Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

SAA TATU NA NUSU NITAWEKA SEHEMU YA KWANZA YA OPARESHENI YA PILI


Oparesheni ambayo ilitekelezwa na SAS (Special Air Services) dhidi ya wapiganaji 'masharobaro' makatili nchini Sierra Leon...



Stay tuned...
Am waiting
 
Msisitizo: Nifollow na hakikisha umesubscribe kwenye uzi huu ili kupata update za haraka nikiweka kitu


OPERATION ZA KIJASUSI ZA KIHISTORIA ZILIZOFANIKIWA ZAIDI

b6d41d0877e130572419fd57795c94e7.jpg



Niliandika kuhusu Oparesheni Entebbe na kuahidi kuwa nitaandika kuhusu Operesheni nyingine za kijeshi mpaka tukamilishe idadi ya Operesheni tano zakihistoria ambazo zina mengi ya kujifunza na kusisimua.



Leo hii nitaandika kuhusu operesheni hii nyingine ambayo ina mengi ya kujifunza na kusisimua.

4928c6571ae857d766955ba10b0b6710.jpg



OPERATION BARRAS







Mwaka wa Utekelezaji: 10 September 2000



Watekelezaji: British Army



Kitengo cha weledi: SAS (Special Air Services)



Nchi: Uingereza/Sierra Leon



Watu wa Kukumbukwa: Foday Kallay, Brigedia John Holmes









SEHEMU YA KWANZA





Kaika miaka ambayo nchi ya Siera Leon ilikuwa kwenye vita kali ya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1991 kuliibuka kikundi hatari nchini humo ambacho kilijulikana kama WEST SIDE BOYS (muda mwingine wakijulikana pia kama West Side Niggaz au West Side Junglers) ambao walikuwa na makao makuu yao katika kijiji cha Magbeni na Gberi Bana karibu kabisa na mto maarufu wa Rokel.





Kikundi hiki mwanzoni kilianza kama sehemu ya wapiganaji wa kikosi cha Armed Forces Revolutionary Coucil ambao walikuwa wanaunga mkono wapiganaji wa Revolutionary United Front kuipinga na ili kuing’oa serikali ambayo ilikuwa madarakani.





Wapiganaji wengi wa kikundi hiki cha West Side Boys walikuwa-recruited tangu utotoni kwa wazazi wao kuwawa na wao kutekwa na baadae kufanywa kuwa wapiganaji watiifu wa kikundi hiki.

Kwa kiwango kikubwa kikundi hiki kiliundwa na vijana wenye umri wa kati nah ii ilipelekea kikundi hiki licha ya kujihusisha na mapigano ya kijeshi lakini kilikuwa kinajinasibu na kujiendesha kwa tamaduni za kimarekani za muziki wa kufokafoka (rap) na tamaduni za hip-hop.





Labda nikiwa mahususi zaidi, kikundi hiki kilimuhusudu mno mwanamuziki wa rap Tupac Shakur pamoja na mtazamo wa ‘Kigangstaa’ ambao huwa anaudhihirsha kwenye muziki wake. Hii ndio sababu ya chaguzi ya jina la kikundi hiki ambao rasmi kabisa wao wenyewe walikuwa wanajiita ‘West Side Niggaz’ lakini kutokana na sababu za kimaadili kufanya vyombo vya habari kushindwa kutumia neno ‘Niggaz’ ndipo vyombo vya habari vikaondoa neno ‘Niggaz’ na kuweka ‘Boys’.





kikundi hiki kilikuwa kinajuliakana kwa umaarufu wake wa ukatili uliopitiliza ambao hasa unaaminika ulitokana na historia ya wapiganaji wake namna ambavyo walipatikana ambapo nilieleza awali kuwa wengi wao waliingizwa kwenye kikundi hiki tangu utotoni baada ya kutekwa kutoka kwenye familia zao. Jambo la msingi ambalo tunapaswa kulifahamu ni kwamba hawakutekwa tu hivi hivi na kuchukuliwa na kisha kuingizwa kundini, bali ilikuwa inafahamika wazi kwamba, watu wa kikundi hiki wakivamia kijiji kwa lengo la kuchukua watoto wa kiume mateka, kabla ya kuondoka nao walikuwa wanawalazimisha kuua familia zao kwa ukatili mkubwa.





