake chini ya Waziri wake Mkuu, Moise Tshombe, huku akiungwa mkono na Ubelgiji na makampuni makubwa ya uchimbaji madini, Kujitenga kwa Katanga ilitoka mapema tu baada ya uhuru, kwani siku chache baada ya uhuru kuliibuka machafuko yaliyosababishwa na wanajeshi wa jeshi la Congo ambao pamoja na kutaka maslahi zaidi na kupandishwa vyeo, lakini walishinikiza kuondolewa kwa wanajeshi wa kibelgiji ndani ya jeshi la Congo.

Lumumba alijibu malalamiko ya askali hao kwa kuwapadisha vyeo askali hao, kwa kumteua mkuu wa majeshi wa kwanza mweusi Victor Lundula kuwa mkuu wa jeshi, na Joseph Desire Mobutu kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi, Ukiachilia mbali madai ya wanajeshi hao, pia kuliibuka na jaribio la jimbo la katanga na kasai kutaka kujitenga, Hali hii ilichochea mapigano zaidi kwani wanajeshi wa Tshombe walikuwa wakipambana na wanajeshi wa serikali ya Kasavubu, Hali hiyo ya machafuko, ilipelekea Vikosi vya umoja wa mataifa 'UN' kuingilia kati Kwa lengo la kuzuia machafuko na kutuliza Amani, Umoja wa mataifa wakaunda kikosi maalumu cha " ONUC" chini ya Mswedeni General Carl Von Horn ili kwenda kutuliza hali ya mambo.

Lakini Patrice Lumumba hakuridhishwa na utendaji kazi wa vikosi vya ONUC-UN kwani aliona havifanyi kazi ipasavyo, Hivyo basi alielekea upande wa Umoja wa Usovieti 'USSR' Kwa kuwaomba misaada zaidi juu ya kuirejesha katanga iliyokuwa imeasi, Pasina kuchelewa, majeshi ya Usovieti yaliingia Congo na kuanza kushambulia wapiganaji wa Katanga waliokuwa wanataka kujitenga, Kitendo cha Lumumba kuomba misaada USSR, kiliwachukiza sana mataifa ya magharibi na Marekani, na kuwafanya kuharakisha operation yao haraka, kwani walihofia kuenea kwa itikadi za kikomunisti nchini Congo, Ndipo wakaanza kumshinikiza Rais Kasavubu kumuondoa madarakani Patrice Lumumba, Kasavubu akashawishika na mwishowe akamfuta kazi Lumumba, Lumumba akapinga, Bunge nalo likapinga kitendo cha kasavubu kumfukuza kazi Lumumba kwa kukosoa hatua hiyo kuwa ni kinyume na katiba.

Bunge lilibatilisha maamuzi ya Kasavubu na Lumumba kufukuzana, lakini tayari mtafaruku huo ulikuwa umeingiza wahasimu wakubwa wa kimataifa kutia ndani Marekani na nchi za Ulaya upande wa Kasavubu, na kambi ya kikomunisti upande wa Lumumba.

Septemba14, 1960, Kanali Joseph Mobutu akiwa mnadhimu wa jeshi, akashawishiwa kufanya mapinduzi kwa kuhaidiwa madaraka na ulinzi, baada ya makubaliano baina ya Marekani na Mobutu na kwa kupewa nguvu na CIA, alitangaza kuingilia kati mtafaruku huo kwa kunyakua madaraka akidai kushikilia hadi mwishoni mwa mwaka 1960, yaani Desemba 1960. Kisha akaagiza kufukuza nchini Kongo Warusi na Wachek wote, Lumumba akawekwa kizuizini ndani ya Makazi ya Waziri Mkuu kwa kisingizio cha kumpa ulinzi, lakini akambakiza Kasavubu madarakani kama Rais, kisha kuwatupa nje ya serikali wafuasi wote wa Lumumba.

Kwa kuhofia Lumumba angeweza kurejea madarakani, November 19, 1960, Baraza la Usalama la umoja wa mataifa, chini ya shinikizo la Rais Dawight D. Eisenhower, ulitangaza kuitambua serikali ya Kasavubu na Mobutu, hata hivyo maafisa wa ujasusi wakawasilisha mpango wa mwisho wa kumwua Lumumba, mbele ya rais Dwight Eisenhower na Allan Dulles, operation Barracuda ikaenda kutekeleza kwa kumuua kabisa Lumumba, operation hiyo iliratibiwa chini ya mwanasayansi Dakta Sidney Gottlieb, Frank Carlucci na James Angleton

Wakati operation Barracuda ikiendelea kutekeleza kwa ufanisi mkubwa, na kwakushirikiana na Wabelgiji nao walikuwa na mpango wao upande wa pili huku wao wakiwa wamepewa jukumu la kuvuruga na kuchochea moto, kwa kuwashirikisha wakina Mobutu, Tshombe na wataalamu wa nje, huku operation hiyo Ikiwa imepewa baraka na Mfalme Boudouin wa Ubelgiji. Lumumba akiwa kizuizini nyumbani kwake kwenye makazi ya Waziri mkuu mjini Leopardville, tarehe hiyo 12/9/1960, huku nyumba yake ikiwa imezungukwa na askari wa Umoja wa Mataifa waliosheheni silaha nzito nzito, Usiku huo huo akiwa chini ya ulinzi mkali, wafuasi wake walijipenyeza na kufanikiwa kumtorosha Lumumba na kumkimbiza mafichoni Stanleyville, Lumumba aliamua kuhamia Kasangani, ngome yake kisiasa, ili kuanzisha utawala wake huko kwa lengo la kuikomboa Kongo.

Safari yake ilichukuwa siku kadhaa kwa vile alikuwa anasimama mara kwa mara kusalimia umati wa watu uliokuwa wanamngojea, bila kujua kuwa taarifa za kutoloka kwake Kinshasa zilimfikia Mobutu, na tayali askali wa Mobutu walikuwa wakimfatilia kwa nyuma, hatimae Lumumba akakamatwa Desemba1, 1960, akiwa nusu ya safari kabla ya kuingia Stanleyville. Kutokana na kunyimwa ulinzi wa Vikosi vya Umoja wa Mataifa, alipigwa sana, kisha akarejeshwa Leopoldville kwa ndege chini ya ulinzi na alipofikishwa mbele ya Mobutu, alifungwa kamba mikononi na kutemewa mate usoni na Mobutu huku akiambiwa: “Haya sema! Uliapa ungenimaliza, sasa ni mimi ndiye nitakayekumaliza”.

