Only in Tanzania !

DSC00769[1].JPG
Unakaona ka-STK kwa mbali nyuma ya hiyo plate number ya Waziri?
 
baada ya hayo maajabu suluhisho ni nini?? tuendelee kuyavumilia??hilo nalo ni ajabu jingine wananchi kujua matatizo yao, kuyataja kujua chanzo cha matatizo lakini wakabaki wakilalamika tu! that can only happen in Tanzania!wapiga kura kuhongwa pilau that also can only happen in Tanzania!
 
Madini yake yanasafirishwa kontena kwa makontena kwa ndege usiku na mchana but tunaambiwa ni udongo tu ule. Jamani jamani iMnauma sana sana, kama ni udongo tu huyo mwekezaji kwa nini aingie gharama za kusafirisha kwa ndege na walinzi kibao? hao walinzi wanalinda udongo usiokuwa na dhamani? Machozi yananitoka. "ONLY IN TZ"
 
Nchi yenye Wafanyakazi wa Serikali Wa Wizara Moja wenye taalum zinazofanana Wanaolipwa Mishahara Tofauti. Mfano wanaitwa wa Wakala na Serikali Kuu. Nchi isiyojali Seniority na Experience ya Wafanyakazi wake. Wa Zamani anaachwa kuendelezwa Mpya anaendelezwa.
 
kweli only in tz:
1. Kubadilishana vyandarua+walimu 47 kwa dhahabu, almasi, tanzanite na wanyama pori. Only in tz.
2. Kupandisha twiga kwenye ndege,can only be done in Tanzania.
3. Rais, Waziri mkuu, Mwanasheria mkuu, na Waziri wa katiba kupingana hadharani wakati wanakaa meza moja ya baraza la mawaziri. This is definately in Tz n only in Tz...
3. Kuwa na wanachama uchwara wanaoendekeza siasa za majitaka za C C Mabwepande.. Can only b found in Tz.

Kuwa na rais anaewaita wanafunzi wanaopata mimba mashuleni wana KIHEREHERE badala ya kutafuta njia ya kusolve tatizo. Only in Tz.
 
nch ambayo usalama wa taifa una2mikia CHAMA badala ya taifa...nch ambayo viongoz wakuu wana chochea udini!,ONLY IN TZ
 
Ni katika Tanzania pekee ambapo unamuona SPIKA wa Bunge anakuwa pia Mwenyekiti [active] wa Board ya Kampuni kama Vodacom Tza na bado anaendelea salama na kazi kipindi chake chote, kama ilivyotokea kwa Spika kabla ya Mzee Sitta.
 
Chombo chenye kuhabarisha ukweli (mwanahalisi) kinafungiwa, ila chombo chochezi gazeti la an-nuur na radio imaan vikiachwa
Raisi Mbovu ambaye katika utawala wake Njaa ilikuwa kali
shida ilikuwa haisemeki ndiye anayepewa sifa kubwa tena
anataka kutangazwa kuwa mwenye heri.
 
watumishi halali (acha wale watumishi hewa) serikalini kupokea mshahara mwisho wa mwezi bila kuufanyia kazi....inaruhusiwa tanzania pekee!
 
Ukichunguza vyema utagundua kuwa TANZANIA ni nchi ya kipekee, inaendeshwa kwa namna ya pekee sana..ona baadhi ya vitu ambavyo vinaisababisha TANZANIA iwe very unique..

1. Tanzania ndio nchi pekee ambayo kiongozi wake mkuu, yaani raisi hajui kwanini nchi anayoingoza ni maskini.

2. Tanzania ndio nchi pekee ambayo kiongozi wake mkuu, yaani raisi hajui kwanini nchi anayoiongoza haina viwanda.

3. Tanzania ndio nchi pekee ambayo nchi inakuwa kwenye “CRISIS” za kidini, kiuchumi, na kisiasa lakini mkuu wa kaya anakaa kimya bila kutoa tamko wala muongozo.

4. Tanzania ndio nchi pekee ambayo mawaziri wake hawajui ni lini nchi hii ilizaliwa na kwa Muunganiko wa nchi zipi.

5. Tanzania ndio nchi pekee ambayo wanyama wake asili wanasafirishwa nje ya nchi kupitia viwanja vyake vya ndege bila hata watumishi wa viwanja hivyo kujua na hata usalama wa Taifa kufahamu hilo.

6. Tanzania ndio nchi pekee ambayo usalama wa Taifa wanafanya kazi ya kulinda usalama wa chama kilichopo madarakani badala ya kulinda usalama wa Taifa.

7. Tanzania ndio nchi pekee ambayo kwa siku TEMBO thelathini(30) wanauwawa kwenye hifadhi zetu na hakuna mtu anayestuka wala kushangaa.

