Onyo: Dr. Magufuli asizomewe tena

Onyo: Dr. Magufuli asizomewe tena

Tumechoshwa na vitendo vya kuzomewa kwa mgombea wetu. Kuanzia kule Mbeya na hata hapa Dar es Salaam,Dr. Magufuli amekuwa akizomewa na kuoneshwa wazi kuwa hatakiwi. Yeye hujikaza kisabuni tu. Hutetemeka lakini huimarika.

Amewakosea nini hadi mumzomee? Wana-Dar es Salaam hamna tabia hiyo. Mmekuwa watiifu kwa CCM kwa muda wote. Mmekuwa hata wavumilivu kuitwa wala-miguu ya kuku. Kiwewapata nini? Nani kawaondoa utii kwa CCM?

Mkimzomea tena Dr. Magufuli,nasi tutamzomea wenu hata kwa kuigiza kwenye giza. Mnapaswa kumshangilia Dr. Magufuli na kumpa kura zenu. Msimzomee na kumnyima kura tafadhari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Kwamba wakimzomea na nyire mtamzomea wao, hahahaha VUTA-NKUVUTE bwana!
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa nini mna tabia ya kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.Hivi unaamini kabisa kwamba hao waliokuwa wanamzomea Magufuli wamekunywa viroba.Si kweli.Ukweli ni kwamba hao ni watu walioichoka CCM.Ni matusi kuwaambia watu na akili zao wamekunywa viroba.Mnazidi kuwatia watanzania hasira.Inabidi muukubali ukweli,CCM ni chumvi iliyoharibika,haina budi kutupwa.Kujifariji kwamba wanaomzomea Magufuli wamekunywa viroba haitawasaidia.
CCM siasa zetu za kistaarabu. UKAWA wanaendeshwa kwa viroba! Katika hali kama hiyo ni lazima watafanya hizo tabia za kuzomea.

Aidha, UKAWA waelewe kuwa, CCM ina wanachama na wapenzi wengi pia, hivi na sisi tukiamua kuanza hiyo tabia ya zomea zomea, mgombea wao Lowassa atapona kweli?

Rai yangu ni kwamba vijana waache kukubali kutumiwa na wanasiasa kwa kupewa viroba ili kukidhi matakwa yao ya kudhalilisha wagombea. Hii tabia sio nzuri na haikubaliki.
 
napenda sana kuwashukuru wazazi wangu
kipindi kile wananikazania kuhusu elimu sikuwa ninaaelewa umuhimu wake
leo ndio ninaelewa kuwa shule ni kila kitu

wanaozomea ni mafala na malofa ... huwezi kuwa ukawa na akili nzuri na mwenye elimu yako ukakaa barabarani ukazomea unless hujaelimika ila tu umekaa tu muda mrefu darasani.....

Mwambie mama yako akakusomeshe tena. Kuzomewa ni Dunia nzima na sio Tanzania tu. Watu tumeshaona Marais wana zomewa na kurushiwa viatu na wasomi wa hali ya juu sembuse Tanzania. Kuzomewa ni ishara ya jambo fulani na sio matusi. Kuzomewa kwa magufuli ni ishara ya kwamba hakubaliki/ Hajatimiza matarajio ya wale wanao mzomea.
 
Magufuli wakati anapiga pushup jukwaani, muulize juma nyoso alimfanyia nini..... Haaahaahaa
 
Magufuri kazomewa Mbeya, Mkuranga, Bunju na Mbezi Luisi.
 
Magufuli kama Magufuli hana tatizo kabisa,he is a very hard working man! Tatizo ni kakalia tawi bovu ambalo ni SISIEMU!
Kwa hiyo kinachozomewa apo na vijana ni chama chake..na ndo maana ata yeye (JPM) hasemi ichagueni SiSiEmu!
 
napenda sana kuwashukuru wazazi wangu
kipindi kile wananikazania kuhusu elimu sikuwa ninaaelewa umuhimu wake
leo ndio ninaelewa kuwa shule ni kila kitu

wanaozomea ni mafala na malofa ... huwezi kuwa ukawa na akili nzuri na mwenye elimu yako ukakaa barabarani ukazomea unless hujaelimika ila tu umekaa tu muda mrefu darasani.....

Ni hulka ya wasomi fake. Dawa yao ni kupigwa tu.
 
IMG-20220725-WA0016.jpg
 
Back
Top Bottom