Kufatia kukamatwa Lumumba Wafuasi wa Lumumba kule Stanleyville, walipata taarifa hizo za kukamatwa kwa Lumumba, wakiwa wanaongozwa na Antoine Gizenga, walijitangazia serikali yao ya “Free Republic of the Congo” (FRC) na kuanzisha Jeshi la Jamhuri hiyo., kufatia hali hiyo Congo ikasambaratika kwa kugawanyika katika tawala nne, huku kila moja na mfadhili wake wa kigeni. Wakati Serikali ya Mobutu na Kasavubu ikisimamiwa na kupewa nguvu na nchi za Magharibi, Serikali ya Gizenga ilipata misaada kutoka Kambi ya Urusi, na kwa viongozi wanamapinduzi kama Rais Abdel Gamal Nasser wa Misri, wakati Serikali ya Katanga (Elizabethville-Katanga) chini ya Moise Tshombe, ilitegemea msaada wa Ubelgiji ambapo Serikali ya Kasai Kusini, chini ya Albert Kalonji, nayo pia ilipokea usaidizi kutoka kwa Wabelgiji.

Serikali ya Gizenga kwa kushirikiana na Pierre Mulele iliyoundwa kwa jina la Lumumba, na kujiita jeshi la simba ilizidi kupata nguvu kiasi kwamba kufikia Desemba 20, 1960, Serikali ya Jimbo la Kivu, Mashariki mwa Kongo, iliangukia mikononi mwa majeshi ya Gizenga. Kwa kufadhaika na tukio hilo, Mobutu alituma vikosi vyake, lakini vilinyukwa vibaya na kutawanyika, Siku saba baadaye, majeshi ya Gizenga yakaingia na kuteka Katanga ya Kaskazini chini ya Mkuu wa kikosi Laurent Desire Kabila (Baba yake Joseph kabila),na kuanzisha Jimbo la “Lualaba”, huku kukiwa na habari za vuguvugu la mapinduzi nchi nzima kwa lengo la kumrejesha Lumumba madarakani.

Kwa sababu hiyo, Serikali ya Mobutu na Kasavubu iliamua kumhamishia Lumumba jimboni Kasai karibu na katanga kwa Moise Tchombe, kwenye Gereza la Thysville karibu na Elizabethville, kwa mhasimu wake mkubwa, Moise Tshombe, hatua iliyotafsiriwa sawa na kumhukumu kifo, kwa kuwa asingeweza kusalimika mikononi mwa hasimu wake huyo. Alisafirishwa kwa ndege mpaka Katanga, alipo fika huko mpango wa kuuwawa ukaandaliwa, maaskali wa Tchombe ukaitaarifu Uberigiji, maafisa usalama wa Uberigiji, CIA na M16 pamoja na askali maalumu wa shabaha (sniper) kutoka Marekani na Uingeraza ukawekwa sawa kwa kummaliza Lumumba.

Januari 17, 1961, Lumumba na mahabusu wenzake wawili, yani Waziri wa Vijana, Mourice Mpolo na Makamu wa Rais wa Seneti, Joseph Okito, ambao walikamatwa pamoja wakiwa njiani kutorokea Stanleyville, awalichukuliwa kutoka Kambi ya kijeshi ya Thysville iliyopo Jimboni Kasai na Mkuu wa Usalama wa Mobutu, Victor Nendaka, akifuatana na askari watatu wa kabila la Baluba na kupelekwa uwanja wa ndege wa Moanda, Lumumba alipo wasili uwanjani, walikaribishwa kwa vipigo vizito kutoka kwa askari wa Kibelgiji na Katanga, kisha kutupwa nyuma ya gari kupelekwa kwenye nyumba pweke, maili mbili kutoka hapo, nyumba iliyolindwa na majeshi ya Kibelgiji na Polisi chini ya Afisa wa Kibelgiji. Hapo tena, Tshombe na mawaziri wake walishiriki kumpiga na kumtesa kinyama bafuni, kisha watesi hao wakatoka wametapakaa damu mwilini, Huku wakiwa wamelewa chakali, walitangaza Lumumba “auwawe mara moja”.

Ilipo fika usiku wa saa 4:00, tarehe hiyo hiyo 17/1/1961 Lumumba na wenzake wawili walichukuliwa kwa gari hadi kwenye vichaka, maili 30 toka Thysville, Tshombe akiongoza msafara, akiwamo pia Kamishna wa Polisi wa Kibelgiji, Frans Verscheure na walengaji shabaha kutoka Marekani.

Walipofikishwa eneo lililokusudiwa wakapekuliwa, wakiwa wamevaa kaptura na fulana tu, walianza kuuwawa, Huku Lumumba alikuwa wa mwisho kuuawa kwa kupigwa risasi na kikosi cha Askari wenye shabaha na kisha kuzikwa huko huko porini, Kesho yake ya tarahe 18/1/1961 serikali ya Moise Tchombe ikatangaza habari za uongo kwamba Lumumba na wenzake waliuawa na wanavijiji wenye hasira walipokuwa wakijaribu kutoroka kizuizini.

kwa kuhofia kuvuja kwa taarifa za unyama walio fanya, Usiku uliofuata, askali hao wa Uberigiji walikwenda kufukua miili ya Lumumba na wenzake, baada ya kufukuliwa ilisafirishwa hadi Kasenga, maili 120 Kaskazini Mashariki mwa Elizabethville, ambako ilikatwakatwa vipande vipande na kutupwa kwenye pipa la tindikali (Sulphuri acid), na kuyeyuka, mafuvu yao yakasagwa unga, mifupa na meno yakatupwa kwa kutawanywa porini wakati wauaji walipokuwa wakirejea Elizabethville, Asubuhi ya tarehe 20/1/1961, jasusi Larry Devlin aliitaarifu Washington DC kwa code kuwa "Mission 009321 operation Barracuda is over".