8. Tanzania ndio nchi pekee ambayo usalama wa Taifa wanafanya kazi ya kuwakamata na kuwatesa wananchi wake pale wanapokuwa wanapigania haki zao za msingi, hata kama ni za msingi.

9. Tanzania ndio nchi pekee ambayo wabunge wake wanakimbia(WATORO) kwenye vikao vya BUNGE, mpaka wanakwamisha baadhi ya shughuli za BUNGE na nchi kwa ujumla lakini hakuna hatua za dhati kuhakikisha tabia hii inakomeshwa.

10. Tanzania ndio nchi pekee ambayo kuna amri jeshi wakuu zaidi ya mmoja, mwingine anasema TANZANIA IPO TAYARI KWA VITA na mwingine anasema hatuwezi pigana vita na nchi yoyote kwasasa.

11. Tanzania ndio nchi pekee ambayo inaongozwa na familia saba, yaani familia saba zinaamua mustakabali wa watanzania 45+.

12.Tanzania ndio nchi pekee ambayo watuhumiwa wa ufisadi na ujangili wa mali za umma wanadunda mtaani, na wezi wa kuku ndio wanajaza magereza yetu.

13.Tanzania ndio nchi pekee ambayo watuhumiwa wa ufisadi wanaendelea kutesa ndani ya CHAMA TAWALA, tena wakiwa na mipango madhubuti wa kuchukua nchi miaka michache ijayo.

14.Tanzania ndio nchi pekee ambayo mbunge anapewa dakika 15 za kuchangia mawazo yake bungeni kwaajili ya kujenga nchi, anatumia dakika 10 kutukana na kushukuru familia yake na raisi wa nchi. Na dakika 5 kwa kuonyesha udhaifu wa hoja iliyopo mezani na mwisho kuunga mkono asilimia 100.

15.Tanzania ndio nchi pekee ambayo CHAMA TAWALA kimechoka na wananchi wanateseka kwa umaskini, ila kwenye chaguzi mbalimbali bado kinapata ushindi mkubwa na wakushangaza.

16.Tanzania ndio nchi pekee ambayo wanaamini katika uganga na uchawi, badala ya sayansi kiasi kwamba watanzania + VIONGOZI wao walienda kunywa kikombe cha babu na barabara na mawasiliano yakapelekwa ili wananchi wengi wakanywe kikombe wapone.

17. Tanzania ndio nchi pekee ambayo kituo cha habari cha Taifa kinafanya kazi kwa maslahi ya chama tawala na bado hakuna hatua za dhati za kuliondoa hilo.

18. Tanzania ndio nchi pekee ambayo elimu yake inachezewa kama toi na hakuna mtu anayestuka, ndio nchi pekee ambayo “MASS FAILURE” ni kitu cha kawaida na hakuna anayejali na kupanga mikakati ya kuokoa hilo.

19.Tanzania ndio nchi pekee ambayo wagonjwa wanapelekewa ambulance za vibajaji AKA pikipiki za miguu mitatu, wakati watawala wake wanaendesha V8 na VX.

20.Tanzania ndio nchi pekee ambayo mahakama zake zinaongozwa na majaji ambao hawana sifa lakini bado wanafanya kazi bila wasiwasi wala mashaka…maana wana undugu na watu Fulani.

21.Tanzania ndio nchi pekee ambayo ina BODI YA MIKOPO ya wanafunzi wa elimu ya juu, ambayo inatoa mikopo kwa watoto wa vigogo na watawala na kuwaacha watoto maskini na wenye shida toka vijijini. YAANI VIGEZO NI LAZIMA BABA NA MAMA YAKO AWE NA PESA NDIO UPATE PESA.

22.Tanzania ndio nchi pekee ambayo, timu ya michezo inaenda kushiriki kwenye mashindano mbalimbali, viongozi na msafara wa wapambe unakuwa mkubwa kuliko wachezaji na washiri wa michezo hiyo.

23.Tanzania ndio nchi pekee ambayo KATIBU KIONGOZI anakuwa na madaraka makubwa kuliko waziri mkuu na BUNGE.

24.Tanzania ndio nchi pekee ambayo inaunda KAMATI TEULE na KAMATI ZA UCHUNGUZI nyingi, lakini matokeo ya kamati hizo yanakuwa ni kiini macho na wala hayafanyiwi kazi. NI NCHI YA KAMATI TEULE.

25.Tanzania ndio nchi pekee ambayo familia ya mkuu wa kaya inaenda kugombea kwenye chaguzi za chama tawala, na wanapita bila kupingwa, maana ni wateule.

Ndio hii ni Tanzania BANA………ONLY IN TANZANIA.
 
Only Tanzania, zinatumika noti (fedha) mbili tofauti kwenye mzunguko wa fedha
 
Back
Top Bottom