ONYO - kwa wanaotumia mifuko ya mikate

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542

Baraza la Uhifadhi wa Mazingira nchini NEMC limesema halitamvumilia mtu ambaye atabainika kutumia mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na Serikali na kueleza kuwa atakayebainika atahukumiwa kwa mujibu wa sheria inavyosema.


Kauli hiyo imetolewa na Wakili wa NEMC, Vincent Haule wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, cha East Africa Radio ambapo aliulizwa swali kuhusiana na vifungashio vya mikate kutumika kama vifungashio vya bidhaa nyingine.

Mtangazaji Charles William - "kwa watumiaji wa mikate, vipi baada ya kutumia mkate akaamua kutumia mfuko wake kufungia kitu kingine?"

Akijibu swali Wakili wa NEMC, Vincent Haule amesema, "mtu atakayejaribu kufanya hivyo anahitaji adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria, atakuwa amefanya kosa kwa makusudi, atatozwa faini ya laki 2."

Mtangazaji Charles William - kuhusu vifungashio mnachanganya watu, leo mnasema vioneshe bidhaa iliyopo na vithibitishwe na TBS?

Vincent Haule - Kama mwanzo sikusema ni kosa letu, vifungashio vitaje bidhaa iliyopo, kwa mjasiriamali wa ubuyu haitamuathiri sababu si mtengenezaji.
 
Hukuona haya
Screenshot_20190618-152917.jpeg
 
Mikate yote ifungashwe kama mkate wa UNITED kutoka Kenya. Waliompakani na Kenya mnaelewa. Yaani karatasi fulani ambayo ni transparent
 
NEMC wange delegate power kwa raia, tuweze kuwachukulia hatua wale wote wasiotaka kuzingatia sheria za mazingira.
 
kenya wameadvance,ile kifungashio cha mikate ya UNITED kwa hapa bongo sijawahi ona,,pia ile mikate bana iko level ya juu sana
 
Back
Top Bottom