Kule Washington mtu wa kwanza kupata taarifa juu ya kukamilika kwa operation barracuda alikuwa Waziri wa kigeni Jonh Dulles, haraka akamtaalifu mkurugenzi wa CIA, Allan Dulles, na baadae taarifa zikamfikia rais Dwight Eisenhower, Wakati huo Dwight Eisenhower ndio alikuwa anakwenda kumaliza muhura wake wa mwisho madarakani, hata rais aliye mfuata wa 35 Jonh F Kennedy aliendeleza kulinda masrahi ya Marekani nchini Kongo kupitia Shirika lake la Ujasusi la CIA, liliendelea kuhakikisha na kudhibiti nyendo za watawala wa Kongo ili wasije kuegemea upande wa Ukomunisti, Kwa kuthibitisha hili mwandishi Martin Meredith Kwenye kitabu chake cha "The State Of Africa, ameandika, kuwa "Mobutu kwenye safari yake ya kwanza Washington, Mei, 1963, akiwa Mkuu wa Majeshi kwenye Serikali ya Joseph Kasavubu, Rais wa Marekani, John Kennedy alimtamkia Mobutu, "Jenerali, isingelikuwa wewe, Ukomunisti ungetamalaki Kongo", huku Mobutu akimjibu, "Ninafanya niwezalo mheshimiwa raisi".

Martin Meredith kwenye kitabu chake cha "The State Of Africa" ameandika "After operation barracuda completed and his coup in 1965, Mobutu remained on the CIA's payroll for sometime and received regular briefings from Larry Devlin , the CIA station chief in Leopoldville." ( Meredith, State Of Africa, pg 294).

Baada ya "operation Barracuda" kukamilika na Lumumba kuuwawa, hatimae tarehe 21 January 1961, Kasavubu alimteua Mobutu kuwa mkuu wa majeshi ya Kongo, na miezi kadhaa iliyofuata Cyrille Adoula akachaguliwa kuwa Waziri mkuu, Kwa kipindi hiko chote, kulikua na mapambano yaliyokuwa yakiendelea kati ya majeshi ya Mobutu wakishirikiana na vikosi vya UN dhidi ya wapiganaji wa Serikali ya Antone Gizenga na yale ya katanga iliyoongozwa na Moise Tshombe, majeshi ya Moise Tshombe yalishindwa nguvu na Tchombe mwenyewe kukimbilia Northern Rhodesia (Zambia kwa sasa) na baadae Uhispania, Lakini mwaka 1964, Tshombe aliitwa kurudi nchini, ambapo Kasavubu alimteua kuwa waziri Mkuu.

Katika kipindi chake cha uwaziri mkuu Tchombe, alikabiliwa na machafuko kutoka kwa waasi, wakiongozwa na bwana Pierre Mulele na Gizenga, Huyu Pierre Mulele alikuwa mfuasi wa Patrice Lumumba, na aliongoza mapambano dhidi ya serikali kwa lengo la kutaka kumuondosha madarakani Rais Kasavubu, Mapigano yaliendelea kwa muda mrefu sana kati ya wapiganaji wa Mulele na majeshi ya serikali yakishirikiana na majeshi ya UN, Mwisho wa siku Mulele alizidiwa nguvu na kukimbilia nchini Congo-brazzaville.

Kwenye uchaguzi wa March 1965, Moise Tshombe alishinda uchaguzi, kwa hiyo ilibidi awe waziri mkuu wa Congo tena, Lakini kilichotokea ni kwamba Rais Kasavubu alimteua Évariste Kimba kuwa waziri mkuu, Kitendo hiko kiliamsha migogoro zaidi ndani ya nchi ya Congo, Jambo lilomrudisha Mobutu na kuichukua nchi tena kijeshi na kumfuta kazi kasavubu, Mobutu alichukua nafasi hiyo kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi tarehe 25 November 1965.

Hotuba yake ya kwanza baada ya kuchukua madaraka, Mobutu aliuambia umati wa watu mjini Leopoldville katika uwanja mkuu kuwa ‘’tangu wanasiasa wamechukua nchi wameharibu nchi basi kwa miaka mitano hatutakuwa na chama cha siasa wala shughuli za kisiasa’’. Nguvu za bunge zilibaki kuwa ni mhuri tu kabla ya kufutwa kabisa lakini baadae zilirudishwa, na Mobutu alijiimarisha vya kutosha.

Wakati Patrice Lumumba alipokamatwa na kuwawa Mke wake Pauline Lumumba alifanya maadamano makubwa kinshasa kulaana umoja wa mataifa kuhusika kwa kifo cha mme wake, Pauline Lumumba aliiona UN kama kibaraka wa mabeberu, kufatia hatua hiyo Februari 14, 1961, Pauline alifanya maadamano ya kutembea katika vitongoji vya jiji la Kinshasa akiwa kifua wazi (yani matiti nje), akifuatana na wanafunzi 100 na wafuasi wengine wa marehemu mumewake, kwenda makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Maandamano hayo yaliyo kusanya maelfu ya wanawake na wanaume ambao walitembea nyuma ya Pauline huku vichwa vyao vikiwa vimeinama chini, kitendo ambacho kilionesha kupinga mauaji ya Patrice Lumumba.

Pauline Opango Lumumba ni nani?....................

Pauline Opango Lumumba alizaliwa Januari 1, 1937, na kufariki dunia Desemba 23, 2014 akiwa nyumbani kwake jijini Kinshasa, taarifa ya msiba wake ulitangazwa na Lambert Mende msemaji mkuu wa serikali ya Kongo, Pauline anajulikana pia kama "Pauline Opangu Mama ya Taifa", huyu Pauline alikuwa ni mwanaharakati wa Kongo na mke wa Patrice Lumumba, Waziri Mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huru.

Alizaliwa katika kijiji cha Wembonyama, Tarafa ya Sankuru, Jimboni Kasai katika iliyokuwa Belgian Kongo, Aliolewa na Patrice Lumumba mnamo Machi 15, 1951, katika maisha yao Pauline alimzalia Lumumba watoto wanne, ambao ni Patrice, Juliana, Roland na Marie-Christine.

Lumumba na Pauline waiishi katika mazingira magumu katika uhusiano wao na hii ni kutokana na maisha ya kisiasa ya Patrice Lumumba kwani Pauline alitengwa na Lumumba kwa kifungo cha Patrice kwa mara kadhaa, hata hivyo Pauline alivumilia na kuendelea kuwa pamoja na Lumumba katika harakati za ukombozi katika kipindi chote cha kudai uhuru wa Kongo.

