Only in Tanzana, kama huna pesa tupishe!

Only in Tanzana, kama huna pesa tupishe!

Kisa cha kwanza…

Nafika bucha na kuagiza kilo mbili za nyama kawaida. Kwa kuwa najua bei, natoa chenji kamili na kumkabidhi muuza bucha.

Anahesabu na kuniuliza mbona hela haitoshi? Napigwaa butwaa na kumuuliza kwani kulikoni? Ananijibu bei imepanda.

Naanza kulalama na ghafla nyuma yangu nasikia sauti, “Ee bwana kama huna hela tupishe, unatuchelewesha!

Sijakaa sawa sauti ya kike nayo ikadakia, “Wengine bwana, wapuuzi kweli kweli! Mtu huna hela kwani lazima ule nyama?

Taratibu nageuka na kukuta mstari nyuma yangu. Wote wamefura wakinitazama kama vile natoka sayari ya mbali.

Hakuna sura hata moja iliyoonekana kuniunga mkono au hata kushangaa kwa nini bei imepanda karibu mara mbili!
maisha kama hayo niliwahi kuishi. ni yale maisha unaenda bucha kununua nusu kilo ya nyama au utumbo, unakaa foleni, mbele yako jamaa anapimiwa kilo 10 za nyama na kilo 2 za maini, na kilo 5 za samaki. anaenda kuviweka kwenye jokofu ale polepole. akimaliza kupimiwa, inakuwa ngumu sana kumwambia muuza bucha kwamba unaomba nusu ya nyama au utumbo, na pengine nyuma yako kuna mteja wake anayefahamu akifika huwa ananunua kilo kuanzia 5 za nyama. hivyo wewe wa nusu kilo uwasubirishe hao. nilikuwa najifanya sina haraka namwambia wapimie tuhao, naendelea kupiga story hadi wapungue. sasaivi sasa, nawaona watu wanavizia pia kununua nusu kilo wakati mimi nanunua kilo za kutosha tu. huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu, anao uwezo kubadilisha kabisa maisha ya mtu.

Mungu humwinua mnyonge toka mavumbini, na mhitaji toka jaani (jalalani), na kumketisha pamoja na wakui. yeye humwinua amtakaye, na humshusha amtakaye. wenye kiburi hushushwa na Bwana, bali wanyenyekevu huwapa fadhila.
 
Unashangaa nyama imepanda, mwingine kasema kwa sauti , "nikatie nyama isiyo na mifupa Kg 10 za mbwa wangu.
 
Kisa cha kwanza…

Nafika bucha na kuagiza kilo mbili za nyama kawaida. Kwa kuwa najua bei, natoa chenji kamili na kumkabidhi muuza bucha.

Anahesabu na kuniuliza mbona hela haitoshi? Napigwaa butwaa na kumuuliza kwani kulikoni? Ananijibu bei imepanda.

Naanza kulalama na ghafla nyuma yangu nasikia sauti, “Ee bwana kama huna hela tupishe, unatuchelewesha!

Sijakaa sawa sauti ya kike nayo ikadakia, “Wengine bwana, wapuuzi kweli kweli! Mtu huna hela kwani lazima ule nyama?

Taratibu nageuka na kukuta mstari nyuma yangu. Wote wamefura wakinitazama kama vile natoka sayari ya mbali.

Hakuna sura hata moja iliyoonekana kuniunga mkono au hata kushangaa kwa nini bei imepanda karibu mara mbili!
Ndio tunategemea watu wataandamana kupinga kuongezeka gharama za maisha! WaTz hatujielewi!
 
Umeleta hoja nzuri mleta mada, bahati mbaya sana imepokelewa kama huko tunakopatia huduma hizo.
 
Mkuu na nafikilia walikufungia kwenye gazeti la michezo hiyo nyama, maana waliona unaleta mchezo na nyama🤣😂😂
 
Umeleta hoja nzuri mleta mada, bahati mbaya sana imepokelewa kama huko tunakopatia huduma hizo.
Asante sana ERoni umepiga pale pale kwenye kidonda.

Ndio tunategemea watu wataandamana kupinga kuongezeka gharama za maisha! WaTz hatujielewi!
Thubutu...hii inanikumbusha hadithi ya ile jela iliyojaa Watanzania watupu huko ughaibuni. Milango ya hiyo jela haikuhitaji kufuli wala walinzi. Kila aliyejaribu kutoroka wenzake walimkamata na kumrudisha ndani.

Kisa cha mwisho kitafuata...
 
Nilikuambia. Unaona majibu yao?

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Kwa mbali nakumbuka zile kejeli kutoka kwa baadhi ya mamlaka...
  • Hata mkila nyasi, ndege tunanunua!
  • Kama huna nauli ya kivuko, piga mbizi!
  • Kama unapinga tozo, hamia Burundi!
Na nyingine nyingi tu...only in Tanzania!
 
Hatuna lugha nzuri kwakweli watanzania...tumevurugwa
 
Back
Top Bottom