Only in tanzania

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Jana nilikuwa naangalia Taarifa ya Habari nikakutana na Habari kwamba kuna Shule moja ys Secondari huko kanda ya Ziwa inaitwa Lake Wanafunzi na Walimu Wanakunya na Kukojoa Vichakani kwa Ukosefu wa Vyoo: Nikakumbuka Kuna Mpango wa Kuwafanya Wakazi wa Dar Es Salaam Waendeshe Magari juu kwa juu yaani wawe wanapasua Anga za Manzese nk kuelekea Posta na Vimotokaa vyao.

Hii Kali Wakati wengine wanajisaidia Vichakani, wengine wanapita hewani na Magari in ze sem sem Kantri
 
Sasa unataka nani akawajengee choo? Yani wazasi wa hilo eneo wameshindwa kuchimba choo? Hawana mikono?
Wanaweza kuzaa tuuu! Kuwasomesha hawawezi wala kuchimba choo hwawezi?
 
Sasa unataka nani akawajengee choo? Yani wazasi wa hilo eneo wameshindwa kuchimba choo? Hawana mikono?
Wanaweza kuzaa tuuu! Kuwasomesha hawawezi wala kuchimba choo hwawezi?

Hivi ni kazi ya Wazazi kuchimba choo cha Shule ee! Nilikuwa Sijui
 
lakini huo ni uzembe wao,ina maana rais akawachimbie choo? hiyo haiwezekani, ndio maana kuna ngazi mbalimbali za uongozi, hawana mbunge hao watu?.....kutokana na matatizo yao itabidi watie akili mwaka huu wa uchaguzi wasichemshe...otherwise wataendelea kujisaidia machakani miaka mingine mitano ijayo
 
Got the Message? Au Mpaka waje Wahisani kuchimba Choo?
 
Ndhani system ya kusuburi serikali ifanye kila kitu inatuharibia sana sometime, sio kazi nzito sana kuweka angalau vyoo vya shimo.

Lakini hii ya barabara za kupasua anga ndo nasikia leo, kweli uchaguzi unakaribia!
 
......Huo ni uzembe wa wananchi wa eneo hilo, na hili tatizo si Tanzania peke yake ni Africa kwa ujumla.
 
Imagine wewe ndio Rais wa nchi unaambiwa shule ya secondary lake iliyoko Mwanza haina choo! Tena si shule ya serikali ni ya wazazi! Hawana choo mtu anailaumu serikali!!
Tutafika kweli! How much does it cost kuchimba choo cha shimo! Siamini kama watu ni wavivu wa kufikiri kiasi hiki!
 
Mkapa alisema watanzania ni wavivu wa kufikiria, mkamjia juu na kuanza kumtupia lawama. Sasa jamani mpaka choo unataka ujengewe?. Aliyejenga shule hiyo hakufikiria kujenga choo?. Tusipende kufanyiwa kila kitu na serikali, tujitegemee kadri tutakavyoweza na misaada ije pale tuliposhindwa kabisa kufanya wenyewe.
 
Miaka ya 1980s nilitembelea Nsumba sec School,Mwanza,shule ilikuwa na students kama 400 hivi,walikuwa na vyoo vay shimo,walikuwa wanaita Ubush.Ukitoka huko unanuka shati,suruali etc.Kumbuka kulikuwa na flash toilet lakini vilikuwa blocked miaka na miaka.

Kulikuwa na msaada wa NoRAD kuvuta maji ,baadae alikuja mwalimu mkuu mmoja i think 1984,akavitengeneza vyoo hivyo watu wakawa wanaflash tu.Lakini hakuna toilet paper,walikuwa wanatumia makaratasi kwa kuyakunjakunja.

Sishangai hali hiyo ya Lake Sec School,ni shule maarufu mjini Mwanza.Shuke zote ni kama Lake tu.Wanasema pimo la maendeleo ni kuwa na vyoo vya ndani.
angali nchi kama Ujerumani kama wato milllion 80 ,twice as much as Tanzania ,watu wanakunya vyoo vya ndani vya kuvuta!Hawashiki mavi kama sisi!
 
Back
Top Bottom