Pauline alikua mke wa waziri mkuu wa kwanza na Baba wa taifa la Congo, Patrice Emiery Lumumba, Pauline akiwa na umri wa miaka 23 tu alishuhudia mumewe akikamatwa, kuteswa na hadi kuuwawa kwake chini ya vibaraka wakiwa wanaongozwa na mabepari.

Pauline anakumbukwa kama mwanamke shujaa na mzalendo wa Afrika kwa kuweza kumsaidia mumewe kwenye harakati za siasa, Alikua ni miongoni mwa wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na chama kilichoanzishwa na mumewe kilichoitwa "Mouvement National Congolais" (MNC).

Hadi dakika ya mwisho mumewe anakamatwa walikua pamoja kwenye gari aina ya Reunalt 219 ambayo Lumumba alikua anajaribu kutoroka nalo kuelekea Stanleyville (sasa Kisangani), kufatia uasi uliokuwa ukiongozwa na Mobutu Seseseko, kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufika Kisangani (Stanleyville wakati huo) kwani maadui zake walimnyakua na kwenda kumtesa hadi kufikia kifo chake kwa kupigwa risasi na kuyeyusha mwili wake kwa kutumia acid huko jimboni Shaba (Katanga ya sasa).

Mwanzoni baada ya Kifo cha Lumumba Pauline aliungana na wakina Mulele, Antonne Kizenga na Lindula huko kisangani katika kuongoza jeshi liloitwa "Simba" kupinga kupinduliwa Lumumba, na kuirudisha serikali halali madarakani, Familia ilikua inapitia kwenye kipindi kigumu sana wakati huu. Madhila yote yanatokea Pauline alikua na miaka 23 tu lakini ilibidi akabiliane nayo yote yanayoendelea katika umri wake huo kutokana na njia ya mumewe aliyoamua kuishi kwa kuwapigania watu wa taifa lake,

Mnamo Februari 14, 1961, Pauline alitembea katika vitongoji vya jiji la Kinshasa akiwa kifua wazi (yani matiti nje), akifuatana na wanafunzi 100 na wafuasi wengine wa marehemu mumewake, kwenda makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Maandamano hayo yaliyo kusanya maelfu ya wanawake na wanaume ambao walitembea nyuma ya Pauline huku vichwa vyao vikiwa vimeinama chini, kitendo ambacho kilionesha kupinga mauaji ya Patrice Lumumba.

Katika makao makuu ya UN, Pauline, pamoja na Albert Lumumba, Joseph Lutula na mtoto mdogo (aliyeitwa Marie-Christine) wa Pauline, ambaye alikuwa amembeba mgongoni, alikutana na Rajeshwar Dayal, mwakilishi wa UN nchini Kongo, Kufuatia mkutano huo, UN ilikubali kusaidia kuupata mwili wa Lumumba ili ufanyiwe mazishi ya Kikristo katika mji mkuu wa Leopoldville (sasa Kinshasa), Hata hivyo Maombi hayo ayakufanikiwa na mwili wa Lumumba haukupatikana, jambo hilo lilimuumiza sana Pauline.

Bibie Pauline aliamua kuomboleza msiba wa mumewe akiwa na waombelezaji waliomuunga mkono kwa kutembea kwa miguu katika mitaa ya mji wa Leopoldville (sasa Kinshasa). Wakati anaomboleza kwa kutembea mitaani, alikua kifua wazi (matiti nje) kama uonavyo kwenye picha na hii aliifanya kuonyesha hasira zake na kupinga juu ya mauaji yaliyomkuta mumewe Lumumba kwamba ni ya uonevu hakustahili kufanyiwa hivyo.

Lakini pili ishara hiyo ya mwanamke kutembea huku matiti yakiwa nje kwa mila za kiafrika ni ishara ya kutoa Laana na hisia kali kwa watendaji walio husika, kwa Pauline tukio lile alifanya kutoa laana kwa kuwalaani wote wakongo walio husika katika Mauaji ya mume wake Patrice Lumumba, na ukweli laana ile aikumuacha salama Mobutu miaka 48 baadae kwani nae alikufa kifo cha aibu kwa kansa iliyo ozesha korodani zake na kuzikwa na watu 4 kama mbwa, Wengi ya watu walio husika katika mauaji ya Lumumba laana ya Pauline iliwafuata kwani vifo vyao vilikuwa kama mbwa koko, kwani wengi wao walikufa kwenye vita ya kuuangusha utawala wa Mobutu Seseseko mwaka 1997.

Pauline Opango alitembea umbali wa kilimeta 10 kuelekea kwenye kituo cha umoja wa mataifa. Na hili swala la kuandamana kwa wanawake wa kiafrika wakiwa maziwa wazi sio geni sana lilishatokea pia nchini Nigeria mwaka 1929, wanawake wa Aba walipokua wanawapinga wakoloni wa kiingereza. Waliandamana maziwa yakiwa wazi hadi kwenye nyumba za vibaraka wao.

Bibie Pauline baada ya kuomboleza msiba wa mumewe kwa mtindo ule aliamsha hisia kwa wauwaji wa mumewe na kunza kumuandama hadi alipo amua kukimbilia uhamishoni nchi mbalimbali ikiwemo Misri ambako huko alipokelewa na Nasser Gamal na kupewa hifadhi ya kisiasa, Pauline alirudi Kongo mwaka 1990 baada ya serikali ya Congo kumtabua Lumumba kama ni shujaa wa taifa hilo.

Bibie Pauline aligoma kuolewa na hadi anafikia kufariki akiwa na miaka 78 bila ya kuwa na mwanaume mwingine. Na hii aliifanya kwa ajili ya kulinda heshima ya mumewe, kuonyesha mapenzi aliyokua nayo juu ya mumewe na pia alisema hakuona mwanaume mwenye kaliba kama ya Patrice Lumumba.

Mnamo Desemba 23, 2014, akiwa na umri wa miaka 78, Pauline alikufa akiwa amelala nyumbani kwake Kinshasa, Kongo, Pauline alifariki wiki mmoja baada ya kurudi kutoka mjini Paris alikokua akipatiwa matibabu.

Sasa tumfahamu Patrice Lumumba mwenyewe..........................