Hii ilifanywa na viongozi wa kikundi hiki ili kuwapandikizia roho ya ukatili watoto hawa na kuua kiini cha ubinadamu wao na kuwafanya wajione na kutenda kama ‘wanyama’. Lengo lao hili lilitimia kwani kuna muda wakati wa vita hii ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leon kikundi cha ‘West Side Boys’ kiliibuka na kuwa moja ya vikundi vya wapiganaji ambavyo vilikuwa vinaogopwa zaidi.





Licha ya kuwa vitani na kufanya ukatili wa kila aina lakini wanachama wa kikundi hiki hawakuwa nyuma katika ‘kula maisha’ kwani walifahamika kuishi maisha ya ‘kigangstaa’ kama ambavyo wanaona kwenye muziki wa hip-hop wa kimagharibi. Walijulikana sana kwa kutumia sana bangi, cocaine, pombe na muda mwingine kuvaa mavazi ya kimagharibi mno licha ya kuwa vitani.





Silaha zao nyingi walipata kwa kubadilishana na almasi ambazo zilikuwa zinapatikana katika njia tata sana vitani mpaka kufikia wakati zikaitwa jina la ‘blood diamonds’. Magari yao karibia yote waliyokuwa wanayatumia kwa usafiri mengi walikuwa wameyateka kutoka kwenye misafara ya misaada ya chakula ya UN.







Sasa basi,



Kama ambavyo nimeeleza kuwa kikundi hiki cha West Side Boys mwanzoni kilikuwa kinaendeshwa na waasi wa Revolutionary United Front ambao walikuwa wanapambana ili kuiondoa serikali madarakani, lakini kuna muda baadae waligeuka na kuanza kupigana upande wa serikali, yaani baadae walipigana dhidi ya mabosi wao wa Revolutionary United Front.


8be894a07bd6079265310b405c515174.jpg


d0e0570a4550776f3612430c8a1b64b0.jpg

WAPIGANAJI WA "WEST SIDE BOYS"


Baada ya nchi kuanza kutulia katika miaka ya mwanzoni mwa 2000, vikundi vyote vya wapiganaji vilipewa ‘ofa’ ya kuingizwa rasmi katika jeshi la nchi. Vikundi vingi vilipokea ofa hii kwa mikono miwili lakini wapiganaji wa West Side Boys walikataa ofa hii na kuendelea na harakati zao za msituni kutokea katika makao makuu yao ya kijiji cha Magbeni na Gberi Bana.





Ikumbukwe kwamba katika vita hii, nchi ya Uingereza ilikuwa inaunga mkono serikali kwa kipindi chote cha maiaka 11 ya vita hii ya wenyewe kwa wenyewe.



Mwezi May mwaka 2000 kikosi maalumu cha wanajeshi wa Uingereza kiliingia nchini Sierra Leon kwa lengo moja kuu la kutekeleza operesheni malumu la kusaidia kuondoa nje ya nchi hiyo raia wa Uingereza na wa nchi za jumuiya ya madola ambao bado walikuwa nchini humo. Zoezi hili lilipewa jina la ‘Operation Palliser’. Wanajeshi ambao walikuwa wamepewa jukumu hili walikuwa na amri ya kutojihusisha na mapambano yoyote ya kijeshi bali waelekeze nguvu zao kwenye kusaidia raia wa uingereza na nchi za jumuiya ya madola kuondoka nchini humo, kwa lugha nyingine hii ilikuwa ni ‘non-combat operation’.



Kama sehemu ya mkakati wao wa uokozi kikosi hiki cha jeshi la uingereza viliweka chini ya himaya yake mji wa Freetown na uwanja wa ndege wa Lungi, ambao ndio kiwanja kikuuu cha ndege nchini Sierra Leon. Baada ya hapo liliendeshwa zoezi maridhawa la kuwaondoa nchini humo raian wote wa nchi za jumuiya ya madola ambao walikuwa tayari kwa hiari yao kuondoka nchini humo.



Baada ya Oparesheni Palliser kukamilika kikosi kile cha awali kiliondoka nchini Sierra Leon na kisha kuingizwa kikosi kingine kidogo kilichojulikana kama STTT (Short Term Training Team) ambacho kazi yake kuu waliyopewa ilikuwa ni kulisuka upya kimafunzo jeshi la Sierra Leon.





