Hivi Chadema hakuna anaefaa kuwa Katibu Mkuu zaidi ya Slaa? mbona kuna vijana hodari na wachapakazi wenye maadili kama Zito Kabwe?
Chadema kinahusishwa na udini na ukanda! Slaa ni Padre na mlei wa Kanisa aliesaini mkataba wa KIFISADI wa MOU 1992 akiwakilisha Kanisa na Edwad Lowasa kama Waziri ktk Serikali ya awamu ya Pili!
kama mnataka kufuta hisia za kidini Chadema hamna budi kumsimamisha Mgombea urais mwingine mwenye sifa za uongozi na asie na kashfa za kifisadi, kimaadili au za kidini!
Slaa ni msalaba wenu na mkiendelea kumlea na kumuenzi, basi mjue Chadema itafia mikononi mwake!
Asiejua kifo aangalie kaburi! NCCR iko wapi?
The way unaongelea CDM ni kama wewe sio mwanachama wao.
Kama kweli wewe si mwanachama kwanini unaingilia mambo yao?
Acha chama kiamue nani awasimamie. Kila mtu ana historia, kila mtu ana dini.
Kama chama na wanachama wameridhika na Dr. Slaa, basi watampigia kura
Haijalishi kama alikua padre, coz hatowakilisha kanisa katoliki, atawakilisha CDM
On the other hand, kusema Dr. Slaa hafai ila Zitto Kabwe ndie anafaa ni uchochezi
Zitto mwenyewe kasema atatii maamuzi ya chama, na amesema wengi wanafaa
halafu wewe unakuja kusema hivo na unajua that is a hot question in CDM
Nahisi mchango wako ni wa kuchochea zaidi, sio wa kuleta mwangaza.
That said, naheshim hatua yako ya ku-express mtazamo wako hata kama sikubaliani nayo.
BTT: I think itakua vema Josephine akanushe, au aeleze kwanini anagombea
after all, she is a Tanzanian citizen, CDM member, ana haki ya kugombea
hasa kama anahisi ana uwezo wa kuwakilisha Kawe kuliko mbunge wa leo.