Patrice Emery Élias Okit'Asombo Lumumba alikuwa ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo na ndie mwasisi wa taifa hilo alikuwa mwanasiasa na kiongozi akiwa na umri wa miaka 34 tu kwani alizaliwa tarehe 2 Julai,1925 huko katika kijiji cha Katakakombe wilaya ya Onalua katika jimbo la Kasai magharibi (Occidental Kasai) , na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu tarehe 30 Juni, 1960 baada ya kushinda katika uchaguzi wa serekali za mitaa.

Patrice Emery Élias Okit'Asombo Lumumba kiasili anatoka katika kabila dogo la Batetela ambalo ni Jamii ya KABILA kubwa la Luba, Ingawa Lumumba alizaliwa katika familia ya kikatoliki lakini alipata elimu yake ya msingi kwenye shule ya kiprotestanti iliyokuwa karibu na nyumbani kwao, alifaulu vema na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya seminari ya kikatoliki, baadaye alijiunga na chuo cha posta cha serikali ya kikoloni na kuhitimu akiwa na ufaulu wa juu zaidi.

Lumumba alijiunga kwenye umoja wa wasomi wa kiafrika( évolué- kwa kifaransa), huku akiandika makala na mashairi kwenye magazeti na majarida kwenye mji wa Kindu-Port-Empain uliopo katika jimbo la Manyema kwa sasa, huko mashariki ya kongo-DRC, baadae aliendelea na kazi huko katika mji wa Léopoldville (kwa sasa Kinshasa) kama karani wa shirika la posta National-mè postal, baadae alihamishiwa mji wa Stanleyville (kwa sasa Kisangani) uliopo katika jimbo la Ubangi province, ambapo huko alikuwa mhasibu wa shirika hilo.

Akiwa huko kisangani Mwaka 1955, alichaguliwa kuwa Raisi wa chama cha wafanyakazi wa serikalini katika mkoa huo, Hiki kilikuwa kichocheo kikubwa cha kuchukiwa na serikali ya kikoloni, kama haitoshi Lumumba alijiingiza katika harakati za kupinga uonevu na mateso ya wabelgiji, Pia alijiunga na chama cha kileberali cha ubeligiji (Belgian Liberal Party), Mwishoni mwa mwaka 1955, Lumumba alikamatwa Kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za shirika la posta, Mahakama ilimkuta na hatia na kumhukumu kwenda jela miaka miwili na baadae kupunguziwa adhabu baada ya kuthibitika kuwa alizirudisha fedha hizo, Lumumba alikiri kuchukua fedha hizo ili kuimarisha harakati za kuanzisha chama cha siasa.

Lumumba alivyo ingia kwenye siasa................

Asubuhi moja ya tarehe 1 December mwaka 1958, Ujumbe wa Chama cha kupigania Uhuru Afrika Mashariki Kati na Kusini (PAFMECSA) ulikuwa umetua jijini Kinshasa wakielekea Accra kwenye Mkutano wa nchi za Africa ulioitishwa na Rais Kwame Nkrumah wa Ghana mwaka 1958 (All Africa Conference), Ujumbe huu ulimjumuisha Julius Nyerere wa Tanzania, Abdurahman Babu wa Zanzibar, Tom Mboya wa Kenya na Kanyama Chiume wa NyasaLand, Wakiwa jijini humo, Kanyama Chiume na Babu wakawa wanatembea tembea mjini kusubiri ndege ya kuwabeba kuwapeleka Accra, walikuwa pale kwa siku 5 hivi, Katika kuuliza uliza kuhusu harakati za ukombozi katika Kongo, ndio wakaambiwa kuna kijana anapigapiga kelele mjini pale anaitwa Lumumba, wakaomba kumwona, Wakashangaa namna ambavyo habari za kupigania Uhuru Kongo hazijulikani kabisa nje ya Kongo, Walivutiwa sana na Lumumba, Wakamkatia tiketi ya ndege (Tom Mboya ndio alitumia fedha za wapigania uhuru wa Kenya kununua tiketi ya Lumumba), Wakaenda naye Accra, Afrika ikamjua Lumumba, Mapambano ya Kongo yakapata nguvu kubwa na hatimaye Uhuru ukapatikana.

Lumumba alipo rejea kutoka Ghana alirudi na mtazamo mpya wa kudai Uhuru wa nchi nzima, mwanzono Lumumba alikuwa akidai haki za wakongo na kutaka Waberigiji watoe usawa kwa Raia wa Kongo, lakini safari hii baada ya kurejea kutoka Accra mtazamo ulibadirika na Sasa alitaka Kongo kuwa huru kutoka kwenye makucha ya ukoloni, hivyo Lumumba Mara hii alikuwa moto zaidi.

Katika kikao cha Mwalimu Nyerere wa Tanganyika na Rais Ahmed Sekou Toure wa Guinea, Lumumba ndiye alikuwa mfasiri maana yeye alijua Kiswahili na Kifaransa, Mwalimu alijua Kiingereza na Kiswahili na Sekou Toure alijua Kifaransa tu, Lumumba kama mwanamapinduzi na mwanaharakati wa kweli aliimarika zaidi kwa mateso, kifungo na hata udhalilishaji aliofanyiwa, huku kiu yake ya mabadiliko na kutaka kuona Waafrika wanakuwa huru na kuheshimiwa ikamsukuma kuanzisha chama cha kwanza cha kisiasa mwezi oktoba,1958 kikiwa na muono wa kitaifa kilichoitwa (Mouvement National Congolais) yaani MNC.

Harakati kali zilizoongozwa na Patrice Lumumba, ziliwatisha wabelgiji hivyo kuanzisha mchakato wa kutoa uhuru ‘bandia’, Hivyo serikali ya kikoloni ya Ubergiji walitangaza uchaguzi kwa kuanzia na uchaguzi wa serikali za mitaa, mbinu hii chafu ya kuweka vibaraka iligunduliwa na chama cha MNC, Lumumba ambae alijipatia umaarufu kipindi hicho na kubatizwa jina la ‘The Black Mesiah’ aliongoza maandamano kupinga mpango huo wa kikoloni.

Lumumba na wenzie 10 walikamatwa kwenye mji wa Stanleyville kwa tuhuma za kuchochea machafuko na ghasia ambazo zilipelekea watu 30 kufariki, Lumumba alihukumiwa kwenda jela miezi sita, akiwa gerezani wanaharakati wa chama chake waliendelea kupambana na kushinda uchaguzi huo kwa asilimia zaidi ya 90%.