Kikosi hiki cha STTT kiliundwa na batalioni ya pili ya The Royal Anglian Regiment ambao ilipofika mwezi July mwaka huo 2000 walipumzishwa na nafasi yao kuchukuliwa na batalioni ya kwanza ya The Royal Irish Regiment (1 R IRISH) ambao sasa wao ndio walifanya kazi nchini Sierra Leon kama STTT.





Shughuli za kulifunda jeshi la Sierra Leon ikaendelea kwa mafanikio makubwa na kwa muda wote huu kikosi hiki kipya cha STTT kilikuwa salama kabisa nchini humo.





Lakini ilipofika siku ya tarehe 25 August mwaka 2000 msafara wa magari ya kijeshi ya STTT ulitoka kambini kwao eneo la Waterloo na kuelekea eneo linaloitwa Masiaka kuwatembelea walinda amani kutoka nchi ya Jordan ambao walijumuishwa katika kikosi maalumu cha Umoja wa Mtaifa ambacho kilikuwa nchini humo kikijulikana kama *UNAMSIL*.



Ulipofika muda wa chakula cha mchana wakiwa huko Masiaka walipata taarifa kuwa hatimaye kikundi cha West Side Boys wamekubali ombi la serikali la kuweka silaha chini na kujisalimisha.

Taarifa hii ya kijeshi ilikua imetolewa pasipo usahihi wa asilimia mia. Tofauti kabisa na taarifa hii kueleza kuwa West Side Boys wamekubali kuweka silaha chini, lakini uhalisia ulikuwa ni kwamba kuna wapiganaji wapatao kama 200 tu kutoka kikundi cha West Side Boys ndio ambao walikuwa wamekimbia kikundi chao na kwenda kujisalimisha kwa majeshi ya serikali, lakini kikundi chenyewe halisi bado kilikuwa na wapiganaji wapatao 400 ambao bado walibakia kuendeleza harakati zao.





Taarifa hii ilikuwa ni ya kutia moyo mno kutokana na Group la vijana hawa wa West Side Boys kusumbua mno vichwa vya majeshi ya serikali pamoja na vikosi vingine ambavyo vilikuwemo nchini Sierra Leon. Kama ilivyo Ada ya wanajeshi wote wanapopokea taarifa hii inakuwa kana kwamba hakuna haja ya kusubiri zaidi mpaka pale ambapo watahakikisha kama ni kweli walichokisikia kilikuwa ni sahihi na labda ndani ya Mwezi huu jeshi la nchi hiyo litakuwa limepiga hatua kubwa na labda hatimaye Simulizi za kutisha za vijana wa West Side Boys hawatazisikia tena.





Kwa hiyo ulipofika muda wa kurejea kambini kwao Waterloo, kamanda wa msafara huu wa kikosi hiki cha STTT (1R IRISH) alishauri kuwa wajiridhishe kuhsu taarifa hiyo ya vijana na West Side Boys kuweka silaha chini.


a928e63aebd007ce89e657ee03e1df47.jpg

WEST SIDE BOYS


Sasa basi, ukiwa unatoka eneo la Masiaka kwenda Wasterloo au Waterloo kwenda Masiaka, maeneo fulani ya kati kati kuna barabara inachepuka kulekea kwenye kijiji cha Magbeni ambacho kama nilivyoeleza awali kuwa kilikuwa kinatumiwa na West Side Boys kama makao makuu yao.





Kwa hiyo, Meja Alan Marshall, kamanda wa msafara akaamuru kuwa wachepuke kufuata barabara hiyo mpaka kijijini Mgbeni ili kuthibitisha taarifa ambayo walikuwa wameipata kuwa vijana hao walikuwa wameweka silaha chini.



Msafara ukashika kasi kukaribia kabisa kijiji cha Mgbeni. Lakini wakiwa wamebakiza kama kilomita mbili tu kuingia kwenye kijiji hicho walishangaa ghafla tu mbele yao imetokeza gari aina ya Bedford ambayo imefungwa mizinga ya kudungua ndege imewaziba njia mbele yao. Kufumba na kufumbua kila upande… nyuma, mbele… kushoto, kulia… walikuwa wamezungukwa na mamia ya wapiganaji wa West Side Boys wakiwa wamewanyooshea bunduki.



Msafara wao (STTT) ulikuwa na wanajeshi 11 tu, lakini vijana hawa wa West Side Boys ambao walijitokeza ghafla walikuwa si chini ya 150 au 200. Kwa maana hiyo ilikuwa dhahiri kabisa hawakutakiwa kuanzisha mapambano ya risasi kwani ndani ya sekunde kadhaa tu wangeuwawa. Hivyo basi hawakuthubutu hata kuinui silaha zao na kuwanyooshea ‘vichaa’ hawa wa West Side Boys ili walau waonekane hawakuwa na nia mbaya yeyote ile.



Baada ya kuwekwa chini ya ulinzi, walinyang’anywa silaha zote pamoja na magari yao ya kijeshi aina ya Land Rover zenye ‘Wimik’ (Weapons Mount Installation Kit (Tazama picha)) na kisha wakaongozwa kwa miguu kutoka pale walipokamatwa na kuvuka mto Rokel na kuingia kijiji cha Gberi Bana ambako ndiko kwenye makazi ya kiongozi wa kikundi hiki, mwanajeshi mwenye mbwembwe na ukatili usiomithilika, ‘Brigedia’ Foday Kallay.





Baada ya wanajeshi hawa mateka wa STTT kufikishwa tu mbele yake, kitu cha kwanza ambacho ‘Brigedia’ Faday Kallay alikifanya ni kuinua simu na kupiga London, serikali ya Uingereza.



Simu ilivyopokelewa… Brigedia Faday Kallay hakutaka salamu au kujieleza sana… moja kwa moja akaelekea kwenye hoja zake.





“this is brigadier Foday Kallay…get a piece of peper and a pen.!” Kallay alijieleza kwa lafudhi yake mbovu ya kiafrica cha magharibi.



“what for?” aliyepokea simu akamuuliza.



“I want you to write down a list of my demands.!!” Brigedia Faday Kallay akongea kwa kujiamini.



“demands for what.!?” Aliyepokea simu aliuliza kwa mshangao zaidi.



“…I have eleven of your soldiers… and if you don’t comply to my demands they are going to be dead in 48 hours.!” Brigedia Fadaya Kallay aliongea kwa sauti thabiti na kujiamini kabisa.







Japokuwa kwa kiasi fulani vita ya wenyewe kwa wenyewe hapa nchini Sierra Leon ilikuwa inaishia ishia… lakini kwa upande wa nchi ya Uingereza, siku hii ya August 5, 2000 walikuwa kana kwamba wanaingia upya kwenye ‘vita’ ya kwao na kikundi cha West Side Boys.

Jambo baya zaidi vijana hawa walikuwa hawaogopi kifo… ilikuwa ni kana kwamba nafsi zao zilikuwa tayari ziko kuzimu na ni miili tupu ilikuwa inatembea… hivyo kama Uingereza ilitaka kuwapata tena wanajeshi wake wakiwa bado hai… basi walipaswa kupiga kila hatua kuanzia sasa kwa umakini na weledi uliotukuka.



df90bf7e3c948b0f91b128c820553af0.jpg

MFANO WA LAND ROVER YENYE 'WIMIK' AMBAZO ZILIKUWA KWENYE MSAFARA KUTOKA MASIAKA NA KUPITA KIJIJI CHA MGBENI NA KUTEKWA


Itaendelea....




THE BOLD - 0718 096 811 (Namba kwa wale ambao wangependa kujiunga na group langu la WhatsApp (kuna ada 5,000/- kwa mwezi)... Tafadhali usipige


pia usisahau kutembelea tovuti yangu https://jamii.app/JFUserGuide
 
Mkuu The Bold, hivi kwa hapa nyumbani hakuna Operation ambayo imewahi kufanywa na wakuu wa hizi mambo ambayo unaweza kutuletea simulizi murua kabisa? Kwa mfano labda OPERATION NGORONGORO ile walitimua wasomali..sijui ilipewa jina gani..yan kuanzia uingiaji wa wasomali,utekaji,polisi walivyoenda baadae intelijensia na hatimae jeshi na kuwapoteza kabisa hao jamaa, angalau tuone na majina tofauti kama Ole Nangolo, Ole Syapa kwenye mazingira ya nyumbani.
 
Kisa huyo jamaa kumuua ni nini???
It is all about fame and fortune. Yoni was a rising military star. He was going up the ladder quickly.
Major General Yakutiel who was also killed in Lebanon in 1982 conflict knows better
 
Back
Top Bottom