Hilo lilipelekea kuachiwa huru ili kuhudhuria mkutano huko mjini Brussels ulioridhia kutoa uhuru kwa nchi ya Kongo, Katika uchuguzi mkuu uliofanyika mwezi Mei, 1960 chama cha MNC kikiongozwa na Lumumba kilishinda na kupata haki ya kuunda serikali, Katika uchaguzi huo chama cha Patrice Lumumba MNC kilipata viti 33 kati ya siti 55 zilizokuwepo, na kujunyakulia jumla ya kura 521,187 sawa na 23.4% ya kula zote, huku cha pandikizi cha Waberigiji cha Joseph Kasa-Vubu kilichoitwa ABAKO kilipata viti 12, na kura za jumla 210,542 ambazo ni sawa na 9.5% ya kura zote, kwaiyo hii ilimaanisha kuwa Lumumba na MNC ndio washindi na kupelekea Patrice Emery Lumumba kutangazwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo iliyo huru tarehe 30 Juni, 1960, kushindwa kwa Kasavubu kuliwaumiza sana Waberigiji, hivyo wakaanzisha cheo cha uraisi ili tu kibaraka wao Kasavubu apate uongozi, hivyo Joseph Kasavubu akawa Raisi asiye na mamlaka yote.

Wakati wa sherehe za uhuru zilizofanyika kwenye Jumba la Taifa (Palace de la National, Kinshasa) Lumumba hakuwekwa kwenye ratiba ya watakaohutubia, Raisi Joseph Kasavubu na Mfalme wa Ubeligiji Baudouin walitoa hotuba zao zilizojaa sifa kwa wabelgiji, jambo hilo lilimkera sana Lumumba, alisimama kwa ujasiri na kutoa maneno ambayo nimeyaeleza huko nyuma kwenye makala hii.

Baada ya Uhuru Lumumba aliunda serikali, Patrice Emery Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo akiwa na umri wa miaka 37 tu na kwa kweli mabeberu hawakumruhusu kuongoza nchi yake kwa uhuru kuanzia siku ya kwanza ya Uhuru wa Taifa hilo, Akiwa kijana wa miaka 27 alianza mapambano ya kupigania Uhuru wa nchi yake, alifungwa, alipigwa, aliteswa na kudhalilishwa kwa kila namna na maafisa wa Kibeligiji lakini hakukata tamaa na alihakikisha Taifa lake linapata ukombozi wa kweli. Mabeberu, kwa tamaa ya utajiri wa Kongo kamwe hawakutaka nchi hiyo ipate uhuru wa kweli, Kwa kutumia vibaraka wao kama Tshombe, Kasavubu na Mobutu, Wabeligiji na rafiki zao Wamerekani walihakikisha wanammaliza mkombozi huyu.

Mobutu ambae alikuwa kijana wa Lumumba ndie kwa sehemu kubwa alitumika kumuangamiza Lumumba, ikumbukwe kuwa Mobutu alikuwa kijana wa Lumumba, ni Lumumba ndie aliye muingiza Mobutu kwenye siasa, ni Lumumba ndie aliye mpandisha cheo Mobutu mpaka kuwa kiongozi aliyejulikana nchini Kongo, nje ya yote Mobutu alikuwa Katibu binafsi wa Lumumba kwenye Chama cha ukombozi cha MNC.

Mwanzoni Mobutu alikuwa askari, aliyekuwa akiandika kwa kutumia jina bandia kuhusu mambo yaliyo kuwa yanayoendelea katika siasa nchini kongo katika gazeti jipya lilianzishwa na wakoloni wa Kibelgiji liloitwa "Actulites Africaines".

Mnamo mwaka 1955, aliacha jeshi na kuwa mwandishi wa habari, akiliandikia gazeti la Leopoldiville daily L'Avenier. Miaka miwili baadae alikwenda Ubelgiji kuchukua habari juu ya maonyesho ya 1958 ya World Exposition, alibakia huko kupata mafunzo ya uandishi wa habari.

Muda huu Mobutu alishakutana na vijana wengi wa Kikongo wasomi ambao walipinga utawala wa kikoloni, Alianza urafiki na Patrice Lumumba na alijiunga na chama cha Lumumba cha Mouvement National Congolais (MNC). Mobutu hatimae aliteuliwa kua msaidizi maalum wa Lumumba ingawa watu walishaanza minong'no kuwa Mobutu anafanya kazi na shirika la ujasusi la Ubelgiji, Lumumba alipo elezwa habari juu ya mashaka ya Mobutu alisema kuwa " Joseph (Mobutu) swahiba yake anaye mwamini sana kamwe hawezi kufanya hivyo", lakini baadae Mobutu alimsaliti na kushiriki kwenye kifo cha kikatili cha Patrice Lumumba.

Wakati Lumumba akiwa gerezani kule Katanga aliandika barua kwenda kwa wakongo kupitia kwa mkewe, Katika barua yake hiyo ya mwisho aliyomwandikia mkewe, Baadhi ya maneno ya barua hiyo maarufu na yenye heshima mpaka leo imekuwa ikitunzwa mpaka Leo ambayo barua hiyo ujumbe wake unasomeka;....

‘"…….naandika maneno haya nikiwa na shaka kama yatakufikia au nitakuwa hai, kipindi chote cha mapambano yangu sijawahi kuwa na shaka juu ya ushindi wa mwisho wa mapigano matakatifu, ambayo tumejitolea maisha yetu.

Kile tunaitakia nchi yetu ni haki ya kuwa na maisha yenye utu na kuheshimika toka kwa wabeligiji na vibaraka wao.

Hakuna mateso wala vitendo vyovyote vya kinyama vitakavyonifanya kuomba huruma, Ni bora kufa Kwa heshima, nikiamini kabisa na kujiamini kuhusu hatma ya nchi yangu kuliko kuishi kwenye utumwa na kuvunja misingi yangu. Ipo siku historia itasema; sio historia itakayoandikwa Umoja wa Mataifa, Washington, Paris au Brussels, lakini historia itakayofundishwa katika nchi zilizoondoa ukoloni na vibaraka wake.

Afrika itaandika historia yake iliyojaa utu na heshima, itakuwepo daima historia ya utukufu na utu’
Msinililie, wazalendo wenzangu, najua kuwa nchi yangu, inayoumia sana hivi sasa, itaweza kulinda Uhuru wake.

Idumu Kongo! Idumu Afrika
Mimi Patrice."'...

Wakati Patrice Emery Lumumba anauwawa nchi ya Kongo ilikuwa ipo chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa, Askari wa kulinda amani wa Ghana walipoona Lumumba amekamatwa na askari wa Mobutu walitaka kumwokoa na kumweka chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa lakini wakuu wa Umoja wa Mataifa wakasema hiyo sio kazi yao, sio ‘mandate’ yao, Wakuu wa Umoja wa Mataifa walisahau kabisa kwamba Lumumba alikuwa ni Mbunge na hivyo alikuwa na Kinga na hadhi ya Kulindwa kwa mujibu wa sheria za umoja wa mataifa, Lakini kwa kuwa umoja wa Mataifa wenyewe walikuwa wanafanya kazi ya Ubeligiji na Marekani kupitia mission maalumu, waliacha Lumumba, adui yao mkubwa, auwawe.

Ni miaka 61 Sasa toka Patrice Lumumba auwawe kupitia operation Barracuda, Lumumba alitaka uhuru kamili wa Kongo DRC na wa bara la Afrika, Lumumba hakutaka uhuru wa bandia, ndio maana damu yake ilimwagika kwa kudai Uhuru kamili, Lumumba alitaka utajiri wa Kongo DRC na Afrika utumike kwa ajili ya kuendeleza waafrika, Leo tunaona Afrika inaendelea kunyonywa na mataifa makubwa, Uchumi wa Afrika umemezwa kabisa kabisa na nchi nyingine, aliyoyakata Lumumba miaka 61 iliyopita ndio yanarejea safari hii, tena safari hii yanarejea kwa baraka za viongozi wa kiafrika wenyewe.

Nchi yenyewe ya Kongo ambayo Lumumba aliipambania na kutoa uhai wake bado imegubikwa na mauaji, Mamilioni ya wananchi wa Kongo wameuwawa huko mashariki toka mwaka 1996, Umoja wa Mataifa ambao ulishiriki kuhujumu Uhuru wa Kongo na uhai wa Lumumba bado wapo Kongo na wanaendelea kubariki machafuko na uvamizi wa mataifa ndani ya aridhi ya Kongo DRC, hali Sasa ni tofauti Waafrika wenyewe kwa wenyewe tunatumika dhidi yetu, Lumumba alishirikiana na wenzake kama Nyerere, Nkrumah, Kenyatta nk katika kupigania uhuru, ila viongozi wa sasa wa Afrika wanashirikiana na mabeberu kuinyonya Afrika.

Labda nikukumbushe kitu ili ujue ni kwanini Kongo DRC ilionwa muhimu kiasi hicho mpaka mabeberu kuigeuza shamba la bibi, hapa unatakiwa ujiulize kwanini ni Kongo? Waberigiji wana msemo wao usemao "Kongo ni nyama ya tembo kwa mabeberu", msemo huu humanisha kwamba nchi ya Kongo DRC inaponzwa na raslimali zake, madini, aridhi, eneo la kimkakati na utajiri ilionao ndio huiponza toka kipindi cha Uhuru mpaka Sasa.

Hii Inamaana kwamba.........................

Taifa la Kongo limejaliwa rasilimali nyingi sana kuliko taifa lolote lile dunia, Kongo ndio sehemu ya utajiri wa dunia, hii ni kwasababu rasilimali za dunia nzima nusu yake zipo Kongo, kila jimbo la Kongo linautajiri wa madini na vivutuo lukuki.

Hii ni kwamba...................

Kwanza, Kongo ina asilimia 80 ya ardhi ya Congo inafaa kwa kilimo, ni nchi yenye eneo kubwa sawa na Ulaya Magharibi, yani England, France, Germany, Italy, Netherland, Spain, Portugal, Belgium, Austria, nk.

Pili, Kongo ina hazina ya asilimia 10 ya shaba ya dunia nzima, Asilimia 30 ya cobalt ya dunia nzima, dhahabu, Almasi, Platinum, Bauxite, Lead (risasi), madini ya fedha, Zink, pia Kongo inazalisha asilimia 80 ya madini ya Coltan yanayotumika kutengeneza Simu, Sumaku, iPods, na injini za 'Jet'. Kongo pia ni tajiri wa Uranium. Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, Marekani waliipiga miji miwili ya Japan kwa mabomu ya atomic, Hiroshima na Nagasaki, Mabomu yale yalitengenezwa kwa madini ya Uranium iliyochimbwa Kongo.

Tatu, Mto Congo ni mto wa pili kwa Ukubwa duniani, una maporomoko ya Inga water falls, yanayoweza kuzalisha umeme na kusambazwa Africa na Ulaya kwa Pamoja.

Nne, nchi ya Kongo kuna aina 1100 za madini katika nchi yote ya Kongo, Utajiri wa madini peke yake unakaribia dola trilioni 32, sawa na uchumi wa marekani na Ulaya kwa Pamoja.

Tano, nchi ya Kongo ina Mafuta ambayo bado ayajaanza kuchimbwa, Misitu, wanyama, vivutio vya utalii vilivyopo Ituri na milima ya Virunga pamoja na mito na mabonde yenye unyevu na rutuba, maziwa, bahari, ni vivutio vyenye kuvutia duniani.

Sita, Miaka ya 1890s, wakati wa ugunduzi wa Rubber (mpira) iliyotumika kutengeneza mifuko, matairi ya baiskeli, pikipiki na magari, Kongo ilikuwa mzalishaji mkuu wa dunia, baada ya soko la mpira kushuka Kongo imebaki ndio nchi yenye mashamba makubea ya rubber plantation duniani.

Hata hivyo Leo hii, ni Miaka 126 baada ya mwandishi Joseph Conrad kuitabiria Kongo kuwa moja kati ya mataifa tajiri duniani, bado ni moja kati ya mataifa madogo na masikini wa kutupwa duniani.

Operation Barracuda aikutamatisha uhai wa Patrice Emery Élias Okit'Asombo Lumumba pekee bali ilizima ndoto nzima ya Uhuru wa nchi ya Kongo DRC na matumaini kwa Waafrika wote.

Operation Barracuda ndio mission pekee kubwa ya kijeshi kufanyika Afrika ambayo ilishirikisha mataifa mengi ya kibeberu, lakini ndio operation ambayo mataifa hayo yalitumia nguvu kubwa Katika kuifanikisha.

Viva Lumumba, viva Afrika.....

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2021, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 1848909View attachment 1848910View attachment 1848911View attachment 1848912View attachment 1848913View attachment 1848914View attachment 1848915View attachment 1848917View attachment 1848916View attachment 1848918View attachment 1848920View attachment 1848921View attachment 1848922View attachment 1848919View attachment 1848923View attachment 1848924View attachment 1848926View attachment 1848925
View attachment 1848931View attachment 1848928View attachment 1848929View attachment 1848930View attachment 1848934View attachment 1848932View attachment 1848933View attachment 1848935View attachment 1848936View attachment 1848939View attachment 1848940View attachment 1848942View attachment 1848941View attachment 1848944View attachment 1848943View attachment 1848945View attachment 1848946View attachment 1848947
Ukisoma "HEART OF DARKNESS" kila kitu kilichoandikwa humu utakikuta. Huyu jamaa alijitahidi Sana, kutafsiri novel nzima sio mchezo.
 
Nyuzi kali kama hizi huwa tuna like kwanza then tunarudi nyuma kusoma neno kwa neno.
 
Uzi haujatembea. Wana JF tunakwama wapi.
Kusoma bado ni mtihani mpaka karne hii kwa mtu mweusi. Hakika tuna safari ndefu.
Laiti utajiri huu wa Kongo ungekua hapa kwetu, leo tungekua ni sisi ndio tunalia na kusaga meno.
Ukiisoma hii unasisimkwa na kulengwa na machozi. Mpaka kesho naikumbuka documentary yake kichwani mwangu. Iliniliza.

Apumzike kwa amani Lumumba 'Son of Africa'. Bega kwa bega mpaka peponi kesho siku ya hukumu.
 
Hata hapa Tanzania hizi makala ipo siku zitaanza kujitokeza,,, japo ni kwa kificho sana ila kuna mengi yanaendele...

Hususani Raisi JPM kifo chake ndio huwa sielewi hadi leo ilikuwaje...
 
Ukisoma "HEART OF DARKNESS" kila kitu kilichoandikwa humu utakikuta. Huyu jamaa alijitahidi Sana, kutafsiri novel nzima sio mchezo.
Hivi kwanini wabongo tunapenda kukosoa tu na kujifanya wajuaji? Kila mtu anafahamu kwamba ukitaka taarifa lazima usome vitabu mbali mbali na kucompile ili kupata picha nzima. Sasa unaposema mtu katafsiri tu ulitegemea asitumie kitabu chochote?

Comred Mbwana Allyamtu kafanya narration nzuri na flow inayoeleweka na kuvutia, na huo ndio uandishi. Tujifunze kutoa appreciation sio kuleta ujuaji tu.
 
Hata hapa Tanzania hizi makala ipo siku zitaanza kujitokeza,,, japo ni kwa kificho sana ila kuna mengi yanaendele...

Hususani Raisi JPM kifo chake ndio huwa sielewi hadi leo ilikuwaje...
Mkuu ni Covid 19 which coincided with heart failure. Top doctors wa JKCI mbona wana data zote, hakuna mission yoyote ni changamoto ya kiafya iliyokuwepo muda mrefu. Hata kampeni si uliona alikua anachoka sana?
 
OPERATION BARRACUDA: "MISSION HATARI ZAIDI YA KIJASUSI KUFANYIKA AFRIKA" ILIYOSUKWA KUTAMATISHA MAISHA YA PATRICE LUMUMBA, NA KUZIMA NDOTO YA KILE KILICHOITWA MUSTAKABALI WA KONGO
Mkuu kwanza hongera kwa uzi wenye madini ya kutosha namna hii, tunahitaji watu kama nyie ili JF irudi katika ubora wake.

Lakini kwenye issue ya Lumumba nadhani alikosea kuonyesha msimamo wake mapema sana. Ilitakiwa ajifanye kibaraka mpaka pale nchi nzima iwe imetulia alafu sasa ndio aonyeshe makucha yake.

Mfano Felix Tshisekedi si umeona alijifanya kibaraka wa Kabila ila alipopewa tu Urais akahakikisha amekamata idara zote muhimu ndio akaonyesha makucha yake. So nadhani Lumumba hakua mwanasiasa otherwise ingekua ngumu kummaliza.
 
Operation ya jiwe nayo naisubiri nayo niikakati kama ya lmb

Time will tell kikubwa afya
 
Hivi kwanini wabongo tunapenda kukosoa tu na kujifanya wajuaji? Kila mtu anafahamu kwamba ukitaka taarifa lazima usome vitabu mbali mbali na kucompile ili kupata picha nzima. Sasa unaposema mtu katafsiri tu ulitegemea asitumie kitabu chochote?

Comred Mbwana Allyamtu kafanya narration nzuri na flow inayoeleweka na kuvutia, na huo ndio uandishi. Tujifunze kutoa appreciation sio kuleta ujuaji tu.
Pole Sana na sijuhi unashida gani,naona unakurupuka tu, uwe unatuliza akili kwanza aliyekosoa ni nani, kutaja kitabu na kusema mtu kajitahidi kutafsiri Novel ndiyo kukosoa? au hujuhi maana ya kukosoa au hukuelewa nilichokiandika? inaonekana hasira zinakusumbua. Ulitakiwa utoe komenti yako usonge mbele, na pia sio lazima appreciation unachokiona bora na cha maana mimi naweza kuona cha kawaida kwahiyo tusipangiane namna ya kukomenti.
 
Asante sana kwa kuweka sawa..... Tujifunze kujifunza
 
Pole Sana na sijuhi unashida gani,naona unakurupuka tu, uwe unatuliza akili kwanza aliyekosoa ni nani, kutaja kitabu na kusema mtu kajitahidi kutafsiri Novel ndiyo kukosoa? au hujuhi maana ya kukosoa au hukuelewa nilichokiandika? inaonekana hasira zinakusumbua. Ulitakiwa utoe komenti yako usonge mbele, na pia sio lazima appreciation unachokiona bora na cha maana mimi naweza kuona cha kawaida kwahiyo tusipangiane namna ya kukomenti.
Kwenye hiyo makala hakuna huu upuuzi wa kutafsri....
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom